Somo la 11: Familia za Imani

Swahili
Somo la 11: Familia za Imani
Year: 
2019
Quarter: 
2
Lesson Number: 
11

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Majuma mawili yaliyopita, tulijadili changamoto za kukabiliana na upotevu. Mojawapo ya matatizo makubwa ya kupoteza kitu ni kwamba tunakabiliana na mabadiliko, na watu wengi wangependa kuepuka mabadiliko. Vipi kama mabadiliko yanakuja kutokana na mahitaji ya kuboresha uelewa wetu wa kiroho? Vipi kama mabadiliko huja kutokana na kushindwa kwetu kuelewa au kukumbuka mapenzi ya Mungu kwetu? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi jinsi ya kufanya mabadiliko chanya na kuepuka mabadiliko hasi!

 

 1. Ukuaji wa Kiroho

 

 1. Soma Matendo 10:1-2. Kazi ya Kornelio ni ipi? (Yeye ni askari wa Kirumi, na akida wa kikosi cha jeshi. Mojawapo ya maoni yanasema kuwa Kornelio alikuwa akiongoza kundi la askari 600.)

 

  1. Kwa nini askari wa Kirumi aliwekwa kwenye kituo cha Kaisaria? (Huu ulikuwa mji mkuu wa Rumi, makao makuu ya jeshi. Walihitaji askari ambao walikuwa watiifu kikamilifu kwa Rumi.)
   1.  Hapa adui ni nani? (Wayahudi wasiokuwa watulivu.)

 

  1. Tunafahamu nini kuhusu imani za kidini za Kornelio? (Yeye ni mwongofu wa dini ya Kiyahudi.)

 

   1. Ni kipi tunachokifahamu kuhusu familia hii?

 

    1. Ni athari gani uliyonayo kwenye familia yako?

 

   1.  Biblia inatuthibitishiaje uchaji wake? (Inatuambia kuwa aliwasaidia wahitaji na kuomba mara nyingi).

 

   1.  Unalinganishaje uchaji wa Kornelio na wako?

 

 1. Soma Matendo 10:3-4. Linganisha na Matendo 3:1. Muda huu ni wa muhimu kiasi gani? (Ni saa ya maombi kwa Wayahudi. Hii inaashiria kuwa Kornelio alikuwa akiomba wakati alipopata maono.

 

  1. Kwa nini Kornelio alichaguliwa kwa ujumbe huu kutoka kwa Mungu? (Maombi yake na sadaka zake kwa maskini.)

 

 1. Soma Matendo 10:5-8. Je, Kornelio alitii jambo hilo papo kwa papo?

 

  1. Je, Kornelio anaelewa kwa nini anatuma watu? (Hapana. Anatii tu.)

 

  1. Kornelio anatuma aina gani ya askari? (Mtu mwingine mshika dini.)

 

  1. Kwa nini Kornelio anawatuma watu watatu wakati mmoja tu angeweza kupeleka ujumbe? Kwa nini alimjumuisha askari? (Idadi kubwa ilionesha heshima kwa Petro. Ilidhihirisha kuwa mtu huyu hakuwa tu mpuuzi fulani mwenye ujumbe wa ajabu. Askari alithibitisha kuwa huu ulikuwa ujumbe  rasmi na kuthibitisha kuwa ulitoka jeshini.)

 

 1. Soma Matendo 10:9-11. Kipi ni kipaumbele chako, kula au kuomba? Je, ungedumu kuomba, au ungeshuka chini na kujiandaa kula?

 

  1. Endapo Petro asingedumu katika maombi, kisa hiki kingeendeleajie?

 

  1. Utaona kuwa Mungu aliwafikia wote wawili - Kornelio na Petro - walipokuwa kwenye maombi. Je, unaomba mara kwa mara?

 

 1. Soma Matendo 10:12-15. Kama una nabii kanisani kwako, kama mtu akisema ana ujumbe kutoka kwa Mungu, jukumu lako ni lipi (Kuuthibitisha kwa maandiko.)

 

  1. Je, Petro amefanya hivyo? (Ndiyo)

 

  1. Awali, Petro anaikataa sauti kwa sababu inapishana na maandiko, hususani Kumbukumbu la Torati 14:3-21. Je, Petro aache uchambuzi wake katika hatua hiyo na kuukataa ujumbe?

 

 1. Soma Matendo 10:16-17. Je, Petro alikataa tu jambo aliloliona na kulisikia? (Hapana. Anajaribu kuoanisha maandiko na kile alichokipitia.)

 

  1. Unadhani dunia inazunguka huku Mungu akiwa ndiye mdhibiti, ingawa hajishughulishi na mambo ya ndani? (Mpangilio wa muda unaonesha Bwana anajishughulisha na mambo ya kina.)

 

 1. Soma Matendo 10:18-20. Petro anajaribu kutafakari maono. Kwa nini Roho Mtakatifu anamwambia aende bila kusita akiambatana na wageni watatu?

 

  1. Tafakari jambo hili kidogo. Mungu anataka kubadilisha mawazo ya Petro juu ya kuchangamana na watu wa Mataifa. Jambo la kwanza Mungu analofanya ni kumpa changamoto kwa imani alizonazo. Jambo jingine alilofanya ni kupanga matukio kuwa sehemu ya changamoto. Kisha Mungu anaelekeza jambo analotakiwa kulitekeleza katika mazingira hayo.)

 

 1. Soma Matendo 10:21-22. Unadhani wageni waliamini kuwa Petro angeweza asiafiki kwenda pamoja nao? (Ndiyo.)

 

  1. Wanasema jambo gani ili kumshawishi aje? (Wanataja mambo chanya ya Kornelio katika maisha yake ya kidini. Wanasema wana kibali cha mbingu.)

 

   1. Angalia jinsi Bwana anashughulika na pande zote za tatizo!

 

 1. Soma Matendo 10:23. Je, Petro ameanza kubadili misingi ya imani yake? (Soma Matendo 10:28 na Matendo 11:2-3. Pamoja na hili, Petro anawaalika watu wa Mataifa kuwa “wageni wake” na anakubali kwenda pamoja nao.)

 

 1. Soma Matendo 10:24-26. Unafikiriaje kuhusu matendo ya Kornelio? Zingatia kuwa kazi yake ni kuweka mamlaka dhidi ya Wayahudi wasio watulivu. Anapaswa kuhakikisha wanafahamu kwamba Rumi ndiye mtawala. (Sina hakika kama matendo yake ni jambo ambalo angetamani wasimamizi wake walifahamu. Lakini, Kornelio analifanya hili mbele ya wengine – ikiwemo asakari aliyemtuma kwa Petro.)

 

 1. Soma Matendo 10:27-29. Je, Petro amelegeza msimamo wake juu ya nyama najisi? Ikiwa sivyo, amefanya nini sasa? (Hajalegeza msimamo. Amekuwa katika uelewa wake wa kiroho. Tunaweza kuazima kanuni muhimu ya roho katika torati. Hakimu anapoamua juu yatorati mbili zinazokinzana, jukumu lake la kwanza ni kuona kama torati zote mbili zinaweza kupewa tafsiri. Paulo anatatua mgongano bayana kati ya Biblia na ujumbe wa wakati huo kutoka kwa Mungu kwa kuamua kuwa ujumbe kuhusu wanyama najisi haukuwa juu ya wanyama, bali juu ya watu. Paulo hakutupa torati za kale kwa ajili ya mpya, alipata namna ambayo zote zingeweza kuzingatiwa.)

 

 1. Kornelio anamweleza Petro kile malaika alichomweleza. Soma Matendo 10:33-35. Je, Kornelio yuko wazi kwa ukuaji wa kiroho? Je, Petro yuko radhi kwa ajili ya ukuaji wa kiroho? (Hiki ni kisa cha kiwango cha juu kuhusu mabadiliko. Katika muktadha wa uhasama kati ya Wayahudi na watu wa Maitaifa, wanaume wawili wako tayari kwa Mungu kuwabadilisha mitazamo yao kwa ajili ya kufanikisha ufalme wa Mungu.)

 

  1. Rafiki, una utayari wa kiasi hicho kuongozwa na Mungu? Je unachochea aina hiyo ya uelewa katika familia yako?

 

 1. Kusahau Ukuaji

 

 1. Soma Waamuzi 2:6-7. Uzoefu wa watu hawa ni upi? (Waliishi kipindi ambacho Bwana alimtumia Yoshua kuwapatia ushindi.)

 

 1. Soma Waamuzi 2:8-10. Mabadiliko ya kiroho yalitokeaje hapa?

 

 

  1. Kipi tunachoweza kukifanya ili kuhakikisha kuwa hili halitokei katika familia zetu? Ni kwa jinsi gani tunaweza tukazuia hili kutokea kwa kizazi kijacho?

 

 1. Soma Waamuzi 2:11-13. Utaona kuwa vifungu vinazungumzia Mungu kuwatoa watu wake utumwani kutoka Misri. Unadhani kwa nini rejea hii inajumuishwa? (Kizazi hiki kimesahau historia! Sio tu kwamba walisahau kuwa Mungu alilishinda taifa lenye nguvu kubwa kuliko mataifa yote duniani, bali pia walisahau kuwa Mungu aliawapa wazazi wao ardhi ambayo sasa walikuwa wakiishi kwayo.)

 

 1. Soma Waamuzi 2:14-15. Hii inachocheaje mabadiliko ya kiroho? Hii inachocheaje kujifunza masomo kupitia historia?

 

 

 1. Rafiki, unaona namna tatu ambazo mabadiliko ya kiroho yalitokea? Mosi, Mungu atawaongoza walio waminifu kuelekea mabadiliko ambayo anaamini ni ya msaada. Pili, kama tukisahau mafundisho ya kale, mabadiliko ya kiroho hutokea ambayo hutupeleka katika njia isiyo sahihi. Tatu, Mungu analeta mabadiliko ya kiroho kwa kuwaruhusu maadui wetu kutudhuru na kutuletea shida kubwa. Ungependa kubadilika kwa jinsi ipi? Kwa nini usimwombe Roho Mtakatifu akubadili kama alivyombadili Petro?

 

 1. Juma lijalo: Wameona Nini Nyumbani Mwako?