Mfumo wa Kanisa na Umoja

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Mathayo 28, Waefeso 5, Mathayo 20)
Swahili
Year: 
2018
Quarter: 
4
Lesson Number: 
12

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Una taswira gani ya umoja kanisani? Lengo linapaswa kuwa lipi? Tunaangalia katika maeneo yanayotuzunguka na kuona aina mbalimbali za makanisa. Ikiwa makanisa mbalimbali yanaunda “taswira pana,” kwa nini tutarajie jambo tofauti kwenye “taswira ndogo” ya kanisa letu mahalia? Vipi kuhusu “taswira ya kati” ya madhehebu yetu? Je, turekebishe ufafanuzi wetu wa umoja kanisani? Je, inatosha kwamba sote tuko chini ya uongozi wa Yesu? Hebu tufungue Biblia zetu na tuone kile inachotufundisha!

 

  1.    Kristo na Kanisa

 

    1.    Soma Mathayo 28:16-17. Yesu amefufuka. Tatizo gani linaarifiwa kwenye vifungu hivi? (Baadhi ya wanafunzi walitilia shaka kama kweli yule alikuwa Yesu – walitilia shaka kama kweli alikuwa amefufuka.)

 

      1.    Hii inazungumzia nini kuhusu uaminifu na ukweli/unyofu wa Biblia? (Kama haya yangekuwa maelezo ya uongo, yasingeelezea mashaka yoyote.)

 

      1.    Vifungu hivi vinazungumzia nini kuhusu umoja?

 

    1.    Soma Mathayo 28:18-20. Yesu anawaambia nini wale wenye mashaka? (Kwamba amepewa mamlaka yote.)

 

      1.    Yesu anamaanisha nini anaposema kuwa amepewa mamlaka yote “mbinguni?”

 

      1.    Tunatakiwa kufanya nini katika kujibu suala la Yesu kuwa na mamlaka yote? (Kuwafanya watu kuwa wanafunzi kwa kuwabatiza na kuwafundisha. Tunafanya hivi tukijua kwamba Yesu yu pamoja nasi siku zote.)

 

        1.    Hii inazungumzia nini kwa wale waliotilia shaka? (Acha kuwa na mashaka. Kazi yako ni kuwasaidia wengine waweze kuamini.)

 

    1.    Soma Waefeso 5:23-24. Hebu tujikite kwenye uhusiano kati ya Yesu na Kanisa. Kichwa cha kanisa ni nani? (Yesu.)

 

      1.    Unadhani inamaanisha nini kwa kanisa “kumtii” Kristo? (Tukiangalia vifungu vya Mathayo tulivyovisoma hivi punde, inamaanisha kwamba kwanza tunakiri kuwa Yesu ana mamlaka yote mbinguni na duniani. Pili, inamaanisha kuwa tunahusishwa kwenye majukumu ya kubatiza na kufundisha.)

 

      1.    Hii inazungumzia nini kuhusu kanisa na mfumo? (Yesu anaposema kuwa yeye ni “kichwa” cha Kanisa, hiyo inaashiria mfumo. Jambo la dhahiri kuhusu mfumo ni kurahisisha kile alichokiamuru Yesu.)

 

      1.    Je, kuhusishwa kwenye upelekaji injili, kufundisha, au vyote viwili ndio vigezo vya chini kabisa kwa mtu kuchukuliwa kuwa sehemu ya Kanisa la Yesu hapa duniani?

 

    1.    Soma tena Mathayo 28:20 na Waefeso 5:24. Maelekezo ni kwamba tufundishe utii kwa “kila alichoamuru [Yesu].” Tunapewa wito wa kuyatii maelekezo haya. Ninapoangalia katika maeneo mbalimbali, ninaona makanisa mengi yakifundisha mambo mengi tofauti. Nina mashaka kama kuna kanisa lolote kati ya makanisa hayo linalodhani kuwa haliko sahihi. Tunaelezeaje jambo hili?

 

      1.    Hebu tuangalie mathayo 28:19-20 kwa umakini. Tunaona kanuni na mafundisho gani hapa? (Ubatizo. Utatu Mtakatifu. Utii. Uwepo wa Mungu.)

 

        1.    Unapotafakari kila mojawapo ya mambo haya, je, unaweza kuona kwamba kila moja lina mtanuko wa asili? Ubatizo unahusu kuhesabiwa haki kwa imani. Uwepo wa Mungu unahusu Roho Mtakatifu.)

 

      1.    Je, haya ndio mambo pekee tunayopaswa kuwa tunayafundisha? (Hapana. Yesu anasema katika Mathayo 28:20 kwamba tunapaswa kufundisha utii kwa “yote niliyowaamuru.”)

 

        1.    Kama unakubaliana kwamba jibu sahihi ni “Hapana,” je, sharti tuhitimishe kwamba kwa dhahiri Kanisa la Kikristo halina mfumo kutokana na mambo yote haya tofauti? Hebu tuangalie jambo hilo katika sehemu inayofuata.

 

  1.   Umoja Katika Mafundisho

 

    1.    Soma Tito 1:9, 2 Timotheo 2:17-18 na 2 Petro 2:1. Je, makanisa yote tofauti-tofauti yanafundisha ukweli? (Kama tuwaonavyo manabii wa uongo katika Agano la Kale, vivyo hivyo tunaonywa juu ya walimu wa uongo katika Agano Jipya.)

 

    1.    Soma 1 Wakorintho 1:10-13. Je, mgawanyiko huu unahusu mafundisho ya uongo? (Hapana. Hii ni migawanyiko holela isiyo na msaada wowote. Washiriki wanaonekana kutoelewa nani aliye kiongozi wa Kanisa.)

 

    1.    Soma 1 Wakorintho 12:12-13. Kanisa linalinganishwa na kitu gani? (Mwili.)

 

      1.    Vitu gani vinafanana hapa? (Ubatizo na Roho Mtakatifu.)

 

    1.    Soma 1 Wakorintho 12:14-18. Unazungumzia nini juu ya hii migawanyiko? (Isipokuwa tu kama tutasema kuwa makanisa mengi tofauti-tofauti yanaonesha kuwa Shetani ametushinda, nadhani namna bora ya kuangalia jambo hili ni kupitia kwenye lenzi ya ufafanuzi huu. Makanisa mengi yanafundisha mafundisho ya msingi yaliyobainishwa kwenye Mathayo 28:18-20. Hata hivyo, kila kanisa lina mchango wake wa pekee katika injili. Kwa mfano, Jeshi la Wokovu linasisitiza masuala ya kijamii. Wapentekoste wanasisitiza uwezo wa Roho Mtakatifu. Waadventista Wa Sabato wanasisitiza Sabato na ujio wa Mara ya Pili. Kazi yote hii inafanyika chini ya uongozi wa Yesu.)

 

  1. Uongozi wa Kiutumishi (wa Kutumikia)

 

    1.    Soma Mathayo 20:20-22. Asante, mama! Hawa “Ndio, twaweza” wanaomjibu Yesu ni akina nani? (Jina la mama ni Salome na majina ya wana ni Yakobo na Yohana. Kwa dhahiri, hawa wana wapo wakati mama wao anapoomba nafasi za uongozi wa juu kabisa kwa ajili yao. Hivyo ndio sababu wanaweza kujibu swali la Yesu kwa kusema “Twaweza.”)

 

    1.    Soma Mathayo 20:24. Kwa nini wale kumi wanakasirika? Je, wamegundua kwamba mama zao ni duni? (Kwa dhati kabisa, hii inatuonesha kuwa wanafunzi wote walitaka kuwa na nafasi za juu katika ufalme wa Yesu ujao.)

 

      1.    Je, unaliona jambo hili kama ni la ajabu? Je, unataka kupandishwa cheo kazini? Je, ungependa kuongoza nchi?

 

      1.    Maombi haya ya uongozi yanachukulia dhana gani kwa kumtazamia Yesu? (Hawatafuti kuchukua nafasi ya Yesu. Wanaelewa kwamba yeye ndio kiongozi.)

 

    1.    Soma Mathayo 20:25-28. Yesu anasema kuwa “watawala” Kanisani hawapaswi kuwa “wakubwa” juu ya wengine au “kutumia mamlaka” kwa wengine. Badala yake, wanapaswa kutumikia na kuwa watumwa. Unawezaje kuwa na mfumo ikiwa hakuna mtu hata mmoja anayetumia mamlaka na kila mtu anamtumikia mtu mwingine?

 

      1.    Je, hii inaendana na Waefeso 5:23-25?

 

      1.    Je, hii inaendana na Waebrania 13:17? (Kama unashangaa kwamba “viongozi” inamaanisha viongozi wa kanisa, soma Waebrania 13:7.)

 

    1.    Soma Matendo 15:23-29. Hii inaashiria nini kuhusu mamlaka ya kanisa?

 

      1.    Je, wanafunzi wengi kati ya wanafunzi wa Yesu waliomsikia Yesu akizungumza kuhusu mamlaka katika Mathayo 20 walikuwepo kwenye mkusanyiko huu? (Kubainisha alichokimaanisha Yesu kwa uongozi kutotumia mamlaka kunaongozwa kwa kuangalia kile wasikilizaji wake walichodhani kuwa anakimaanisha. Katika Matendo 15 tunawaona viongozi wanaotumia mamlaka yao kukomesha mgawanyiko na mtafaruku. Sidhani kama Yesu anasema kuwa kamwe viongozi wa kanisa hawapaswi kutumia mamlaka – hitimisho hilo haliendani na mifano mingi kwenye Agano Jipya. Anachokizungumzia Yesu ni kuhusu kutafuta nafasi za uongozi kwa sababu mtu anatamani uwezo na mamlaka juu ya wengine. Wito wa viongozi ni kuwatumikia watu.)

 

    1.    Soma 1 Timotheo 5:17-19. Viongozi wanatumia mamlaka ya aina gani hapa?

 

      1.    Unaona uongozi gani wa kiutumishi kwenye vifungu hivi? (Inawazungumzia viongozi “wakihubiri na kufundisha.” Hivyo, wao ni watumishi kwa maana ya kwamba wanafanya kazi hii.)

 

    1.    Soma 2 Wakorintho 13:10. Hapa Paulo anatumia mamlaka gani?

 

    1.    Soma 1 Wakorintho 5:1 & 4-5. Mamlaka gani yanatumika hapa? (Kumwondosha mtu kwenye ushirika.)

 

    1.    Soma 2 Timotheo 3:16-17. Maneno mawili yananasa akilini mwangu: “kuonya” na “kuadibisha.” Nani afanyaye hivi? (Yumkini ni viongozi wale wale wanaofundisha.)

 

      1.    Je, matendo haya yanaendana na kuwa kiongozi mtumishi?

 

      1.    Angalia tena 1 Wakorintho 5:5. Lengo la nidhamu ya kanisa ni lipi? (Kumfanya mshiriki mkaidi kutambua dhambi yake na kutubu. Sio kutomsamehe.)

 

    1.    Rafiki, sasa mtazamo wako juu ya umoja kanisani ukoje? Vifungu tulivyojifunza vinaonyesha mfumo huru chini ya uongozi wa Yesu – hivyo uwepo wa madhehebu yote ya aina mbalimbali haioneshi kwamba tumeshindwa na Shetani. Mfumo wa jumla unadhamiria kupeleka injili na kufundisha. Kama kwa namna fulani wewe si sehemu ya juhudi hizi, kwa nini usiutoe moyo wako kwa Yesu leo na uungane na mfumo wake?

 

  1.   Juma lijalo: Urejeshwaji wa Mwisho na Umoja.