Somo la 10: Jinsi ya Kushiriki kwa Furaha

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Marko 3, Waebrania 10, Matendo 16, 1 Wakorintho 12)
Swahili
Year: 
2020
Quarter: 
3
Lesson Number: 
10

 

 

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Umepitia uzoefu gani kwenye karantini ya ugonjwa wa COVID-19? Kwa kuwa hili ni janga la dunia, ninahisi kuwa angalao watu wote wanaosoma ujumbe huu wamepitia uzoefu wa mabadiliko kimaisha kutokana na kirusi hiki. Badiliko moja kubwa kwangu ni kukaa nyumbani. Nilifundisha masomo yangu ya shule ya sheria kwa njia ya mtandao. Nilifanya kazi zangu za kimahakama kutokea nyumbani. Pia nilifundisha darasa langu la kujifunza Bibla na kuhubiri kutokea nyumbani. Nilichokikosa ni mwingiliano wa kuonana na watu nje ya nyumbani kwangu! Somo letu juma hili linahusu kutenda kazi kwa kushirikiana na wengine ili kuutangaza Ufalme wa Mungu. Je, unatazamia tena kufanya kazi na wengine? Je, hilo linakupatia hisia za furaha? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi kuhusu furaha ya kufanya kazi na wengine ili kuutangaza Ufalme wa Mungu!

 

  1.    Vikundi Vidogo Vidogo vya Kujifunza Biblia

 

    1.    Soma Marko 3:13-14. Unadhani kwa nini Yesu aliwachagua wanafunzi kumi na wawili ili afanye nao kazi?

 

      1.    Kwa nini hachagui idadi kubwa? (Kifungu kinasema “wapate kuwa pamoja naye.” Hii inaashiria uamuzi halisi juu ya idadi ya marafiki wa kila siku.)

                        

    1.    Soma Waebrania 10:23-25. Unaposoma vifungu hivi, je, unadhani kuwa hii inazungumzia suala la kwenda kanisani kila mara? (Inaweza kuwa inarejelea uendaji kanisani wa kila mara.)

 

      1.    Unapoenda kanisani, je, unawatia moyo washiriki wengine na kuwachangamsha kuwa na upendo na matendo mema?

 

      1.    Au, huwa unazungumza kikawaida na washiriki wengine, na kisha unakwenda nyumbani? (Huenda hii inaakisi tabia yangu, lakini ninapokwenda kanisani huwa ninazungumza kwa muda mfupi na watu kadhaa. Sio mahali ninapojifunza vya kutosha kutoka kwa watu wengine ili kutafakari jinsi ya kuwahamasisha wengine kwa ufanisi zaidi katika kazi zao.)

 

    1.    Tafakari tena sehemu ya Waebrania 10:25 inayohusu kutiana moyo. Mhubiri au mwalimu wa Biblia anapaswa kututia moyo kama kikundi, lakini ni watu wangapi ambao wewe binafsi huwa unawatia moyo?

 

      1.    Kwa miongo kadhaa nimekuwa sehemu ya vikundi vidogo vidogo vya kujifunza Biblia. Katika vikundi hivyo nimepata kuwafahamu wanadarasa, kufahamu habari za maisha yao, na kuelewa yale yanayowatia wasiwasi. Haya ni mambo ambayo nisingeweza kuyafahamu kwa kukutana tu na watu na kuzungumza nao kwa muda mfupi kanisani.

 

    1.    Soma Matendo 16:11-13. Paulo anatafuta nini siku ya Sabato? (Anawatafuta wale wanaomwabudu Mungu.)

 

    1.    Soma Matendo 16:14-15. Lidia anaongolewa baada ya kumsikia Paulo akiielezea injili. Unaona manufaa gani kufundishwa katika kikundi kidogo? (Vikundi vidogo vidogo havitishii sana. Mtu ambaye inawezekana asiweze kuongea kwenye kundi kubwa atajisikia huru kufanya hivyo kwenye kikundi kidogo.)

 

      1.    Je, utajisikia huru zaidi kumkaribisha mtu asiye mshiriki kwenye kikundi kidogo badala ya kumkaribisha mtu huyo kanisani?

 

      1.    Je, unadhani kuwa mtu asiye mshiriki ana uwezekano mkubwa wa kukubali ukaribisho kwenye kikundi kidogo kuliko ukaribisho wa kuhudhuria kanisani?

 

  1.   Ufanisi wa Kikundi Kidogo

 

    1.    Soma Matendo 20:16-17. Paulo anasafiri merikebuni na kupita Efeso, lakini anataka kuongea na wazee wa kanisa la Efeso. Kwa nini Paulo hakusafiri tu kwenda Efeso? (Hakutaka kucheleweshwa kwa kukutana na kanisa zima.)

 

      1.    Je, umegundua kuwa mikutano midogo midogo inafanya matumizi yako ya muda yawe na ufanisi?

 

    1.    Soma Matendo 20:18 na Matendo 20:28-29. Kama ningekuambia “uwazingatie kwa makini” washiriki wa kanisa, ungetekelezaje jambo hilo kama ungekuwa mchungaji wa kanisa?

 

      1.    Je, ungewatembelea watu majumbani? Je, ungewapigia simu?

 

        1.    Kiuhalisia ungefanya hivyo mara ngapi?

 

      1.    Tuseme kwamba unawatembelea watu majumbani mara mbili kwa mwaka? (Sina kumbukumbu kwa mchungaji wangu yeyote kutekeleza hilo, lakini tuchukulie kwamba hili lilifanyika. Je, hiyo itakuwa “uzingativu makini?”

 

    1.    Angalia tena Matendo 20:28. Paulo anawaitaje wazee? (“Waangalizi.” Huyu ni mtu anayesimamia.)

 

      1.    Unadhani hiyo inamaanisha nini? (Wale “wanaoliangalia kwa makini lile kundi.”)

 

      1.    Sina uhakika muundo wa kanisa lako ukoje, lakini makanisa mengi yana mchungaji anayesaidiwa na wazee wa kanisa mahalia. Fikiria endapo wazee wote wangekuwa na kikundi kidogo cha kujifunza Biblia kila juma. Ni mara ngapi wangekuwa wakiangalia hali ya washiriki?

 

      1.    Endapo wazee wangeambiwa kuwasilisha taarifa kwa mchungaji pale washiriki wa kanisa walipohitaji msaada, mchungaji angekuwa na “ufuatiliaji” wa kila juma wa washiriki wote. Je, unaweza kupendekeza njia rahisi au isiyoogofya kwa mchungaji kuwafuatilia washiriki wake kila mara?

 

    1.    Je, unapenda kwenda nyumbani kwa marafiki wako? Je, kikundi kidogo cha kujifunza Biblia ni njia nzuri ya ushirikishwaji?

 

  1. Muundo wa Kikundi Kidogo

 

    1.    Soma 1 Wakorintho 12:12-14. Hii inaashiria kuwa kanisa linafanana na mwili wa mwanadamu. Analojia hii inaashiria nini kuhusu mfumo wa kanisa? (Inaashiria kuwa linapaswa kuwa na utaratibu.)

 

      1.    Je, unadhani vikundi vidogo vinasaidia kulipangilia kanisa?

 

      1.    Vipi kama ukiwaweka washiriki wote wanaotekeleza jukumu linalofanana kanisani kwenye kikundi kimoja kidogo?

 

        1.    Je, hilo litawasaidia kutimiza kazi yao? Au, huu ni utaratibu uliovuka mipaka? (Nilitengeneza mfumo uliowapanga washiriki wote wa kanisa kwenye vikundi vidogo vidogo kwa kuzingatia majukumu yao ya jumla kanisani. Mfumo huo haukukubaliwa kamwe. Nina uhakika sehemu ya tatizo ilikuwa ni mtu kuchaguliwa kikundi unachopaswa kujiunga – badala ya kuchagua kikundi chako mwenyewe.)

 

    1.    Soma 1 Wakorintho 12:27-28. Una maoni gani kuhusu kuwa na vikundi vidogo vidogo vinavyoundwa na mitume, manabii, walimu, au watendao miujiza pekee? Ninachokimaanisha hapa ni kuwa kikundi kimoja kidogo kijumuishe manabii pekee? (Hiyo inabainisha tatizo jingine kwenye wazo langu.)

 

      1.    Je, vifungu hivi vinazungumzia chochote kuhusu mchanganyiko bora kwa ajili ya vikundi vidogo vidogo?

 

      1.    Je, unavichukulia vikundi vidogo kama “mkono” au “mguu” (1 Wakorintho 12:21) wa kanisa kubwa, au unavichukulia zaidi vikundi vidogo kama kanisa dogo? (Ingawa bado ninadhani kupangilia vikundi vidogo vidogo kwa kuzingatia kazi za kanisa ni jambo la manufaa, inaonekana vinafanya kazi vizuri ikiwa vitafanana zaidi na kanisa dogo.)

 

  1.   Kikundi Kidogo cha Mungu

 

    1.    Soma Waebrania 1:1-2 na Yohana 1:1-3. Nani anayehusika kwenye uumbaji? (Vifungu hivi vinamtaja Baba na Mwana, ambaye pia anaitwa Neno.)

 

    1.    Soma Mwanzo 1:1-3. Nani mwingine anatajwa hapa kuhusiana na uumbaji? (Roho wa Mungu.)

 

    1.    Soma Mathayo 28:18-19. Kwa nini Yesu aliamuru kuwa Wakristo wote wabatizwe “kwa jina” la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu? (Kwa sababu wanafanya kazi pamoja.)

 

      1.    Unadhani kwa nini anafanya kazi katika “kikundi kidogo?” (Soma Yohana 16:7-8 na Yohana 14:26. Tunaona kuwa Yesu na Roho Mtakatifu wanashirikishana kazi zao. Wanasaidiana.)

 

    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 6:4. Je, hii inakinzana na maelekezo ya ubatizo wa Yesu? (Hapana. Mtafaruku huu wa juujuu unatatuliwa na fundisho la Utatu Mtakatifu – kwamba Watatu hawa ni kitu Kimoja.)

 

    1.    Rafiki, kufanya kazi katika vikundi vidogo vidogo ilianzia kwa Mungu. Kila mtu anataka kuwa sehemu ya, Wachungaji wanahitaji kuchunga makundi yao, kujadili Biblia na watu wengine hutusaidia kujifunza, na watu wengi wanapenda kuhusiana kijamii (socialize). Kwa nini usiyaweke mambo yote haya pamoja kwa kuunda au kujiunga na kikundi kidogo cha kujifunza Biblia? Kama unatafuta nyaraka kwa ajili ya kujifunza, nenda kwenye sehemu ya hifadhi ya nyaraka (archive) kwenye tovuti ya www.GoBible.org.

 

  1.    Juma lijalo: Kueleza Habari za Yesu.