Yesu Kristo ni Nani?
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Mjadala unaendelea unaohusu asili ya Yesu. Je, alikuwa tu mtu mkuu, nabii mzuri, au alikuwa Mungu kamili na mwanadamu kamili? Je, alikuwa Masihi, Mwana wa Mungu? Luka, kama ambavyo tulikwishaona, ameshawishika kikamilifu juu ya kile anachokiandika. Hadi sasa ameshaweka kwenye kumbukumbu kimaandishi kwamba Gabrieli na malaika walisema kuwa Yesu alikuwa Mungu. Hebu tuzame na tuendelee kuvumbua zaidi anachokiandika Luka ambacho Yesu alikisema kumhusu yeye binafsi!
- Nazareti
- Soma Luka 4:14-15. Yesu anapata sifa gani njema? (“Kila mtu alimtukuza.”)
- Soma Luka 4:16-21. Yesu anamaanisha nini anaposema “maandiko haya yametimia masikioni mwenu?” (Maneno haya yanatoka kwenye Isaya 61:1-2 na Isaya 42:7. Huu ni unabii unaohusu kuwekwa huru na kuponywa. Hii inaashiria kwamba Yesu atawaweka huru na kuwapponya Wayahudi, ikimaanisha kwamba yeye ni Masihi.)
- Soma Luka 4:22. Watu waliitikiaje? (Inaonekana walivutiwa sana, lakini walisema, “Hebu subiri kidogo, hivi huyu siye mwana wa Yusufu, yule afanyaye kazi ya useremala?”)
- Soma Luka 4:23. Je, Yesu anayatambua mawazo yao? (Ndiyo.)
- Wanafikiria nini? (Mara baada ya “Hebu subiri kidogo,” wanakumbuka visa kuhusu miujiza ya Yesu, na hivyo wanadhani kwamba muujiza mmoja au miwili itawasaidia kuthibitisha kuwa wanapaswa kuyaangalia madai yake kwamba yeye ni Masihi.)
- Soma Luka 4:24-27. Je, Yesu atawatendea muujiza? (Hapana!)
- Kwa nini hawatendei? (Kwanza, Yesu anasema hawatamkubali kwa sababu wanafahamu mahali alipokulia. Pili, anasema kwamba Mungu ana utaratibu wa kuwasaidia watu wasio Wayahudi, wakati ambapo Wayahudi wana uhitaji.)
- Jiweke kwenye nafasi ya Wayahudi wa Nazareti. Je, ungeitikiaje jambo hili? (Ningejisikia kufedheheka. Kwa nini usinipe nafasi ya kuamini? Kwa nini uchukulie kwamba sitaamini, na kisha unitukane kwa kusema kwamba Mungu anawasaidia wasio Wayahudi?
- Kwa nini hawatendei? (Kwanza, Yesu anasema hawatamkubali kwa sababu wanafahamu mahali alipokulia. Pili, anasema kwamba Mungu ana utaratibu wa kuwasaidia watu wasio Wayahudi, wakati ambapo Wayahudi wana uhitaji.)
- Soma Luka 4:28-29. Je, ungekasirika kiasi hicho? (Hapana. Ningejisikia kufedheheshwa tu – nisingekuwa na hasira kiasi cha kujaribu kumwuua Yesu.)
- Je, Yesu alikuzwa kwenye mji uliojaa wendawazimu – watu wenye tatizo la kushindwa kudhibiti hasira zao? Au, je, unaweza kuelezea tabia hii? (Musa aliwaambia katika Mambo ya Walawi 24:16 kwamba watu wanaojihusisha na makufuru wanapaswa kuuawa. Hii inathibitisha uelewa wetu juu ya alichokisema Yesu katika sinagogi. Walimwelewa kwamba alidai kuwa yeye ni Masihi – Mungu ajaye ambaye atawaokoa. Kwa hiyo, kwa mujibu wa Musa Yesu alitakiwa auawe (endapo hakuwa Masihi). Luka anatuonesha alichokisema Yesu na jinsi makutano walivyokielewa.)
- Soma Luka 4:30. Unawezaje kutembea katikati ya watu wanaotaka kukuua? Je, njia bora sio kuanza kukimbia kwa mwendo wa kasi kadri uwezavyo? (Luka anatutaka tufahamu kwamba jambo kubwa lisilo la kawaida lilitokea. Yesu alitembea katikati ya watu kana kwamba alikuwa haonekani.)
- Jambo hili linasema nini kumhusu Yesu? (Alisema kwamba yeye ni Masihi, na baada ya hapo Mungu alimlinda.)
- Pepo
- Soma Luka 4:31-34. Kwa nini Luka anaandika kauli ya pepo? (Malaika walioangushwa kutoka mbinguni pamoja na Shetani wanamjua Yesu, na wanajua kwamba yeye ni “Mtakatifu wa Mungu.”)
- Unadhani pepo wanafikiria kuwa Yesu ana nia gani juu yao? (Kuwaangamiza.)
- Soma Luka 4:35-37. Kwa nini watu hawakutoa maoni kuhusu kile alichokisema pepo kumhusu Yesu? (Hawakuwa wakisifia ushuhuda wa pepo, lakini sasa Luka ametuambia kwamba malaika ambao hawakuangushwa (Luka 2:9-13) na malaika walioangushwa wanathibitisha kwamba Yesu ni Mungu.)
- Soma Luka 4:31-34. Kwa nini Luka anaandika kauli ya pepo? (Malaika walioangushwa kutoka mbinguni pamoja na Shetani wanamjua Yesu, na wanajua kwamba yeye ni “Mtakatifu wa Mungu.”)
- Wanafunzi
- Soma Luka 9:18. Jiweke kwenye nafasi ya Yesu. Kwa nini unauliza swali hili? (Sehemu kuu ya utume wa Yesu ilikuwa ni kuwafanya watu wafahamu kwamba yeye ni Masihi. Alikuwa anapima maendeleo yake.)
- Soma Luka 9:19. Je, jibu hili linatia moyo? (Wanadhani kwamba Yesu ni mtu wa pekee, lakini si Masihi.)
- Soma Luka 9:20-21. Yesu anapatia jibu kwa usahihi kabisa. Kwa nini Yesu anawaambia wasiseme jambo ambalo anataka lifahamike? (Soma Luka 9:22. Picha zilizopo kwenye kitabu cha Agano Jipya la Robertson zinatuonesha kwamba tukio hili lilitokea baada ya kuwalisha watu 5,000, kipindi ambacho watu walijaribu kumfanya Yesu kuwa Mfalme (Yohana 6:15). Luka 9:22 inabainisha kwamba Yesu ana mtiririko wa matukio. Yesu alikuwa makini kuweka uwiano sahihi wa kutukia kwa mambo – kutenda mambo ambayo yatawafanya watu hapo baadaye waamini kwamba yeye ni Masihi, lakini wakati huo huo akiepuka kuanzisha mapinduzi sasa hivi.)
- Soma Luka 9:23-27. Ikiwa makutano wanataka kumfanya Yesu kuwa Mfalme, na Yesu anajali sana jambo hili, unadhani wanafunzi wanataka nini?
- Mfululizo wa mafungu haya unazungumziaje mawazo ya wanafunzi? (Bila shaka walitaka sana kuliko mtu mwingine yeyote yule, Yesu atangaze kwamba yeye ni Mfalme. Lakini, Yesu anawaambia kwamba jambo hili ni gumu sana – kwamba utukufu utakuja baadaye sana. Kwanza, kinachotakiwa ni kujitoa.)
- Angalia jambo la pekee sana analolisema Yesu katika Luka 9:27. Je, Yesu anasema kwamba ujio wake Mara ya Pili utatokea wakati bado wangali hai? Tunafahamu kwamba jambo hilo halikutokea.
- Yohana Mbatizaji
- Soma Luka 7:17-20. Kwa nini Yohana Mbatizaji anauliza jambo kama hilo? (Maoni ya Jamieson, Fausset na Brown yanabainisha kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa kifungoni kwa muda wa mwaka mmoja. Soma tena Luka 3:4-5. Bila shaka Yohana alishangaa kwa nini Yesu bado alikuwa hajafanya mambo haya makubwa – na kumweka huru kutoka kifungoni wakati akitenda mambo hayo. Jambo hili lilimpa mashaka.)
- Vipi kuhusu wewe, je, mara nyingine huwa unakuwa na mashaka pale mambo yanapokuwa kinyume na matarajio yako? (Fikiria kile alichokisema Yesu kumhusu Yohana “hakuna aliye mkuu kuliko Yohana.” Luka 7:28.)
- Soma Luka 7:21-23. Unalichukuliaje jibu la Yesu? Je, anamjibu Yohana? (Nadhani anamjibu Yohana bila kusema kwa mahsusi kwamba yeye ni Masihi. Anamtia moyo Yohana kwamba “asianguke,” asikate tamaa kutokana na Yesu kutotenda kila ambacho Yohana alikitarajia.)
- Soma Luka 7:17-20. Kwa nini Yohana Mbatizaji anauliza jambo kama hilo? (Maoni ya Jamieson, Fausset na Brown yanabainisha kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa kifungoni kwa muda wa mwaka mmoja. Soma tena Luka 3:4-5. Bila shaka Yohana alishangaa kwa nini Yesu bado alikuwa hajafanya mambo haya makubwa – na kumweka huru kutoka kifungoni wakati akitenda mambo hayo. Jambo hili lilimpa mashaka.)
- Kugeuzwa/Kubadilishwa
- Soma Luka 9:28-31. Watu hawa ni akina nani? (Musa alifufuliwa kutoka mautini (Yuda 9) na Eliya alichukuliwa mbinguni akiwa hai (2 Wafalme 2:11). Hawa ni wawakilishi kutoka mbinguni wakiwakilisha wale watakaofufuliwa kutoka katika wafu, na wale watakaobadilishwa wakiwa hai katika ujio wa Yesu Mara ya Pili.)
- Hapa wanajadili mada gani? (Mjadala wa Yesu kurejea mbinguni! Walikuwa wamemkosa sana na bila shaka walidhani Yesu alikuwa na hamu sana ya kurejea mbinguni.)
- Soma Luka 9:32. Je, Petro, Yohana na Yakobo wameona nini? (Soma tena Luka 9:27-28. Sasa tunaona utabiri wa Yesu kwamba wapo “kati ya hawa waliosimama hapa ambao hawataonja mauti kabisa, hata wauone kwanza ufalme wa Mungu” unatimia siku nane baadaye! Yesu alikuwa hazungumzii kuhusu ujio wake Mara ya Pili.)
- Soma Luka 9:33-34. Kwa nini Petro anazungumza mambo yasiyo na mantiki? Jambo gani lilitokea wakati akiendelea kuzungumza? (Petro alikuwa amejaa hisia kali, akidhani kwamba anatakiwa kusema jambo fulani, lakini hajui aseme nini. Wakati huo huo wingu lilitokea likawatia uvuli na tukio hilo ni la kuogofya sana.)
- Soma Luka 9:35-36. Yesu ni nani? (Luka anaweka kumbukumbu kimaandishi kwamba Mungu alisema kuwa Yesu ni Mwanaye!)
- Rafiki, je, una maoni gani kumhusu Yesu? Tunao ushuhuda wa Agano la Kale kuhusu Masihi anayekuja. Tunao ushahidi wa malaika, wale ambao hawakutenda dhambi na wale waliotenda dhambi. Tunayo kauli ya Yesu kwamba yeye ndiye utimilifu wa unabii, na tunao uthibitisho wa Mungu kwamba Yesu ni Mwanaye. Luka anatutaka tuwe na uhakika kabisa juu ya imani yake kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu. Vipi kuhusu wewe, je, utaithibitisha imani yako kwamba Yesu ni Mungu?
- Soma Luka 9:28-31. Watu hawa ni akina nani? (Musa alifufuliwa kutoka mautini (Yuda 9) na Eliya alichukuliwa mbinguni akiwa hai (2 Wafalme 2:11). Hawa ni wawakilishi kutoka mbinguni wakiwakilisha wale watakaofufuliwa kutoka katika wafu, na wale watakaobadilishwa wakiwa hai katika ujio wa Yesu Mara ya Pili.)
- Juma lijalo: Wito wa Uanafunzi.