Somo la 11: Kumbukumbu la Torati Katika Maandiko Yaliyofuata

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
2 Wafalme 22, Mika 6
Swahili
Year: 
2021
Quarter: 
4
Lesson Number: 
11

Somo la 11: Kumbukumbu la Torati Katika Maandiko Yaliyofuata

(2 Wafalme 22, Mika 6)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, huwa unapenda kunukuliwa? Ninachukulia kwamba hii ni namna chanya, tofauti na kunukuliwa kwa jambo ambalo usingepaswa kulisema! Kwa ujumla, pale unaponukuliwa hiyo inaonyesha kuwa ulichokisema ni cha muhimu. Kinaweza kutumika kunufaisha maisha ya watu wengine. Wanataaluma wengi huandika makala kwenye majarida (journals) kwa ajili ya wanataaluma na umma kwa ujumla. Kama makala yako inanukuliwa na watu wengine, hiyo inaonyesha thamani ya makala yako halisi (original). Je, unafahamu kwamba Agano la Kale linafanya vivyo hivyo? Mara nyingine waandishi waliofuatia huwanukuu waandishi wa zamani wa Biblia. Juma hili tunazigeukia kauli zilizotolewa katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambazo zinanukuliwa kwingineko katika Agano la Kale. Kama jambo fulani katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati kinastahili kujitokeza mara ya pili kwenye Biblia, basi lazima jambo hilo litakuwa la muhimu! Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tuzichambue baadhi ya nukuu hizi kutoka kwenye kitabu cha Kumbukumbu la Torati!

  1.    Utambuzi/Ugunduzi
    1.    Soma 2 Wafalme 22:3-5. Jambo gani linatendeka kwenye “nyumba ya Bwana” (hekalu)? (Inakarabatiwa.)
    1.    Soma 2 Wafalme 22:6. Je, wanalirekebisha tu hekalu? Kufanya marekebisho madogo madogo? (Hii si kazi ndogo. Ukarabati unahitaji mbao mpya na mawe. Huu unaonekana kama ukarabati mkubwa.)
    1.    Soma 2 Wafalme 22:8-10. Kitu gani kilionekana wakati wafanyakazi wakifanya ukarabati? (“Kitabu cha Torati.”)
      1.    Unadhani waliopata kitabu walidhani kuwa ni cha muhimu? (Ndiyo. Sio tu kwamba Kuhani Mkuu anakichukua, bali anapewa msaidizi wa Mfalme na Mfalme – ambaye anatambua kile ambacho kitabu inakizungumzia.)
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 31:24-26. Kifungu hiki kinasema kuwa Kitabu cha Torati ni kipi? (Kumbukumbu la Torati!)
      1.    Inawezekanaje Kitabu cha Torati kipotee hekaluni? (Badala ya kupotea kutokana na uzembe, baadhi ya watoa maoni wanaamini kuwa watu wa Mungu walipokuwa wanaongozwa na wafalme waovu waliomkataa Mungu baadhi ya makuhani walikificha kitabu cha Kumbukumbu la Torati ili kiwe salama.)
      1.    Unadhani walipata nakala halisi ya kitabu cha Kumbukubu la Torati? (Hii inaashiria kuwa inawezekana ilikuwa nakala halisi iliyohifadhiwa pamoja na sanduku la agano.)
    1.    Soma 2 Wafalme 22:11-13. Kwa nini Mfalme Yosia amefadhaika sana? Je, haipaswi kuwa furaha kubwa kupata kitabu cha Kumbukumbu la Torati kilichopotea? (Majuma mawili yaliyopita tulijadili ahadi na vitisho vilivyopo katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati sura ya 28-30. Bila shaka Mfalme Yosia alikisoma kitabu hiki na kutambua kuwa hawakuwa watiifu. Utaona kuwa kifungu cha 13 kinarejelea “hasira kubwa” kutokana na kutomtii Mungu.)
    1.    Soma 2 Wafalme 23:1-2 na uilinganishe na Kumbukumbu la Torati 31:10-12. Mfalme Yosia alikuwa anasahihisha jambo gani? (Kitabu cha Kumbukumbu la Torati kilisomwa hadharani kila baada ya miaka saba. Mfalme Yosia alikuwa anafidia usomaji ambao haukufanyika kwa muda mrefu!)
    1.    Soma 2 Wafalme 23:3-5. Ni yepi yaliyokuwa matokeo ya kusoma kitabu cha Kumbukumbu la Torati? (Mfalme Yosia pamoja na watu wake waliahidi kuwa watiifu. Waliondoa sanamu kutoka hekaluni na kuwafukuza kazi makuhani walizitolea sanamu sadaka.)
      1.    Watu wa Mungu wanawezaje kutangatanga mbali sana kiasi cha kudhani kwamba kuwepo kwa sanamu hekaluni lilikuwa jambo sahihi kulitenda?
    1.    Kisa hiki kinatufundisha nini juu ya umuhimu wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati maishani mwetu? Je, unakisoma angalau mara moja kila baada ya miaka saba?
      1.    Kitabu hicho kinatuambia nini juu ya umuhimu wa kusoma na kujifunza Biblia yote?
  1.   Umefunguliwa Mashtaka
    1.    Soma Mika 6:1-2. Je, umewahi kumsikia mtu “akishtakiwa?” Hiyo inamaanisha nini? (Katika mfumo wa sheria wa Marekani inamaanisha mashtaka ya jinai yametolewa dhidi ya mtu fulani.)
      1.    Ni nani anayeshtakiwa hapa? Na wanashtakiwa na nani? (Watu wa Mungu wanashtakiwa na Mungu.)
      1.    Ni nani atakayesikiliza kesi hii ya Mungu dhidi ya Watu? (Milima na vilima!)
        1.    Ni kwa jinsi gani uchafu uliolundikana unaweza kuwa hakimu? (Hauwezi. Dhana iliyopo ni kwamba milima ni vitu visivyobadilika.)
    1.    Soma Mika 6:3. Hili ni shtaka la namna gani? Linajumuisha maswali mawili?
      1.    Unadhani Mungu anasema nini kwenye maswali haya? Anapazia sauti malalamiko gani? (Swali la kwanza linauliza juu ya Mungu kuwadhuru watu. Swali la pili linauliza juu ya Mungu kuwakera au kuwasumbua watu. Mashtaka ni kwamba watu wanamtendea Mungu kana kwamba ni mdudu mharibifu.)
      1.    Je, Mungu anasema kuwa watu wana mtazamo mbaya dhidi yake?
    1.    Soma Mika 6:4-5. Unadhani Mungu anadhani kuwa jibu gani linastahili kwenye maswali yake? (Hajawadhuru. Amewatendea mema tu. Mungu amewaokoa kutoka utumwani. Amewapatia viongozi wazuri. Amewakinga dhidi ya vita vya kiroho.)
      1.    Chukulia kwamba wewe ni mlima. Unatoa hukumu gani kwenye mashtaka yaliyoletwa na Mungu? (Tukitafakari juu ya kile ambacho Mungu amekitenda kwa watu wake, ni vigumu kuchukuliwa kama mdudu mharibifu. Badala yake, yeye ni baraka daima.)
    1.    Soma sehemu ya mwisho ya Mika 6:3. Mungu anadai nini katika kujibiwa mashtaka yake? (Anataka jibu. Anataka watu wake watafakari mtazamo wao.)
    1.    Soma Mika 6:6-7. Tuchukulie kwamba hili ndilo jibu la watu na kwamba Mungu hazungumzii juu ya kila jambo. Unalielewaje jibu hili? (Unaweza kulielewa hili kama watu wakisema kuwa watafanya jambo lolote ili kumfurahisha Mungu, au unaweza kulielewa kama watu wakisema “Haiwezekani wewe kupendezwa!” “Tunaweza kufanya chochote unachokitaka na bado usiwe na furaha.”)
      1.    Je, kweli watu wanamjua Mungu? (Hawazungumzii juu ya kutoa kafara “mzaliwa wao wa kwanza” kama wangekuwa na haja ya kumfurahisha Mungu. Rejea hii inanifanya nifikiri kuwa uwezekano mkubwa ni kwamba watu wanatoa jibu la kejeli – kamwe hatuwezi kukufurahisha wewe Mungu.)
    1.    Soma Mika 6:8. Mungu anawaomba nini watu wake? Anataka kushughulikia kesi gani dhidi ya watu wake?
      1.    Unaona tofauti gani ya msingi kati ya ofa (offer) ya watu na ombi la Mungu? (Watu wanazungumzia kafara. Mungu anazungumzia matendo.)
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 10:12-13. Je, Mika anaelezea kwa ufupi kitabu cha Kumbukumbu la Torati? (Hii inaonekana kufanana sana na kitabu cha Kumbukumbu la Torati.)
      1.    Je, kitabu cha Kumbukumbu la Torati kinajumuisha mahitaji ya ziada? (Kinazungumzia juu ya kuzitii amri. Lakini, utaona kwamba kinasema kuwa amri zinatolewa kwa manufaa ya watu. Dhana iliyopo ni kwamba hiki si kitu unachompatia Mungu, bali unajipatia wewe mwenyewe.)
    1.    Angalia tena Mika 6:8. Je, hili ni gumu kulitenda? Linalinganishwaje na kile ambacho watu walikuwa wanakisema katika Mika 6:6-8? (Ni rahisi zaidi na lina mantiki zaidi.)
      1.    Hebu tuangalie kila moja ya huu wajibu. Inamaanisha nini “kutenda haki?” (Usiwapendelee watu.)
      1.    Inamaanisha nini “kupenda rehema?” (Kufurahia kuwatendea watu wengine mambo mema. Uwe na huruma.)
      1.    Inamaanisha nini “kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako?” (Hili linaweza kuwa na changamoto. Uelekeo wa maisha yako unaendana na mapenzi ya Mungu. Ingawa kitabu cha Kumbukumbu la Torati kinaahidi baraka kwa kutenda hili, unapewa wito wa kuwa mnyenyekevu kuhusiana na baraka zako.)
      1.    Hebu tuliangalie hili kwa mtazamo “mpana zaidi.” Hapa uko nje ya mapenzi ya Mungu, unapaswa kufanya nini? Je, unapaswa kutoa kafara? Je, unapaswa kujipigapiga juu ya dhambi za nyuma? Au, unapaswa kuamua kufanya vizuri zaidi katika siku zijazo?
    1.    Rafiki, sehemu za nukuu za kitabu cha Kumbukumbu la Torati tulizojifunza juma hili zinahusiana na kuwa na uhusiano chanya na Mungu. Mungu anataka uhusiano wa aina hiyo na wewe. Anachokitaka Mungu kitayabariki maisha yako. Kwa nini usijitoe, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kuwa na uhusiano wa namna hiyo katika siku zijazo?
  1. Juma lijalo: Kumbukumbu la Torati Katika Agano Jipya.