Somo la 2: Ninaona, Ninahitaji, Ninachukua

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Malaki 3, Luka 7, Waebrania 11, 2 Wakorintho 8)
Swahili
Year: 
2018
Quarter: 
1
Lesson Number: 
2

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Somo letu la Luka 12 juma lililopita lilitufundisha mambo muhimu. Kwanza, Luka 12:30 inatuambia kuwa Baba yetu wa mbinguni anafahamu kwamba “tunahitaji” viyu ambavyo “ulimwengu wa kipagani unavikimbilia.” Pili, Luka 12:31 inatuambia kuwa ikiwa tutautafuta ufalme wa Mungu, Mungu atatupatia vitu ambavyo ulimwengu wa kipagani unavitafuta. Huo ni ujumbe wa kufurahisha sana, ujumbe ambao haueleweki kirahisi. Hebu tuendelee na somo letu juma hili kwa kuangalia kile ambacho Biblia inatufundisha kuhusu kupokea na kutoa kwa watu wengine!

 

  1. Mungu Atuahidiye Mali

 

    1. Pitia kwa haraka haraka Kumbukumbu la Torati 28:1-14 na usome Malaki 3:8-11. Mambo mengi yameandikwa dhidi ya kile kinachoitwa “injili ya usitawi.” Kimsingi injili hiyo inasema kuwa wafuasi wa Mungu watakuwa matajiri. Kwa kuzingatia Kumbukumbu la Totari 28 na Malaki 3, je, hii dhana ya usitawi imejengwa kwenye ahadi za Mungu? (Hicho ndicho hasa kinachoonekana kuahidiwa kwenye hizi rejea mbili.)

 

      1. Angalia tena Malaki 3:10. Kifungu hiki kinasema kuwa utajiri wa aina gani huwajia walio waaminifu katika zaka na sadaka? (Kinasema kuwa hutakuwa na nafasi kwa ajili ya kuhifadhi huo utajiri. Hiyo inaonekana kama ilivyokuwa kwa mkulima wetu juma lililopita aliyebarikiwa sana kiasi cha kujenga ghala mpya ili kuhifadhi utajiri wote huu.)

 

        1. Kuna baadhi ya watu wanaobainisha kwa usahihi kabisa kwamba Malaki 3:10 inazungumzia “baraka” na si “fedh” Unaelewaje asili ya baraka zilizoahidiwa katika Malaki 3? (Kwanza, kutuambia kwamba “hatutakuwa na nafasi ya kutosha” kwa dhahiri inaonekana kuwa ni baraka za vitu. Hata hivyo, Malaki 3:11 inaondoa mashaka yote kwa sababu kwa mahsusi kabisa inazungumzia mafanikio ya mkulima kutokana na mazao yake. Kwa kiasi fulani Mungu anazungumzia mafanikio yetu ya vitu.)

 

      1. Unapotafakari vifungu hivi, je, vinaonekana kuashiria kwamba Mungu ni aina fulani hivi ya mashine sarafu (ya kuuza bidhaa ndogondogo) ya mbinguni yenye ukarimu – kwamba toa zaka na sadaka nawe utapata malipo zaidi ya yale unayoweza kuyahifadhi kwa sasa? (Hivyo ndivyo hasa jinsi mambo haya yanavyoonekana kuwa.)

 

 

        1. Je, kuna sababu nyingine yoyote ile inayoweza kutufanya tuamini kwamba hivyo sivyo Mungu awaziavyo? Soma Luka 12:31. Kifungu hiki kinatuambia kuwa lengo la Mungu kwetu ni lipi? (Kuutafuta Ufalme wa Mungu badala ya kutafuta (au kuwa na wasiwasi juu ya) vitu. Ujumbe wa Luka 12:22-31 ni kwamba hatupaswi kuufanya utajiri kuwa kipaumbele chetu. Ikiwa kweli Mungu anajitoa kuwa mashine inayozalisha na kuongeza fedha zetu, huo utakuwa ni mvuto wa moja kwa moja wa ukumbatiaji mali. Hicho sicho anachokimaanisha Mungu.)

 

    1. Soma Mathayo 7:9-11. Je, unataka kuwapatia wanao vitu? Ikiwa ndiyo, toa sababu na kisha uelezee kwa nini hiyo haikufanyi wewe kuwa “mashine sarafu?” (Tunawapa watoto wetu vitu kwa kuwa tunawapenda. Unaweza kuwa beuzi na kusema kuwa hiyo inaonekana kuwa kama mashine sarafu, lakini ukweli ni kwamba tunafanya hivyo kwa sababu tunawapenda.)

 

    1. Soma Mathayo 7:12. Je, “torati na manabii” zinatutendea nini? (Zinatupatia njia bora ya namna ya kuishi. Upendo wa Mungu kwetu unamfanya atupatie vitu vizuri, kama ilivyo kwa upendo wetu kwa watoto wetu unavyotufanya tuwapatie vitu vizuri. Wazazi wangu walitaka niwe na mafanikio na mwenye usitawi. Mungu anayo malengo hayo hayo kwa ajili yetu, na anatupatia torati yake ili kusaidia azma hiyo itimie.)

 

    1. Soma Waebrania 11:32-35. Isipokuwa kwa sehemu ya mwisho ya kifungu cha 35, je, haya ndio maisha ambayo ungependa kuwa nayo? Je, haya ndio maisha ambayo Mungu anataka uwe nayo?

 

    1. Soma Waebrania 11:35-38. Hebu subiri kidogo! Tunayaelezeaje matokeo haya? Je, Kumbukumbu la Torati 28 na Malaki 3 hazikuahidiwa kwao pia?

 

    1. Soma Waebrania 11:39-40. Akina nani ambao hawakupokea yote yale yaliyoahidiwa? Je, ni watu wa Mungu tu walioelezewa katika Waebrania 11:35-38? (Ikiwa huna uhakika, soma Waebrania 11 yote. Anachokimaanisha Mungu ni kwamba wafuasi wake walikuwa na viwango mbalimbali vya mafanikio na usitawi. Hata hivyo, hakuna hata mmojawao aliyepokea ahadi kamili ya Mungu hapa duniani.)

 

      1. Unadhani Mungu anamaanisha nini kuhusu tamaa ya vitu na mafanikio katika Waebrania 11, na inahusianaje na Kumbukumbu la Torati 28 na Malaki 3? (Mungu anataka kutupatia karama kubwa, Mungu anataka kutusitawisha. Hata hivyo, ulimwengu wa dhambi unaingilia kati ili kwamba hakuna hata mmoja kati yetu atakayepokea ahadi kamili ya Mungu hadi tutakapofika mbinguni.)

 

        1. Hiyo inakufanya uichukulieje injili ya usitawi? (Ikiwa ahadi kamili inatimia mbinguni na katika ulimwengu utakaofanywa upya pekee, basi juhudi zetu hapa duniani zinapaswa kujikita katika kuutangaza Ufalme wa Mungu – jambo ambalo ndilo hasa Yesu alilolielekeza katika Luka 12:31.)

 

    1. Hivyo basi, jambo hili linatendekaje kivitendo? Hebu tugeukie kwenye mfano halisi katika sehemu inayofuata.

 

  1. Maisha Kivitendo

 

 

    1. Soma 2 Wakorintho 8:1-2. Hebu subiri kidogo! Hawa ni Wakristo wanaopitia “majaribu makali” na “umasikini wa kutupwa.” Unayaelezeaje matokeo haya? Je, ni kwa sababu hawamtii Mungu, hawaupatii Ufalme wa Mungu nafasi ya kwanza, au hawana ukarimu kwa Mungu? (Kwa dhahiri ni wakarimu. Paulo anawaita “ndugu na dada,” hivyo inaonekana wanamfuata Mungu.)

 

      1. Inawezekanaje kuwa na furaha na ukarimu katikati ya majaribu na “umasikini wa kutupwa?” (Kifungu cha 1 kinatuambia kuwa inatokana na “neema.” Huu ni ushahidi zaidi wa wao kuwa na uhusiano sahihi na Mungu.)

 

      1. Ikiwa Mungu anawaonesha neema, kwa nini basi hawaufurahii utajiri? (Hii inaanza kutupatia taswira kamili wa kile kinachoweza kumaanishwa kwa baraka za Mungu. Tunaunganisha furaha na ukarimu kwa utajiri. Lakini, neema ya Mungu inafanya jambo hili liwezekane bila haja ya utajiri.)

 

    1. Soma 2 Wakorintho 8:3-4. Je, Paulo anawasihi watu wa Makedonia kutoa? (Hapana. Paulo anasema kuwa hilo lilikuwa wazo lao. “Walisihi kwa udharura” kutoa fedha zao.)

 

      1. Kwa nini waombe kutoa vitu vyao wakati wako kwenye umasikini wa kutupwa? (Hii inaakisi upendo wao kwa Wakristo wenzao.)

 

    1. Soma 2 Wakorintho 8:5. Paulo anasema kuwa watu wa Makedonia kwanza walijitoa nafsi zao kwa Bwana na kisha kwa Paulo na Tito. Je, mpangilio huo ni muhimu? (Ndiyo. Karama ya Paulo na Tito ilikuwa ni matokeo ya “mapenzi ya Mungu.” Mabadiliko haya ya mtazamo, yanayosababishwa na Roho Mtakatifu, ndio yanayozuia mwelekeo wetu wa asili wa uroho/ulafi.)

 

    1. Soma 2 Wakorintho 8:6-7. Je, tunahitaji msaada kupata “neema ya utoaji?” (Kazi ya Tito ilikuwa ni kuwasaidia kwa jambo hilo.)

 

      1. Unapoangalia orodha ya vitu ambavyo Wakorintho walifanikiwa, je, hii inaashiria kwamba Mkristo anaweza kuanguka katika eneo la utoaji, lakini si kwenye vipengele vingine vingi muhimu?

 

        1. Ikiwa umejibu, “ndiyo,” je, hiyo inamaanisha kuwa kila mmoja wetu anapaswa kutafakari kwa mahsusi jinsi tulivyo kwenye mizania ya ukarimu/uroho?

 

    1. Soma 2 Wakorintho 8:8. Je, umetiwa moyo kwamba Paulo hafanyi suala la ukarimu kuwa amri? (Kwa dhahiri linaonekana kuwa suala lenye kubadilika kwa urahisi kuliko alivyosema Mungu katika Malaki 3!)

 

      1. Umewahi kumsikia mwenzi wako akisema, “sitakwambia ufanye hivi, lakini kama unanipenda na ni mwenzi mwema kama mume/mke wa ndugu yangu, nawe ungenitendea jambo hili?”

 

        1. Ikiwa ndivyo, je, ulilichukulia jambo hilo kama amri? (Hilo linaonekana kufanana kabisa na kile anachokisema Paulo. Ikiwa upendo wako ni wa dhati, na ikiwa wewe ni mtu wa dhati kama wale watu wa makedonia, utakuwa mkarimu!

 

        1. Hii inatuambia nini kuhusu uhusiano kati ya ukarimu na upendo?

 

 

    1. Soma 2 Wakorintho 8:9. Je, watu wa Makedonia, au Wakristo wengine wa dhati, ndio watu halisi wa kuwalinganisha? (Hapana. Yesu alikufa kwa mateso makali kwa ajili yetu kutokana na upendo wake kwetu. Hiyo ndio alama yetu teule (rejea yetu).)

 

    1. Soma Wagalatia 5:22-23. Tunda la kwanza la Roho Mtakatifu lililoorodheshwa ni lipi? (Upendo.)

 

      1. Hii inatusaidiaje kulinganisha hali waliyokabiliana nayo watu wa Makedonia na ahadi ya Mungu ya baraka za vitu kwa wale wanaomfuata? (Ikiwa lengo letu la kwanza ni kuusaka Ufalme wa Mungu, basi upendo unapaswa kuakisiwa katika maisha yetu. Ingawa matokeo ya jumla ya utii ni maisha yenye baraka, baadhi ya watu wanapitia matatizo makubwa, yakiwemo majaribu na umasikini. Hata katika matatizo hayo wafuasi wa Mungu wanapaswa kuakisi upendo wake kwa kuwa wakarimu kwa watu wengine wenye uhitaji.)

 

    1. Rafiki, ukiona kwamba unahitaji msaada katika idara ya upendo/ukarimu, kwa nini usimwombe Roho Mtakatifu akusaidie?

 

  1. Juma lijalo: Mungu au Mali?