Somo la 13: Kuingia Katika Umilele
Somo la 13: Kuingia Katika Umilele
(Waebrania 11, Ufunuo 21)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2026, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani.
Utangulizi: Shughuli yako unayoipenda zaidi ni ipi? Nilipokuja kijana nilipenda kufanya mambo yaliyohusisha msisimko na dalili ya hatari. Mambo kama vile kuendesha pikipiki msituni, kuteleza juu ya maji, au magari ya mwendokasi. Kile ambacho sikuwahi kukipenda ni hatari ambayo sikuweza kuidhibiti kwa kiwango kinachowezekana kimantiki, kama vile reli za burudani (roller-coasters) au michezo ya aina hiyo. Kwa kweli sikujali sana kuhusu kula. Kwa kuwa sasa nimezeeka, napenda msisimko kwa kiwango kidogo na ninapenda kula zaidi. Kumsifu Mungu huleta furaha. Baadhi ya dhana za watakatifu walioko mbinguni, kwa kweli, zinakatisha tamaa. Je, shughuli unayoipenda ni jambo ambalo utalifurahia mbinguni pia? Kwa wale wanaofurahia kula, Biblia ina marejeo kuhusu kula na kunywa mbinguni. Je, unatumia kiasi gani cha muda kujitafakari na umilele? Hebu tuchunguze Biblia ili kutusaidia mawazo yetu kuhusu umilele!
- Je, Watu Wagumu ni Salama Kuokolewa?
-
- Baadhi ya watu wamewahi kuniambia kuwa ni lazima tuwe “salama kuokolewa.” Unadhani hilo linamaanisha nini? (Ninalielewa kumaanisha kuwa ikiwa tabia yangu haijaafikiana vya kutosha na mazingira ya mbinguni, basi sitakuwepo huko kwa sababu mimi si salama.)
-
-
- Una maoni gani juu ya madai haya ya kidini?
-
-
-
- Una picha gani akilini kuhusu watu ambao ni “salama kuokolewa?”
-
-
-
-
- Je, taswira hiyo inaendana na kutumia saa nyingi ukiwa umekaa mawinguni ukipiga kinubi?
-
-
-
- Soma Waebrania 11:32. Unafikiri watu hao walipenda kufanya nini katika muda wao wa ziada?
-
- Soma Waebrania 11:33-34. Aina gani za shughuli zinabainishwa hapa? (Kwa kiasi kikubwa ni mapigano! Nyingi ya shughuli hizi zilihusisha ujasiri, hatari, migogoro, na imani kuu – kushinda falme, kutekeleza haki, kupokea ahadi, kuepuka kifo, na kuwa hodari vitani.)
-
-
- Je, hawa ni watu dhaifu? (“Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu.”)
-
-
-
- Je, watakuwepo mbinguni?
-
-
- Soma 1 Samweli 16:16-18. Kifungu hiki kinamwelezeaje Daudi? (Alikuwa mpiga kinubi, ambalo ndilo jambo alilolitaka Paulo.)
-
-
- Ni sifa gani nyingine za Daudi zinatajwa ambazo hazihusiani na uwezo wake wa muziki? (Ni jasiri na “mtu wa vita.” Ana mwonekano mzuri, na “Bwana yu pamoja naye.”)
-
-
- Soma Luka 23:39-43. Unadhani shughuli alizopenda kufanya zaidi yule mtu ambaye Yesu alimwahidi wokovu zilikuwa zipi? (Anakiri kwamba matendo yake ya zamani yanahalalisha kusulubiwa kwake.)
-
-
- Kwa namna gani alikuwa salama kuokolewa?
-
-
- Wakati wa utume wa Yesu, alichagua watu wa aina gani kuwa wanafunzi? Je, walikuwa na tabia za kawaida? Je, walikuwa na nguvu za kiume kwa viwango cha chini?
-
-
- Unadhani walifanya nini katika muda wao wa ziada kabla hawajakutana na Yesu?
-
-
-
- Hata Daudi, mpiga kinubi “aliyethibitishwa” hakuwa aina ya mtu mnyenyekevu wa kupita kiasi, upole wa kupita kiasi, na udhaifu unaolingana na picha ya kawaida ya waliookolewa wakiketi mawinguni wakipiga vinubi.)
-
-
- Nimekuuliza mfululizo wa maswali kuhusu watu ambao tutakutana nao mbinguni. Nimeuliza kuhusu kile unachodhani walikifanya katika muda wao wa ziada kwa sababu kile tunachokifanya katika muda wetu wa ziada mara nyingi huonesha shughuli tunazozipenda zaidi. Dhana iliyo nyuma ya maswali haya ni kwamba mbinguni tutakuwa na uhuru wa kufanya yale tunayoyafurahia – na bila shaka kujifunza mambo mengine ya kufurahisha zaidi kuyatenda. Je, unakubaliana na dhana hii?
- Tunachokijua Kuhusu Mbingu
-
- Soma Ufunuo 21:2-3 na Ufunuo 21:15-17. Je, vipimo hivi vinaonekana kuwa vya kiishara kwako? Au huu ni ukubwa halisi wa Yerusalemu Mpya? (Maelezo haya mahsusi yanaashiria kwamba ni vipimo halisi. Na mji huo ni mkubwa sana. Ukivichambua vipimo hivyo vinaonesha kwamba, mji huo ni wa mcheduara wenye urefu wa maili 1,380 (kilomita 2,220) kila upande. Kuta zake zina unene wa futi 216 (mita 66). Inaonekana Yerusalemu Mpya ni jengo kubwa sana la makazi!)
-
- Soma Ufunuo 21:18-21. Mbali na mji huo kujengwa kwa dhahabu safi “kama kioo kiangavu,” mawe gani mengine ya thamani ni sehemu ya ujenzi wake? (Yaspi, Samawi, Akiki, Zamaradi, Oniksi, Karnelia, Krisolithi, Berili, Topazi, Krisopraso, Yakinthi na Amethisto. Pia una lulu kubwa sana kwenye malango yake.)
-
-
- Mungu anataka kuonesha nini anapofunua kwamba Yerusalemu Mpya imejengwa kwa mawe na madini ya thamani? Anavuta hisia gani za silka za kibinadamu?
-
-
-
- Hili linadokeza nini kuhusu jinsi utakavyoishi mbinguni? (Huku si kujinyima. Hii ni anasa.)
-
-
- Soma Luka 9:23. Unapatanishaje kifungu hiki na anasa ya kushangaza ya mbinguni? (Yesu alijikana kwa kiwango cha juu sana ili kuja duniani kutuokoa. Lilikuwa jambo la muda mfupi. Maisha yetu hapa duniani ni ya muda mfupi, na kwa kuzingatia mfano wa Yesu tunapaswa kujikana nafsi kwa kusudi la kutangaza injili.)
-
- Soma Ufunuo 22:1-2. Je, tutakuwa na matunda safi mapya (fresh) mbinguni? Lengo la matunda hayo maalumu ni lipi? (Kwa ajili ya afya na uponyaji. Yanatupatia uzima.)
-
- Soma Mwanzo 2:16-17. Ukitafakari kuhusu Ufunuo 22:2 unaweza kuhitimisha kuwa ungelazimika kula tunda lile lile kwa mwezi mzima. Ulinganifu huu wa Edeni unatufundisha nini? (Kama ilivyo kwa Edeni, mbinguni kutakuwa na aina nyingi za matunda kwa ajili ya chakula.)
-
- Hebu tuangalie tena Ufunuo 22:1-2. Tunajua kwamba Yerusalemu Mpya ni mcheduara mkubwa wenye urefu wa maili 1,380 (kilomita 2,220). Mto wa Uzima unaanzia juu kabisa kwenye kiti cha enzi cha Mungu. Unadhani unapitiaje umbali huo wote wa maili 1,380? (Maelezo haya hayaendani na maporomoko ya maji. Nadhani mji huo una sehemu kubwa iliyo wazi katikati. Mto unatiririka kutoka ghorofa moja hadi nyingine, ukiwa na Mti wa Uzima na barabara kuu pande zote mbili. Ninafikiria kwamba makazi yetu binafsi yatakuwa na roshani (balcony) zinazotizama barabara na mto huo. Tunaweza kunyoosha mkono na kuchuma matunda kutoka kwenye Mti wa Uzaima.)
- Uhakikisho Hasi
-
- Katika kazi zangu za kushughulikia kesi mahakamani jinsi vyama vya wafanyakazi vinavyotumia fedha zake, nilijifunza neno, “hakikisho hasi.” Hili ni jambo ambalo wahasibu hulitoa katika mapitio (si ukaguzi kamili) ambalo kimsingi linamaanisha, “Hatusemi kuwa kila kitu katika vitabu hivi ni sahihi, lakini hatujapata makosa yoyote makubwa.” Soma Isaya 25:8 na Ufunuo 21:4. Ni mambo gani ambayo hatutayaona mbinguni? (Kifo, machozi, maombolezo, kilio, maumivu, aibu, na hofu kuhusu siku zijazo.)
-
- Angalia tena Ufunuo 21:4. Hili lina umuhimu gani katika kuishi maisha bora?
- Ibada na Kazi
-
- Soma Isaya 25:9. Hii inatuambia nini kuhusu mtazamo wetu mbinguni? (Furaha! Shangwe!)
-
- Soma Ufunuo 22:3-4. Ni mambo gani mawili ambayo vifungu hivi vinatuambia kuwa tutayafanya mbinguni? (Kumwabudu Mungu. Na kumwona uso kwa uso.)
-
- Soma Ufunuo 7:9-10 na Ufunuo 5:11-13. Je, umewahi kumsifu Mungu ukiwa umesimama katika kundi kubwa la watu? (Kwa neema, mimi hupata kufanya hivyo mara kwa mara ninapohudhuria ibada katika Chuo Kikuu cha Regent. Kuimba sifa za Mungu pamoja na kundi huinua moyo wangu kuelekea mbinguni. Ninapenda jambo hilo!)
-
- Soma Mathayo 8:11. Ni jambo gani jingine tutalifanya mbinguni? (Tutakula pamoja na watu mashuhuri wa Biblia! Je, una maswali yoyote ambayo ungependa kumuuliza Ibrahimu?)
-
- Soma Mathayo 26:29. Ni nani mwingine tutakayekula naye? (Yesu! Tuna picha ya jumla kwamba ulaji utakuwa sehemu ya shughuli zetu za kufurahisha mbinguni.)
-
- Soma Isaya 65:21-22. Je, unapenda kuumba au kutengeneza vitu? Hii ni sehemu ya furaha ya mbinguni!
-
- Soma Ufunuo 22:3 na Mwanzo 3:17-19. Ufunuo 22:3 inatwambia nini kuhusu kazi yetu mbinguni? (Laana imetoweka. Kazi haitakuwa ya maumivu wala ya taabu mbinguni.)
-
- Rafiki, ikiwa hamu yako ya kwenda mbinguni imepungua kutokana na dhana ya kwamba itajaa watu wa kuchosha wanaofanya mambo ya kuchosha, natumaini somo hili limebadilisha mtazamo wako. Watu ambao Biblia inatuambia kuwa watakuwepo mbinguni si watu wa kuchosha. Mazingira yetu ya mbinguni si ya kuchosha! Nami nina uhakika kwamba yale tutakayokuwa tukiyafanya mbinguni yatakuwa ya kusisimua na yenye kutosheleza. Kwa nini usimwombe Yesu, sasa hivi, akuokoe ili mustakabali (maisha yako ya baadaye) wako uwe pamoja na Mungu?
- Juma lijalo tunaanza mfululizo mpya wa masomo juu ya Waraka wa Kwanza na wa Pili kwa Wakorintho.
