Somo la 9: Kanisa na Elimu

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Luka 10, Mathayo 5, 2 Wathesalonike 3)
Swahili
Year: 
2020
Quarter: 
4
Lesson Number: 
9

Somo la 9: Kanisa na Elimu

 

(Luka 10, Mathayo 5, 2 Wathesalonike 3)

 

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Kwenye suala la kufundisha Biblia, je, kanisa si kitovu cha elimu? Elimu ni mchakato wa kubadili mawazo. Wakati mwingine mabadiliko hayo ni kujifunza tu jambo ambalo hapo awali hukuwa na ufahamu wowote wa jambo hilo. Wakati mwingine, elimu hubadili mtazamo. Ikiwa makanisa ni “mahala salama,” ambapo kila mtu anatarajiwa kuacha kuelezea mtazamo usiokubaliwa na wengi, mitazamo inaweza kubadilishwaje kwenye mada nyeti? Juma hili tunajikita kwenye kisa alichokielezea Yesu kuhusu kuwasaidia wahitaji. Je, uongozi wa kanisa letu ni kielelezo katika jambo hili? Je, kuna ukomo kiutendaji kuhusu mtu tunayepaswa kumsaidia? Hebu tuchimbue somo letu na tujifunze angalao sehemu ya kile Biblia inachokifundisha kuhusu uongozi na utoaji msaada!

 

  1.     Uongozi Motoni?

 

    1.     Soma Luka 10:30. Yerusalemu ni makao makuu. Mji wa Yeriko, ambao uko umbali wa maili 15 tu kutoka Yerusalemu, ni mji wenye eneo kubwa. Wasafiri wengi husafiri kati ya miji hii miwili. Uhalifu ulikuwa tatizo kubwa kwa wale wanaosafiri kupitia njia hii. Mazingira yanatuambia nini kuhusu mtu huyu? Je, hakuwa mwangalifu?

 

      1.     Je, mtu mwangalifu, mwenye busara atasafiri na watu wengine?

 

      1.     Je, inawezekana kuwa hata mtu mwangalifu, mwenye busara anaweza kuvamiwa na kuibiwa? (Maoni fulani niliyoyasoma yalitaarifu kuwa hata kama mtu angechukua tahadhari zote bado angeweza kuuawa au kuibiwa kwenye barabara hii.)

 

    1.     Soma Luka 10:31. Kwa nini Yesu anasema, “kwa nasibu” kuhani alikuwa mahali hapa? (Kuhani alikuwa hatafuti kukutana na jambo hili. Alikuwa haendi kumsaidia mtu huyu. Kuhani alikuwa anawazia mambo mengine.)

 

      1.     Je, kuhani alimwona mtu huyu aliye “karibu ya kufa?” (Ndiyo. Yesu anatuambia kuwa alimwona.)

          

      1.     Je, kuna sababu yoyote kwa nini kuhani “alipita kando?” (Ninachokiwazia ni kwamba huu ulikuwa ni mtego. Mara tu kama ningeenda kumsaidia mtu huyu, wanyang’anyi wangenirukia na kunishambulia kwa kunipiga.)

 

      1.     Je, kuna suluhisho fulani hivi linalotokana na ulegezaji masharti ambapo kuhani angeweza kubakia salama kwa kiasi kikubwa, wakati huo huo akijaribu kuelewa kama huu ulikuwa mtego na ni kwa kiasi gani mtu huyu alihitaji kusaidiwa?

 

    1.     Soma Luka 10:32. Tunapewa kweli zile zile kama kwa Mlawi. Hatuna maelezo yanayomhusu mtu huyu aliyeibiwa wala cheo chake. Kwa nini Yesu anaelezea kazi za wawili hawa? (Ni watu muhimu kwenye kisa hiki kama tutakavyoona hivi punde.)

 

    1.     Soma Luka 10:33. Je, Msamaria anakuwa mpumbavu? (Anajihatarisha. Lakini, hiyo inamaanisha hana ubinafsi – anampendelea mtu aliyeibiwa kuliko usalama wake mwenyewe.)

 

      1.     Tunaambiwa kuwa wewe ni mbaguzi wa rangi kama unazingatia asili ya mtu (mbari). Kwa nini Yesu anatuambia asili ya mtu aliyeonesha huruma? (Kuhani na Mlawi walikuwa Wayahudi. Tunajua asili yao. Samaria ilikuwa ni eneo fulani na hivyo Yesu anazungumzia suala la kijiografia, sio mbari. Lakini, tunafahamu kuwa Wasamaria walikuwa ni uzao wa ndoa zisiziruhusiwa kati ya Wayahudi walioachwa na watu wa Babeli na mataifa yaliyoishi katika eneo lile.)

 

    1.     Soma Luka 10:34-35. Kama ungekuwa hujawahi kusoma kisa hiki hapo kabla, je, ungeshangaa? (Dini inapaswa kuzingatia kuwapenda wengine. Hawa ni viongozi wa dini, hivyo wanapaswa kuwa kielelezo cha kuwajali wengine. Wasamaria walikuwa na imani za dini hafifu na utamaduni hafifu, kwa mujibu wa Wayahudi. Imani yangu ni kuwa mtu aliyeishi katika kipindi hicho angeweza kufikiria kuwa Msamaria anaweza kuwa mnyang’anyi, lakini kuhani na Mlawi kamwe asingekuwa mnyang’anyi.)

 

    1.     Hiki ni kisa alichokitengeneza Yesu. Kinawaweka viongozi wa dini kwenye hali mbaya. Kwa nini Yesu anafanya hivi?

 

  1.   Jirani Yako

 

    1.     Huenda tusiweze kujibu kikamilifu swali la awali bila kupata muktadha zaidi. Hebu tuangalie kilichomsababisha Yesu kuelezea kisa hiki. Soma Luka 10:25. Je, hili ni swali la kweli? Ni ni swali nyofu na la dhati? (Hapana. Ni jaribu.)

 

    1.     Soma Luka 10:27-29. Je, mwanasheria huyu ameachwa mdomo wazi na jibu la Yesu? Je, mwanasheria amesogea kutoka kwenye “jaribu” hadi kwenye kuujali wokovu wake mwenyewe? (Nadhani.)

 

      1.     Anachokimaanisha Yesu kwenye kisa hiki ni kuelimisha kuhusu jirani yetu ni nani. Je, Yesu angetoa ujumbe huo huo endapo kuhani ndiye angekuwa amemsaidia mtu aliyeibiwa? (Ndiyo.)

 

        1.     Kutokana na muktadha huu, je, kuna sababu yoyote kwa nini Yesu aliwafanya viongozi wa Kiyahudi waonekane watu wabaya?

 

    1.     Soma Luka 18:9-11. Yesu anabainisha tatizo gani miongoni mwa viongozi wa Kiyahudi? (Waliamini walikuwa wenye haki na waliwatendea wengine kwa kebehi.)

 

      1.     Hii inaashiria nini kuhusu njia ambayo Yesu alijenga kisa chake katika Luka 10? (Kuwafanya viongozi wa Kiyahudi kuwa watu wabaya sio upindishaji bandia, inaakisi mtazamo wa baadhi ya viongozi kwamba watu wengine wanapaswa kudharauliwa.)

 

    1.     Soma Luka 10:36-37. Yesu anasema tunathibitisha kuwa jirani wa wengine kama tutawahurumia. Je, kuna mengi zaidi ya kujifunza kutokana na kweli za ziada ambazo tumezijadili hadi kufikia hapa? (Wayahudi waliwadharau Wasamaria, licha ya hayo bado Yesu alimfanya Msamaria kuwa shujaa wa kisa!)

 

      1.     Kumfanya Msamaria kuwa shujaa wa kisa kunatufundisha nini kuhusu yule tunayepaswa kumsaidia? (Tunapaswa kuwasaidia watu ambao katika hali ya kawaida tusingewasaidia.)

 

      1.     Hivi karibuni, nilikuwa nikihubiri mahubiri yanayobainisha kuwa Biblia inamhusu Yesu, na haituhusu sisi. Ikiwa kisa hiki kinamhusu Yesu, tunapaswa kuchukua ujumbe gani kutoka kwenye kisa hicho? (Yesu aliyaacha maisha yake mbinguni ili kuwaokoa viongozi wa Kiyahudi, Wasamaria, na hata watu wanaochukua uamuzi wa kipumbavu.)

 

  1. Matumizi Halisi Maishani (Practical Application)

 

    1.     Soma Mathayo 5:16 na uangalie thamani ya elimu ya Luka 10. Tunatakiwa tuamue aina ipi ya “nuru” tunaipeleka kwa wengine. Je, kisa tulichokisoma hivi punde kinahusika kwa mtu aliyesimama kando ya barabara bila kudhuriwa, lakini anaomba fedha?

 

      1.     Kama umesema kitahusika, ungekitumiaje?

 

      1.     Nimewahi kufanya kazi kwenye kituo cha watu wasio na makazi katika eneo ninaloishi. Ninaposafiri kwenda mahali hapo, ninawaona watu wakiwa wamesimama umbali fulani kutoka kwenye nyumba hiyo ya watu wasio na makazi, wakiomba fedha. Nina uhakika kuwa wanaishi kwenye kituo hicho, lakini wanajaribu kuokoteza fedha za ziada. Utakitumiaje kisa cha Luka 10 kwa watu hawa?

 

      1.     Siku hizi, kila mtu anayesimama (au kukaa) kando mwa barabara akiomba fedha ni mdogo kiumri kuliko mimi. Kimsingi, pia ni masikini kuliko mimi. Utakitumiaje kisa cha Luka 10 kwenye hali inayonikabili?

 

        1.     Je, ungebadili mawazo yako endapo wangekuwa wanavuta sigara?

 

    1.     Soma 2 Wathesalonike 3:6 na 2 Wathesalonike 3:10-13. Tuliposoma habari hii hapo kabla kwenye kisa cha Luka 10, tulipaswa kujifunza nini?

 

      1.     Je, kisa cha Luka 10 kina chochote cha kuzungumzia kuhusu watu wazima ombaomba wanaoomba fedha barabarani kwenye sehemu magari yanaposimama? (Sidhani kama kuna chochote inachokizungumzia. Kisa cha Luka 10 kinahusu hali ya dharura.)

 

    1.     Angalia tena 2 Wathesalonike 3:6. Hii inahusika kwa “ndugu” na inatuambia “tujitenge.” Ombaomba wengi ninaowaona wana alama ndogo inayoashiria kuwa hawana makazi maalumu au wana njaa na mara nyingi huwa wanamrejelea Mungu. Je, hiyo inawafanya wawe “ndugu?”

 

      1.     Ikiwa wao si “ndugu” je, hamasa ya kufanya kazi bado inahusika?

 

      1.     Kama tunasema kuwa kazi yetu ni kuwapelekea wengine “nuru,” je, hiyo inaashiria kuwa kile tunachojifunza kanisani kuhusu jinsi tunavyohusiana kwenye kazi kina mafundisho ya kuwapelekea walimwengu?

 

      1.     Inaonekana dhahiri kuwa taarifa za ziada kuhusu ombaomba ni za muhimu katika kutoa majibu sahihi kwenye maswali haya? (Kumpatia mtu dola moja ni rahisi kuliko kusimama na kuanza kuuliza maswali. Unadhani Msamaria angefanya nini kwenye hali kama hii?

 

    1.     Rafiki, tukiachilia mbali suala la watu wazima ombaomba, Yesu anatufundisha kuwa wajibu wetu wa kutoa msaada kwenye hali ya udharura haina ukomo. Je, utamwomba Roho Mtakatifu aufanye moyo wako uendane na mapenzi ya Mungu?

 

  1.   Juma lijalo: Elimu Katika Sanaa na Sayansi.