Somo la 2: Fundisho la Musa la Historia

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Kumbukumbu la Torati 1-3
Swahili
Year: 
2021
Quarter: 
4
Lesson Number: 
2

Somo la 2: Fundisho la Musa la Historia

(Kumbukumbu la Torati 1-3)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, wewe ni mwanafunzi wa historia? Ikiwa jibu ni, “hapana,” unatakiwa kuanza kujifunza historia! Tuna mchungaji mpya kanisani kwangu ambaye alizaliwa nchini Cuba. Baba yake pia alikuwa mchungaji na aliteswa na serikali ya Cuba kwa kuyatenda mapenzi ya Mungu na kupeleka injili kwa watu wengine. Mchungaji wetu mpya anaifahamu historia hii vizuri sana. Anapoona vitisho juu ya uhuru wetu kutoka kwa watu wenye mawazo kama ya viongozi wa Cuba, anapatwa wasiwasi mkubwa. Sehemu ya historia tunayotakiwa kuifahamu ni historia ya watu wa Mungu. Musa aliamini kuwa historia ilikuwa ya msingi na anaanza nayo juma hili. Hebu tuzame kwenye somo letu la historia ya Kibiblia!

  1.    Mwanzo Mpya
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 1:3. Mungu anawapatia ujumbe gani watu wa Mungu? (Ujumbe kutoka kwa Mungu unaohusu kile ambacho Mungu aliwataka wakifanye.)
      1.    Zingatia tarehe. Ni tarehe gani? (Siku ya kwanza ya mwezi wa kumi na moja ya mwaka wa arobaini.)
    1.    Soma Hesabu 20:1. Miriamu alifariki lini? (Mwezi wa kwanza. Kwa kulinganisha sehemu iliyosalia ya sura hii na kifungu chetu kinachofuatia tunajua kwamba huu ulikuwa mwaka wa arobaini.)
    1.    Soma Hesabu 33:38. Haruni alifariki lini? (Siku ya kwanza ya mwezi wa tano wa mwaka wa arobaini.)
      1.    Miriamu alifariki katika mwezi wa kwanza wa mwaka huo, Haruni alifariki mwezi wa tano wa mwaka huo, na sasa Musa anatoa ujumbe wake wa mwisho katika mwezi wa kumi na moja wa mwaka huo. Unadhani watu walichukuliaje mambo haya?
    1.    Soma Hesabu 14:34-35. Ni nini lilikuwa tatizo la watu wa Mungu miaka arobaini iliyopita? (Hawakumtumaini Mungu.)
      1.    Watu wanapaswa kuhitimisha nini kuhusiana na kile kinachotokea katika mwaka wa arobaini? (Mungu ni wa kutumainika. Anatimiza neno lake. Mwishoni mwa miaka arobaini wale walioshindwa kumtumaini Mungu wanakufa na uzao wao sasa unajiandaa kuingia Kaanani.)
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 1:8. Kama ungekuwa mwanafunzi wa historia, na ungekuwa miongoni mwa watu wa Mungu, ungefanya nini? (Kumtumaini Mungu. Nisingetenda kosa lile lile kama walilolifanya babu zangu waliofariki. Ningeichukua na kuimiliki nchi.)
  1.   Historia ya Uongozi
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 1:9-10 na Kumbukumbu la Torati 1:12-13. Musa alimtumaini nani katika kuwachagua viongozi wenye busara? (Watu. Viongozi hawakuwachagua viongozi wengine. Watu ndio waliowachagua.)
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 1:14-16. Baada ya watu kuwachagua viongozi, Musa alifanya nini? (Aliwapangilia na kuwapatia maelekezo.)
      1.    Hilo linatufundisha nini, ikikwa fundisho lipo, kuhusu ushirika wa kanisa katika zama za leo?
  1. Historia ya Uongozi Ulioshindwa
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 1:19-21. Watu walipaswa kujibuje amri hii ya kumiliki nchi? (Walipaswa kujibu “Ndiyo!” Fikiria tofauti ambayo ingefanywa kwenye maisha ya wale watumwa ambao punde tu walikuwa wamewekwa huru. Badala yake, walifariki jangwani, jambo ambalo Musa alilielezea (katika kifungu cha 19) kama “kubwa la kutisha.”)
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 1:22-23. Musa anakumbuka kuwa alikubaliana na hili pendekezo la upelelezi. Je, unakubaliana kwamba hilo lilikuwa jambo sahihi kulifanya?
      1.    Ikiwa sivyo, kwa nini hukubaliani? (Mungu alikuwa anawaongoza. Alikuwa akiwaongoza kupitia jangwani. Hawakuhitaji hizi taarifa za ziada.)
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 1:24-26. Tunaweza kuona baada ya utambuzi kwamba kuwatuma wapelelezi lilikuwa wazo baya. Hebu jiulize, je, kuna sababu yoyote kwa nini walipaswa kudhani kuwa lilikuwa wazo baya? Hapo awali nilipendekeza kuwa hawakuwa na haja ya taariza za ziada. Lakini, je, taariza za ziada huwa ni jambo baya?
      1.    Angalia tena Kumbukumbu la Torati 1:25. Taarifa ambazo wapelelezi walizileta zilithibitisha tu kile ambacho Mungu alikiahidi. Kwa nini wahitaji uthibitisho huo?
      1.    Ni ishara ipi ndogo inayoonyesha kwamba hawakumtumaini Mungu kama walivyopaswa kumtumaini?
    1.    Soma tena Kumbukumbu la Torati 1:22 na usome Kumbukumbu la Torati 1:28. Je, taarifa hii inaendana na jukumu walilopewa wapelelezi? (Ndiyo. Walitakiwa kuangalia “habari za njia itupasayo kuipandia, na za miji tutakayoifikia.”)
      1.    Tunapaswa kujifunza nini kutokana na hili? (Mungu ameonyesha kuwa yeye ni mvumilivu. Lakini, kama tutakuwa na busara tutakuwa makini katika mipango yetu ili kuepuka matendo yanayoshindwa kuonyesha tumaini (imani) katika kile ambacho Mungu ametuamuru kukifanya.)
    1.    Musa anawakumbusha historia ya uasi na sababu ya kukaa kwao jangwani kwa miaka arobaini. Soma Kumbukumbu la Torati 1:37-38. Musa anaonyesha uwezo gani wa kiuongozi? (Anakiri kosa lake. Hawalaumu watu wengine. Anamsaidia mtu atakayechukua nafasi yake. Hajaribu kumhafifisha.)
  1.   Kupatia kwa Usahihi
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 2:24-25. Mungu anafanyaje kazi kwa kushirikiana na watu wake? (Anawaambia watu wasonge mbele. Mungu anapandikiza “utisho na hofu” kwenye mioyo ya wapinzani wao.)
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 2:26-28. Je, hii ni njama? Hila? (Soma Kumbukumbu la Torati 2:29. Israeli ilipita kwa amani katika nchi za Seiri na Moabi. Ujumbe unasema kuwa hatima yao ni kupita hapo hadi kufika Yordani. Hivyo, ninadhani wangepita kwa amani kupitia nchi ya Mfalme Sihoni. Mungu alijua Mfalme Sihoni angekuwa mkali na asingekubaliana na hili ombi lenye mantiki.)
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 2:32-34. Hakuna manusura aliyebaki hai. Unapatanishaje hilo na Mungu mwenye upendo tuliyemjadili juma lililopita?
      1.    Soma Mwanzo 15:16. Haya ni maneno yaliyotolewa na Mungu kwa Ibrahimu kuhusiana na ushindi wa Kaanani. Hii inatuambia kuwa Mungu anafanya nini? (Juma lililopita tulijadili kwa kuzingatia Gharika. Juma hili tumepitia hukumu aliyoitoa Mungu kwa wale waliokufa jangwani badala ya kuingia Kaanani. Huu ni mfano mwingine wa hukumu ya Mungu kutekelezwa. Mfalme Sihoni angeweza kuwaruhusu watu wa Mungu wapiti bila matatizo yoyote.)
      1.    Soma Isaya 55:6-9. Hii inatuambia nini kuhusu malengo ya Mungu kwetu na uwezo wetu wa kumwelewa Mungu kikamilifu? (Mungu anatutaka tumgeukie kwa ajili ya msamaha. Mungu ana huruma kwa waovu na wasio na haki. Wakati huo huo tunatakiwa kuzitumaini hukumu za Mungu kwa kuwa mawazo yake na njia zake zi juu ya mawazo na njia zetu.)
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 3:1-2 na Kumbukumbu la Torati 3:4-5. Kuna jambo gani lisilo na kifani kuhusu kuitwaa miji yote hii? (Soma Kumbukumbu la Torati 1:28. Miji hii iliyozungukwa na kuta kubwa ilikuwa mojawapo ya sababu kubwa ya watu wa Mungu kukataa kuingia miaka arobaini kabla. Sasa, wanaonekana kuishinda kiurahisi miji yenye ulinzi mzuri iliyozungukwa na kuta kubwa.)
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 2:10-11 na Kumbukumbu la Torati 3:11. Mojawapo ya maoni ya Biblia yanatuambia kuwa kitanda hiki kilikuwa na ukumwa wa futi 13.5 x 6 au mita 4 x 1.8 na kilitengenezwa kwa chuma! Mtu huyu ana urefu kiasi gani? (Isipokuwa tu kama alipenda kitanda kirefu, mtu huyu alikuwa na urefu wa futi kumi na mbili!)
      1.    Angalia tena Kumbukumbu la Torati 1:28. Watu kama Mfalme Ogu ndio watu ambao wapelelezi walitoa taarifa zao. Miji yenye kuta iliyolindwa na watu wenye urefu unaofikia futi kumi na mbili! Ni matatizo gani maishani mwako yaliyo magumu kiasi cha Mungu kushindwa kuyashughulikia?
    1.    Rafiki, historia ya Biblia inatufundisha nini? Inatufundisha kumtumaini Mungu. Inatufundisha kuwa kumkataa Mungu ni jambo baya sana. Inatufundisha kuwa Mungu anawawazia baraka kubwa wale walio waaminifu kwake.
  1.    Juma lijalo: Agano la Milele.