Somo la 11: Kudhihirisha Tumaini la Marejeo Maishani

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Mhubiri 8, Mathayo 25 & 26)
Swahili
Year: 
2019
Quarter: 
3
Lesson Number: 
11

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Kama tunadhani kwamba tunapaswa kuishi maisha sawa sawa na maelekezo ya Biblia na kuwafundisha wengine kufanya vivyo hivyo, je, matokeo yake ni kwamba tutakuwa na mbingu ndogo duniani? Je, imani hiyo ina mantiki? Au, je, uwepo wa dhambi ni kizuizi cha kudumu cha kwenda mbinguni hapa duniani? Je, Wakristo wanakosolewa kwa usahihi kwa kuufanya Ujio wa Yesu Mara ya Pili kuwa suluhisho la matatizo? Bwana anapotutaka tuombe, “Ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni” (Mathayo 6:9-10), je, kutatua matatizo hapa duniani ni suala la kumwachia Mungu? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujizunze zaidi!

 

  1.    Njia ya Wastani

 

    1.    Soma Mhubiri 8:14. Je, kuna thawabu inayoweza kutabirika kwa kuishi maisha sahihi? Je, kutenda kilicho sahihi kunaweza kuleta matokeo ya kimbingu duniani? (Sulemani anasema kwamba wakati mwingine anachokiona ni kinyume chake tu. Watu wabaya wanapata mambo mazuri na watu wema wanapatwa na mambo mabaya.)

 

      1.    Je, hicho ndicho nawe pia umekiona?

 

      1.    Ikiwa ndivyo, unadhani kwa nini hilo ni kweli?

 

    1.    Soma Mhubiri 8:12-13. Je, hiki si kinyume cha kile tulichokisoma hivi punde? Je, Sulemani anazungumza kutoka pande zote mbili za kinywa chake? (Hapana. Kwa mara nyingine Mfalme Sulemani anabainisha kile ambacho mtu yeyote mwenye akili ya kawaida amekiona. Maisha ni mazuri kama unamtii Mungu, na mabaya kama humtii Mungu. Hata hivyo, kuna mambo mengine yanayoakisi ukweli kwamba tunaishi kwenye dunia ya dhambi.)

 

    1.    Soma Mhubiri 8:15. Hili linaendanaje na kile tulichokijadili hivi punde? Je, hili ndilo lengo la “mbingu ya hapa duniani?” (Tunatakiwa kutumia vizuri kile tulicho nacho sasa. Dhana ya kwamba kuna chanzo kamili na athari za kimahusiano maishani sio kweli kwa asilimia 100 hapa duniani. Hivyo, Sulemani anaelezea kwamba utii kwa Mungu ndio kanuni, na unapaswa kujaribu kuyafurahia maisha.)

 

  1.   Watu Wenye Talanta

 

    1.    Soma Mathayo 25:14-15. Ni mtu gani huyu asafiriye? (Huu ni mfano juu ya Yesu kuondoka kwenda mbinguni wakati wanafunzi wake wakimsubiri hadi ujio wake wa Mara ya Pili.)

 

      1.    Kwa nini watumishi wanapewa viwango tofauti? (Kifungu kinasema “kila mtu kwa kadri ya uwezo wake.”)

 

        1.    Hii inaashiria nini kuwahusu wanadamu? (Tumeumbwa sawa mbele za macho ya Mungu, lakini Mungu pia anatambua kuwa tuna uwezo tofauti.)

 

    1.    Soma Mathayo 25:16-18. Unadhani mtu mwenye talanta tano ni mtumishi mwaminifu zaidi kuliko mtu mwenye talanta mbili?

 

    1.    Soma Mathayo 25:19-23. Je, Mungu anamtendea tofauti mtu aliyejipatia faida mara mbili zaidi? (Hapana. Tuna talanta tofauti, lakini kilicho cha muhimu ni uaminifu kwa kile tulichopewa.)

 

      1.    Je, umegundua matokeo kwa hawa watumishi wenye bidii? (Furaha!)

 

    1.    Soma Mathayo 25:24-27. Je, ingetosha kwa mtu mwenye talanta moja kuweka fedha benki? (Inaonekana hivyo.)

 

      1.    Utaona kwamba mtu huyu mwenye talanta moja anasema kuwa “aliogopa.” Aliogopa nini? Ubepari? Kuwekeza? Alimwogopa bwana wake?

 

    1.    Soma Mathayo 25:28-30. Talanta hizi ni kitu gani? Je, ni fedha? Je, ni talanta za asili? Je, ni fursa maishani?

 

      1.    Je, mtu mwenye talanta moja anaweza kuchukuliwa kama “mmojawapo wa walio wadogo” kwa sababu alikuwa na talanta chache, na akaishia kutokuwa na talanta yoyote?

 

        1.    Kuna baadhi ya watu wasemao, “Ukitaka kujua Mungu yu upande wa nani, watafute wale wanaofanya vibaya, na unaweza kujua Mungu yu upande wao.” Mfano huu unafundisha nini kuhusiana na dhana hiyo? (Si ya kutumainiwa.)

 

      1.    Tunapata fundisho gani la kiroho kutokana na huu mfano? (Mungu anatutaka tuwe na bidii kwa kile alichotupatia.)

 

      1.    Unadhani inamaanisha nini kupata talanta nyingi zaidi? Je, hiyo inaweza kuwa ni kuwasaidia miongoni mwa walio wadogo?

 

      1.    Ikiwa mtu mwenye talanta moja ni mmojawapo wa hawa walio wadogo, kwa nini bwana anachukua talanta yake na kumpa mtu mwenye talanta nyingi? (Sidhani kama kwa ujumla Biblia inatangaza habari za kuchukua kutoka kwa maskini na kumpa tajiri. Lakini, kuna dhana kubwa kwenye Biblia kwamba kutokutii na kutomtumaini Mungu huishia kwenye maisha yasiyo na mafanikio. Zingatia kile tulichokisoma hapo awali kutoka katika kitabu cha Mhubiri. Hizi kanuni za jumla si za kweli mara zote.)

 

  1. Njaa, Kiu, na Harufu Nzuri

 

    1.    Soma Mathayo 25:34-37 na Mathayo 25:40. Hii inafuatia baada ya mfano wa “talanta” tuliojifunza hivi punde. Je, hii mifano miwili inahusiana? Je, ina ujumbe mmoja? Je, ina ujumbe tofauti?

 

      1.    Je, mifano hiyo inatufundisha kuwa kwenda mbinguni ni suala la kuzidisha talanta zetu na kuwasaidia wenye njaa na kiu?

 

    1.    Soma Mathayo 26:6-9. Tuchukulie kwamba wanafunzi, kama ilivyo kwako, walikuwa wanazingatia mifano ya talanta na njaa na kiu. Je, hitimisho lao litakuwa asilia na la dhahiri kutokana na kile walichokisikia? (Naam! “Talanta” ya mwanamke imemwagika. Wenye njaa na kiu bado wana njaa na kiu.)

 

    1.    Soma Mathayo 26:10. Mungu anauchukuliaje mwitiko wa wanafunzi wake? (“Wanamsumbua” huyu mwanamke. Wanachokisema si sahihi.)

 

    1.    Soma Mathayo 26:11. Yesu anasema nini kuhusu maskini? Je, hili ni tatizo lililo na suluhisho la “mbinguni hapa duniani?” (Yesu anatuambia kuwa tatizo la maskini na umaskini litaendelea kuwepo hapa duniani.)

 

    1.    Hebu turejee nyuma kidogo na tusome tena Mathayo 25:40. Hii inaongezea nuru gani kwenye matendo ya mwanamke huyu? (Mwanamke huyu hakumsaidia Yesu kwa kuzunguka kupitia kuwasaidia maskini, bali alimsaidia Yesu moja kwa moja.)

 

      1.    Je, wanafunzi walijichukulia kwamba wao ni maskini? Je walijichukulia kuwa wenye njaa na kiu? (Hawasemi kwamba angeweza kuyauza haya marhamu na kugawanya mapato kwa wanafunzi.)

 

      1.    Ikiwa wanafunzi hawakujichukulia kuwa ni maskini, je, walimchukulia Yesu kuwa ni maskini? (Hapana. Kama wangefanya hivyo, wasingelalamika kwamba thamani ya marhamu haya ingeweza kuwasaidia maskini.)

 

    1.    Soma Mathayo 26:12-13. Tunajifunza nini katika hili? (Kuwasaidia wenye njaa na kiu ni njia moja ya kuonesha upendo wa Mungu, lakini si njia pekee. Tunaweza kuwaonesha upendo wote wanaotuzunguka, na si tu wale walio na hitaji la msaada.)

 

      1.    Hebu turejee nyuma na tusome tena kile anachokisema katika Mhubiri 8:15. Je, hiki ni kitu kile kile ambacho Yesu anakisema kwa wanafunzi wake? Utakumbuka kwamba Yesu alikuwa “ameegemea meza” wakati mwanamke alipommiminia marhamu.

 

      1.    Je, hitimisho juu ya kile tulichokisoma ni hitimisho ambalo tunaweza kuwa na uhakika nalo? (Tukiwa waaminifu kwa kile tulichonacho, Mungu atatubariki. Kuwasaidia hawa walio wadogo huakisi upendo wa Mungu. Kuisaidia familia yetu huakisi upendo wa Mungu. Angalia 1 Timotheo 5:4.)

 

      1.    Je, kuna hitimisho katika hili ambalo halina uhakika sana? (Inaonekana anachokimaanisha Sulemani ni kiasi. Naam, mambo mabaya yanaendelea kutokea hapa duniani. Lakini hatupaswi kuyazingatia kwa kuyapa kipaumbele. Kuyafurahia maisha pia ni jambo la muhimu. Baadhi ya mambo mabaya ni matokeo ya kutomtii Mungu, na hilo husababisha tatizo la kudumu.)

 

      1.    Huyu mwanamke ambaye hakutajwa jina anaonesha “kiasi?” (Hakuna uthibitisho kwamba mwanamke huyu ni tajiri, tofauti na kuwa na hii marhamu ya ghali. Aliimimina yote kwa Yesu.)

 

      1.    Ikiwa unayafuatilia masomo haya mara kwa mara utaona kwamba kila mara huwa ninakutaka usome Malaki 3:10-12. Jambo gani la muhimu limeachwa bila kubainishwa hapa? (Zaka ni asilimia kumi. Mungu angeweza kuibainisha kivingine, “Tunza asilimia tisini na utabarikiwa sana.”)

 

        1.    Je, hii inaunga mkono njia ya Sulemani – yafurahie maisha kwa asilimia tisini yako?

 

      1.    Wimbo unanijia akilini, “Yote namtolea Yesu, moyo wangu ni wake.” Je, mashairi haya yalitungwa na mbumbumbu wa Biblia? (Ninalielewa hili kumaanisha kwamba nimejitoa kwa Mungu kwa asilimia mia moja na ninayatenda mapenzi yake. Kudhamiria kuyatenda mapenzi yake ndio sababu ya sisi kujadili ile asilimia tisini.)

 

    1.    Soma Mhubiri 3:12 na Mhubiri 5:19. Hii inaunganishaje dhana ya furaha na kicheko na kazi? (Mungu anataka tuwe na furaha maishani, hata katika kazi zetu. Hii inaelekea kuelezea kwamba yule mtu mwenye talanta tano alifurahia kazi yake kwa ajili [niaba] ya Mungu, wakati yule mwenye talanta moja aliogopa. Kuitangaza injili, kuwasaidia wenye njaa na kiu, kuipenda familia yetu, huleta furaha.)

 

    1.    Soma Mathayo 26:14-16. Unadhani ni kwa bahati tu kwamba kisa cha mwanamke mwenye marhamu na kisa cha Yuda vinafuatana kwenye Biblia?

 

      1.    Yuda anatofautianaje na mwanamke mwenye marhamu? (Mwanamke anamtolea Yesu kwa ukarimu katika siku zake za mwisho hapa duniani. Yuda anatafuta kunufaika kutokana na siku za mwisho za Yesu.)

 

        1.    Kuna fundisho gani kwetu? Nani aliyeishia kuwa na furaha?

 

    1.    Rafiki, usiachane na ukweli kwamba unaokolewa kwa neema pekee. Imani, na si matendo, ndio njia pekee ya kwenda mbinguni. Ni ukweli maishani kwamba tuenende sawa sawa na imani zetu. Mifano ya Yesu inatufundisha kwamba imani inabadili namna yetu ya maisha. Kuishi kwa mujibu wa imani yetu kwa ujumla huleta furaha. Je, utadhamiria, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kuyaelewa mapenzi ya Mungu kwa ajili ya maisha yako na utembee katika mapenzi yake?

 

  1.   Juma lijalo: Kupenda Rehema.