Somo la 3: Kizimba cha Ndege

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Kutoka 14-17, 1 Petro 1
Swahili
Year: 
2022
Quarter: 
3
Lesson Number: 
3

Somo la 3: Kizimba cha Ndege

(Kutoka 14-17, 1 Petro 1)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Nimesoma kisa kinachohusu jinsi kizimba cha ndege kilichofunikwa kinavyomsaidia ndege kujikita kujifunza wimbo mahsusi. Unayafahamu maneno, “akili ya ndege?” Hii sio sifa! Je, watu wanafanana na ndege? Je, wanatakiwa kuwa makini ili kujifunza mafundisho ya msingi? Je, mateso ni njia ya kutufanya tujikite kwenye usikivu wetu? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

  1.    Mtego
    1.    Soma Kutoka 14:1-3. Tunaendelea na safari ya watu wa Mungu wakiondoka Misri baada ya miaka 400 ya kuishi hapo, sehemu ya mwisho wakiishi utumwani. Nani anayeelekeza wapi watu wanapotakiwa kwenda? (Mungu.)
      1.    Farao anapaswa kuhitimisha nini juu ya hekima ya kuondoka kwao? (Wametatanishwa, “wakizurura,” na kimakosa wamechukua njia yenye ukomo.)
    1.    Soma Kutoka 14:4. Kuingia kwenye mtego huu wa dhahiri unamsababisha Farao afanye nini? (Anawafuatilia watu wa Mungu. Kwa dhahiri anataka mkuwarejesha kama watumwa.)
      1.    Nani anawajibika kwa mambo yote haya? (Hitimisho lenye mantiki kutokana na vifungu hivi ni kwamba Mungu ndiye anayewajibika. Hata hivyo, unaweza kupambanua “Nami nitaufanya uwe mgumu moyo wa Farao,” Mungu aliongoza safari ya watu wake, hali iliyomsababisha Farao aamini kuwa walikuwa mtegoni na kwenye hali hatarishi.)
      1.    Mungu anasema kuwa nia yake ni ipi katika jambo hili? (Wamisri watajua kwamna Yeye ni Bwana.)
    1.    Soma Kutoka 14:9-11. Watu wanatoa mwitiko gani kwenye hali hii? (“Wakaogopa sana.” Walitishika!)
      1.    Watu walimgeukia nani? (Mungu na Musa.)
        1.    Jambo gani liliwafanya waombe msaada? (Halikuwa ombi la msaada. Yalikuwa ni malalamiko ambapo walimlaumu Musa.)
    1.    Soma Kutoka 14:12. Je, kweli hivyo ndivyo walivyoliangalia jambo hili? Ikiwa ndivyo, kwa nini waliondoka? (Soma Kutoka 5:20-21. Lilikuwa tatizo la muda mrefu kwamba watu hawakuwa na uelewa mmoja na mpango wa uokozi.)
    1.    Soma Zaburi 23:1-3. Je, kuwa na hofu juu ya mustakabali wao ni jambo ambalo watu walipaswa kulitarajia? Je, hilo ni jambo unalopaswa kjulitarajia?
    1.    Soma Kutoka 14:13-14. Ni kwa jinsi gani Musa anaamini jinsi “maji ya utulivu” yatakavyokuja? (Pale tunapoamua kuwa watazamaji kwenye pambano. Mungu alisema kuwa anathibitisha kwamba yeye ni nani, na kimsingi Musa anasema, “Angalieni tu jinsi mambo yanavyotendeka.”)
    1.    Soma Kutoka 14:15-16. Je, Musa na Mungu hawakubaliani juu ya kinachotakiwa kutendeka? Musa anasema watizame na Mungu anasema waendelee kusonga mbele? (Musa hakuelewa mpango kamili.)
      1.    Je, “kutazama” na “kuendelea kusonga mbele” ni ushauri mzuri kwetu pale tunapoona mustakabali unaoogofya? (Ndiyo. Hilo sio pambano letu, tunatakiwa kufuata maelekezo ya Mungu.)
    1.    Soma Kutoka 14:20-22. Je, hili ndilo suluhisho ambalo watu wa Mungu wangeweza kulibashiri?
      1.    Je, hofu iliyazinga mawazo yao?
      1.    Je, watu walitakiwa kufanya jambo lolote tofauti na kutii?
      1.    Sehemu gani ya ulinzi wao ilikuwa ni jambo lipitalo akili ya kawaida (supernatural)? (Hakuna jambo hata moja lililokuwa ndani ya uzoefu wao. Kwanza, wingu linashuka kati yao na jeshi la Wamisri. Wingu linawatia Wamisri giza na Waisraeli wanapata nuru. Kisha upepo unayagawa maji na kukausha vilindi vya bahari.)
    1.    Soma Kutoka 14:23-25. Wamisri walifikia hitimisho gani kuhusu uwezo wa Mungu?
      1.    Watu gani, hatimaye, walikuwa mtegoni kabisa? (Sio watu wa Mungu.)
    1.    Soma Kutoka 14:26-28. Utahitimisha nini kuhusu maana ya Zaburi 23 (somo letu la kwanza katika mfululizo wa masomo haya) kama ungekuwa umepitia uzoefu huu katika kipindi kifupi tu kilichopita?
      1.    Je, ungejutia hofu yako ya awali?
    1.    Soma Kutoka 14:31. Je, watu wamefikia hitimisho lile lile ambalo nawe ungelifikia?
  1.   Suuza na Rudia
    1.    Soma Kutoka 15:22-24. Watu walipaswa kuwa na mjibizo (reaction) gani?
    1.    Soma Kutoka 15:25. Je, hili ni suluhisho lipitalo akili ya kawaida (supernatural)? (Kamwe gogo la mti lisingeweza kuyafanya maji machungu yawe matamu. Hivyo, hili ni suluhisho lipitalo akili ya kawaida. Lakini, halionekani kuwa hivyo katika hali ya kawaida.)
    1.    Soma Kutoka 16:2-3. Mara hii malalamiko yanahusu nini? (Chakula. Awali ilikuwa maji, sasa ni chakula.)
    1.    Soma Kutoka 16:4. Mungu anatatuaje tatizo hili? (Kwa kutumia muujiza upitao akili ya kawaida. Anaahidi kunyeshea “mvua ya mkate” kwa ajili yao. Sehemu iliyosalia ya Kutoka 16 inaelezea jinsi jambo hili lilivyotendeka.)
    1.    Soma Kutoka 17:1-4. Hapo awali tuliwahi kupitia njia hii mahsusi. Unayaelezeaje malalamiko haya, ambayo yalikuwa makubwa sana kiasi kwamba Musa alidhani kuwa watu wangeweza kujaribu kumuua?
    1.    Unaweza kuelezea kwa nini watu walikuwa na mjibizo (react) huo kwa kuzingatia miujiza ya nyuma? Kwa ufupi ni kwamba waliokolewa dhidi ya jeshi la Wamisri, waliokolewa dhidi ya tatizo la maji, waliokolewa dhidi ya tatizo la chakula, na sasa wanakabiliana na tatizo la maji kwa mara ya pili. Je, wao ni wapumbavu? Je, mawazo yao hayakuwa na uzingativu wa kutosha katika Bahari ya Shamu?
  1.      Mjibizo wa Mungu na Mjibizo Wetu
    1.    Nimeruka sehemu ambayo Mungu anatoa maelekezo mahsusi ya jinsi ya kuzuia anguko hili la imani linalojirudiarudia. Soma Kutoka 15:25-26. Hii inaendanaje na tatizo? (Tukiliangalia jambo hili kwa namna wanavyoliangalia Wayahudi na Wakristo wengi, basi utahitimisha kwamba unatakiwa kufanya kazi kwa juhudi ili kuepuka tatizo la kutishwa na mustakabali ujao na kuwa na wasiwasi juu ya magonjwa.)
      1.    Je, hitimisho hilo lina mantiki yoyote kutokana na visa anavyotuambia Mungu kabla tu ya kutoa “sheria (amri) na kanuni?” (Hapana. Katika visa vyote watu walitakiwa kumtumaini Mungu. Hawakufanya chochote ili kulishinda tatizo isipokuwa tu kutoa ushirikiano kwa Mungu alipokuwa anatatua tatizo.)
        1.    Je, hii inaashiria maana ya kina ya “sheria na kanuni” ya Mungu? (Ndiyo! Amri na sheria za Mungu zote zinahusiana na imani/tumaini. Je, unapenda kuishi maisha mazuri? Je, unataka kuepuka hofu na kufurahia malisho ya majani mabichi na maji ya utulivu? Usimpinge Mungu. Mtii tu. Mungu hakujaribu, anakupatia kivuli. Angalia jinsi Mungu anavyopata ushindi!)
    1.    Soma 1 Petro 1:6-7. Kwa kuzingatia kile tulichokijadili hivi punde, inamaanisha nini kujaribiwa kwa “uhalisia” wa imani yetu? (Je, tutamtumaini Mungu? Je, tutatazama kwa ujasiri wakati akipata ushindi?)
      1.    Kwa jinsi nilivyokiangalia kifungu hiki siku za nyuma ni kwamba ninapigwa na kuishiwa nguvu ya kuhimili ili kuthibitisha imani yangu. Kwenye visa vyetu watu walikabiliana na hofu halisi na matatizo makubwa. Ingekuwa heri sana kwao kama wangemtumaini tu Mungu na kumtizama akitenda kazi. Hapo ndipo Mungu anataka imani yetu ifikie.)
    1.    Soma 1 Petro 1:8-9. Ni nini yaliyo matokeo ya mtazamo wa aina hii ya imani? (Furaha! Kufurahia! Ujasiri katika wokovu wetu.)
      1.    Je, hii inaonekana kukinzana kabisa? Kwamba tunakabiliana na matatizo kwa furaha na nderemo? (Tunaweza kuelewa jinsi jambo hili linavyofanya kazi kupitia kwenye visa hivi.)
    1.    Rafiki, je, sasa unahitaji furaha, nderemo, na kufurahia ili viwe kiini cha maisha yako? Biblia inatuambia kuwa hili linawezekana (lengo halisi) hata kama tunakabiliwa na changamoto za kutisha. Je, utampokea Yesu kama Mchungaji na Mwokozi wako sasa hivi ili uweze kuishi katika furaha?
  1.   Juma lijalo: Kuitazama Sura ya Mfua Dhahabu.