Somo la 4: Yesu, Ndugu Yetu Mwaminifu

Mambo ya Walawi 25, Waebrania 2, 13
Swahili
Year: 
2022
Quarter: 
1
Lesson Number: 
4

Somo la 4: Yesu, Ndugu Yetu Mwaminifu

(Mambo ya Walawi 25, Waebrania 2, 13)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Nimebarikiwa kuwa na ndugu mwaminifu. Vipi kuhusu wewe? Kuna uhusiano mwingi mbaya tena wa kutisha miongoni mwa wanafamilia. Kuna ndugu wa damu ambao hawawezi kuzungumza. Wapo wazazi na watoto wasiopendana. Uhusiano wangu wote wa kifamilia ni mzuri, na ninadhani sababu ya msingi ya uhusiano huu ni kwamba sisi sote tunampenda Bwana. Somo letu juma hili linamhusu Yesu kama Ndugu yetu mwaminifu. Hebu tuzame kwenye somo letu la kitabu cha Waebrania na tujifunze zaidi!

 1.    Ukombozi wa Shamba
  1.    Soma Mambo ya Walawi 25:23. Kulikuwa na kanuni gani ya msingi inayohusu shamba kwa Waebrania wanaoingia Kaanani? (Mungu alimiliki nchi yote. Lakini, watu waliruhusiwa kuwa na haki ya kumiliki inayoendana na hiyo kanuni ya msingi.)
  1.    Soma Mambo ya Walawi 25:24-25. Hapa lengo la msingi la Mungu ni lipi? (Kufanya shamba liendelee kuwa ndani ya familia. Unaweza kuuza na kununua shamba, lakini hatimaye Mungu anataka familia izuie na kumiliki shamba lake.)
   1.    Kwa nini lengo hilo? Vipi kama wanafamilia sio wakulima wazuri sana? (Shamba ndio njia ambayo ungeweza kujitegemeza kimaisha. Kanuni hii inapaswa kuwakinga watu dhidi ya njaa.)
  1.    Soma Mambo ya Walawi 25:26-28. Kama ungekuwa mwekezaji wa shamba, je, sheria hii ni nzuri? (Ungeweza kupoteza fedha kutokana na mazao hafifu, lakini sio kwenye kipande cha ardhi. Kama ardhi ingekombolewa, ungekuwa na matumizi ya ardhi katika kipindi cha mpito na ungerejesha fedha zako zote kwa ajili ya uwekezaji katika miaka ijayo. Nadhani, kivitendo, hii ni sawa na kufupisha mkataba.)
   1.    Vipi kuhusu Jubileii – kurejeshwa kwa shamba kwa mmiliki halisi baada ya miaka 50? Je, hiyo ni haki? (Kama ningekuwa mnunuzi, ningeliangalia jambo hili kama ukodishaji kwa kipindi cha miaka 50, na nisingelipa kiwango kikubwa kama ambavyo ningenunua ardhi ya kudumu.)
   1.    Hebu turejee kwenye swali langu kuhusu wakulima wasio hodari au wavivu kurudishiwa shamba lao baada ya kuliuza. Je, mfumo huu unaonekana kuwa wa haki kwako? Je, unazawadia juhudi na uhodari? (Huu ni mfumo wa kibepari kwa kuwa unaimarisha haki ya kumiliki shamba binafsi. Pia unahamasisha matumizi fanisi ya shamba. Hebu fikiria kupoteza ardhi yako kwa muda wa miaka hamsini! Hiki kitakuwa kichocheo cha kufanya kazi kwa bidii.)
   1.    Kanuni hii inayohusu shamba inatenda nini kwenye uhusiano wa kifamilia? (Inaweka uwajibikaji wa msingi kwa matumisi fanisi ya shamba mikononi mwa familia. Hawa ni watu wanaowaelewa vizuri wahusika.)
 1.   Ndugu Yetu Mkombozi
  1.    Soma Waebrania 2:14-15. Je, Yesu ametukomboa sisi, wanafamilia yake?
   1.    Angalia maneno, “wale ambao....kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa.” Hiyo inamaanisha nini? (Inamaanisha kuwa wanadamu wadhambi hawana haja tena ya kuogopa mauti. Sisi si watumwa tena wa hofu hii.)
  1.    Soma Waebrania 2:17. Unaona uhusiano gani kati ya Yesu kutukomboa na ukombozi wa Kilawi wa shamba? (Dhana inayofanana ni kwamba Yesu, baada ya kuwa mmoja wetu, anaelewa hali yetu vizuri sana. Kwa kuweka ukombozi wa shamba ndani ya familia walioielewa hali vizuri walipewa wajibu wa utatuzi.)
 1. Nje ya Kambi Tukiwa na Yesu
  1.    Soma waebrania 13:12. Inamaanisha nini kwa Yesu kuteseka “nje ya lango?” (Soma Yohana 19:16-17. Yesu alisulubiwa nje ya malango ya Yerusalemu.)
  1.    Soma Waebrania 13:13-14. Utaona kwamba hii inarejelea mambo mawili ambayo tumekuwa tukijifunza: uhusiano wetu wa pekee na Yesu, na haki yetu ya kumiliki mali kwa kumzingatia Mungu. Inamaanisha nini kwa sisi kwenda “nje ya kambi” na Yesu? (Kwamba tutajifunganisha naye badala ya kufifananisha na ulimwengu.)
   1.    Uamuzi huu unahusiana na haki ya kumiliki shamba. Yesu anatuwazia nini? (Hapa hatuutafuti mji, tunaitafuta Yerusalemu Mpya – mji utakaokuja.)
  1.    Soma Waebrania 13:15. Ni njia ipi ya msingi ambayo tunajihusisha na Yesu na sio ulimwengu? (Tunamtukuza Yesu. Tunamkiri Yesu. Hili ni jambo lililonenwa. Ni “tunda la midomo.”)
  1.    Soma Waebrania 13:16. Ni kwa jinsi gani nyingine tunajihusisha na Yesu? (Tunatenda mema na kushiriki kile tulicho nacho.)
   1.    Leo tuna mwelekeo wa watu kuamua kushiriki kile ambacho wengine (ambao wanadhani wanaweza kukimudu) wanacho. Hawa ni watu ambao kwa ujumla hawatoi msaada (charity) vitu vyao vingi, wanataka tu kuwalazimisha watu wengine kutoa vitu vyao. Je, hilo liko ndani ya mawanda (scope) ya kile kinachopendekezwa hapa? (Hapana. Rejea ya “sadaka” inamaanisha kuwa umechangia kutokana na mali yako mwenyewe.)
 1.   Kujifunza Kutoka kwa Ndugu Yetu
  1.    Je, umejifunza jambo chanya kutoka kwa ndugu zako? Mara zote kaka yangu alikuwa mtu mchangamfu sana. Watu wengine walivutiwa naye. Ingawa alikuwa mdogo kwangu, nilijifunza mambo mengi kutoka kwake kwenye eneo la kuwa muwazi na urafiki na watu wengine.
  1.    Soma Waebrania 12:1. “Mashahidi” hawa ni akina nani? (Hii ni rejea ya Waebrania 11 inayonukuu majina ya mashujaa wengi wa Biblia.)
   1.    Kwa nini mashahidi hawa ni wa msaada katika kuweka kando “kila mzigo mzito na dhambi” tulio nao? (Maisha yao yanatutia moyo.)
  1.    Angalia tena Waebrania 12:1. Utaona kuwa “mizigo mizito” maishani inatofautishwa na “dhambi,” na muktadha unakwenda kasi ya “mbio.” Uzito unakutendea nini kwenye mbio? (Unakupunguzia mwendo. Unaweza kukuzuia usimalize mbio.)
   1.    “Mizigo” gani inaathiri utendaji wetu kwenye mbio zetu maishani? (Hii ni mitazamo na hisia zenye madhara. Hizi si dhambi, bali zinatupunguzia tu mwendo.)
   1.    Je, dhambi ni jambo ambalo tunapaswa kujishughulisha nalo? (Ndiyo. Inatudhuru katika mbio yetu maishani.)
  1.    Soma Waebrania 12:2. Tunaweza kujifunza nini kutoka kwa Ndugu yetu Yesu? (Tunao mfano na utiwaji moyo wa mashahidi wa Sura ya 11, na tunao mfano wa “Mwanzilishi na Mtimizaji wa imani yetu!)
   1.    Kifungu hiki kinasema jambo gani mahsusi ambalo tunapaswa kujifunza kutoka kwa Yesu? (Kwamba bila kujali jambo lolote linaloendelea au kutokea maishani, tunapaswa kujikita kwenye furaha ambayo tutakuwa nayo mbinguni.)
   1.    Ninayafurahia maisha. Sifichi ukweli kwamba mimi ni Mkristo. Vipi kuhusu wewe? Je, maisha yako yanakuendea vizuri sana?
    1.    Unadhani watu wangapi wanastahimili jambo kama maumivu na aibu ya msalaba? (Sio watu wengi – angalao sio wengi wasomao somo hili.)
    1.    Kama ungekuwa Shetani, ungefanya nini ili kuwavuruga watu mawazo wasizingatie furaha ya mbinguni? (Mateso yanatufanya tuwe wazingativu. Kuyafurahia maisha kuna uwezekano mdogo wa kutufanya tuwe wazingativu.)
  1.    Soma Waebrania 12:3-4. Waebrania wana hali gani? (Wanapambana na kukabiliana na uasi. Wanakabiliana na hofu ya kweli ya kuzimia mioyo na kuchoka.)
   1.    Je, ushauri huu bado unafaa kwetu leo? (Wakristo wa dhati wanakabiliana na uasi unaozidi kusambaa nchini kwangu. Lakini, tishio hilo sio kubwa kama hili.)
   1.    Waebrania 12:4 inapozungumzia “mapambano yako dhidi ya dhambi,” je, inarejelea dhambi zako binafsi? (Huenda. Angalia vifungu vya Waebrania 12 ambavyo tumevisoma hivi punde. Mwandishi anamrejelea mshindani au adui ambaye tunaweza kukabiliana naye katika mbio. Bila kujali kama mpambano unahusiana na jambo lililo ndani au nje yako, wito ni kusalia kuwa mwaminifu.)
  1.    Rafiki, Yesi ni Ndugu yetu. Ametukomboa kama familia ilivyokomboa shamba katika mfumo wa Kilawi. Ameteseka, kwa ajili yetu, zaidi ya vile tuwezavyo kuteseka. Ameshinda kwa ajili yetu! Je, utakubali kuungana naye leo na kushiriki na wengine utambulisho wako kama ndugu Yake?
 1.    Juma lijalo: Yesu, Mpaji wa Pumziko.