Somo la 6: Kwa Nini Ufasiri Unahitajika?

(Luka 24, Waebrania 11, Yohana 9)
Swahili
Year: 
2020
Quarter: 
2
Lesson Number: 
6

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Wajukuu wangu wameanza kujifunza kusoma. Nilitizama video ya mmojawao akisoma Biblia yake. Alipokutana na neno gumu zaidi, alitamka herufi kwa sauti, na kisha kuangalia kama neno linaleta mantiki kwenye sentensi hiyo. Kamwe hatupaswi kubainisha kwa kina jinsi maneno ya Biblia yanavyofanya kazi pamoja ili kuleta mantiki. Ni njia gani bora ya kutekeleza jambo hili? Hebu tuone kile Biblia inachotufundisha kwenye mada hii!

 

 1.     Imani

 

  1.     Soma Luka 24:36-37. Kitu gani kilisababisha wanafunzi wadhani kwamba Yesu alikuwa roho (mzuka)? (Wafu wanaowatembelea watu si watu halisi.)

 

  1.     Soma Luka 24:38. Yesu anasema jambo gani hasa? Angalia kwa kina kilicho nyuma ya swali lake? (Kwa nini mnadhani kwamba bado ningali nimekufa?)

 

  1.     Soma Luka 24:39-40. Hebu tuangalie namna Yesu anavyobadili jinsi wanavyomchukulia. Yesu anatumia njia gani ya kwanza kabisa? (Anawapatia uthibitisho halisi. Anawataka watumie hisia zao za macho na mguso. Mikono na miguu ya Yesu inaonyesha alama za kuteswa kwake.)

 

   1.     Katika zama za leo kuna jambo gani lenye kufanana la kumsaidia mtu kutafsiri Biblia kwa usahihi? (Kuonesha jinsi Biblia ilivyokubadilisha au jinsi ilivyombadilisha mtu mwingine.)

 

  1.     Soma Luka 24:41. Kwa nini wanafunzi hawakuamini hisia zao za macho na mguso? (Walizidiwa furaha. Lilikuwa jambo “jema mno kuwa la kweli.”)

 

  1.     Soma Luka 24:42-43. Hii ina tofauti gani na kuonesha mikono na miguu yake? (Bado huu ni uthibitisho halisi, lakini pia unahusisha uelewa wao juu ya tofauti kati ya wanadamu na mizuka kwa kuzingatia mchakato wa maisha na uhai.)

 

   1.     Katika zama za leo kuna jambo gani lenye kufanana la kumsaidia mtu kuitafsiri Biblia kwa usahihi? (Badala ya kuelezea kwa haraka haraka maisha ya mtu aliyebadilika, utaonesha jinsi wanavyoyakabili matatizo kwa namna tofauti. Mchakato wao wa fikra umebadilika.)

 

  1.     Soma Luka 24:44-45. Sasa Yesu anabadilije mtazamo wao? (Anaigeukia Biblia ili kuthibitisha kwamba hiki ndicho kilichopaswa kumtokea.)

 

   1.     Jambo lenye kufanana katika zama za leo ni kumfundisha asiyeamini kwa njia ya kujifunza Biblia. Kwa nini Yesu hakuanza uthibitisho wake kwa Biblia?

 

    1.     Je, katika jambo hili kuna fundisho lolote kwetu leo?

 

  1.     Soma Luka 24:46-48. Yesu ananukuu Biblia. Mawazoni mwake naona anaifikiria Hosea 6:1-3. Hebu tuisome. Yesu ameongeza kipengele gani kipya kwenye uthibitisho wake kwamba amefufuka? (Ananukuu kifungu ambacho si tu kwamba kinaonesha siku ya tatu ya urejeshwaji, bali pia kinaweka msimamo kwa wanafunzi wake – “watasonga mbele” katika kutambua kazi ya Yesu kama mashahidi wake. Jambo gani linaweza kuwa bora zaidi ya unabii unaobainisha kazi ya mtu unayejaribu kumshawishi?)

 

  1.     Soma Luka 24:49. Wanafunzi watapewa uthibitisho gani mwingine wa ziada? (“Watavikwa” uwezo wa Roho Mtakatifu!)

 

   1.     Je, umetafakari kuongezea jambo hili kwenye uelewa wako wa Biblia?

 

    1.     Je, Roho Mtakatifu atakazia “au kutia changamoto” uelewa wako wa Biblia?

 

    1.     Je, unapaswa kumwalika asiyeamini kutazamia maelekezo/mwongozo wa Roho Mtakatifu?

 

  1.     Soma Waebrania 11:6. Takwa kuu kwa ajili ya kuitafsiri Biblia ni ipi? (Imani! Imani kwamba Mungu anaweza kubadili mambo.)

 

 1.   Ukomo wetu

 

  1.     Soma Yohana 9:1-2. Kitu gani kiliwafanya wanafunzi waamini kwamba upofu ulitokana na dhambi? (Uelewa wao wa kiroho umechujwa kupitia imani zilizopo.)

 

   1.     Je, hili ni tatizo kwetu katika kuielewa Biblia?

 

  1.     Soma Yohana 9:3. Kitu gani kinatakiwa ili kumwamini Yesu? (Wanafunzi waliweka kando imani yao kwamba dhambi ilisababisha jambo hili.)

 

  1.     Yesu anamponya kipofu. Hebu turuke vifungu kadhaa na tusome Yohana 9:14-16. Nini kiliwazuia Mafarisayo wasiamini kwamba Yesu alimponya mtu huyu? (Ilikuwa ni uelewa wao wa Biblia na asili ya dhambi.)

 

   1.     Kitu gani kiliwahamasisha wengine kujenga hoja kwamba Yesu hakuwa mdhambi? (Uelewa wao wa Biblia kwamba wadhambi wasingeweza kutenda miujiza.)

 

   1.     Je, unaona kwamba tuna uelewa wa Biblia wa aina mbili tofauti ambao matokeo yake ni ma-hitimisho tofauti?

 

    1.     Tunapaswa kuepukaje tatizo hili? Je, linaweza kuepukika? (Mafarisayo wanajenga hoja kwamba uelewa wao wa Biblia unamzuia Yesu kutotenda muujiza huu. Kundi jingine linaukubali muujiza na wajibu wa Yesu katika muujiza huo. Hili kundi la pili linaangalia uelewa sahihi. Kwa kuzingatia uelewa wa kundi la pili inatusaidia kuweka kando fikra yetu ya awali katika kuielewa Biblia.)

 

  1.     Soma Yohana 9:19-22. Kitu gani kinatia hamasa jibu la wazazi wa yule kipofu? (Wanaogopa “kutengwa na sinagogi.”)

 

   1.     Je, hii inaakisi tatizo katika zama za leo pale tunapojaribu kuielewa Biblia? Je, tunaogopa kufikia ma-hitimisho ya namna fulani kutokana na jinsi washiriki wenzetu kanisani wakatavyoyachukulia?

 

   1.     Tukisoma maoni ya viongozi wa mwanzo wa kanisa letu, tunaona ushawishi wa kutoruhusu kile tulichokiamini siku za nyuma ili kudhibiti uelewa wetu wa sasa. Hata hivyo, kanisa linatusihi tushikilie “nguzo” na tujikite kwenye “msingi thabiti” wa imani ya sasa. Kipi kilicho sahihi? Je, yote mawili hayako sahihi?

 

  1.     Soma Yohana 9:30-34. Kilichoogopwa kilitimia – yule mtu anatupwa nje ya sinagogi. Unaifikiriaje mantiki ya mtu huyu aliyekuwa kipofu lakini sasa anaona?

 

   1.     Mantiki ni ya muhimu kiasi gani katika kuielewa Biblia? Je, inaweza kuwa mtego? (Ingawa ninaelewa maonyo kuhusu majivuno na fikra ya kibinadamu, ninaamini kwamba mantiki ni ya muhimu kama ilivyoonyeshwa na huyu mtu aliyekuwa kipofu hapo awali. Unakumbuka majuma mawili yaliyopita kuhusu mjadala wetu juu ya mtumishi asiye mwaminifu (Luka 16:8), na jinsi bwana wake alivyomsifia kwa kuwa “mwerevu?” Hiyo inatoa ushauri kuhusu matumizi ya akili ya kawaida.)

 

   1.     Unachukuliaje kitendo cha huyu mtu aliyekuwa kipofu hapo kabla kushindwa kuwakubalia viongozi wa dini? (Kushindwa kwake kukubali kunatokana na mkusanyiko wa uelewa wake juu ya kile kilichomtokea na imani zake za kidini. Hiyo ni tofauti kinyume na kutokuwa mtiifu tu.)

 

  1.     Soma Yohana 9:39-41. Je, tunapambana na upofu katika kuitafsiri Biblia? Tunawezaje kutatua hali hii? (Katika kisa chetu Yesu anaingilia kati kutatua upofu wa wale wanaohitaji tiba. Katika zama za leo, tunaweza kumwita Mungu katika mfumo wa Roho Mtakatifu, ikiwa tuko radhi, ili kutibu upofu wetu.)

 

  1.     Soma 2 Petro 3:15-16. Ni rahisi kiasi gani kuielewa Biblia kwa usahihi? (Kifungu hiki kinatuambia kwamba baadhi ya mambo yaliyoandikwa na Paulo ni “magumu kuyaelewa.”)

 

   1.     Tunahatarisha kitu gani tukiipotosha Biblia? (Uzima wetu wa milele. Tunapaswa kuwa makini sana katika kujifunza ili kujaribu kuufikia uelewa sahihi.)

 

    1.     Je, hili ni suala la akili? Ukitafakari nyuma katika zama tulipokuwa shule, baadhi ya wanafunzi walielewa somo vizuri zaidi kuliko wengine. Je, kuna baadhi, ambao hawana akili sana, wana tatizo kidogo katika kuielewa Biblia? (Sote tuna fursa sawa ya kumwendea Roho Mtakatifu. Wale wanaodhani kwamba wao ni werevu, wanaweza kuwa kwenye nafasi ya chini kutokana na majivuno ya maoni na ushauri.)

 

  1.     Rafiki, je, utaiendea Biblia kwa mawazo chanya juu ya ukweli wake? Je, utamwomba Roho Mtakatifu akuongoze kwenye uelewa sahihi wa Neno? Kwa nini usifanye uamuzi huo sasa hivi?

 

 1. Juma lijalo: Lugha, Kifungu, na Muktadha.