Viongozi wa Kanisa la Kwanza

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Matendo 6-8)
Swahili
Year: 
2018
Quarter: 
3
Lesson Number: 
4

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Je, ungependa kumtendea Mungu mambo makubwa? Je, tamaa yako ya kutenda mambo makubwa inahafifishwa na ukweli kwamba kazi uliyopewa na kanisa ni ya kawaida? Kwa mfano, “kuongoa roho” si kazi yako, badala yake kazi yako ni kuratibu chakula kinacholetwa na washiriki kanisani ambacho wanakila kwa pamoja baada ya ibada. Juma hili tunamwangalia mtu anayesimamia chakula katika suala la ushuhudiaji. Kazi yake ilikuwa ni kugawa chakula. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

 

  1.    Pambano

 

    1.    Soma Matendo 6:1. Madai ya ubaguzi ni yapi? (Si madai yaliyojengwa juu ya msingi wa dini au mbari, bali yamejengwa juu ya asili ya utaifa. Yanaonekana kuwa ni madai ya kiutamaduni zaidi.)

 

      1.    Unadhani mashtaka ni ya kweli? Au, je, hii ni aina ya madai ya uongo yanayoibuka kutokana na tofauti za kiutamaduni na matokeo yasiyotarajiwa? (Hatuna taarifa za kutosha kutuwezesha kufahamu.)

 

    1.    Soma Matendo 6:2-3. Je, wanafunzi kumi na wawili wanaamini kuwa mashtaka ni ya kweli? (Kimsingi wanachoamua ni kwamba hawataki kushughulika nacho. Wanakubaliana kusimika kundi la viongozi watakaohakikisha kuwa ugawaji wa chakula unafanyika kwa haki.)

 

      1.    Wanaangalia vigezo gani kwa viongozi saba wa kugawa chakula? (Watu wenye kujawa Roho Mtakatifu na wenye hekima.)

 

        1.    Kwa nini wanatakiwa kuwa na hekima? (Madai ya ubaguzi kati ya tamaduni tofauti ni suala gumu. Ni vigumu kujua jinsi ya kutatua tatizo kwa uhakika bila kusababisha ubaguzi zaidi.)

 

    1.    Soma Matendo 6:5. Utakumbuka madai ya msingi ni kwamba wajane wa Kiyunani walikuwa wanapuuzwa. Majina yote haya ni ya Kiyunani. Je, kuna cha kujifunza katika jambo hili? (Kwa dhahiri, kuhusishwa kwa Wayahudi wa Kiyunani ni jambo la muhimu. Hata hivyo, majina yanaweza yasiakisi kwa usahihi asili yao kiutamaduni.)

 

        1.    Nani aliyefanya uchaguzi hapa? Je, ni wale Kumi na Wawili? (Hapana. Washiriki wa kanisa la awali. Huu haukuwa uchaguzi uliofanywa na uongozi.)

 

          1.   Kwa nini? (Huu ni uthibitisho zaidi kwamba wale wanafunzi Kumi na Wawili walitaka jukumu hili liondolewe kutoka kwao.)

 

    1.    Soma Kutoka 6:4. Wale Kumi na Wawili watajikita kufanya nini? (Maombi na kulihudumia neno.)

 

    1.    Tunapaswa kujifunza nini kutoka kwenye hivi vifungu vinne? (Usinependa malalamiko yaendelee kukereketa. Bila kujali kama ni ya kweli au la, ungependa kuyashughulikia kwa namna fulani na si kuyapuuzia. Kuwaacha walalamikaji wawe na mkono katika kutafuta suluhu ni jambo la msingi. Uwajibikaji kanisani unapaswa kuzingatiwa. Ikiwa uwajibikaji ni mpana sana basi mambo ya ndani yaliyo ya msingi yanaweza kusahaulika. Watu wote waliopo kwenye uongozi wanapaswa kujawa Roho Mtakatifu, hata kama wana kazi inayoonekana kuwa ya kawaida sana (isiyosisimua). Kuwa na hekima pia ni muhimu.)

 

    1.    Soma Matendo 6:6-7. Toleo la Biblia yangu linasema, “Basi, neno la Mungu likasambaa.” Je, kuna uhusiano kati ya ukuaji na suluhisho la ubishani? (Nadhani hiki ndicho anachokiwaza mwandishi. Anatutaka tufahamu kwamba kutatua tatizo hili kanisani kulilifanya kanisa likue.)

 

  1.   Stefano

 

    1.    Soma Matendo 6:8-10. Kazi ya Stefano ni ipi? (Soma Matendo 6:2. Wale Kumi na Wawili walitakiwa kushughulika na kazi ya utume na Stefano alitakiwa “kuhudumu mezani.”)

 

      1.    Kwa nini Stefano anajihusiaha na kazi ya utume? Je, amesahau wajibu wa kazi yake? Je, anaingilia kazi ya wale Kumi na Wawili? (Hakuna kitu kwenye maelezo haya kinachoashiria kuwa Stefano anafanya jambo lolote baya. Hii inatuambia kuwa ni fursa ya kila mtu kanisani, bila kujali majukumu rasmi, kupeleka injili.)

 

      1.    Tuna sababu gani nyingine ya kutufanya tuamini kuwa kazi ya utume ni sehemu ya kazi sahihi ya Stefano? (Kifungu cha 10 kinatuambia kuwa Roho Mtakatifu ananena kupitia kwa Stefano. Pia tunasoma kuwa anatenda “maajabu na ishara kubwa.” Kwa dhahiri, Mungu anaitangaza kazi ya utume ya Stefano.)

 

    1.    Soma Matendo 6:11. Wapinzani wa Stefano hawawezi kushindana na hoja zake. Tunafahamu nini kuhusu ukweli wa mashtaka yaliyoletwa dhidi ya Stefano? (Ikiwa kundi la watu linafanya mambo yake kwa siri, ikiwa “wanawashawishi” watu walete mashtaka, basi unafahamu kuwa mashtaka yana walakini.)

 

      1.    Tunajifunza nini katika kufanya uamuzi kuhusu mtu aliye sahihi kwenye mdahalo? (Ikiwa upande mmoja unaacha kujenga hoja zinazostahili, na badala yake unatumia mashambulizi ya kisheria yenye hila au mashambulizi ya kimwili, basi hiyo inakupa ishara ya kwamba nani yuko sahihi.)

 

    1.    Soma Matendo 6:12-15. Unadhani inamaanisha nini kusema kuwa uso wa Stefano “ulikuwa kama uso wa malaika?”

 

      1.    Kama ungekuwa mjumbe wa baraza, na mtu anayekabiliwa na mashtaka akawa na “uso kama wa malaika,” unapaswa kuhitimisha nini?

 

    1.    Soma Matendo 7:1-3. Tunajuaje kwamba Stefano ni mwanasheria? (Swali aliloulizwa lina jibu la “ndiyo” au hapana.” Badala ya kujibu swali, Stefano anaendelea na miaka mingine 49!)

 

    1.    Ninakukaribisha usome vifungu 49 vinavyofuata, lakini kwa ajili ya mjadala wetu hebu turuke chini na tusome Matendo 7:54-58. Huu ni mchakato gani wa kisheria? (Stefano hajibu swali aliloulizwa, badala yake, anaelezea historia ya uhusiano wa Israeli na Mungu. Ananukuu kwamba Israeli iliwapinga na kuwaua manabii wa Mungu hadi kufikia hatua ya kumwua Yesu. Katika kujibu jambo hilo, makutano wanakasirika na kumwua. Haya ni machafuko kamili kwa mujibu wa mchakato wowote wa kisheria.)

 

    1.    Soma Matendo 7:59-60. Kwa nini wasishtakiwe kwa dhambi hii? Stefano amemaliza tu kuelezea kwa nini mababu wao na sasa wao walikuwa na hatia ya uasi na kutokuwa waaminifu kwa Mungu. Mauaji yake yanaendana na maelezo ya dhambi ambazo amezielezea hivi punde.

 

      1.    Unadhani Mungu anayashikilia mauaji ya Stefano dhidi ya wale waliomuua kutokana na hasira? (Soma Luka 11:4. Suala hili haliangalii kama walikuwa wanatenda dhambi, kimsingi walikuwa wanatenda dhambi. Suala lililopo ni kuwasamehe wale wanaotutendea dhambi.)

 

      1.    Je, umewasamehe wale waliotenda dhambi dhidi yako?

 

  1. Sauli/Paulo

 

    1.    Soma Matendo 8:1. Sauli (ambaye baadaye anajulikana kama Paulo) anaielewa sheria na anayaelewa Maandiko. Anawezaje kuidhinisha mauaji ya Stefano? (Sote tunatenda mambo yasiyo na mantiki kwa sababu tunataka kuona matokeo fulani. Sauli alidhani kuwa Wakristo wanalidhuru kanisa lake.)

 

      1.    Unadhani kwa nini mitume walibaki Yerusalemu?

 

      1.    Soma Matendo 1:7-8. Unadhani mitume waliyaelewaje maelekezo haya kutoka kwa Yesu?

 

    1.    Soma Matendo 8:2-3. Kama ungekuwa umeongolewa hivi karibuni na kuwa Mkristo, je, kitendo hiki kingekufanya udhamirie zaidi au kidogo kusalia kwenye imani yako mpya? (Kauli ya kwamba Sauli alikuwa anayaangamiza makanisa inatuambia kuwa watu walikuwa wameogopeshwa, na huenda waliachana na imani zao mpya.)

 

    1.    Soma Matendo 8:4-8. Tuchukulie kwamba Shetani au malaika wake ndio wanaohamasisha haya mateso. Mkakati wao unafanyaje kazi? (Nadhani unalipuka kwa kwenda kinyume cha matarajio. Badala ya kuangamiza kazi ya Mungu, wanaisambaza.)

 

      1.    Tafakari jambo hili kidogo. Matokeo haya si yanatabirika? Je, hii inamaanisha kuwa Shetani si mwerevu kwa kiasi hicho? (Soma Warumi 8:28 na Mwanzo 50:19-20. Kamwe hatutakiwi kuuacha mkono wa Mungu katika tathmini yetu. Anayachukua mambo yaliyokusudiwa kuwa mabaya na kuyabadili kuwa mambo mazuri. Pia ninaamini kuwa akili ya Shetani imezingwa kwa hasira na chuki yake.)

 

    1.    Soma Matendo 8:14-17. Je, hii ndio sababu ya mitume kusalia Yerusalemu? (Kanisa jipya linahitaji uongozi. Lilihitaji “makao makuu.” Hii iliwaruhusu watu kutoa mrejesho na mitume kwenda maeneo waliyohitajika.)

 

    1.    Rafiki, kama unatamani kumtendea Mungu mambo makuu, mwombe akujaze Roho Mtakatifu na ayaongoze maisha yako. Kwa nini usifanye hivyo sasa hivi?

 

     Juma lijalo: Uongofu wa Paulo.