Somo la 13: Neema, Upendo, na Ushirika
Somo la 13: Neema, Upendo, na Ushirika
(2 Wakorintho 13)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2026, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani.
Utangulizi: Somo letu la mwisho katika mfululizo wetu wa Wakorintho wa 1 & 2 linatafakari hitimisho na maonyo ya Paulo kwa Wakristo wa Korintho. Kwa kurudiarudia hitimisho lake linarejelea “kipimo.” Kama profesa, hilo ni neno ninalolielewa. Lakini Paulo anaonekana kugeuza mchakato wa kawaida wa kupima. Anasema Wakorintho wanampima yeye, mwalimu wao! Paulo anageuza hili na kuwataka wajijaribu wenyewe. Haya yote yanahusu jambo gani? Habari njema kwa wale wote wanaopitia kipimo ni kwamba Paulo anawatakia neema katika kupimwa. Hebu tuzame kwenye somo letu la 2 Wakorintho 13 na tujifunze zaidi!
- Vipimo vya Majaribio
-
- Soma 2 Wakorintho 13:1. Kama mtu akikwambia, “Hii ni mara ya tatu ninakuja kushughilikia suala hili,” je, ungedhani hilo ni jambo jema au baya? (Kwa haraka haraka, hii inaonekana kama mtu aliyeghadhibika. Kwa nini niongee na wewe mara tatu ili kukufanya utende jambo sahihi?)
-
- Soma 2 Wakorintho 13:1-2. Je, uko sahihi kwamba Paulo amekasirika? (Ndiyo. Anasema kuwa amewaonya na kusema kuwa endapo atakuja tena “hatawahurumia.”
-
- Angalia tena 2 Wakorintho 13:1. Inaonekana kuwa jambo la ajabu sana kwamba Paulo ananukuu kipimo cha uthibitisho (mashahidi wawili au watatu) kuhusiana na kuwaonya Wakorintho kwamba kama atawatembelea hatawahurumia. Unadhani kwa nini Paulo ananukuu kipimo cha ushahidi?
-
-
- Una maoni gani juu ya manufaa ya hiki kipimo cha ushahidi? Na ni nani anayepata manufaa yake? (Soma Kumbukumbu la Torati 19:15. Hiki ni kipimo cha ushahidi cha kweli na cha haki kabisa kwa mtu anayetuhumiwa kutenda kosa. Unatarajia jambo kama hili katika nchi zilizo na mfumo wa haki wa kimahakama. Kimsingi, Paulo ananukuu kipimo cha Mungu.)
-
-
- Soma 2 Wakorintho 13:2-3. Nani anayenufaika na kipimo hiki cha ushahidi? (Kila mtu. Utaona kwamba katika kifungu cha 2 Paulo anasema kuwa hatawahurumia, lakini kifungu cha 3 kinataarifu kuwa Wakorintho wanatafuta uthibitisho kwamba Kristo ananena kupitia kwa Paulo. Kwa hiyo wote wawili, yaani, Paulo na Wakoritho, wanashtakiwa kwa jambo fulani. Utakumbuka kwamba juma lililopita tulijifunza tatizo la walimu wa uongo. Hukumu inapoelea kanisani tunatakiwa kukumbuka kutenda haki kwa wote wanaoshtakiwa.)
-
-
- Kichwa cha somo letu ni “Neema, Upendo, na Ushirika.” Je, sehemu hii ya mwanzo inaonekana kama ujumbe kuhusu neema au upendo? (Kutenda haki ni muhimu kwenye suala la neema na upendo.)
-
- Kumjaribu Paulo
-
- Hebu tuangalie tena 2 Wakorintho 13:3. Ikiwa swali ni uthibitisho wa mamlaka ya Paulo ya kuzungumza kwa niaba ya Yesu, kwa nini Paulo anaandika kuhusu uweza wa Mungu? Kwani si Paulo, na wala si Mungu, ndiye anayejaribiwa?
-
-
- Kama Paulo ndiye aliye chini ya hadubini, Wakorintho wanadai uthibitisho wa namna gani kutoka kwa Paulo? Wanatarajia nini?
-
-
-
- Hebu tusimame kidogo na tutafakari kama wanasheria. Nani anayetuhumiwa kutenda kosa? (Paulo anatuhumiwa kusema uongo kuwa anazungumza kwa niaba ya Mungu.)
-
-
-
-
- Sasa tumia kanuni ya “mashahidi wawili au watatu.” Nani aliye na mzigo wa uthibitisho? (Kama Wakorintho ndio washtaki, wana mzigo wa uthibitisho, na lazima waje na mashahidi wawili au watatu ili kuonyesha kwamba Paulo hazungumzi kwa niaba ya Mungu.)
-
-
-
- Rudi nyuma kidogo na utafakari kile tulichokisoma. Paulo anaanza kusema kuwa hatawahurumia, na Wakorintho wanaonekana kusema, “Kwa nini tudhani unazungumza kwa niaba ya Mungu?” Je, hili linakatisha tamaa? (Kwa upande wangu hili linaonekana zaidi kama makubaliano ya awali ya mashtaka. Tunakubaliana viwango/vipimo vya ushahidi na tunaangalia nani anayeshtakiwa kwa lipi.)
-
- Soma 2 Wakorintho 13:4. Paulo anasema nini kuhusu kuwa dhaifu na imara? (Paulo ana hoja ya kuvutia sana. Anasema kuwa yeye ni dhaifu, jambo ambalo nina shaka kama ndio aina ya uthibitisho ambao Wakorintho wanautafuta. Lakini Paulo anasema kwamba Yesu alisulubiwa katika udhaifu lakini sasa ni “uweza wa Mungu.” Anachokimaanisha Paulo ni kwamba kuwa dhaifu ni jambo sahihi kwa ajili ya kufanyia majaribio uweza wa Mungu. Na Paulo atakuja kwa uweza kwa wale walio nje ya msitari.)
-
- Soma 2 Wakorintho 13:5. Wakorintho wanataka Paulo athibitishe kwamba Kristo ananena kupitia kwake. Paulo anapendekeza kipimo gani cha kushangaza? (Anawaambia wajijaribu! Je, wapo katika imani? Je, Yesu Kristo anakaa ndani yao?)
-
-
- Ni kwa jinsi gani kujichunguza wao wenyewe kutasaidia kujibu changamoto yao kwa Paulo? Paulo alipeleka injili Korintho. Kama Kristo anakaa ndani yao kwa dhati, wao wenyewe ni Ushahidi kwamba Kristo amekuwa akitenda kazi kupitia huduma ya Paulo.)
-
-
-
- Je, hii inamaanisha mjadala wa awali wa Paulo kuhusu udhaifu hauna maana? (Hapana. Unawaambia kuwa wamekuwa wakitumia kipimo kisicho sahihi kumhukumu Paulo. Uweza wa Mungu unaweza kufanya kazi kupitia udhaifu wa dhahiri wa kibinadamu, kama Kristo alivyosulubishwa katika udhaifu lakini anaishi kwa uweza wa Mungu.)
-
-
-
-
- Je, unakubaliana na Paulo kwenye jibu sahihi la kipimo kinachopaswa kutumika kwa Paulo na kwa Wakorintho? (Jambo la ajabu ni kwamba, ni kipimo kinachoangalia uelewa wa udhaifu – uelewa wa kwamba Mungu pekee ndiye anayeweza kutufanikisha.)
-
-
-
- Soma 2 Wakorintho 13:6. Paulo anatarajia kuwa uchunguzi wao utawaonesha nini kumhusu? (Kama watatambua kazi ya Mungu ndani yao, wanapaswa pia kutambua kuwa Paulo hajashindwa kipimo.)
- Lengo la Mamlaka ya Kiroho
-
- Soma 2 Wakorintho 13:7. Je, Paulo anajitetea? (Haonekani kufanya hivyo. Anasema kuwa wanaweza kudhani kuwa ameshindwa kipimo.)
-
-
- Ni kwa jinsi gani kushindwa kipimo ni jambo zuri? (Inaonesha kuwa kipaumbele cha Paulo ni Wakorintho. Anataka wafanye kilicho sahihi, hata kama machoni mwao amepata alama dhaifu kwenye kipimo.)
-
-
- Soma 2 Wakorintho 13:8. Paulo anamaanisha nini anaposema kuwa hawezi kutenda neno lolote kinyume na kweli? (Lengo la Paulo ni kutangaza ukweli.)
-
- Soma 2 Wakorintho 13:9. Paulo anataka kumsaidia nani? (Paulo anawatanguliza Wakorintho. Anataka wafanyiwe urejeshwaji (restored) hata kama bado yeye binafsi yu dhaifu.)
-
- Soma 2 Wakorintho 13:10. Paulo anasema kuwa lengo la nidhamu ya kanisa ni lipi? (Ni kulijenga na si kubomoa kanisa.)
-
-
- Unapotafakari kile alichokiandika Paulo, je, ana shauku kubwa zaidi kushinda pambano au kuwafanyia urejeshaji Wakorintho? (Paulo anatanguliza shauku za Wakorintho.)
-
- Lengo
-
- Soma 2 Wakorintho 13:11-12. Ni nini lengo la Paulo kwa kanisa la Korintho? (Anataka lifanyiwe urejeshaji. Anataka wawe na maelewano wao kwa wao.)
-
-
- Ahadi gani inaambatana na wito wa Paulo kwa ajili ya upatanifu (harmony) na amani? Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nao.)
-
-
-
- Je, unajisikia kama umepanda roller coaster (mchezo wa gari la mwendo wa kasi kwenye reli za burudani)? Ni punde tu Paulo amewaandikia Wakorintho kuhusu mtafaruku unaokuja na kipimo. Je, sasa anaandika kuhusu amani na upendo? Je, unaweza kuona mantiki yoyote katika hili? (Kutenda mapenzi ya Mungu. Kujazwa Roho wake Mtakatifu. Kuachana na dhambi huleta amani na upendo. Hilo ndilo lengo la Paulo kwa Wakorintho.)
-
-
- Soma 2 Wakorintho 13:12. Kwa nini kuwasalimia watu wengine kwa busu? (Fikiria kama mgogoro ulikuwa mkubwa sana kiasi kwamba washiriki walijisikia kuwapiga ngumi washiriki wenzao. Unaweza kupata hisia hizo kwa kusoma vifungu 1-10. Huu ni mtazamo tofauti kabisa. Hiki ndicho anachokitaka Paulo kwa Wakorintho.)
-
- Soma 2 Wakorintho 13:13. Je, washiriki wengine wa kanisa wana shauku ya kujua kinachotokea katika kanisa la Korintho? (Ndiyo.)
-
-
- Hilo linapaswa kuwaambia nini Wakorintho? (Hii si kwa ajili yenu pekee. Huu ni ujumbe kwa Wakristo wote kwa nyakati zote. Tunatakiwa kutafakari ushawishi wetu.)
-
- Utatu
-
- Soma 2 Wakorintho 13:14. Kwa nini neema na Yesu vinaunganishwa? Kwa nini upendo na Mungu vinaunganishwa? Kwa nini ushirika na Roho Mtakatifu vinaunganishwa? (Yesu alipoishika sheria kwa niaba yetu, alipokufa kwa niaba yetu, alituonesha neema kubwa/kuu. Aliteseka kama tulivyopaswa kuteseka, ili tuweze kuishi naye milele. Mungu Baba alitupenda kwa upendo mkuu kiasi kwamba alikuwa tayari kumtoa Mwanaye kwa ajili ya wokovu wetu. Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu na kwa kufanya hivyo tunakuwa na ushirika na Mungu.)
-
- Rafiki, wakati mwingine tunahitaji kipimo cha kweli na uaminifu cha endapo tunaelewa na kutumia kanuni za Mungu maishani mwetu. Neema ya Mungu hutuingiza kwenye msitari kwa mapenzi yake na kuzaa upendo na ushirika miongoni mwetu. Je, utakuwa tayari kupimwa na Mungu?
- Juma lijalo: Tunaanza mfululizo wa masomo uitwao, “Karama ya Unabii.”
