Somo la 7: Pumziko, Uhusiano, na Uponyaji

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Mwanzo 42-46, 50
Swahili
Year: 
2021
Quarter: 
3
Lesson Number: 
7

Somo la 7: Pumziko, Uhusiano, na Uponyaji

 

(Mwanzo 42-46, 50)

 

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Juma lililopita tulijifunza juu ya mparanganyiko katika familia ya Yusufu na matokeo ya kutisha ya huo uhusiano mbaya. Yusufu anapata mateso, lakini Mungu anambariki. Baraka ya Mungu inaweza isiwe dhahiri sana kwa mtazamaji wa kawaida. Lakini, tunauona mkono wa Mungu katika maisha ya Yusufu. Ni kwa jinsi gani mtu mwenye haki, kama Yusufu, ataonyesha hisia zake kwenye uovu wa makusudi na wa kutisha dhidi yake? Inamaanisha nini kusamehe kweli kweli? Tunawezaje kuingia mahali tunaposamehe na kupata pumziko? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

  1.    Yusufu na Nduguze
    1.    Soma Mwanzo 42:1-2. Yakobo ni mtu mwenye utajiri mwingi. Anawezaje kuzungumzia habari za kufa wakati ana ng’ombe wengi sana? (Maneno haya machache yana mambo mengi sana ndani yake. Wanawe wamepigwa butwaa sana kutokana na mabadiliko ya ghafla ya utajiri kiasi kwamba wanakaa tu pale huku wakikodoleana macho, wasijue nini cha kufanya.)
    1.    Soma Mwanzo 42:3-5. Ni nini kilichokuwa chanzo cha madhara ambacho Yakobo alikiogopa kwa Benyamini?
      1.    Unadhani Yakobo ana mashaka juu ya kifo cha Yusufu?
    1.    Soma Mwanzo 42:6. Je, hii inakukumbusha juu ya ndoto zozote zilizotokea huko nyuma? (Angalia Mwanzo 37:5-8. Sasa unasema kuwa nani aliyempa Yusufu ndoto?
    1.    Soma Mwanzo 42:7. Kama ungekuwa Yusufu, ungewaambia nini ndugu zako? Je, ungejisikia msamaha moyoni mwako?
    1.    Soma Mwanzo 42:8-11. Utaona kwamba kifungu cha 9 kinahusisha ndoto za Yusufu na madai yake kwamba wao ni wapelelezi. Unaona mantiki gani katika hili? (Bado ndoto hazijatimia. Ndoto ya pili ilionyesha familia yake yote ikiinama chini. Hivyo, yusufu anaweza kuwa anafikiria jinsi anavyoweza kufanya ili familia yake yote iende Misri.)
      1.    Kaka wakubwa wa Yusufu walifanya nini ili ndoto za Yusufu zisiweze kutimia? (Kile kile walichokitenda ili kufanya ndoto zake zisitimie, kumuuza utumwani, ndio chanzo za utimilifu wa ndoto zake!)
      1.    Je, wao ni “watu wa kweli,” kama wanavyosema katika kifungu cha 11? (Hawakuwa wapelelezi.)
    1.    Soma Mwanzo 42:12-14. Je, Yusufu anashawishika kulipiza kisasi? Je, angekuwa anatenda haki kuwatupa ndugu zake wote gerezani kwa kadiri ambavyo naye alikuwa gerezani?
    1.    Soma Mwanzo 42:15-17. Una maoni gani kuhusu njia hii ya kutafuta uthibitisho? Itakuwa vigumu kiasi gani kwao kuthibitisha kuwa wao si wapelelezi? (Sina uhakika jaribu hili linathibitisha kitu gani. Kama walikuwa wanadanganya, wangeweza kumleta mtu yeyote mwenye umri mdogo kama “ndugu yao mdogo.” Jaribu hili linaleta mantiki kwa sababu Yusufu anaujua ukweli.)
      1.    Vijana walipokuwa korokoroni, unadhani walijadiliana tatizo la dhahiri lililopo kwenye “jaribu” hili?
    1.    Soma Mwanzo 42:18-20. Yusufu anarekebisha jaribu. Hataki wote wasalie gerezani, isipokuwa mmoja anayekwenda kumchukua ndugu yao mdogo. Kwa nini anabadilisha jaribu? (Ninaona pambano likiendelea moyoni mwake. Mwelekeo wake wa kwanza ulikuwa ni kuwafunga wote gerezani isipokuwa mmoja hadi Benyamini aje. Lakini, anatulia na kumwacha mmoja wao pekee gerezani.)
      1.    Tunajifunza nini katika badiliko la moyo wa Yusufu? (Hata mashujaa wakuu wa imani wanapambana na ulipizaji kisasi.)
      1.    Kwa nini Yusufu anachagua jaribu hili? (Anataka kujua uhusiano wao na ndugu yake mdogo.)
      1.    Kwa nini Yusufu anawaita kuwa ni wapelelezi, akiapa kwa jina la Farao (“kama aishivyo Farao”), na kuwafunga gerezani? (Anawapa kionjo cha maisha yake ya zamani aliyoyaishi Misri.)
    1.    Soma Mwanzo 42:21-22. Kwa nini ndugu hawa wanahusianisha jinsi walivyomtendea Yusufu na maswahibu yanayowapata sasa? (Walikumbushwa habari za Yusufu kutokana na amri ya kumpeleka Benyamini Misri. Hii inaonyesha kuwa bado wana dhamiri za hatia.)
    1.    Soma Mwanzo 42:23-24. Kama ungekuwa Yusufu, Reubeni aliposema “kwa hiyo damu yake inatakwa tena,” je, ungeshawishika kusema “Uko sahihi! Ulipizaji unakuja sasa hivi?”
      1.    Badala yake, Yusufu analia. Kwa nini?
      1.    Ndugu hawa wanapata mwelekeo? Sasa, mmoja wao pekee ndiye yuko gerezani. Kwa nini Yusufu alimchukua Simeoni? (Maoni ya Biblia ya Wycliffe yanasema kuwa kwa kawaida Simeoni alikuwa mkatili sana kati ya ndugu zake wote. Angalia Mwanzo 49:5-7 kwa uthibitisho zaidi kuhusu kawaida hii.)
        1.    Ikiwa maoni haya yako sahihi, hii inatufundisha nini kuhusu msamaha?
    1.    Soma Mwanzo 42:25-28. Kuna ubaya gani kurejeshewa fedha zako? Kufanya ununuzi Misri inahitaji kufanya majadiliano juu ya bei kweli kweli! (Tayari walishatuhumiwa kutokuwa waaminifu. Hii inaweza kuchukuliwa kama ushahidi.)
      1.    Kwa nini ndugu hawa wanahusianisha matatizo yao na Mungu?
    1.    Ndugu hawa wanakwenda nyumbani, wanaelezea hali ilivyokuwa kwa baba yao Yakobo. Hataki kuwaruhusu wamchukue Benyamini na hawarejei hadi hali yao ya chakula inapokuwa mbaya zaidi. Soma Mwanzo 43:15-18. Unaichukuliaje hofu yao? (Wana hofia kuwatokea kile walichomtendea Yusufu! Watakuwa watumwa.)
    1.    Soma Mwanzo 43:26-31 na Mwanzo 43:33-34. Kwa nini Yusufu alitoa maelekezo kwamba Benyamini apewe chakula kingi zaidi? (Alitaka kuona ndugu zake wataonyesha hisia gani kwenye upendeleo.)
    1.    Yusufu anatoa maelekezo kwa msimamizi wake kuwapatia ndugu zake nafaka, kuwarejeshe tena fedha zao, na kuweka kikombe chake cha kifalme kwenye gunia la nafaka la Benyamini. Baada ya kuondoka, Yusufu anamtuma msimamizi kuwakamata na kuwashutumu kwa wizi. Kikombe kinapatikana kwenye gunia la Benyamini, na wanalazimishwa kurudi. Inaonekana kama Benyamini anaweza kuuawa na ndugu wengine kuwekwa utumwani, lakini adhabu inapunguzwa na kuwa ya utumwa kwa Benyamini pekee. Hebu rejesha saa nyuma, kama huyu angekuwa Yusufu na ndugu zake wakati Yusufu alipokuwa na umri wa miaka 17, ndugu zake wangesema nini? (Vyema! Mchukue kutoka mikononi mwetu.)
    •    Soma Mwanzo 44:30-33 ili kuona anachokisema Yuda kuhusu kumwacha nyuma Benyamini. Mambo yamebadilikaje?
      1.    Unadhani kitu gani kingetokea kama ndugu hawa wangeridhika kumwacha nyuma Benyamini?
        1.    Je, Yusufu angewasamehe kama wangekuwa hawajabadilika?
  1.   Yusufu Anasamehe
    1.    Soma Mwanzo 45:1-7. Angalia kile anachokisema Yusufu kuhusu mpango wa Mungu kwa ajili ya maisha yake na maisha ya familia yake. Je, Yusufu ana uchungu mkubwa kuhusu miaka 13 aliyoitumia utumwani na gerezani?
      1.    Vipi kuhusu wewe? Je, umefikia hatua aliyoifikia Yusufu? Je, unaweza kuuona mkono wa Mungu ukitenda mambo mazuri na mabaya maishani mwako?
      1.    Unaona uhusiano gani katika Mwanzo 45:7 kati ya Yusufu na Yesu? (Utaona kwamba Yusufu anaona taswira pana zaidi – watu wa Mungu wanahifadhiwa/wanatunzwa kwa ajili ya siku zijazo.)
    1.    Yusufu anaikaribisha familia yake Misri, ndugu zake wanakwenda nyumbani na kumweleza Yakobo habari njema sana kwamba Yusufu ndiye mtawala wa Misri. Soma Mwanzo 45:25-46:4. Kwa nini Mungu anaruhusu jambo hili wakati anajua kuwa uzao wa Yakobo watakuwa watumwa nchini Misri?
    1.    Yakobo anafariki na nduguze Yusufu wanaogopa. Soma Mwanzo 50:15-19. Yusufu anasema nini anapouliza kama yeye ni “badala ya Mungu?”
      1.    Hii inatufundisha nini kuhusu msamaha? (Dhambi hutendwa dhidi ya Mungu.)
    1.    Soma Mwanzo 50:20-21. Yusufu anaonyesha mtazamo gani kwa nduguze? (Msamaha.)
    1.    Soma Waefeso 4:32, Mathayo 6:14-15, na Luka 23:34. Je, tunatakiwa kuwasamehe watu kabla hawajaomba msamaha? (Kwa mahsusi Yesu alifanya hivyo. Mtazamo wa msamaha haugeukii kile mtu mwingine anachokifanya.)
    1.    Rafiki, wakati mwingine maisha hayaendi kama tunavyotaka yaende. Nyakati zingine watu wanatutendea mambo ya kutisha. Fundisho tunalolipata kutokana na maisha ya Yusufu ni kwamba tunatakiwa kumtumaini Mungu na kuwa na huruma kwa maadui zetu. Tunatakiwa kusamehe. Watu wengine wanaweza kudhamiria kutudhuru, lakini Mungu anaweza kubatilisha kila dhamira ovu. Je, utakubali kumtumaini Mungu na kuwa na mtazamo wa msamaha?
  1. Juma lijalo: Huru Kupumzika.