Somo la 2: Anguko

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Mwanzo 3
Swahili
Year: 
2022
Quarter: 
2
Lesson Number: 
2

Somo la 2: Anguko

(Mwanzo 3)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, umegundua kwamba kuna “aina” mbalimbali za personalities? Kwa kusema hivyo ninamaanisha watu wanapenda kuangukia kwenye makundi fulani ya kutafakari juu ya maisha na kuishi. Imani yangu ni kwamba Shetani ni mkuu kwenye mada hii, na ana “mwelekeo wa njia” kwa wale wenye njia kama hizo za fikra na matendo. Hebu tuangalie kama tunaweza kupindua meza juma hili. Kama Shetani ana mipango fulani ya kuhamasisha dhambi, tunapaswa kuona kile tunachoweza kujifunza juu ya njia ya Shetani ili kusaidia kutukinga dhidi ya kuanguka dhambini. Fuatana nami tunapoendelea kuchunguza kwa kina dhana hii katika kitabu cha Mwanzo 3!

    I.     Jaribu la Eva

        A.     Soma Mwanzo 3:1. Je, huyu ni nyoka mwerevu? “Nyoka” ni kitu gani? (Soma Ufunuo 12:9. Huyu si mwingine bali Shetani, mwovu! Anawadanganya wanadamu na tunaiona kazi yake hapa.)

            1.     Kwa nini joka huyu analinganishwa na wanyama wengine? Ni kwa jinsi gani Shetani ni mnyama? (Hitimisho lenye mantiki ni kwamba Shetani amechukua sura ya nyoka. Nyoka hawana uwezo wa kuongea.)

            2.     Kama ungekuwa kocha wa maisha ya Eva, ungeshauri kuwa anapaswa kufanya nini ili kujibu swali hili? (Angeondoka.)

            3.     Unalichukuliaje swali la Shetani? (Kwa jinsi lilivyo ni swali la kipumbavu. Naam, waliweza kula matunda ya miti ya bustani.)

                a.     Hii inatufundisha nini kuhusu njia ya Shetani ya kuwafanya wanadamu watende dhambi? (Lengo la kwanza la Shetani ni kutufanya tushirikiane naye. Kutufanya tujisikie kuwa na hadhi ya juu. Eva alikuwa na ujasiri wa kujibu kwa sababu kwa dhahiri huyu alikuwa ni nyoka asiyejua lolote.)

        B.     Soma Mwanzo 3:2-3. Je, Eva anaelezea kwa usahihi kanuni ya Mungu? (Soma Mwanzo 2:16-17. Mungu hakujumuisha chochote kwenye kanuni yake tofauti na katazo la kula matunda ya miti ya bustani.)

            1.     Utaona kwamba Mungu alitoa kanuni kwa Adamu, na sio kwa Hawa. Unadhani Adamu aliongezea sehemu inayohusu kutokugusa kwa sababu alidhani alikuwa anamsaidia mkewe? Alikuwa anaangalia mustakabali wake kwa kumwambia asithubutu hata kuligusa tunda?

            2.     Soma Kumbukumbu la Torati 4:2. Mungu anasema nini kuhusu kuongezea neno katika neno lake? (Tunaweza kudhani kuwa tunatenda wema kwa wale tunaowalinda kwa kuwasaidia kukaa mbali na dhambi. Lakini kuongezea neno ni ukiukwaji wa amri ya Mungu.)

        C.     Hebu turukie mbele kidogo. Soma Mwanzo 3:6. Eva alifanya nini kabla hajala tunda? (Alitathmini mwonekano wake, na akaligusa.)

            1.     Alipoligusa tunda na hakufa, je, hilo lilimtia hamasa kula tunda? (Ninadhani lilimtia hamasa. Hii inafafanua kosa kubwa la kutia chumvi kile anachokikataza Mungu.)

    II.     Mpango wa Mchezo wa Shetani

        A.     Soma Mwanzo 3:4-5. Hebu tuchambue jinsi Shetani alivyomjaribu Eva. Unadhani kuwa Shetani aliweka mipango makini jinsi atakavyomwingia Eva? (Sina shaka. Sio tu kwamba hili lilikuwa tukio la muhimu sana katika pambano kati ya wema na uovu, lakini hakuna uthibitisho wowote kwamba Shetani alikuwa na uwezo wa kuwafikia Adamu na Eva ili kuwajaribu nje ya tukio hili. Hii inaonekana kuwa kipimo walichokubaliana Mungu na Shetani.)

        B.     Angalia tena Mwanzo 3:3 na usome Mwanzo 2:9. Mwanzo 3 inasema kuwa Mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya umewekwa wapi? (Miti hiyo ipo “katikati” ya bustani. Hii inaashiria kuwa miti hiyo iko sehemu moja katikati ya busatani.)

            1.     Kwa nini? Huu ni ushahidi kwamba Edeni ilitengenezwa kwa uelewa na makubaliano ya pamoja. Hakuna shaka yoyote kwamba Shetani alileta jaribu lake bora kabisa kwenye pambano hili.)

        C.     Hebu turejee nyuma na tusome tena Mwanzo 3:4. Je, kumpinga Mungu ni msingi wa kuingia majaribuni?

            1.     Unapotaka kuwa makini na jaribu, unapaswa kuhitimisha nini unaposikia au kusoma jambo linalokinzana na Biblia? (Unatakiwa uwe makini sana! Hapa ndipo mahali ambapo watu wengi wanaamua kwamba watatumia hekima yao na kufanya uamuzi kwamba nani yuko sahihi. Kosa baya namna gani!)

            2.     Tofauti na neno la Mungu, je, palikuwepo na ushahidi wowote kwamba Shetani alikuwa anadanganya? (Kimantiki Eva hakuamini kwamba hakuwa kiumbe wa kufa kwa sababu ya uwepo wa Mti wa Uzima na ukweli kwamba mara kwa mara (inaonekana hivyo) alikuwa akila matunda ya mti huo. Kwa kujazilizia hoja hii angalia Mwanzo 3:22-24.)

        D.     Soma Mwanzo 3:5. Nina mashaka kama kupingana na Mungu moja kwa moja kungekuwa na mafanikio. Shetani aliongezea nini ili kufanya jaribu lake liwe na ushawishi zaidi? (Alitoa wito wa kutoridhika – atafanana na Mungu. Ulikuwa wito wa njama – Mungu alikuwa anamnyima Eva kitu fulani.)

            1.     Soma Mwanzo 1:27-28. Je, Shetani alikuwa anampatia Hawa kitu ambacho hakuwa nacho tayari? (Tayari alikuwa anafanana na Mungu. Suala la msingi lilikuwa ni kama angeamini uamuzi wa Mungu juu ya hali yake ya uelewa na kama angemtumaini Mungu kwenye suala la adhabu ya kifo.)

                a.     Eva alipokuwa anafanyia kazi suala hili mawazoni mwake, Adamu alifanya nini katika uamuzi wake wa kumlinda Eva kwa kutia chumvi kwenye amri ya Mungu? (Alipogusa tunda na hakufa, alihitimisha kuwa Mungu alidanganya.)

                b.     Tumewadanganya watoto wetu na wanafunzi wa shule za kanisa mambo mangapi linapokuja suala la amri za Mungu?

    III.     Jaribu la Adamu

        A.     Soma Mwanzo 3:6. Kifungu kina utata kuhusu muda ambao Adamu “alikuwa pamoja na Eva.” Je, inawezekana kuwa alikuwa amesimama pembeni mwa Eva wakati Shetani alipoanza kuzungumza naye kwanza? (Inaonekana hilo haliwezekani. Kwa hakika angesema jambo. Kwa hakika wangejadili jambo hili pamoja. Hii pia ingempa Adamu fursa ya kusahihisha kile ambacho kimsingi Mungu alikisema kuhusu kuligusa tunda.)

            1.     Mantiki inaonyesha kuwa Adamu alijitokeza wakati gani? (Wakati Eva alipokuwa anakula tunda. Hakuna kingine chochote kinacholeta mantiki kwa upande wangu.)

        B.     Mwanzo 3:6 haielezei kwa nini Adamu alikula tunda alilopewa na Eva. Soma 1 Timotheo 2:13-14 kwa ajili ya ufafanuzi. Nadhani Paulo anadhamiria kifungu hiki kizungumzie jambo chanya kumhusu Adamu. Je, unadhani hii inatoa maoni chanya au hasi kumhusu adamu?

            1.     Jambo gani ni bora zaidi mawazoni mwako, kutenda dhambi kwa makusudi au kutenda dhambi kwa sababu ulidanganywa?

            2.     Hebu tujadili asili ya jaribu la Adamu. Je, unadhani kuwa kwa makusudi Shetani alimlenga Eva kwanza?

                a.     Ikiwa ndivyo, je, hiyo inamaanisha kuwa Adamu alikuwa na uwezekano mdogo wa kuanguka kwenye udanganyifu wa Shetani?

                b.     Ikiwa ndivyo, hiyo inaashiria nini kuhusu wanandoa wanaokabiliana na jaribu kwa pamoja?

                c.     Anguko la Adamu linatufundisha nini kuhusu mkakati wa Shetani juu ya matumizi ya wale tuwapendao? (Hitimisho lenye mantiki ni kwamba Adamu alimchagua Eva dhidi ya Mungu. Hatupaswi kutenda kosa hilo.)

    IV.     Anguko la Mwanadamu

        A.     Soma Mwanzo 3:9-12. Hivi punde tumejadili kwamba Adamu alianguka kwa sababu hakutaka kumwacha Eva. Hapa Adamu anafanya nini? (Anamlaumu Eva!)

            1.     Kwa nini? Hii ina mantiki yoyote? Ikiwa Adamu alikuwa radhi kuuacha mustakabali wake ili awe na Eva, kwa nini anamwambia Mungu kuwa dhambi ilikuwa kosa la Eva? (Bado dhambi haikuwa halisi kwa Adamu pale alipomchagua Eva. Sasa kwa kuwa ametambua athari za awali, mtazamo wake unabadilika.)

                a.     Je, umetenda dhambi na mtu ambaye ulidhani atasimama pamoja nawe, na kisha ukaona matokeo tofauti kabisa? Je, huo ndio mkakati wa Shetani?

            2.     Adamu anamlaumu nani mwingine? (Mungu! Anasema Mungu alimpatia Eva.)

            3.     Tafakari jambo hili. Kama umesikitika kwa jinsi familia na marafiki wanavyoitikia dhambi zao, tafakari jinsi Adamu, aliyeumbwa akiwa mkamilifu, alivyoitikia.

        B.     Soma Mwanzo 3:13. Eva anamlaumu nani? (Nyoka.)

        C.     Soma Mwanzo 3:14. Hii inaleta mantiki gani? Kama Shetani alichukua sura ya nyoka, kwa nini nyoka anaadhibiwa? (Soma Ufunuo 12:9. Ninadhani kimsingi adhabu hii inaelekezwa kwa Shetani. Anatupwa duniani. Mustakabali wake u pamoja na mavumbi ya nchi.)

        D.     Rafiki, kisa hiki kinahusu kumtumaini Mungu pale tunapokabiliana na jaribu. Mtumaini bila kuongezea chochote kwenye amri zake. Litumaini neno la Mungu wakati watu wengine wanalihoji. Mara zote mtangulize Mungu. Je, utadhamiria, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kuishinda mikakati ya Shetani kwa kumtumaini Mungu?

    V.     Juma lijalo: Kaini na Hiba (Legacy) Yake.