Mmisionari wa Kwanza
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Kila mtu anapaswa kuwa mmisionari wa aina fulani, je, ni sawa? Huenda ulidhani kuwa wewe sio mzuri vya kutosha kushiriki habari njema za Yesu? Ibrahamu ni mojawapo ya watu wanaokubalika sana katika Biblia, na yeye ni shujaa wa imani. Lakini, Ibrahamu alikuwa na mambo yatakayowatia moyo watu kati yetu tunaotambua upungufu (udhaifu) wetu. Hatupaswi kusubiri kuuendeleza ufalme wa Mungu hadi udhaifu wetu unapokuwa umetoweka, kwa kuwa Ibrahamu pia anatufundisha kuhusu mibaraka na kuuendeleza na kuupeleka ujumbe wa Mungu. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia linalohusu kisa cha Ibrahamu na tuangalie mgogoro uliopo kati ya kuwa na upungufu (udhaifu) na kubarikiwa!
- Muda wa Kuondoka
- Soma Mwanzo 12:1 na Mwanzo 12:4. Sio wengi wenu mnaosoma habari hii mna umri wa miaka 75. Hata hivyo, Mwanzo 25:7 inatuambia kuwa Ibrahimu aliishi miaka 175. Ikiwa tutahusisha umri huo na urefu wa maisha yetu ya sasa, miaka 75 inaweza kuwa kama umri wa miaka miaka 35 hivi. Ungekuwa na mipangilio ipi endapo Mungu angekuamuru hivyo katika umri wa miaka 35?
- Mungu alisema kuwa Ibrahimu aelekee wapi? (Hakusema. Ibrahimu anaondoka kutoka mahali panapofahamika kuelekea mahali pasipofahamika kabisa.)
- Soma Mwanzo 12:2-3. Watu wengi wanahamia katika sehemu mpya ya nchi (au dunia) ili kutafuta kazi nzuri zaidi. Mungu anamwahidi Ibrahimu nini? (Kwa dhahiri, Ibrahimu atakuwa mtu wa muhimu.)
- Hii ahadi aliyoahidiwa Ibrahimu inafahamika sana kwa wanafunzi wa Biblia. Je, unadhani kuwa Mungu anatenda mambo hayo hayo kwa watu wake leo? Hususani ninarejea sehemu inayohusu kutubariki na kuwalaani wale wanaotulaani. (Wale wanaosoma masomo haya kila mara wanafahamu kwamba mara kwa mara huwa ninabainisha udhaifu (upungufu) wangu. Lakini, miaka mingi iliyopita, niligundua jambo la kushangaza. Katika kesi zangu kubwa zinazohusu uhuru wa dini, mara kwa mara mambo mabaya yalikuwa yanawatokea wapinzani wangu. Mashuhuda muhimu walikuwa wanafariki, mawkili wa upande pinzani walikuwa wanaachishwa kazi. Wateja wangu walishinda hizo kesi zote. Nilipozungumzia jambo hilo kwa mawakili wengine, kwa mzaha walinishauri kwamba nitoe onyo kimaandishi kwa wapinzani wangu wa siku zijazo watakaojihusisha na kesi mahakamani zinazohusu uhuru wa dini.)
- Soma Mwanzo 12:5. “Na hao watu waliowapata huko.” Je, Ibrahimu anamiliki watumwa? (Maoni ya Keil na Delitzsch katika Agano la Kale yanasema kuwa watu hawa ni watumwa wa kike na wa kiume ambao Ibrahimu na Lutu walikuwa wamewapata. Kimahsusi yanakataa tafsiri ya “roho walizozipata,” ambayo inahitimisha waongofu kwa dini ya Ibrahimu.)
- Soma Mwanzo 12:6-7. Mungu anapendekeza nini kuhusu Wakaanani? (Kwamba wataondoshwa kutoka katika hii nchi.)
- Hebu tujadili suala hili. Kwa upande mmoja tunaambiwa kwamba wale watakaomlaani Ibrahimu watalaaniwa, tunaambiwa kuwa Ibrahimu ana watumwa, na tunaambiwa kuwa atachukua nafasi (ninachukulia hivyo) ya watu wa asili wanaoishi katika hii nchi. Hii inaonekana kama vile Mungu anawapendelea watu wake dhidi ya watu wengine. Ikiwa unakubaliana, je, jambo hili bado linatokea leo? Je, Mungu ana upendeleo kwa watu fulani?
- Sasa angalia upande wa pili wa sarafu. Tunaambiwa kuwa Mungu alidhamiria kuwabariki wale waliombariki Ibrahimu, na kwamba watu wote watabarikiwa kupitia kwa Ibrahimu. Unaelezeaje jambo hili, kwamba Mungu anadhamiria kumbariki kila mtu, lakini watu fulani wanatokewa na mambo mabaya? (Ujumbe wa jumla uliopo kwenye mafungu haya ni kwamba wale wanaomchagua Mungu wanabarikiwa. Kubarikiwa sio hukumu kamili inayotokana na kumfuata Mungu, kwa sababu tunawafahamu watu wema ambao wametokewa na mambo mabaya. Ayubu ni mfano ambao Mungu aliutumia kutufundisha jambo hili.)
- Soma Mwanzo 12:1 na Mwanzo 12:4. Sio wengi wenu mnaosoma habari hii mna umri wa miaka 75. Hata hivyo, Mwanzo 25:7 inatuambia kuwa Ibrahimu aliishi miaka 175. Ikiwa tutahusisha umri huo na urefu wa maisha yetu ya sasa, miaka 75 inaweza kuwa kama umri wa miaka miaka 35 hivi. Ungekuwa na mipangilio ipi endapo Mungu angekuamuru hivyo katika umri wa miaka 35?
- Mke
- Soma Mwanzo 12:10. Je, maisha ya Ibrahimu hayana tatizo lolote? (Hapana. Ameathiriwa vibaya sana kwa njaa kubwa.)
- Soma Mwanzo 12:11-13. Unaufikiriaje mpango wa Ibrahimu?
- Imani kiasi gani kwa Mungu inaakisiwa kwa kitendo hiki? (Hakuna imani kabisa.)
- Soma Mwanzo 12:14-17. Kwa mara nyingine, tunaona kuwa Ibrahimu anapendelewa na magonjwa yanatokea kwa Farao. Je, kitendo hiki kinaonekana kuwa kibaya machoni mwako?
- Soma Mwanzo 12:18-20. Uko upande wa nani hapa? Nani anayeonyesha tabia ya hali ya juu? Ibrahim aliyesema uongo, au Farao anayemwondosha Ibrahimu (pamoja na vyote alivyokuwa navyo) mara alipofahamu ukweli kuhusu Sara? (Nahisi wasomaji wengi watamhurumia Farao.)
- Kuna kipi cha kujifunza hapa? (Ibrahimu alimtii Mungu kwa kukubali wito wa utume. Mungu anaendelea kumng’ang’ania Ibrahimu pamoja na kwamba anaonesha udhaifu wa tabia na kuingia matatani kwa kutomtumaini Mungu.)
- Angalia kwa makini matendo ya Mungu. Je, ungetenda mambo kwa njia tofauti endapo wewe ndiye ungekuwa Mungu? (Kwa dhahiri, Ibrahimu alimwangusha Mungu. Kama ilivyo dhahiri, ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu inakabiliana na kizingiti ikiwa mkewe ataungana na nyumba ya Farao. Kwa kuwa Ibrahimu hamwambii Farao ukweli, Mungu aliubainisha ukweli kwa njia ya mateso ya magonjwa. Utagundua kwamba Mungu anaendelea kumng’ang’ania Ibrahimu hata pale alipomwangusha Mungu.)
- Vita
- Soma Mwanzo 14:1-4. Chanzo cha vita ni kipi? (Wafalme wa Sodoma na Gomora waliasi dhidi ya Mfalme Kedorlaoma wa Elamu.)
- Soma Mwanzo 14:11-12. Nani aliyeathirika kiumiliki (Lutu na mali yake.)
- Soma Mwanzo 14:13-14 na Mwanzo 14:17. Je, Mungu ametenda wema kwenye ahadi yake kwa Ibrahimu? (Soma Mwanzo 14:18-20. Ndiyo, Melkizedeki anauhusianisha ushindi na Mungu.)
- Soma Mwanzo 14:16 na Mwanzo 14:21. Mfalme wa Sodoma ana uwezo mkuwa wa kujadili kwa kiasi gani? (Ibrahimu ametoka kuwashinda wafalme walioishinda Sodoma. Ibrahimu angeweza kutenda kile alichokitaka.)
- Soma Mwanzo 14:22-23. Kwa nini Ibrahimu anajali kile ambacho huyu mfalme anakifikiria au kukisema? (Ibrahimu anautaka ulimwengu ufahamu kwamba Mungu ndiye aliyemtajirisha. Sasa tunaona jinsi Ibrahimu anavyoipokea mibaraka ya Mungu na kuitumia kumpa Mungu utukufu. Ibrahimu anashuhudia ukweli kwamba Mungu ndiye Muumba wa mbingu na nchi.
- Mashaka
- Soma Mwanzo 15:1-3. Hii inalinganishwaje na Mwanzo 12:2? (Bado Mungu hajatimiza ahadi yake.)
- Tunajifunza nini kutokana na malalamiko ya Ibrahimu kwa Mungu? (Tunapaswa kumruhusu Mungu ayafahamu yale tunayoyataka. Hiyo inaonesha kwamba bado tunadhani kuwa yeye (Mungu) ndiye suluhisho la matatizo. Lakini, pia tunajifunza, kutokana na hali iliyokuwa inamkabili Ibrahimu, kwamba tunatakiwa kuwa wavumilivu.)
- Soma Mwanzo 15:4-5. Ikiwa Mungu hajatimiza ahadi moja, kuingia kwenye ahadi ya pili ambayo ni kubwa zaidi ndilo jibu (suluhisho)? (Soma Mwanzo 15:6. Hii ilitosheleza kwa Ibrahimu na inapaswa kutosheleza kwetu. Mungu alimpendelea Ibrahimu, lakini bado alikuwa hajatimiza sehemu ya muhimu ya ahadi yake.)
- Soma Mwanzo 15:7-8. Je, Ibrahimu ni mtu mweye kutumaini kikamilifu? (Hapana! Anaulizia uthibitisho wa ahadi kuhusu kuirithi nchi.)
- Katika mafungu kadhaa yanayofuatia (Mwanzo 15:9-15) Mungu anatenda mambo mawili. Anaingia mkataba rasmi na Ibrahimu kuhusu nchi (hicho ndicho kinachomaanishwa na sehemu za wanyama) na Mungu anaelezea siku zijazo zilizo “karibu” kwa ajili ya uzao wa Ibrahimu.) Soma Mwanzo 15:16. Kwa nini Waamori wataondoshwa kutoka katika nchi yao? (Hawajamchagua Mungu. Dhambi yao “itakapojaa pomoni” watapoteza ardhi yao.)
- Katika siku chache zilizopita nchi ya Marekani ilifikia kiwango kipya katika kuikumbatia dhambi. Je, sheria iliyotumika kwa Waamori inatumika leo kwa Marekani na nchi nyingine zote?
- Unadhani kwa nini Mungu alirasimisha ahadi yake kwa Ibrahimu? Kwa nini aingie “mkataba?”
- Soma Mwanzo 15:1-3. Hii inalinganishwaje na Mwanzo 12:2? (Bado Mungu hajatimiza ahadi yake.)
- Imani ya Kimisionari ya Kweli
- Soma Waebrania 11:8-10. Nini kilicho kitovu cha kweli cha imani ya Ibrahimu? (Si kile kilichomtokea maishani, badala yake ni Yerusalemu Mpya.)
- Ikiwa maisha hayatupatii kile tunachodhani Mungu alituahidi, tunapaswa kufanya nini? (Kwanza, tunatakiwa kujiangalia. Hatupaswi kuuangalia ukamilifu, kwa kuzingatia yaliyomtokea Ibrahimu. Lakini, tunapaswa kuangalia endapo matendo yetu ndio yaliyosababisha matatizo yetu. Pili, tunatakiwa kuwa na mtazamo mpana wa mibaraka ya Mungu.)
- Soma Waebrania 11:11-12. Kiini cha imani ya Sara ni kipi? (“Alimhesabu [Mungu] kuwa mwaminifu.” Swali la msingi ni endapo sisi tunamtumini Mungu. Hiyo ndio dhana ya kisa cha Ayubu, mtu ambaye kwa hakika maisha yake hayakumwendea kama ilivyoahidiwa.)
- Soma Waebrania 11:13-16. Ikiwa tunamtumaini Mungu, ikiwa tutazikaribisha ahadi zake kwa ajili ya siku zijazo, je, Mungu atafanya nini? (Hatatuonea haya na atatuandalia mji!)
- Rafiki, je, ungependa Mungu akuandalie mji? Sote tuna udhaifu (upungufu). Swali ni endapo tutamchagua Mungu na kumtumaini. Je, utakubali kufanya hivyo sasa hivi?
- Soma Waebrania 11:8-10. Nini kilicho kitovu cha kweli cha imani ya Ibrahimu? (Si kile kilichomtokea maishani, badala yake ni Yerusalemu Mpya.)
- Juma lijalo: Mmisionari Asiyetarajiwa.