Somo la 10: Kumwabudu Bwana

(Nehemia 12, 1 Mambo ya Nyakati 25)
Swahili
Year: 
2019
Quarter: 
4
Lesson Number: 
10

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Mitindo ya ibada! Unataka kuanzisha ugomvi? Wewe kuwa tu na msimamo thabiti kwenye suala hilo. Baadhi ya makanisa yanatatua jambo hili kwa kutumia mitindo tofauti ya ibada kwenye huduma tofauti-tofauti. Je, kuna unachokipendelea? Hudhuria kwenye huduma inayoakisi mtazamo wako. Katika kanisa langu la zamani, tulikuwa na aina tofauti-tofauti za muziki katika Sabato tofauti-tofauti. Suluhisho hilo liliwafurahisha watu baadhi ya nyakati. Kanisa langu la sasa lilianza na imani thabiti hususan kuhusu mtindo wa ibada kwa sababu waanzilishi waliamini ilikuwa muhimu katika kuwafikia wasioamini. Mtazamo wao juu ya muziki ndio mtazamo wangu, hivyo umekuwa uchaguzi mwepesi kwangu. Suala halisi sio kile ninachokipendelea au unachokipendelea, bali Biblia inatufundisha nini kuhusu muziki na ibada? Hebu tuzame kwenye somo letu na tujifunze zaidi!

 

 1.     Ibada na Ukuta

 

  1.     Soma Nehemia 12:27. Ni nini sababu ya mkusanyiko huu? (Kuuweka wakfu ukuta wa Yerusalemu.)

 

   1.     Utaiita hiyo kuwa ni ibada? (Wanauweka wakfu ukuta kwa nani? Ikiwa wanauweka wakfu kwa Mungu, basi nitasema kwamba hiyo ni ibada.)

 

   1.     Mwelekeo wa jumla wa uwekaji wakfu ni upi? (“Walisherehekea kwa furaha.”)

 

    1.     Je, hiyo inaakisi kile kinachoendelea kanisani kwako wakati wa ibada?

 

   1.     Walitumia aina gani ya muziki? (Waliimba. Vifaa vya muziki vilivyobainishwa ni matoazi, vinanda na vinubi. Nadhani tunavielewa vinanda na vinubi. Kwa mujibu wa jicho langu lisilo la kitaalam, kinubi kinaonekana.) kuwa ni kifaa kati ya gitaa na kinanda. Ni chombo cha muziki kilicho na kamba.)

 

   1.     Ni nini uliokuwa jumbe wa muziki wao? (Kutoa shukrani!)

 

    1.     Je, umefanyia uchambuzi muziki unaouimba kanisani?

 

    1.     Nilipokuwa nikikua sehemu kubwa ya muziki ilionekana kuwashangilia wafuasi wa Mungu na si kumshangilia Mungu. Je, hilo ni tatizo?

 

    1.     Je, umeukosoa wimbo wa kuabudu kwa kuwa ni mwepesi na unarudia beti lile lile? Ikiwa ndivyo, soma Ufunuo 4:8 na uelezee mambo yanayofanyika katika makao makuu.

 

  1.     Soma Nehemia 12:28-29. Nani aliyeimba? (Watu walioteuliwa kuimba walisafiri kwenye uwekaji wakfu.)

 

   1.     Je, kuna fundisho katika hili kwa ajili ya ibada kanisani?

 

  1.     Hebu turukie chini na tusome Nehemia 12:43. Mada kuu katika ibada hii ni ipi? (Kufurahia.)

 

   1.     Je, hiyo ndio mada kuu kwa ajili ya ibada kanisani kwako?

 

   1.     Je, ibada yako inafaa zaidi kwa ibada au kwa kulala?

 

   1.     Ninakumbuka kutembelea kanisa fulani ambapo mchungaji alihubiri kwa muda mrefu sana na kwa namna isiyo ya kupendeza kiasi kwamba niliishia kulala. Nina uhakika nililala kwa muda mfupi sana. Lakini, nilipoamka na kuwaangalia watu niligundua kwamba kila mtu kanisani pia alikuwa amelala. Nilipomwambia mke wangu jambo hili, alinijibu kwamba tulikuwa tunasali, na ndio sababu kila mtu alikuwa amefumba macho. Swali langu na jibu lake vilionekana kuwa kichekesho kwamba tulikuwa na kipindi cha kutisha cha kukaa kimya wakati wa hayo maombi.

 

  1.     Angalia tena sehemu ya mwisho ya Nehemia 12:43. Ni nani mwingine ambaye hakuweza kulala katika kipindi hiki cha huduma ya ibada? (Majirani! Biblia inatuambia kuwa sauti ya furaha “ilisikiwa mbali.”

                                   

 1.   Ushirika wa Ibada

 

  1.     Soma Nehemia 12:31 na Nehemia 12:38-39. Tafakari jinsi jambo hili lilivyoonekana. Hii inaakisi nini? (Ushirika. Maandalizi. Mtupo wa jicho kwa jinsi mambo yanavyoonekana. Nina uhakika mlolongo huu wa mambo ulionekana kuwa wa kupendeza.)

 

   1.     Kanisa lako lipo kwenye nafasi gani katika suala la ushirika wa ibada yenu? Je, liko pamoja? Je, kuna mtu anayezingatia jinsi mambo yanavyoonekana?

 

    1.     Je, unakumbuka mifano yoyote ya ibada iliyoonekana kuwa nzuri na iliyopangiliwa vizuri?

 

    1.     Je, unakumbuka mifano yoyote ya ibada iliyoonekana kuwa mbaya na isiyo na mpangilio?

 

    1.     Sababu ya ibada kuwa mbaya na isiyo na mpangilio ni ipi? (Huduma za ibada zinakuwa hazina mpangilio watu wanaposhindwa kutenga muda wa kutenda mambo kwa uzuri. Inaakisi uhaba wa maandalizi na kutoyazingatia mambo.)

 

  1.     Majuma mawili yaliyopita nilihubiri kwenye kanisa dogo lililokuwa na mimbari nzuri. Unapanda juu yake na inapendeza sana. Ninakumbuka kanisa jingine dogo nililolitembelea ambapo upande wa mbele wa kanisa ulikuwa na bomba la maji lililo nje ya ukuta na lilikuwa na mwonekano wa kutisha. Ninahisi washiriki wa kanisa walikuwa wamezoea kuona bomba hilo kiasi kwamba hawakulifikiria kwa namna yoyote. Katika kanisa la kwanza washiriki waliolijenga walikuwa mahsusi sana kwa kila kitu kilichojengwa. Katika kanisa la pili, hawakujali sana. Mfano upi kati ya hii miwili unafanana na kanisa lako?

 

  1.     Soma 1 Mambo ya Nyakati 25:1-2 na 1 Mambo ya Nyakati 25:6-7. Angalia rejea inayojirudiarudia ya usimamizi na mafunzo. Je, wale wanaoshiriki kwenye huduma ya ibada kanisani wanapaswa kusimamiwa na kufundishwa?

 

   1.     Huwa ninaombwa kuhubiri mara kwa mara. Kwa baraka za Mungu na juhudi kubwa kwa upande wangu, nadhani matokeo humpa Mungu utukufu. Hata hivyo, hakuna mtu hata mmoja aliyewahi kuniomba niimbe. Unadhani ni kwa sababu gani?

 

   1.     Ninapofundisha au kuhubiri, kamwe sijaribu kupenyeza wimbo hata kidogo. Unadhani ni kwa sababu gani?

 

   1.     Je, kanisa linapaswa kuwa na uchaguzi kidogo katika kuwachagua waimbaji kuliko wahubiri? Je, waimbaji (au wale wanaosali, wanaotoa wito wa sadaka, au kusoma maandiko) wanapaswa kupenyeza hubiri kidogo?

 

    1.     Je, kanisa linapaswa kuwa na sheria kali dhidi ya uhubiri ambao haujaombwa au kuidhinishwa? Au, je, vitu visivyoombwa au kuidhinishwa ni ishara ya uongozi wa Roho Mtakatifu? (Kamwe sipendi kumzimisha Roho Mtakatifu, lakini ninadhani usimamizi na mafunzo vyote ni vya muhimu kwa ustawi katika ibada.)

 

 1. Dhabihu na Ukuta

 

  1.     Soma tena Nehemia 12:43. Unadhani watu (kimsingi makuhani) walikuwa wanafanya nini “walipotoa dhabihu nyingi?” (Walikuwa wanatoa wanyama kafara.)

 

   1.     Uchinjaji wanyama unaendana vipi na furaha? (Mojawapo ya maoni yamebainisha kwamba hizi ni “kafara za shukrani.” Watu wanaweza kushiriki kwenye ulaji wa kafara hizi. Hii ni sawa na uchomaji nyama (nyama choma) mkubwa!)

 

  1.     Soma 1 Yohana 1:7-9. Hii inaashiria nini juu wa wafuasi wa Mungu?

 

   1.     Hapo awali tulibainisha ukweli kwamba watu walikuwa wanaweka wakfu ukuta. Nikashauri kwamba ilikuwa ni aina fulani hivi ya ibada kwa sababu walikuwa wanauweka wakfu kwa Mungu. Inawezekana kwamba walikuwa wanauweka wakfu ili uwe ukuta imara? Ukuta wa kuwashinda maadui wao?

 

   1.     Je, itakuwa sahihi zaidi, kutokana na kile tulichojifunza hadi kufikia hapa, kuhitimisha kwamba walikuwa wanafurahia usalama wa ukuta uliokamilika kujengwa?

 

   1.     Kwa nini walihitajika kujenga upya ukuta? (Kuna sababu mbili zinazoweza kukubalika kwa uwekaji wakfu huu. Kwanza, Yerusalemu ilianguka kwa sababu watu wa Mungu hawakuwa waaminifu kwake. Nadhani walitaka kusafisha (kutakasa) kila kitu, ikiwemo ukuta, ili kuufanya kuwa sehemu ya mji mtakatifu wa Mungu. Pili, ukuta ulikuwa chanzo cha ulinzi na ishara kwamba walikuwa wameushinda upinzani wa maadui wao. 1 Yohana 1:7 inatuambia kwamba kuwa na uhusiano sahihi na Mungu ndilo lengo letu. Hilo, na kuwashinda maadui wako, ndizo sababu mbili nzuri za kufurahi na Mungu.)

 

  1.     Hebu tuangalie vifungu viwili vinavyounganisha kifungu tulichokisoma hivi punde. Soma 1 Yohana 1:6 na 1 Yohana 1:10. Ni mambo gani mawili makubwa tunayopaswa kuyaepuka? (Kuishi maisha yasiyoakisi uhusiano wetu na Mungu. Kujidai kwamba tunaishi maisha makamilifu wakati kiuhalisia hatuishi hivyo.)

 

   1.     Mambo haya yanaakisi vipi kwa hali ya chini kwenye utukufu wa Mungu?

 

  1.     Soma Nehemia 12:46. Je, maisha yetu yanapaswa kuakisi nyimbo zetu? (Ndiyo! Nyimbo ni njia moja ya mawasiliano. Maisha yetu yanapaswa kuwa ya kumsifu na kumshukuru Mungu!)

 

 1.   Juma lijalo: Watu waliorudi nyuma.