Mavazi ya Mwana Mpotevu

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Luka 15)
Swahili
Year: 
2011
Quarter: 
2
Lesson Number: 
10

Utangulizi: Yesu anatuambia katika Luka 7:47 kuwa wale wanaosamehewa dhambi nyingi, hupenda sana. Wale wanaosamehewa kidogo, hupenda kidogo. Je, umekuwa “mwema” maishani mwako mwote? Je, ulikuwa mtiifu kwa wazazi wako, uongozi wa shule na mamlaka ya nchi? Je, umekuwa kanisani mara zote na bado upo kanisani? Kama ninakuelezea wewe, basi kubaini wakati mahsusi ulipobadilika (kumkiri Mungu) ni vigumu, sawa? Kama huna uzoefu hata mmoja kati ya haya, je, mara zote umekuwa ukijikuta matatani? Kama umekuwa mtu “mbaya,” lakini sasa umo kanisani, bila shaka kwa wazi kabisa unakumbuka uzoefu wako wa ubadilishwaji (wa kumkiri Mungu). Sasa basi sote tunajijua kuwa tu watu wa namna gani, vipi kama Mungu akituambia kisa ambacho dhana yake ni kwamba watu wema hawaingii kwenye Ufalme wa Mbingu? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na kujifunza zaidi!

I.    Mpango/Mtego

A.    Soma Luka 15:1-2. Elezea hadhira inayomsikiliza Yesu?

1.    Ni kundi gani lilikuja kwa kupenda lenyewe na ni kundi gani lilikuja na malalamiko? (Yesu hakuwa na shida kuwaleta wadhambi wa dhahiri kwenye mikutano yake. Hata hivyo, watu “wema” walikuwa wakilalamika/wakinung’unika.)

2.    Je, wadhambi wa dhahiri wanakusanyika kanisani kwako kila Sabato?

a.    Kama sivyo, je, unafundisha kama Yesu alivyofundisha?

b.    Baini kama ungekuwa ukilalamika kuhusiana na kufurika kwa wadhambi?

B.    Pitia kwa haraka haraka Luka 15:3-10. Yesu anaelezea visa viwili kuhusu kitu kilichopotea na kupatikana. Tunaelewa haya kuwa mafumbo ya “Ufalme wa Mbingu” – visa kuhusu wale wanaopotea na mtazamo wa Mungu dhidi ya kuwapatia uzima wa milele.

II.    Mwana Mdogo

A.    Soma Luka 15:11-12. Tafakari fungu hili kutoka katika mtazamo wa baba. Je, mwana mdogo anataka nini? Je, hataki nini? (Anataka fedha zako. Hakutaki wewe. Anataka maisha yawe kana kwamba umefariki.)

1.    Wazazi hebu niambieni, je, hii inaleta hisia gani?

B.    Unafikiri ni kwa jinsi gani baba anatunza utajiri wake? (Fungu linasema “sehemu ya shamba” na “vitu/mali.” Kiyunani kinatafsiri neno “vitu/mali” kuwa ni “bios” au uzima. Mkulima anapopunguza sehemu ya ekari yake kwa theluthi moja (mdogo anapata theluthi moja, angalia Kumbukumbu la Totari 21:17), maisha yake, hadhi yake katika jamii, inapungua. Ardhi ni uzima wake.)

C.    Soma Luka 15:13-16. Kama ungekuja kwa mwana mdogo na akakuomba mkopo, je, nini kingekuwa kisa chake? Je, ni katika misingi ipi angesema kuwa angekulipa? (Ingekuwa asili kwa yeye kulaumu njaa. Sio “kosa lake!” Atapata fedha zake.)

D.    Soma Luka 15:17. Je, inamanisha nini kwamba “alipozingatia moyoni mwake?” (Alitambua kuwa alikuwa ameshindwa. Vyovyote vile ilivyokuwa kutokana na athari ya njaa, alikuwa katika hali mbaya kifedha.)

1.    Je, kushindwa mara nyingine ni mbaraka?

E.    Soma Luka 15:18-19. Je, unadhani mwana alikuwa akifanyia mazoezi/akikariri haya maneno alipokuwa akitembea kurejea nyumbani?

1.    Elezea mwanzo wa  nafasi ya mjadala ya mwana? (Maelezo mazuri ya Tim Keller kuhusu Mungu Mtapanyaji, yaani, Mungu mtapanyaji wa upendo wake, uangalizi wake na neema yake (ambayo sehemu kubwa ya hili somo yameegemea) yanaelezea kuwa mwana alitaka kuajiriwa ili kwamba aweze kulipa kile alichokuwa amechukua kutoka kwa baba.)

III.    Baba

A.    Soma Luka 15:20. Je, baba, ambaye alikuwa amefedheheshwa/ameaibishwa na kutupiliwa mbali/kuachwa na huyu mwana mbinafsi, anamtenda mwana kama vile mwana alivyomtenda?

B.    Soma Luka 15:21-24. Je, ni kwa kiwango gani nafasi ya mjadala wa mwanzo wa mwana uliokaririwa unatoka? (Kukiri/kutubu peke yeke. Kujitolea kwake kulipa kunamezwa na ukaribishaji wa baba.)

1.    Je, sherehe inawakilisha nini kwenye visa vya Yesu vya Ufalme? (Ufalme wa Mbingu: Mathayo 22, Luka 14. Angalia pia Ufunuo 19.)

2.    Mwana mdogo anapokaribishwa kwenye sherehe kama mwana mkamilifu, je, hiyo inamaanisha nini? (Ameokolewa. Wokovu unakuja kwake kama zawadi ya bure pale ambapo yeye: a) Alipozingatia moyoni mwake; na, b) Anarejea kwa baba yake kwa kukiri/kutubu. Baba hata hana haja ya kusikia kuhusu kulipwa.)

IV.    Mwana Mkubwa

A.    Soma Luka 15:25-27. Hivi punde tu tumejadili jinsi ambavyo wokovu ni zawadi ya bure kwa mwana mdogo. Je, kweli ulikuwa ya bure? Au, ulikuwa unatoka mfukoni mwa mwana mkubwa? (Kwa hakika ulikuwa unatoka mfukoni mwa mwana mkubwa!)

B.    Soma Luka 15:28-30. Je, mwana mkubwa anajisikiaje kwa kupoteza mali yake kwa mwana mdogo?

1.    Kumbuka kwamba mwana mdogo alijali kuhusu mali ya baba yake, lakini sio baba yake. Je, unaelezeaje mtazamo wa mwana mkubwa dhidi ya baba yake? (Kama alimpenda baba yake, basi angetaka kufurahi pamoja na baba. Badala yake, hamtii kabisa baba yake na mapenzi ya baba. Alimchukulia baba yake kuwa ni mchoyo/mnyimi/mbahili kwake (“mwana-mbuzi” sio “ndama mnono”). Kwa hiyo, mali na sio baba ndio ilikuwa kitu cha msingi kabisa akilini mwake.)

2.    Je, mwana mdogo na mkubwa wana tofauti gani? Je, wana lengo moja (mali na sio baba), lakini wanatofautiana tu njia ya kufikia lengo lao?

3.    Kama wewe ni mshiriki mwaminifu wa kanisa, je, mibaraka ya Mungu na ulinzi wake vina umuhimu kwako kwa kiasi gani?

a.    Je, unathaminije “mali” ya Mungu dhidi ya uwepo wa Mungu?

b.    Je, hii inatengaje kazi maishani mwake: kama una “mali” kidogo, je, una “uwepo” mkubwa wa Mungu? Je, unalazimishwa kumwamini na kumtegemea Mungu kama una vichache?

 4.    Je, mwana mkubwa anaingia kwenye sherehe? (Hapana.)

a.    Kwa nini? Angalia tena kile anachokisema mwana mkubwa. (Yeye ni: a) Bora kupita kiasi kwa ajili ya hili (“Nimekuwa nikikutumikia” wakati mwana mdogo amekuwa na “makahaba”); na, b) Amekasirika kwa ajili ya asili ya wema wa baba. (“Huyu mwana wako” ambaye “umemchinjia yeye ndama aliyenona.”))

b.    Je, mwana mkubwa amepotea milele, na mwana mdogo ameokolewa milele? (Mwana mkubwa haingii kwenye sherehe ya baba yake.)

                                                                                                                 i.    Soma Luka 15:31-32. Je, inamaanisha nini kuwa “ u pamoja nami siku zote?” (Suala ni kama kuwa na “vitu vya Mungu” na kuwa na Mungu (hapa) ni sawa na wokovu. Hili ni swali la kujadiliwa, na ninaweza kukosea kwa hakika, lakini kura yangu ni kwamba kukataa wito wa Mungu kuingia kwenye sherehe kwa sababu wewe ni bora zaidi na unajali sana kuhusu mali yako ni upotevu wa milele.)

             c.    Fikiria ile hadhira ya Yesu. Je, kisa hiki kinafananaje na yale makundi mawili?

                                                                                                                i.    Je, kundi lako ni lipi?

V.    Mtu wa Utume

A.    Unapochukulia visa viwili vya kwanza vya Luka 15, je, nini iliyo mada ya pamoja katika visa hivyo inayokosekana  kwenye kisa cha ndugu wawili (mwana mdogo na mkubwa)? (Hakuna anayejitoa kumtafuta mwana mdogo aliyepotea.)

1.    Kwenye kisa cha ndugu wawili, nani kwa asili anapaswa kwenda kutafuta? (Mwana mkubwa.)

a.    Kwa nini hakutafuta? (Hakutaka mwana mdogo arejee. Alithamini mali yake dhidi ya ndugu yake na dhidi ya furaha ya baba yake.)

b.    Kabla ya anguko lake la kifedha, je, mwana mdogo angechukua muda wake kumtafuta/kumwangalia mwana mkubwa? (Hapana. Alikuwa na mashughuli mengi akifurahia mali yake. Alikuwa amejilenga yeye mwenyewe.)

B.    Je, “Mwana Mkubwa” anayekosekana kwenye  kisa chetu ni nani? (Yesu. Alikuja kututafuta.)

1.    Je, kuna yeyote katika kisa anayetafuta kilichopotea? (Baini kuwa katika Luka 15:20 baba anamwona mwana mdogo na kumkimbilia. Katika Luka 15:28 baba anaacha sherehe na kwenda nje na kumsihi mwana wake mkubwa.)

2.    Kama wewe umo kanisani, je, u mwana mkubwa sahihi kwa wadhambi na watoza ushuru?

3.    Ni kwa kiwango gani kujali kwako kwa ajili ya kutunza mali yako kunakuingilia wewe kuwasaidia “wana wadogo” kanisani kwako?

C.    Rafiki, kama unasoma hili somo, ubashiri wangu ni kuwa wewe ni “mwana mkubwa.” Je, utamwomba Roho Mtakatifu kukupa utambuzi moyoni mwako ili uweza kujibu swali: “Je, ninapenda mibaraka kutokana na kumtumikia Mungu zaidi kuliko ninavyompenda Mungu aliyenifilia?” “Je, matendo yangu mema na kujijali kwangu mwenyewe kutanizuia kuingia kwenye wokovu?”

VI.    Juma Lijalo: Vazi la Harusi.