Somo la 13: Ufufuo wa Musa

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Kutoka 2 & 17, Hesabu 20, Kumbukumbu la Torati 34, Yuda 1
Swahili
Year: 
2021
Quarter: 
4
Lesson Number: 
13

Somo la 13: Ufufuo wa Musa

(Kutoka 2 & 17, Hesabu 20, Kumbukumbu la Torati 34, Yuda 1)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, wewe ni mtu uliye na ndoto na malengo maishani mwako? Je, ulikuwa na ndoto hizo na malengo hayo ulipokua mdogo, lakini kwa sasa hunavyo tena? Kama ulikuwa nazo ulipokuwa mdogo, na mambo hayakukuendea vizuri, ulijisikiaje? Fikiria kwamba Mungu anakujia akiwa na lengo kubwa, na unakubali kusaidia. Kimsingi, unaamini kuwa ulizaliwa ili kutimiza hili lengo. Isivyo bahati, unafanya makosa kadhaa na sasa ndoto yako iko hatarini. Kosa la kwanza ulilitenda ulipokuwa bado mdogo, na kosa jingine linatendeka sasa hivi wakati unakaribia kabisa kuifumbata ndoto yako. Ikiwa umekabiliana na masikitiko yaliyotokana na mvumburuko wa ndoto, basi somo hili ni kwa ajili yako. Hebu tuzame kwenye somo letu la mwisho katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati na tuangalie jinsi Mungu mwenye upendo anavyowatendea wale wanaofanya makosa!

  1.    Kosa la Kwanza
    1.    Soma Kutoka 2:10-12. Unadhani Musa alikuwa anawaza nini alipomuua yule Mmisri mwonevu?
      1.    Kwa nini kifungu cha 12 kinatuambia kuwa Musa alitazama huko na huko ili kuona kama kuna mtu alikuwa anatazama?
      1.    Kumbuka kwamba Musa ni kijana wa binti Farao. Je, anajinasibisha na familia yake ya kifalme au familia yake ya Kiebrania?
        1.    Kama unasema kuwa anajinasibisha na familia yake ya Kiebrania, unadhani ndoto yake ni ipi, lengo lake maishani ni lipi? (Kuwakomboa watu wake kutoka utumwani. Mungu amemweka kwenye nafasi ya pekee kwa kumpatia mafunzo ya kijeshi na uongozi ili atimize kazi.)
    1.    Soma Kutoka 2:13-14. Tukio hili linaathirije mtazamo wa Musa wa kutimiza takdiri (destiny) yake? (Bila shaka alidhani kuwa Waebrania watamsaidia. Huu ni ufunuo mchungu.)
    1.    Soma Kutoka 2:15. Kwa nini hii si sehemu tu ya manufaa ya kuwa mwanafamilia ya kifalme? Sheria za kawaida hazihusiki kwako! (Inawezekana hii inaonyesha kuwa Musa hachukuliwi kama mwanafamilia kamili wa familia ya kifalme.)
      1.    Jiweke kwenye nafasi ya Musa karibu na kisima. Unawaza juu ya jambo gani? (Umetoka kutenda kosa kubwa sana maishani mwako. Mustakabali wako umeharibika kabisa.)
    1.    Soma Kutoka 3:9-10. Miaka arobaini imepita tangu Musa aharibu mustakabali wake. Mungu amefungua fursa gani mpya? Ungejibuje kama ungekuwa Musa?
    1.    Soma Kutoka 3:11-12. Kwa nini Musa hairukii fursa ili hatimaye kutimiza ndoto yake?
      1.    Je, unalisikitikia jibu la Musa?
    1.    Soma Kutoka 5:1. Vifungu tulivyoviruka vinaonyesha kuwa Musa anasita sana, lakini anasonga mbele. Je, ndoto yake na lengo lake kuu maishani sasa vimerejea kwenye msitari kwa ajili ya utekelezaji?
  1.   Kosa la Pili
    1.    Soma Hesabu 20:1-3, na Hesabu 20:5. Zingatia kwamba huu ni mwaka wa arobaini ambapo wamekuwa kwenye safari hii. Kama ungekaa chini na Musa na kumuuliza, “Mambo yanakwendaje,” unadhani angejibuje? (Dada yangu amefariki, na watu wananichukia.)
    1.    Soma Hesabu 20:6-8. Mungu anafanya nini kuhusiana na matatizo ya Musa? (Mungu anatoa suluhisho rahisi.)
    1.    Soma Hesabu 20:9-10. Je, unaona tatizo kwa kile alichokisema Musa kwa waasi? (Musa anarejelea kauli ya “sisi” kuwatokezea maji katika mwamba.)
    1.    Soma Hesabu 20:11 na uilinganishe na Hesabu 20:8. Je, Musa amefuata maelekezo ya Mungu? (Hapana. Mungu alimwambia anene na mwamba. Badala yake, aliupiga mwamba mara mbili kwa fimbo yake.)
      1.    Je, watu wanaelewa juu ya kufeli kwa Musa? (Hapana. Maji yalitoka kama ambavyo Mungu aliahidi.)
    1.    Soma Kutoka 17:3 na Kutoka 17:5-6. Mungu anamwambia Musa afanye nini ili kupata maji kutoka mwambani katika hili tukio la awali? (Anamwambia kulipiga jabali.)
      1.    Unachukuliaje kutokutii kwa Musa? (Hakuna mtu hata mmoja anayefahamu kutokutii kwake. Kwa haraka haraka inaonekana kama dosari ya kiufundi – kuupiga mwamba badala ya kusema nao. Jambo la ziada kwa niaba ya Musa ni kwamba katika hali kama hiyo hiyo alielekezwa na Mungu kuupiga mwamba ili kupata maji.)
    1.    Soma Hesabu 20:12. Mungu anasema kuwa Musa na Haruni “hamkuniamini mimi.” Hilo linawezaje kuwa kweli? Walimjia Mungu ili kupata suluhisho kwenye hili tatizo la hivi karibuni kabisa!
      1.    Angalia tena mambo mengine yote ya kile ambacho Mungu anamwambia Musa – kipengele kinachohusu kutomthibitisha Mungu kama mtakatifu mbele ya macho ya watu. Unalielewaje jambo hili wakati watu hata hawajui kuwa Musa alishindwa kufuata maelekezo? Ama kwa hakika, Musa anashughulikia jambo hili kwa namna ile ile ambayo Mungu alimwelekeza hapo kabla wakati watu walipolalamika kuhusu maji.
    1.    Soma 1 Wakorintho 10:4. Paulo anamaanisha nini anaposema kuwa Yesu ni mwamba, ndiye Mwamba utoao maji? (Mungu ndiye aliyekuwa nyuma ya muujiza wa maji kutoka mwambani. Hebu fikiria mazingaombwe ya maji kutoka mwambani.)
    1.    Angalia tena sehemu ya mwisho ya Hesabu 20:12. Musa na Haruni wanapewa adhabu gani kutokana na dhambi hii? (Njozi ya Musa imekufa. Hataona lengo la juhudi zake zote kubwa. Ana afya njema (Kumbukumbu la Torati 34:7), lakini Mungu hataruhusu hilo litokee.)
      1.    Unadhani Musa alijiuliza kwa nini alizuiwa kuingia katika nchi ya ahadi, lakini waasi waliokuwa wakilalamika wataingia?
    1.    Hebu tupitie maswali yote haya magumu ambayo nimekuwa nikiyauliza kuhusiana na adhabu hii. Unaichukuliaje haki ya Mungu? Maoni ya Paulo juu ya Yesu kuwa “Mwamba” yanatufundisha nini kuhusiana na hali hii? (Mungu anasema kuwa suala lililopo ni kumtumaini Mungu kiasi cha kutosha ili kuthibitisha utakatifu wa Mungu. Kwa kuwa watu hawajui kuhusu maelekezo kamili ya Mungu, hilo si suala la msingi. Badala yake, suala lililopo ni Musa na Haruni kudai kuwa wanaweza kutatua tatizo. Suala lililopo ni kwa wao kufuata njia yao wenyewe ili kutoa maji, kwa kuupiga mwamba. Suala lililopo ni kwamba Musa aliupiga mwamba mara mbili, kana kwamba kuongezea juhudi na nguvu za ziada kutafanya maji yatoke.)
      1.    Je, hii inathibitisha umuhimu wa matendo – kwamba lazima tuwe watiifu ili tuweze kuokolewa? (Baadhi ya watu wanaweza kuangalia jambo hili kama suala la kutokutii. Lakini nadhani suala la ndani zaidi ni kujitumaini badala ya kumtumaini Mungu. Hapa kufeli kwa Musa ni suala la imani na tumaini.)
  1. Mtafaruku
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 34:1 na Kumbukumbu la Torati 34:4. Je, ungejisikia uchungu? Unadhani Musa alijisikia uchungu?
      1.    Je, maisha ya Musa yamefeli na yenye kukatisha tamaa?
      1.    Kwa nini Mungu alimwonyesha Musa nchi? Je, Mungu ni katili? Je, Mungu anataka Musa apate hisia kamili za kufeli kwake?
    1.    Soma Kumbukumbu la Torati 34:5-7. Musa anakufa peke yake. Ana afya njema kabisa. Sababu pekee ya kifo chake ni kosa lake la pili. Huenda alikufa kutokana na kuvunjika moyo. Je, Mungu anatenda haki? Je, unamtumaini Mungu kutenda jambo sahihi?
  1.   Ushindi
    1.    Soma Yuda 1:9 na Mathayo 17:1-3. Mungu anamtendea nini Musa? Anamuingiza katika nchi ya ahadi ya kweli! Mungu anampa Musa thawabu kuu! Musa hapati nafasi ya kuchunguza ishara ya kidunia ya mbinguni (nchi ya ahadi), anakwenda kuishi kwenye kitu halisi. Anakwenda kukaa na Mungu!
      1.    Je, Mungu hana usawa au hatendi haki?
    1.    Hebu tuzungumzie kidogo mfululizo wa matukio haya. Ni yepi ambayo yangekuwa matokeo mazuri kwa Musa? (Kutimiza lengo la maisha yake, kuwaongoza watu kuingia Kaanani, na baadaye kufa na kuchukuliwa mbinguni.)
      1.    Kama tungeiruka dhambi ya Musa, na kisha Mungu akamwambia, “Aisee rafiki, ninakupeleka mbinguni badala ya Kaanani, kule utapafurahia zaidi,” je, hilo lingekuwa sawa kwa Musa?
      1.    Matukio haya ya Musa yanatufundisha nini kuhusu umuhimu wa utiifu kwa amri za Mungu? (Yanatufundisha ukweli ambao ninaendelea kuusisitiza – utii kwa Mungu huyaboresha maisha yako. uUii kwa Mungu huleta utukufu kwa Mungu.
      1.    Matukio haya ya Musa yanatufundisha nini kuhusu kuhesabiwa haki kwa imani pekee? (Hakuna shaka kwamba kwa ujumla Musa alimtumaini Mungu. Musa alifeli kwa kuteleza kwenye suala la kumtumaini Mungu. Kushindwa huko, ambako kulikuwa kukubwa mno kiasi cha kuzuiliwa kuingia Kaanani – lengo la maisha yake – hakukumzuia Musa kuingia kwenye Nchi ya Ahadi ya kweli.)
    1. Rafiki, ikiwa wewe, kama ilivyo kwangu, umewahi kuwa na    maanguko makubwa, basi kisa cha Musa ni hamasisho kubwa. Suala lililopo ni kumtumaini Mungu hata kama unadhani kuwa amekuwa katili sana. Mungu si katili, Yeye ni mkarimu na mwenye upendo! Je, utafanya uamuzi wa kumtumaini sasa hivi?

V.   Juma lijalo: tunaanza mfululizo mpya wa masomo juu ya kitabu cha     Waebrania.