Somo la 9: Shetani na Washirika Wake

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
(Ufunuo 13)
Swahili
Year: 
2019
Quarter: 
1
Lesson Number: 
9

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2019, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Leo nchini Marekani, tuna maonyo mengi ya kipuuzi juu ya hatari za dhahiri. Maonyo haya ni matokeo ya kusikitisha ya kazi za wanasheria. Kama mjuavyo nyote, mimi ni mwanasheria na profesa wa sheria, hivyo ngoja niwaonye kuhusu jambo ambalo huenda tayari mnalifahamu. Somo la leo na la juma lililopita yamejengwa juu ya usomaji wangu wa Biblia. Wasomi wengi wa Biblia hawakubaliani nami. Ninakiri kwa dhati kabisa juu ya elimu yao ya hali ya juu katika maeneo yote isipokuwa katika nyanja ya mantiki. Kwa onyo hilo, hebu tuzame kwenye somo letu la Ufunuo 13!

 

  1.     Joka na Mnyama Mwenye Pembe Kumi

 

    1.     Soma Ufunuo 13:1. Juma lililopita tulifikia uamuzi kwamba Joka Jekundu ni nani? (Ufunuo 12:9 inaelezea kwamba huyo ni Shetani. Sehemu iliyosalia ya sura ya 12 ya kitabu cha Ufunuo inaelezea jinsi Shetani na malaika wake walivyo vitani dhidi ya wafuasi wa Yesu.)

 

      1.     Joka Jekundu anapokuwa amesimama ufukweni, kitu gani kinatoka baharini? (“Mnyama” mwenye pembe kumi, vichwa saba, na vilemba kumi.)

 

      1.     Je, mnyama huyu mwenye Pembe Kumi ni rafiki wa Mungu? (Hapana. Kila kichwa kilikuwa na “jina la makufuru” juu yake. Vichwa vyake saba na pembe zake kumi vinamfanya afanane na Joka Jekundu. Ufunuo 12:3.)

 

      1.     Inamaanisha nini kutokea “baharini?” (Soma Ufunuo 17:15. Hii inatuambia kuwa maji yanawakilisha eneo lenye watu wengi.)

 

    1.     Soma Ufunuo 13:2. Pembe Kumi zinafanana na kitu gani kingine? (Wanyama watokao baharini ambao Danieli aliwaona katika Danieli 7:2-6.)

 

      1.     Hii inaashiria nini kwetu? (Wanyama wa Danieli 7 wanawakilisha historia ya dunia kuanzia kipindi cha Babeli. Hivyo, Pembe Kumi za Ufunuo 13 zina mfanano na hizi mamlaka za dunia zilizotangulia.)

 

      1.     Shetani anampatia nini mnyama mwenye Pembe Kumi? (Nguvu zake, kiti chake cha enzi na “uwezo mwingi.” Pembe Kumi ni wakala wa Shetani!)

 

    1.     Soma Danieli 7:7. Mnyama huyu ana pembe ngapi? (Kumi.)

 

      1.     Je, tunaufahamu utambulisho wa mnyama huyu? (Ikiwa huu ulikuwa unabii juu ya siku zijazo (ambao sasa ni historia), basi huyu mnyama wa nne, Pembe Kumi, ni Ufalme wa Rumi.)

 

    1.     Soma Danieli 7:8, Danieli 7:11, na Ufunuo 13:3-6. Unaona jambo gani lenye kufanana kati ya haya maelezo ya aina mbili tofauti? (Pembe Kumi za wanyama wote wawili zinazungumza mambo ya ujivuni na yenye kupingana na Mungu. Kutokana na rejea za kuabudu na kunena, hii inaelezea nguvu ambazo angalao, kwa kiasi fulani, ni za kidini na zinazompinga Yesu. Wanyama wote wawili walipata jeraha la kutisha, na Ufunuo 13:3 inabainisha kwamba angalao sehemu ya hizi Pembe Kumi inapona jeraha hilo.)

 

    1.     Soma Ufunuo 13:7-8. Jambo gani jingine baya linafanywa na hii Pembe Kumi? (Sio tu kwamba inafanya vita dhidi ya watakatifu, bali pia inawashinda na kuwashurutisha wamwabudu.)

 

    1.     Hiyo Pembe Kumi inayoabudiwa na kuwatesa watakatifu ni ipi? Je, wanyama wenye Pembe Kumi wa Danieli 7 na Ufunuo 13 wanafanana? (Maoni ya kale ya Kiprotestanti (ambayo ndio ninayoyanukuu kwa wingi) yanabainisha Pembe Kumi za Ufunuo 13 kama Rumi ya kipagani na Kipapa. Nadhani kuna ukubali (uhusiano) mkubwa kwamba Pembe Kumi za Danieli 7 ni Ufalme wa Rumi. Nyakati zinakubaliana na jambo hilo. Maoni hayo yanaelezea mateso ya Wakristo kutoka kwa wapagani na Rumi ya Kipapa. Kwa dhahiri, Wakatoliki hawakubaliani na ubainisho wa “Kipapa,” lakini nadhani maeneo ya mlinganisho yanakubaliana kwa kiasi kikubwa sana.)

 

      1.     Angalia tena Ufunuo 13:8. Je, hizi ni siku zijazo? (Lazima iwe hivyo. Hiyo inamaanisha mnyama huyu atakuwepo hadi mwisho, ambayo haijumuishi tafsiri ya kwamba mnyama huyu ni Ufalme wa Rumi pekee.)

 

  1.   Mnyama Aliyepo Juu ya Nchi

 

    1.     Soma Ufunuo 13:11-12. Mnyama huyu wa pili (aliyepo juu ya nchi) anazifanyia nini Pembe Kumi? (Anawafanya wakaao juu ya nchi waziabudu Pembe Kumi.)

 

    1.     Inamaanisha nini kwa mnyama huyu kupanda juu ya nchi? (Ikiwa maji yanamaanisha watu, basi hii inamaanisha eneo lenye watu wachache.)

 

    1.     Huyu mnyama aliyepo juu ya nchi ni nani? (Baadhi ya maoni ya kale ya Kiprotestanti yanambainisha mnyama huyu aliyepo juu ya nchi kama Rumi ya Kipapa, na kanisa langu linafundisha kwamba mnyama huyu ni nchi ya Marekani. Kuna nadharia nyingine kadhaa kuhusu mnyama huyu aliyepo juu ya nchi.)

 

      1.     Hebu tuangalie tatizo la kimantiki kwenye mitazamo yote miwili kuhusu Marekani na Upapa.

 

        1.     Ikiwa mnyama wa juu ya nchi ni Rumi ya Kipapa, je, alihamasisha kuuabudu Ufalme wa Rumi? (Mimi si mwanahistoria mzuri, lakini hilo linaonekana kutoendana na historia.)

 

        1.     Ikiwa mnyama aliyepo juu ya nchi ni Marekani, je, mnyama huyo anahamasisha ibada ya Rumi ya Kipapa? Je, anahamasisha ibada ya Kanisa Katoliki? (Hii ni historia ambayo sina shaka nayo. Marekani imekuwa ikipingana mno na Ukatoliki. Rais John Kennedy alikuwa Mkatoliki, na hilo lilikuwa tatizo kubwa kwenye kampeni zake za uchaguzi. Kwa sasa, vyombo vya habari na tasnia ya masuala ya filamu zinapingana mno na Ukatoliki. Baadhi ya ukosoaji huo unathibitishwa kutokana na kashfa za hivi karibuni, na ukosoaji mwingine unatokana na hasira ya kipagani kwenye msimamo wa Kanisa Katoliki dhidi ya suala la utoaji mimba na ubasha/usenge.)

 

    1.     Soma Ufunuo 13:13-15. Mnyama huyu aliye juu ya nchi anafanya jambo gani jingine?

 

    1.     Soma tena Ufunuo 13:11. Nguvu gani nyingine ya kidunia imehamasisha ibada? (Uislamu.)

 

      1.     Je, Uislamu “ulipanda juu kutoka katika nchi?” (Ndiyo, uliibuka kutoka kwenye eneo lenye watu wachache.)

 

      1.     Je, Uislamu una ”pembe mbili?” (Una maeneo mawili makubwa: Sunni na Shia. Uislamu pia una mafundisho mawili makubwa: hakuna mungu bali Mungu; na Muhammad ni mjumbe/mtume wa Mungu.)

 

    1.     Soma Ufunuo 16:13, Ufunuo 19:20, na Ufunuo 20:10. Mnyama wa pili, yule aliyepo juu ya nchi, anapewa jina gani jingine? (“Nabii wa uongo.”)

 

      1.     Neno “nabii wa uongo” linaashiria nini kuhusu utambulisho wa mnyama aliyepo juu ya nchi?

 

      1.     Ngoja niulize swali lile lile nililoliuliza kuhusu Rumi ya Kipapa na Marekani. Je, Uislamu umewahi kutangaza Rumi ya Kipagani au Rumi ya Kipapa? (Hapana! Kihistoria wamekuwa maadui.)

 

    1.     Tukiangalia historia, Rumi ya Kipapa, Marekani na Uislamu vimeshindwa kuendana na maelezo ya mnyama aliyepo katika nchi. Vipi kama tukiangalia siku zijazo? Soma 2 Wathesalonike 2:1-10 na uilinganishe na Ufunuo 13:13. Unadhani kwamba mafungu haya mawili yanaelezea tukio moja?

 

      1.     Ikiwa yanaelezea tukio moja, je, tayari limeshatokea? (Kwa mujibu wa muktadha huu, Wakristo wanaamini kwamba Shetani ataanzisha tukio bandia la ujio wa Yesu mara ya pili. Kile wasichokijua Wakristo wengi ni kwamba Waislamu wengi wanaamini kwamba Mahdi, ambaye pia anaitwa kuwa mkombozi, atakuja na kutawala dunia kwa kipindi fulani kabla ya “Siku ya Ufufuo.” Wanaamini kwamba Mahdi ataambatana na Yesu.)

 

    1.     Mwangalie huyu mnyama aliyepo juu ya nchi kwa uelewa huu wa siku zijazo unaoshikiliwa na Wakristo na Waislamu. Je, sasa hili linathibitisha mitazamo kadhaa juu ya mnyama aliyepo juu ya nchi? Je, mnyama aliyepo juu ya nchi inaweza kuwa ni muunganiko wa uwezo wa Marekani, Uislamu na Ukatoliki wakati ujio bandia wa mara ya pili utakapotokea? (Ninao marafiki wa Kikatoliki ambao huwa wanatania kwa kusema “Wakatoliki hawasomi Biblia.” Ninachodhani ni kwamba Wakristo wote (ikiwemo Wakatoliki) wasiosoma Biblia zao wataamini kile wanachokiona – kwamba Yesu amekuja. Waislamu watalipokea jambo hili kama Mahdi mtarajiwa. Ubandia huu wa Kishetani wa ujio wa Mara ya Pili utawaleta pamoja wanadamu wote wasio wanafunzi wa Biblia.)

 

    1.     Soma 2 Wathesalonike 2:11-12. Udanganyifu huu utakuwa na nguvu kiasi gani?

 

  1. Alama

 

    1.     Soma Ufunuo 13:16-18. Hapo awali tumejadili dhana ya kwamba alama ya “mkono” au “paji la uso” inamaanisha kwamba ama mtu alilazimishwa au alishawishiwa kuwekewa alama. Ni nini matokeo ya kukataa kujihusisha kwenye hii ibada ya uongo? (Kifo au maafa ya kiuchumi.)

 

      1.     Unapotafakari juu ya nafasi ya Marekani kwenye kipindi hiki cha kutisha, je, hii inaleta mantiki? (Utaona kwamba Marekani ni kiongozi kwenye teknolojia inayoweza kufanya jambo hili liwezekane. Kwa sasa, Marekani inafuatilia miamala mikubwa ya fedha. Waajiri wachache sana nchini Marekani wanawalipa waajiriwa fedha taslim. Ni nadra sana nanunua vitu kwa fedha taslim. Teknolojia imekuwa ya kisasa mno, kiasi kwamba kabla muuzaji hajanirejeshea kadi yangu ya mkopo (credit card), saa yangu inaniambia kuwa akaunti yangu imetozwa fedha!)

 

      1.     Soma Ufunuo 14:6-7. Ni nini mbadala mwingine wa wito wa ibada? (Ibada ya kweli ni kwa Mungu Muumbaji wetu.)

 

        1.     Mabishano gani ya kiteolojia yanahusianishwa na maelezo ya Uumbaji? (Uumbaji, Sabato ya siku ya Saba, ndoa ya jinsia tofauti, uhusiano kati ya wanadamu na wanyama. Sasa unaweza kuona mapambano yakijipangilia!)

 

    1.     Rafiki, hatari ni kubwa. Je, utajitoa kuwa mwanafunzi wa dhati wa Biblia ili usiweze kudanganyika?

 

  1.   Juma lijalo: Injili ya Mungu ya Milele.