Somo la 4: Rehema na Haki Katika Zaburi na Mithali
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: “Haki” na “rehema” ni maneno yenye mvutano wa asili kwa kila moja. Ni haki kukupatia kile unachokistahili! Ni rehema (huenda) kukulinda kupata kile unachostahili. Kama wanufaika wa rehema kuu ya Yesu, tunatakiwa kuwa makini jinsi tunavyozitumia hizi dhana mbili. Hatutaki kuoneshwa rehema kuu na Yesu, na kisha tukashindwa kuwaonesha wengine rehema. Mara zote swali ni hili, “Rehema ni nini katika mazingira haya?” Hebu tuone kile tunachoweza kujifunza kutoka kwenye Biblia kuhusu haki na rehema!
- Njia ya Haki ya Mungu kwa Watu Wanaokandamizwa
-
- Soma Zaburi 9:7-8. Kwa nini Mungu ameanzisha kiti chake cha enzi? (Kwa ajili ya hukumu!)
-
-
- Mungu anatoa hukumu ya aina gani? (Haki (usawa). Hii inamaanisha kuwa Mungu anatenda haki.)
-
-
-
- Angalia majukumu mawili ya Mungu yaliyobainishwa katika Zaburi 9:8. Mungu anausimamia ulimwengu kwa haki, na anatoa hukumu kwa usawa. Je, hiyo inamaanisha kwamba “haki” ya kweli inaakisi haki ya Mungu?
-
-
-
- Hebu tutumie hilo kwenye mgongano wa kisheria unaoendelea sasa hivi nchini Marekani. Hivi karibuni Mahakama Kuu ya Marekani ilitoa uamuzi kwenye kesi ambapo mwoka mikate (baker) alikataa kutumia utaalam wake kutengeneza na kupamba keki ya harusi kwa ajili ya “ndoa” ya mashoga. Mtu yeyote anaweza kununua kitu chochote kutoka dukani kwake, ni vile tu hakutaka kutengeneza keki maalum kusherehekea mambo ambayo mwoka mikate aliyachukulia kuwa si ya haki. Mungu angechukua uamuzi gani kwenye suala hili ikiwa tutatumia vigezo vya Zaburi 9:8? (Haki inamaanisha kuzingatia maadili.)
-
-
- Soma Zaburi 9:9 na Zaburi 9:16-18. Nimesikia ikisemwa, kwa kuzingatia mfululizo wa masomo haya, kwamba mara zote Mungu yuko upande wa watu wanaokandamizwa. Huo ndio unaoonekana kuwa ujumbe wa Zaburi 9:9. Hebu tutumie ujumbe huo kwenye suala letu la mwoka mikate. Je, “wanandoa” mashoga wanakandamizwa na mwoka mikate Mkristo?
-
-
- Je, mwoka mikate anakandamizwa na serikali, ambayo ilimtoza faini na kufunga sehemu ya biashara yake kwa kufuata dhamiri yake ya Kikristo?
-
-
- Angalia tena Zaburi 9:16. Tunapoambiwa kwamba wadhalimu “wamenaswa kwa kazi ya mikono yake,” hii inaashiria kuwa matokeo gani yanatokana na udhalimu? (Matatizo. “Kunaswa” ni kukamatwa kwenye wavu.)
-
-
- Je, mtu aliyenaswa kwenye wavu anakandamizwa? (Ndiyo. Hapa tunaona kwamba kwa kuwa tu mtu “anakandamizwa” haimaanishi kwamba Mungu yuko upande wake. Tunatakiwa kubainisha kwa nini mtu anakandamizwa.)
-
-
-
- Zaburi 9:16 inaashiria kuwa upi ulio msingi wa uamuzi wa kwamba Mungu anasimamia “upande” gani? (Mungu anaunga mkono haki. Wakati mwingine matokeo ya haki ni waovu kukandamizwa.)
-
-
- Soma Zaburi 101:1-4. Mfalme Daudi angefanya nini kama angekuwa mwoka mikate? (Hii zaburi ya Daudi inatuambia kuwa lengo lake ni “kutojihusisha” kufanya mambo ya “kuchukiza” au “maovu.” Hiki ni “kiwango cha dhahabu” kwa wale walio na imani kwa Mungu.)
- Utetezi wa Mungu kwa Maskini
-
- Soma Zaburi 82:1-4. Tatizo gani linaelezewa hapa? (“Miungu” ya watu hutetea vitendo visivyo vya haki na inawapendelea waovu.)
-
-
- Badala yake jambo gani linapaswa kutendeka? (Kuwaokoa wanyonge, wahitaji, maskini na wanaoonewa.)
-
-
-
- Nani anayesababisha matatizo kwa wahitaji na maskini? (Waovu.)
-
-
- Soma Mithali 22:7-9. Mpango wa asili wa mambo ukoje? (Wale wanaokopa fedha wanafanywa kuwa watumwa wa deni. Matajiri wanawatawala maskini. Ikiwa hutendi haki, utakabiliana na balaa. Nguvu zako zitavunjwavunjwa. Kama u mkarimu kwa maskini, utabarikiwa.)
-
-
- Unapata fundisho gani la jumla kwenye kauli hizi kuhusu umaskini na utajiri? (Kwa kawaida Mungu anapangilia mambo ya aina hii.)
-
-
- Soma Mambo ya Walawi 19:15. Mungu anataka haki ya aina gani itendeke? (Haki sawa.)
-
-
- Je, maskini wanapaswa kupokea haki kidogo kwa kuwa wao ni maskini?
-
-
-
- Je, matajiri wanapaswa kupokea haki kidogo kwa kuwa wao ni matajiri? (Jibu kwa maswali yote haya mawili ni “hapana.” Hupaswi kuadhibiwa kwa sababu wewe ni maskini au tajiri.)
-
-
-
- Hii inaashiria nini kuhusu Mungu kuunga mkono upande wa maskini na wanaoonewa? (Inaonesha huwezi kuchukua dhana hiyo. Mungu yuko upande wa haki. Bila kujali kama mtu ni maskini au tajiri, huo si msingi wa hukumu.)
-
-
- Soma Zaburi 146:1-4. Kwa nini tunapaswa kumgeukia Mungu kwa ajili ya utetezi wetu badala ya wanadamu? (Miongoni mwa sababu nyingine, wanadamu hufa!)
-
-
- Soma Zaburi 146:6. Tunapaswa kumtegemea Mungu kutokana na sababu gani nyingine? (Sio tu kwamba yeye ana nguvu sana na aliumba kila kitu, bali pia ni mwaminifu.)
-
-
- Soma Zaburi 146:7-9. Kuna kauli mbili kwenye hivi vifungu vinavyoonekana kukinzana. Tunaambiwa kwamba Mungu “hufungua waliofungwa” na “huwapenda wenye haki.” Kuwafungulia wafungwa ili kuwadhuru wengine sio kitendo cha dhahiri cha upendo. Utatatuje mgogoro huu wa dhahiri? (Kinachoonekana ni kwamba wafungwa wamefungwa kimakosa. Kwa kuwa Mungu “huipotosha njia ya wasio haki” (kifungu cha 9), atawaacha wafungwa hatari wakae gerezani.)
-
-
- Utaona kwamba kifungu cha 7 kinatuambia kuwa Mungu “huwapa chakula wenye njaa.” Je, hiyo inatuweka huru? (Je, sisi si washirika katika kuyatenda mapenzi ya Mungu hapa duniani?)
-
-
- Soma Mithali 10:3-5. Hii inazungumzia nini kuhusu Mungu na njaa? (Mungu hawaachi wenye haki wawe na njaa.)
-
-
- Je, hiyo inamaanisha kuwa Mungu anapendelea wasio haki kuwa na njaa?
-
-
-
- Mtazamo wa Mungu ni upi juu ya uvivu? (Huleta umaskini.)
-
-
-
- Ujumbe wa jumla wa Mithali 10:3-5 ni upi? (Ikiwa una bidii utalishwa na utakuwa na mali. Ukiwa wewe ni mvivu na unapendelea kulala, wewe unaaibisha na ni maskini.)
-
-
-
- Hebu turejee kwenye hii dhana ya kwamba mara zote Mungu yuko upande wa wanyonge. Ingetokea ukamwona mtu mwenye fedheha na maskini, je, moja kwa moja ungesema kwamba Mungu amempendelea mtu huyu? (Kifungu hiki kinafundisha kinyume chake – kinaendana na kanuni za Mungu kwamba mtu mvivu, yule anayependelea usingizi badala ya kazi, hatafanikiwa.)
-
-
-
-
- Mkristo mwenye rehema anapaswa kumfanyia nini mtu mvivu? (Kumhamasisha kufanya kazi na kutumia saa ya kengele ili kumwamsha.)
-
-
-
-
- Bill Clinton alipokuwa rais wa Marekani, wanachama wa vyama vya Republican na Democrat walikubaliana juu ya marekebisho ya Ustawi wa Jamii. Marekebisho hayo yalitengeneza ukomo wa miaka mitano wa masuala ya Ustawi wa Jamii, na idadi ya watu wanaopokea huduma za Ustawi wa Jamii ilipungua sana. Unadhani nini kilitokea kwa maskini kutokana na jambo hili? Je, utapendelea au utapingana na ukomo wa huduma za Ustawi wa Jamii? Mungu anasemaje? (Baada ya marekebisho haya kupitishwa, ajira za akina mama wenye ujuzi mdogo kabisa ziliongezeka, “kiwango cha umaskini kwa watoto weusi na familia zenye mzazi mmoja kilipungua sana kwa viwango vyote vilivyopata kuwepo kihistoria.” (Heritage Foundation Backgrounder No. 1620, February 6, 2003.) Hii inatoa uthibitisho wa mtazamo wa Mungu kwamba kazi ndio tiba ya umaskini.)
-
-
-
-
- Je, hitimisho hili kuhusu kazi kuwa tiba ya msingi kwa umaskini limejengwa kwenye huu msitari mmoja tu wa Biblia? (Hapana. Maelekezo ya Agano la Kale kuhusu masazo ya mavuno na marejesho ya ardhi katika sherehe za Jubilei vinahusu kuwasaidia maskini waweze kujilisha.)
-
-
-
-
- Juma hili nilienda Taco Bell (mgahawa ninaoupenda sana) na mmojawapo wa wafanyakazi alikuwa anaondoka na wanaye wawili wa kiume. Huwa ninauepuka mgahawa huu kwa sababu mfanyakazi huyu hawezi kumudu gharama za kuwapeleka kwenye kituo cha malezi ya watoto na hataki kuwaacha wanaye wakirandaranda ovyo. Bila shaka, si mama wala wanaye wanalichukulia jambo hili kuwa ni la kimaadili. Anafanya kazi. Rehema ni nini? Hapa haki ni ipi?
-
- Katikati ya Barabara
-
- Soma Mithali 30:7-9. Lengo la maisha yetu linapaswa kuwa lipi?
-
-
- Kwa nini utajiri na umaskini vyote ni hatari kwa roho zetu?
-
-
- Rafiki, je, utamwomba Roho Mtakatifu akusaidie kuyaona mazingira yanayohusisha haki na rehema kwa namna ambayo Mungu anayaona?
- Juma lijalo: Kilio cha Manabii.