Kuwa Vile Utakavyo Kuwa

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(2 Petro 1:1-15)
Swahili
Year: 
2017
Quarter: 
2
Lesson Number: 
9

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: “Kuwa Vile Utakavyo” unaonekana kama wito ulioandikwa ukutani mahali pa wazi, au wito uliopitwa na wakati (mchuuko) unaorudiwarudiwa na mtu mrembo sana lakini asiye na akili nyingi (mwerevu). Unawezaje kujizuia kuwa “vile utakavyo?” Ikiwa ningekuuliza kwamba, “Wewe ni nani?” ungejibuje? Ikiwa umejibu kuwa, “Mimi ni Mkristo,” hiyo ndio mada ambayo Petro anatuandikia katika somo letu juma hili. Petro anatupatia maelekezo ya jinsi tunavyopaswa kuwa kwa mujibu wa madai yetu – Wakristo. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tujifunze zaidi!

 

  1. Karama ya Haki

 

    1. Soma 2 Petro 1:1. Tunaipokeaje imani? (Katika hali ya Mungu wetu, na Mwokozi Yesu Kristo.)

 

      1. Je, hicho ndicho tulichokifanya? (Hapana! Ni haki ya Yesu. “Tuliipokea.”)

 

    1. Soma 2 Petro 1:2. Tunaipataje amani tele maishani mwetu? (Kwa kumjua Yesu.)

 

      1. Unatumia kiasi gani cha muda kujifunza zaidi habari za Yesu? (Kama hufurahii amani tele maishani mwako, unatakiwa kutafakari ili utumie muda mwingi zaidi kujifunza habari za Yesu.)

 

  1. Karama ya Uzima

 

    1. Soma 2 Petro 1:3. Je, umewahi kusoma kitabu cha mwongozo (manual) wa gari lako? Tuchukulie kwamba mtu amekupa gari. Je, unaweza kufurahia matumizi kamili ya gari lako kama utakuwa hujasoma kitabu cha mwongozo? (Gari langu halina vitasa vya mlango – vya ndani wala vya nje. Nilitaarifiwa kwamba mtu anayemiliki gari kama langu alifia ndani ya gari lake (pamoja na mbwa wake) kwa kuwa kulikuwa na joto nje ya gari, seli (betri) inayoendesha milango iliishiwa nguvu, na hakuweza kujua jinsi ya kutoka ndani ya gari. Kitabu cha mwongozo kinaelezea jinsi ya kutoka ndani ya gari betri inapokuwa haina nguvu.)

 

      1. Je, tulipewa “kila tunachokihitaji maisha mwetu pamoja na utauwa?” (Ndiyo! Petro anatuambia kuwa kwa uwezo wa Mungu “tulipewa” tunachokihitaji maishani mwetu na kuishi maisha matakatifu.)

 

        1. Je, tunahitajika kusoma kitabu cha mwongozo? (Ndiyo! Utaona kwamba kifungu cha tatu kinasema kuwa “tumekirimiwa vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuit”)

 

      1. Ungehitaji kitu gani kingine endapo ulipewa “kila kitu unachokihitaji” kwa maishani mwako – maisha yanayompendeza Mungu?

 

 

      1. Utaona kwamba mwishoni mwa kifungu cha tatu imeandikwa kuwa Yesu anatuita “kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.” Hii inaashiria nini juu ya usomaji wetu? (Kadri tunavyouelewa “utukufu na wema” wa Yesu, tunaelewa vizuri zaidi anachokifikiria Yesu mawazoni mwake kwa ajili ya maisha yetu.)

 

    1. Soma 2 Petro 1:4. Tafakari kwa makini anachokimaanisha Petro anaposema “tena kwa hayo ametukirimia.” Hayo mambo gani? Ni mambo gani hayo ambayo Mungu ametupatia “ahadi kubwa mno za thamani?” (Jambo ambalo Petro alilibainisha hapo awali ni namna ambayo tunapewa “ahadi kubwa mno za thamani.” Sina uhakika zipi kati ya “hizi” ndizo karama, lakini yumkini Petro anarejea hizi karama zote: imani, neema, amani, maarifa, uwezo wa Mungu, uzima, utauwa, utukufu na utu wema.)

 

      1. Lengo la hizi karama ni lipi? (“Kushiriki katika tabia ya Mungu na kuokolewa na uharibifu uliomo duniani unaosababishwa na tamaa ovu.”)

 

      1. Unatathminije tamaa zako? Ni ni tamaa ovu au umeokolewa dhidi ya hivi tamaa ovu?

 

  1. Juhudi ya Maisha

 

    1. Hadi kufikia hapa tumekuwa tukijadili karama. Sasa Petro anabadili mjadala kuingia kwenye jambo tunalohitajika kulitenda. Soma 2 Petro 1:5 na uilinganishe na 2 Petro 1:1. Petro anaanza kwa kusema kuwa tunapokea imani “katika hali ya … Yesu.” Unawezaje kuendelea kuongezea wema kwenye karama ya imani?

 

      1. Je, hilo ni jambo unaloweza kulifanyia kazi? Au, huo ni mtazamo?

 

        1. Je, unaweza kuufanyia kazi mtazamo? (Wangapi kati yenu mna wazazi waliowaambia, “Muwe wema?” Kwa dhahiri walidhani kuwa hili ni jambo lililo ndani ya uwezo wenu.)

 

    1. Soma tena sehemu ya mwisho ya 2 Petro 1:5. Je, unaweza kujiongezea maarifa? Je, hilo limo ndani ya uwezo wako? (Katika jambo hili, hakuna mjadala. Ukitaka kujifunza jambo, basi unasoma, unakwenda shule, unafanya majadiliano.)

 

      1. Uelewa wa Biblia upo kwa kiasi gani miongoni mwa umma wote kwa ujumla? (Kuna tatizo kubwa sana nchini Marekani. Biblia inafundisha mabadiliko kwa njia ya upendo. Inafundisha mabadiliko kwa njia ya ushawishi. Imani hii ya kidini inaakisiwa kwenye Katiba yetu, na hususani katika Mabadiliko kwenye Katiba ya Marekani. Kuna kizazi kipya ambacho hakielewi uhuru wa maoni wala uhuru wa kuabudu. Kinaamini kuwa ni haki kutumia nguvu na uogofyaji ili kukandamiza uhuru wa maoni na imani za dini wasizokubaliana nazo.)

 

      1. Suluhisho la tatizo hili ni lipi? (Petro amepatia – tunatakiwa kueneza uelewa wa Mungu.)

 

    1. Soma 2 Petro 1:6. Kwa nini Petro anasema kuongezea “kiasi” baada ya kupata maarifa? (Ukielewa kwa ueledi sababu za kutumia njia sahihi, ni rahisi zaidi kuwa na kiasi. Ni tofauti kati ya “Fanya hivyo kwa kuwa nimekuambia,” na “litende jambo hilo kwa kuwa unajua kwamba kwa kufanya hivyo itakusaidia.”)

 

 

    1. Soma tena 2 Petro 1:6. Saburi inafuatia baada ya kiasi. Je, ni kitu kingine tofauti? (Kinaongezea kigezo cha muda. Usiwe na kiasi kwa dakika moja au kwa saa moja au kwa siku moja. Kiasi ni mradi (jambo) wa muda mrefu.)

 

      1. Kwa nini “utauwa” unafuatia baada ya kudhamiria na kujizatiti kuwa na kiasi kwa muda mrefu? (Baada ya yote hayo utauwa unakuwa tabia yako maishani mwako!)

 

    1. Hebu tuangalie jambo jingine kidogo. Je, kuwa Mkristo ni jambo jepesi? (Petro alianza kwa kutuambia kuwa imani ni karama. Zana za kukuza imani yetu ni karama. Tunazitumia zana hizi kuanza safari ya kuuelekea utakatifu. Hilo linahitaji dhamira na juhudi.)

 

    1. Soma 2 Petro 1:7. Ikiwa umewahi kukatishwa tamaa kwa maanguko yako kama Mkristo, hili ni mojawapo ya mafungu ya Biblia yanayotia hamasa sana. Utaona kwamba “utu wema” ni jambo unalolijenga kwenye msingi wa “utauwa.” Hilo linawezekanaje? (Ninawafahamu watu ambao wako makini sana katika mtindo wao wa maisha. Lakini, wana kiwango kichanga cha utu wema maishani mwao. Kama unaona ugumu kuwa mwema, basi kifungu hiki ni habari njema kwako. Utu wema ndio hatua inayofuata zaidi ya utauwa!)

 

    1. Soma tena 2 Petro 1:7. Maadili ya mwisho na makuu katika njia yako ya kuuelekea utakatifu ni yapi? (Upendo. Kama unakatishwa tamaa kwa kutokuwa na upendo, basi unapaswa kuelewa kwamba “upendo” ni summa cum laude, Mkanda mweusi, Eagle Scout, Master Guide (kiwango cha juu kabisa cha mafanikio) cha maisha ya Mkristo!)

 

      1. Hiyo inakwambia nini kuhusu watu wanaosema kuwa, “Unachotakiwa kukifanya ni kuwa na upendo pekee.” “Unaonaje kama utaanza tu kwa kuwa na upendo?” (Hawana taarifa za kina. Upendo wanaouzungumzia hauna maana. Upendo ndio kilele cha safari ya Mkristo kuuelekea utakatifu. Sio hatua ya kwanza.)

 

    1. Soma 2 Petro 1:8-9. Kwa nini tunapaswa kujali kujua kama tupo kwenye njia sahihi kuuelekea utakatifu? (Tupo katikati ya pambano kati ya wema na uovu. Tunapokuwa na hizi tabia, tunakuwa na ufanisi katika kuutangaza Ufalme wa Mungu. Kama hatufanyi hivyo, basi hatuna ufanisi. Tumesahau kile alichotutendea Yesu.)

 

  1. Uchaguzi

 

    1. Soma 2 Petro 1:10-11. Je, Petro anatuambia kuwa lazima tuwe kwenye njia inayouelekea utakatifu ili tuokolewe, ili “kufanya uchaguzi wetu” kama Wakristo uwe wa “uhakika?” (Ninaamini katika uhuru wa maoni katika suala la wokovu. Tulijadili suala hili katika masomo ya nyuma kwenye huu mfululizo wa nyaraka za Petro. Hiyo inamaanisha kuwa tunaweza tusichague kuokolewa. Lakini, sidhani kama hicho ndicho anachokimaanisha Petro hapa, kama tutakavyojadili katika sehemu inayofuata.)

 

    1. Soma Warumi 9:10-16. Hapa tunaona neno “uchaguzi” pamoja na maelezo ya jinsi uchaguzi unavyofanya kazi. Je, hapa “uchaguzi” unamaanisha nini? Uchaguzi huo unafanyikaje? (Kwa dhahiri vifungu hivi vinasema kuwa uchaguzi haubadilishi matendo yetu. Ukisoma sura nzima (Warumi 9), inajenga hoja kwenye mada ya kuhesabiwa haki kwa imani. Inachoelezea ni watu maalumu ambao Mungu anawachagua kuwa mashuhuda wake maalumu. Mungu amekuchagua ili uutangaze Ufalme wake. Baki kwenye njia inayouelekea utakatifu ili uweze kuwa wakili mwenye ufanisi wa hali ya juu.)

 

 

    1. Soma 2 Petro 1:12-15. Je, tunao muda wa kutosha kabisa hapa duniani kukamilisha malengo ya Mungu? (Hapana. Wakati fulani tutayaacha maisha haya ya hapa duniani. Wajibu wetu ni kuifanya kazi yetu iwe ya kudumu kwa kadri inavyowezekana.)

 

    1. Rafiki, je, unaishi kwa kadri ya wito wako na uchaguzi wako? Ikiwa sivyo, kwa nini usimwombe Mungu sasa hivi akusamehe na umwombe Roho Mtakatifu akufanye kuwa shuhuda mahiri wa Mungu?

 

Juma lijalo: Unabii na Maandiko.