Somo la 4: Kukabiliana na Upinzani

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Ezra 4 & 5, 2 Wafalme 17:24, Nehemia 4 & 6)
Swahili
Year: 
2019
Quarter: 
4
Lesson Number: 
4

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Kama unasoma vitabu utakuwa unafahamu kwamba baadhi ya waandishi hawaelezei mada wanazoziwasilisha kwa kufuata mpangilio wa muda. Wanapenda kuzunguka-zunguka. Kusema kweli, mimi ninapendelea njia rahisi badala ya kutumia njia ngumu, hivyo ninapendelea habari zenye mwendelezo wa muda. Pamoja na vifungu vingine tutakavyovisoma, somo letu juma hili linajumuisha kitabu cha Ezra 3-6, lakini Ezra ni mmojawapo wa waandishi wanaopendelea njia ngumu. Haelezei kisa chake kwa kufuata mpangilio wa muda, bali kwa kufuata mpangilio wa mada. Kinachochanganya zaidi ni kwamba baadhi ya matukio tuliyojifunza majuma kadhaa yaliyopita yapo katika siku zijazo kwenye kisa chetu, na baadhi ya matukio tunayojifunza leo tayari tumeshayazingatia. Hebu tuone kile tunachoweza kujifunza kuhusu kukabiliana na upinzani bila kuchanganyikiwa na habari za muda mwafaka!

 

  1.    Marafiki?

 

    1.    Soma Ezra 4:1-2. Kama umekuwa ukifuatilia mfululizo wa masomo haya, unafahamu kwamba hapo awali tulijadili jinsi inavyopendeza unapohamia sehemu nyingine na majirani wako wapya wakajitolea kukusaidia! Kwa nini Ezra anawaita hawa majirani wapya walio wa msaada “maadui?”

 

      1.    Unaweza kuwaita waumini wenzako “maadui?”

 

      1.    Utaona kwamba hapo zamani mfalme wa Ashuru aliwaleta Yerusalemu wale wanaomwabudu Mungu wa kweli. Kwa nini anafanya hivyo?

 

    1.    Soma Ezra 4:3. Je, viongozi wa Israeli wana mtazamo sahihi?

 

      1.    Soma Marko 9:38-40. Je, Yesu angekataa msaada kutoka kwa wale ambao ibada yao si sawa na yake?

 

    1.    Hebu tuone kama tunaweza kujibu maswali haya. Soma 2 Wafalme 17:24-26. Je, umewahi kufikiria kuwatumia simba kama wainjilisti?

 

      1.    Eti, kwa nini watu walioanzisha makazi mapya wadhani kwamba mungu mpya anatawala eneo hilo? (Kulikuwa na imani ya jumla kwamba miungu ilikuwa na mamlaka kwenye maeneo fulani ya kijiografia pekee. Kama uliishi mahali fulani, basi ulitakiwa kumfuata mungu aliyetawala eneo hilo.)

 

        1.    Mungu wa mbinguni anatoshaje kwenye nadharia hii?

 

    1.    Soma 2 Wafalme 17:27-28. Jibu la mfalme wa Ashuru kwa tatizo hili ni lipi?

 

      1.    Unadhani kwamba Mungu aliwapeleka simba kama sehemu ya mipango yake kwa ajili ya uinjilisti? (Hiyo itakuwa haiendani na njia ya kawaida anayoitumia Mungu. Lakini, hii inaleta suala ambalo hatupaswi kulikosa. Watu wanaopitia matatizo mara nyingi wako wazi kusikiliza ujumbe kuhusu Mungu wa kweli. Tunapaswa kuwa makini kwa fursa za aina hii.)

 

    1.    Soma 2 Wafalme 17:29-32. Hatimaye watu walitatuaje suala la nani wanayepaswa kumwabudu? (Walimwabudu Mungu, lakini pia walileta na kuingiza miungu yao ya zamani.)

 

    1.    Soma 2 Wafalme 17:33-35. Mungu aliichukuliaje ibada hii mahuluti (chotara)? (Watu mahalia walidhani kwamba wanamwabudu Mungu, lakini hawamwabudu pale wanapohusisha miungu mingine.)

 

    1.    Soma tena Ezra 4:3. Kwa maelezo haya, niambie kwa nini watu wa Mungu walikataa msaada wa watu mahalia? (Walikuwa na wasiwasi kwamba wangeweza kupenyeza miungu yao ya ziada kwenye ibada.)

 

    1.    Tafakari fundisho la kiroho katika hili. Ikiwa tunamwabudu Mungu wa kweli na pia tunaabudu vitu vingine, Mungu analichukuliaje hili? (Hatumwabudu yeye pale tunapoongezea miungu yetu wenyewe.)

 

    1.    Soma Mathayo 6:5. Unadhani leo tatizo kubwa kabisa ni lipi linapokuja suala la miungu ya uongo? Tunaabudu miungu ipi na hili ni tatizo kubwa kiasi gani? (Tatizo moja kubwa ni kujiabudu wewe mwenyewe. Mara kwa mara ninawasikia watu wakisema kwamba gari au nyumba ni “mungu.” Nina mashaka kama watu wengi wanaabudu magari yao au nyumba zao, lakini wanaweza kuwa na gari zuri au nyumba nzuri ya kujiletea utukufu wao wenyewe.)

 

      1.    Ni kwa namna gani nyingine baadhi ya watu wanajaribu kujitukuza? Unapoombwa kukusanya sadaka, kutoa ombi au kuimba wimbo na ukaongezea hubiri-dogo, je, hilo ni tatizo la kujitukuza?

 

      1.    Unaweka tumaini lako kwa nani? Je, unayatumaini maoni yako kuliko kuyatumaini maoni ya Mungu? Je, unaziamini fedha zako?

 

    1.    Soma Ezra 4:4-5. Je, hii inakushangaza – watu mahalia wanajisikia kukosewa na kujibu kwa namna isiyo ya kupendeza?

 

      1.    Je, jambo hili lingeweza kushughulikiwa kwa kutumia akili zaidi?

 

        1.    Je, watu wa Mungu wangeweza kuwabadili watu mahalia?

 

      1.    Je, tunaogopa sana kuwatukana (kuwafedhehesha) watu? (Ikiwa tunaanza kwa kukiri kwamba walikuwa “maadui,” tunaweza kuamini kwamba wangesababisha matatizo bila kujali watu wa Mungu wangekuwa na mwitiko gani. Wakati mwingine kuwa wazi ni jambo bora zaidi. Lakini, tunatakiwa kuwa na uhakika kwamba Roho Mtakatifu anatuongoza katika kuwa “wawazi.”)

 

  1.   Utiaji Moyo

 

    1.    Soma Ezra 5:1-2 na usome tena Ezra 4:4. Manabii wanasaidia kutatua tatizo gani? (Watu wa Mungu walikuwa wanaogopa kujenga.)

 

    1.    Soma Hagai 1:14. Ni nini matokeo ya kazi ya manabii? (Watu “waliamshwa.”)

 

      1.    Zerubabeli na Yoshua walikuwa na madaraka gani? (Zerubabeli alikuwa Gavana na Yoshua alikuwa Kuhani Mkuu.)

 

      1.    Hii inatufundisha nini kuhusu kuyatatua matatizo kanisani? (Tunawahitaji wale wanaozungumza kwa ajili ya Mungu ili kuwatia moyo viongozi na watu. Roho Mtakatifu anapozungumza na mawazo (akili) yetu mambo yanatendeka.)

 

    1.    Soma Ezra 5:3-4. Maadui walitumia mbinu gani ya kuogofya kujaribu kuwafanya watu wa Mungu warejee kwenye hali ya hofu? (Walitaka majina yao!)

 

    1.    Soma Ezra 5:5. Tunapaswa kuwa na ujasiri kwa nani tunapojisikia woga? (Mungu anatuangalia! Mungu anadhibiti matukio maishani.)

 

  1. Pambano

 

    1.    Soma Nehemia 4:1-3. Je, unafurahia kudhihakiwa?

 

      1.    Hisia gani ilisababisha maneno haya ya dhihaka? (Hasira. Hakuna anayefurahia kudhihakiwa. Kwa ujumla, tunadhani kwamba dhihaka zinakuja kutenda jambo la kipumbavu au kutenda kosa. Hii inaonesha kwamba dhihaka zinaweza zisiwe na cha kujihusisha na makosa kwa upande wetu. Kutenda jambo sahihi inaweza kusababisha hasira na dhihaka.)

 

    1.    Soma Nehemia 4:4-5. Nehemia anakuwa na mwitiko gani kwenye hizi dhihaka?

 

      1.    Soma Mathayo 6:9-12 na Mathayo 5:44. Katika Agano Jipya, kuwasamehe wengine ni msingi wa kusamehewa. Unaweza kulinganisha sala ya Bwana na ombi la Nehemia?

 

      1.    Soma Mwanzo 12:3. Je, Nehemia anamwomba tu Mungu kuenenda sawa na ahadi yake kwa Ibrahimu?

 

      1.    Soma Warumi 12:19. Kwa dhahiri, ombi la Yesu na ombi la Nehemia yana mwelekeo (toni) tofauti kabisa. Toni gani inafanana katika maombi yote mawili? (Wanamtegemea Mungu. Nehemia hajibu mapigo yeye binafsi kwa wale wanaowadhihaki watu wa Mungu.)

 

    1.    Soma Nehemia 4:6. Hii inatufundisha nini kuhusu kuifanya kazi ya Mungu tunapokuwa tunadhihakiwa? (Endelea kuifanya! Zingatia kazi na usijikite kwenye dhihaka.)

 

    1.    Soma Nehemia 4:11 na Nehemia 4:13-14. Je, hii inaweka kigezo sahihi kwa ajili yetu leo? (Soma Luka 22:36-38. Kuna uwanja mpana wa kutokubaliana, lakini nadhani kwamba tunapoyafuata mapenzi ya Mungu tunaweza na tunapaswa kujilinda sisi na familia zetu. Hata hivyo, kama tukiendelea na kisa hiki katika Luka 22 tunaona kwamba Yesu hakutumia upanga kupingana na mustakabali wa mateso yake.)

 

  1.   Utambuzi

 

    1.    Soma Nehemia 6:1-3. Je, Nehemia anatoa jibu la kweli? (Ndiyo, anafanyia kazi suala la kuweka malango.)

 

      1.    Kwa nini mtu yeyote atilie shaka uaminifu wa Nehemia? (Kwa sababu hiyo haiakisi kile anachokifikiria Nehemia. Hataki kukutana nao kwa sababu anajua wanataka kumdhuru.)

 

      1.    Hii inatufundisha nini? (Kuna nyakati tunakuwa na zaidi ya jibu moja la kweli juu ya sababu ya kufanya jambo fulani. Katika jambo hili Nehemia alichagua jibu lenye kuchukiza kidogo.)

 

    1.    Soma Nehemia 6:4-7. Unaweza kumfikiria kiongozi ambaye anakabiliana na upinzani na udanganyifu mara kwa mara? Unapaswa kuwa na mwitiko gani ikiwa unakabiliana na upinzani wa aina hii? (Soma Nehemia 6:8-9. Nehemia anajibu kwa kusema ukweli na kwa ombi.)

 

    1.    Soma Nehemia 6:15-16. Nani anayeishia kuogopa? (Maadui wa watu wa Mungu. Wale wanaoogofya wanaishia kutishiwa.)

 

    1.    Rafiki, kati ya mambo kadhaa tuliyojifunza kuhusu kukabiliana na upinzani, jambo la muhimu kabisa ni kumtumaini Mungu. Je, utamwomba Roho Mtakatifu akusaidie umtumaini Mungu pale mustakabali unapoonekana kuogofya? Kwa nini usimwombe sasa hivi?

 

  1.    Juma lijalo: Kukiuka Roho ya Sheria.