Yesu Aliiteka Mioyo Yao

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Yesu Aliiteka Mioyo Yao
Swahili
Year: 
2016
Quarter: 
3
Lesson Number: 
10

Utangulizi: Kwa miaka mingi, nimekuja kuhitimisha kuwa kile Mungu anachohitaji zaidi katika maisha yangu ni kumtumaini Yeye. Unafikiri ni kipi kikubwa Mungu anahitaji kutoka kwako? Ninafikiri kwamba endapo ningesikia majibu yenu, ningeweza kuyahusisha yote na tumaini. Endapo unafikiri kuwa Mungu anahitaji zaidi utii wako, hiyo inamaanisha kuwa unaweza kuamini ya kuwa maelekezo yake maishani mwako ni bora zaidi. Kama ambavyo tunahitaji kumtumaini Mungu, vivyo hivyo tunapaswa kuwasaidia watu wengine kumtumaini. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tujifunze zaidi!

 

  1. Kumtumaini Yesu

 

  1. Soma Yohana  13:33. Unafikiri wanafunzi walihisi vipi kuhusu jambo hili?

 

  1. Je, ilikuwa pigo kwao kufahamu kuwa walichukuliwa kama “Wayahudi” (Yesu atawaacha na hawawezi kumfuata wala kumpata. Kwa hali hiyo wao ni kama mtu mwingine yeyote yule.)

 

  1. Soma Yohana13:34-35. Suala hili linahusikaje na kuachwa?

 

  1. Soma Yohana13:36-37. Je, unafikiri Petro anazingatia kauli iliyosemwa na Yesu punde ya kwamba “mpendane?” (Hapana! Yeye bado anasumbuliwa sana na Yesu kuwaacha – na kumwacha yeye.)

 

  1. Kwa nini Petro anafikiri angeweza kwenda? (Kwa sababu angeutoa uhai wake kwa ajili ya Yesu.)

 

  1. Je, utayari wa Petro kufa unahusiana na mafungu aliyoyapuuza – ya kwamba wanafunzi wa Yesu wanapaswa kupendana? (Kilele cha tendo la upendo ni kuyatoa maisha yako kwa ajili ya mtu mwingine.)

 

  1. Soma Yohana13:38. Unapotafakari kisa cha Petro kumkana Yesu na kusulubiwa (Mathayo 26-27), je unaweza kuanza kuona ni huzuni kubwa kiasi gani Petro alihisi baada ya kumwangusha Yesu? Umewahi kuhisi huzuni ya namna hiyo?

 

  1. Soma Yohana14:1. Ni jambo gani Yesu anawaomba wanafunzi? (Anawaomba wamwamini yeye.)

 

  1. Soma Yohana14:2-4. Inadhihirika kuwa kumbe wanafunzi wanaweza kumfuata Yesu! Ni tumaini gani kuu la wanafunzi? (Mbinguni!)
     
  2. Hebu turejee tena mambo tete aliyoyasema Yesu. Soma tena Yohana 13:36. Yesu anamaanisha nini asemapo “utanifuata baadaye?” (Kisa cha Yohana 13 kinatokea muda kidogo kabla ya kifo cha Yesu. Yesu anapowaambia wanafunzi wake kuwa hawawezi kumfuata, anaonekana kuzungumzia juu ya mateso na kifo chake. Hapo baadaye watateseka na kufa kwa ajili ya Yesu. Ni mateso na kifo cha Yesu ambavyo vinawapa tumaini la mbinguni – ambalo ndilo eneo watakaloweza kumfuata.)
    1. Mfululizo wa matukio haya; mateso ya Yesu, kusulubishwa na ufufuo vinatufundisha nini kuhusu kuamini? (Ni nyakati zile ambazo tunateseka (au wale tuwapendao wanapoteseka) ndipo kudumisha imani kwa ushindi wa mwisho wa Mungu ndio linakuwa jambo la muhimu zaidi.)

 

  1. Pale Petro anaposema yupo tayari kutoa uhai wake kwa ajili ya Yesu (Yohana 13:37), je hii inaoneesha kuwa Petro kweli anaelewa kwamba Yesu anazungumzia juu ya kumfuata Yeye katika mauti ya msalaba?

 

  1. Soma Yohana 14:5. Inaonekana Tomaso si mwanafunzi mwerevu kati ya wote, lakini nina hakika anauliza swali ambalo wengine wote wangependa lijibiwe. Ni kwa jinsi gani ungejibu swali hili kulingana na ufahamu wako? Ni kwa namna gani wanaweza kumfuata Yesu?

 

  1. Soma Yohana 14:6. Nina hakika Tomaso bado amechanganyikiwa na jibu hilo! Alikuwa akitazamia maelekezo ya eneo halisi. Unaelewaje jibu la Yesu? (Njia ya mbinguni ni “kupitia” kwa Yesu. Kuja kwa Yesu, kifo na ufufuo, endapo tukifahamu na kukubali (“njia na kweli”), vitatupa uzima wa milele.)
     
  2. Soma Yohana 14:8-11. Ni kwa misingi ipi Yesu anatusihi kuwa na imani naye? Kuwa na imani kuwa yeye ni mwana wa Mungu? (Maneno yake, maisha yake na miujiza yake.)

 

  1. Kututumaini Sisi: Lengo
    1. Soma Yohana 14:12. Kwa sababu zipi tutatenda makuu kuliko Yesu? (Kwa sababu Yesu anaenda kwa Baba”)

 

  1. Kwanini unafikiri hiyo ni kweli? (Jibu pekee lenye mantiki linaonekana kuwa sasa tunachukua nafasi ya Yesu hapa duniani kwa maana ya kuleta watu wengi kwa Mungu.)

 

  1. Soma Yohana 13:13-14. Je umeona ahadi hii kuwa ya kweli? Umewahi kuomba jambo kwa jina laYesu na usipate?

 

  1. Nahisi ya kwamba jibu la wengi wetu litakuwa ni “ndiyo.” Kama ndivyo, unaelezeaje jambo hili linaloonekana kuwa ahadi ya wazi? (Muktadha wa ahadi ni huu: kuhamasisha imani na tumaini katika Yesu na Baba, na kuleta utukufu kwao. Je, ombi lako lilikuwa kwa ajili ya kuleta utukufu kwa Mungu au kwako binafsi?)
     
  2. Soma Yohana 14:15-17. Endapo kama sisi sasa ni mawakala wa Mungu, tunao msaada gani? (Roho Mtakatifu.)

 

  1. Hebu na tutafakari hili kwa muda. Yesu anawaambia wanafunzi wamtumaini Yeye, anasema kuwa anaondoka, na sasa sisi ni mawakala wake. Lipi ni jukumu letu lijapo suala la imani? (kwa uchache, inaonekana kuwa tunahitaji watu kutuamini kuwa sisi ni mawakala wa Mungu. Endapo kama Yesu alihusisha kumwamini Mungu na kumwamini Yeye, inaonekana kuwa jukumu hili linawekwa kwetu sasa. Tofauti kubwa ni kwamba Yesu ni Mungu na sisi siyo!)

 

  1. Yesu anasema (Yohana 14:15) “Mkinipenda, mtazishika amri zangu.” Ni kipi haswa Yesu anachoagiza? (Kumwamini Yesu na kufanya wengine kumwamini Mungu.)

 

  1. Soma Yohana 14:18-21. Yesu ametoka kutuambia ya kuwa Roho Mtakatifu anaishi ndani yetu. Sasa anasema ya kuwa sisi (Yesu, Baba na sisi) wote tupo “ndani” ya kila mmoja wetu. Anasema ya kuwa tutamwona. Lugha hii ya ajabu inamaanisha nini? (Kwa uchache, inamaanisha kuwa tuna uhusiano wa karibu sana.)
    1. Kwa mara nyingine Yesu anazungumzia utii na upendo. Nashawishika ya kwamba Yesu alitupatia amri zake ili kufanya maisha yetu kuwa bora, na si kigezo cha kutuhukumu. Mafungu haya yanapeleka ufahamu wetu kwa kina zaidi. Kwa nini kuzishika amri za Yesu kunamruhusu  “kutupenda na kujidhihirisha” kwake kwetu? (Ikiwa Mungu ametupatia amri zake kama ramani kuelekea maisha bora, hiyo inaunganisha upendo wa Mungu na utii. Kumtii Mungu kunafanya maisha yetu kuwa bora zaidi.)
      1. Ni kwa namna gani utii kwa amri za Mungu kunaturuhusu kumuona Mungu kwa ubora zaidi? Ni kwa namna gani hii “inatuonesha’ Mungu? (Amri nyingi zinajikita na namna tuwatendeavyo wengine. Hii inatusaidia kumwelewa Mungu kwa ubora zaidi.)

 

  1. Kututumaini Sisi: Tahadhari
    1. Soma Kumbukumbu la Torati 4:1-2. Ni tahadhari zipi mbili anazotupatia Mungu juu ya amri zake? (Usiongeze wala kupunguza.)
      1. Tukishindwa kufuata ushauri huu, je tunaweza kuibua suala la kutoaminiana? Kwa mfano liko wapi suala la kutoaminiana endapo “tutapunguza” kutoka kwenye sheria zake? (Tukisema tunazishika na hatuzishiki basi sisi ni wanafiki. Lengo la sheria ni kuboresha maisha maisha yetu. Endapo hatufuati sheria yote, vivyo hivyo hatuwezi kupata manufaa kamili ya baraka -  na hilo linamfanya Mungu kuonekana ametuangusha.)

 

  1. Suala la kutoaminiana ni lipi endapo “tutaongeza” kwenye sheria za Mungu? (Tunawapotosha wengine juu ya amri za Mungu. Kukiuka amri iliyoongezwa hakutokuwa na madhara. Hii itaweza kupelekea wengine kukiuka sheria halisi na kupata matokeo mabaya.)
     
  2. Soma Kumbukumbu la Torati 4:5-8. Ni kwa namna gani kufuata sheria za Mungu kunasababisha wale wasiomwamini Mungu kuvutiwa na kumfuata?
     
  3. Soma Matendo 7:9-10. Ikiwa unadhani watu hawatokuamini sababu ya hali yako ya maisha ya “kawaida”, tunaloweza kujifunza jambo gani kutoka kwa Yusufu? Wakati Yusufu alipokuwa Misri, je alianza kwenye nafasi ya kuaminiwa? (Hapana! Alikuwa mtumwa kwanza, na kisha mtumwa aliyetupwa gerezani kimakosa kwa kutenda uhalifu. Hizi sizo nafasi ambazo kiasili zinakupa sifa.)

 

  1. Marafiki, haijalishi hali yako ya kimaisha iko vipi, unaweza kwa pamoja kumwamini Mungu na kuwahamasisha wale wakuzungukao kumwamini pia. Tafakari maisha yako. Je, unamwamini Mungu, je unahamasisha kumwamini Mungu? Endapo jibu lako linakutafakarisha, kwa nini usimwombe Roho Mtakatifu, sasa hivi, akusaidie kumwamini Mungu na kuwahamasisha watu wengine kumwamini Mungu?
     

Juma lijalo: Yesu Akawaambia, “Nifuateni.”