Somo la 4: Kutoka Kwenye Tanuru Hadi Ikulu

Somo la 4: Kutoka Kwenye Tanuru Hadi Ikulu
Swahili
Year: 
2020
Quarter: 
1
Lesson Number: 
4

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

 

Utangulizi: Umewahi kuwa kwenye kundi la watu waliosimama kumsifia mtu? Vipi kama hukukubaliana kwamba sifa hizo za pekee hazikumstahili? Je, ulisimama hivyo hivyo tu? Umewahi kuwa kwenye kanisa ambapo watu waliotaka kufanya agano jipya na Mungu walitakiwa kusimama, na uliridhika na agano lako la sasa? Kama ulisimama kwa kufuata mkumbo, au ulijiangalia namna utakavyoonekana mbele za watu, fikiria kama maisha yako yalitegemea kusimama kwako? Kwa watu wengi, dhambi inawapata kutokana na maamuzi madogo. Sio, kama tunavyojifunza juma hili, uamuzi mmoja mkubwa wa dhahiri, unaojenga mwelekeo wa maisha au kifo. Hebu tuzame tena kwenye kisa chetu cha Danieli na marafiki zake!

 

 1.     Sanamu

 

  1.     Soma Danieli 3:1. Sanamu hii ina urefu sawa na Mnara wa Uhuru (Statue of Liberty) wa Jiji la New York. Unadhani kitu gani kilimhamasisha Mfalme Nebukadreza kutengeneza sanaa hii yenye urefu wa ghorofa kumi? (Ni matokeo ya ndoto tuliyojifunza juma lililopita.)

 

   1.     Je, Nebukadreza amechukua leseni ya sanaa kwenye ndoto yake? (Soma Danieli 2:37-38. Kwenye ile ndoto, kichwa pekee ndicho kilichotengenezwa kwa dhahabu. Kichwa kilimwakilisha Nebukadreza na ufalme wake. Lakini, sasa sanamu yote inaonekana kumwakilisha yeye. Bila shaka ndio maana uso ulitengenezwa kwa sura ya Nebukadreza.)

 

    1.     Tukiachilia mbali majivuno na kiburi/majisifu, kwa nini Nebukadreza anafanya mabadiliko haya? Ingegharimu kidogo kwa kuwa mwaminifu kwenye ndoto! (Kuwa mwaminifu kwenye ndoto kungeutangazia ulimwengu kwamba ufalme wa Nebukadreza ulikuwa wa muda mfupi na utukufu wake ni wa kupita tu.)

 

  1.     Soma Danieli 3:2-3. Je, hii ni “tiketi ya nadra” mjini? Je, hii ni tunu/wakfu ambao ungependa kualikwa ili kuonyesha kwamba wewe ni mtu wa muhimu? (Kama ungekuwa sehemu ya uongozi wa taifa, kama ungekuwa “mfu fulani mkubwa,” basi ungependa kualikwa!)

 

 1.   Changamoto

 

  1.     Soma Danieli 3:4-6. Je, sasa ungependa kualikwa?

 

   1.     Soma Danieli 2:46-47. Ni kwa jinsi gani Nebukadreza alitoka nje kabisa ya msitari?

 

    1.     Unadhani wenye maarifa wengine walikuwa na la kujihusisha na jambo hili? Je, hii ndio njia ya kumrudia Danieli? (Ikiwa ndivyo, basi kwa dhahiri wamesahau kwamba aliyaokoa maisha yao. Hata hivyo, kwa sasa yeye ni bosi wao. Angalia Danieli 2:48.)

 

   1.     Tishio la kifo katika Danieli 3:6 linatuambia nini kuhusu mtazamo wa ulodi wa Nebukadreza? (Kuna jambo haliko sawa ikiwa anawatishia kwa kifo cha papo hapo. Huenda wao ni waaminifu kwa miungu yao. Huenda wenye hekima bado wana hasira kutokana na uzoefu wao wa kunusurika kifo unaokumbushiwa na sanamu hii.)

 

   1.     Tutaona hapo baadaye kidogo (Danieli 3:12) kwamba Danieli hayupo. Hili linawezekanaje? Je, yeye si mtu wa dhahiri kabisa kuliko wote (tofauti na Nebukadreza) kutakiwa kuwepo? (Tutajadili hili kwa kina zaidi baadaye, lakini kutokuwepo kwa Danieli linaonekana jambo lisilo la kawaida kabisa. Zingatia kwamba maoni ya mtu mmoja yanaashiria kwamba tukio hili lilitokea takriban miaka 18 baada ya ndoto.)

 

  1.     Soma Danieli 3:7. Je, palikuwepo na tatizo lolote miongoni mwa watu, kwa mujibu wa kifungu hiki, kuhusiana na kuabudu sanamu? (Hapana.)

 

  1.     Soma Danieli 3:8-12. Unadhani kwa nini wanajimu hawa walijitokeza kutoa taarifa ya marafiki watatu wa Danieli? (Jambo moja la msingi linaweza kuwa kwenye lugha ya “uliowaweka juu ya mambo ya wilaya ya Babeli.” Wanaona wivu juu ya nafasi zao. Fikiria ufidhuli (kuvunjiwa heshima) wa watumwa kupandishwa hadhi na kuwa juu yako! Huenda wanajimu wana hamu ya kutunza heshima ya miungu yao.)

 

   1.     Hapo awali niliuliza kuhusu Danieli. Unadhani marafiki hawa walikuwa miongoni mwa kundi la watu wakati amri ya kuabudu sanamu ilipotolewa? (Sijui. Vinginevyo, ingejulikana mara moja kwamba walikataa. Kwa namna fulani hivi Danieli na marafiki zake waliweza kujiepusha kuwa kwenye kundi amri ilipotolewa.)

 

   1.     Kwa nini wanajimu hawakumtaja Danieli? (Hatujui. Kwangu naona kuna uwezekano mdogo kwamba Danieli alipanga safari kwa ajili yake na bila kuhusisha marafiki zake. Ubashiri wangu bora kabisa ni kwamba wanajimu hawa waliogopa kumwingiza Danieli kwenye changamoto hii.)

 

  1.     Soma Danieli 3:13-14. Unaelezeaje badiliko kati ya Danieli 2:46-47 na mtazamo wa sasa wa Nebukadreza? (Majivuno yanampotosha mtu.)

 

   1.     Kwa mtazamo wa kisheria, unaona jambo gani zuri kwenye vifungu hivi? (Nebukadreza anawapatia “fursa ya kujitetea.” Hachukulii tuhuma kuwa za kweli, anakabiliana na marafiki wa Danieli kwa tuhuma zilizotolewa na kuwaruhusu kujibu.)

 

  1.     Soma Danieli 3:15-16. Nebukadreza anawaonesha rehema gani nyingine? (Anawapatia fursa nyingine. Hii inabainisha kwamba suala la kuabudu sanamu lilikuwa linakuwa jambo la kawaida.)

 

   1.     Marafiki watatu wa Danieli wanapata fursa ya kujitetea, lakini wanasema kuwa hawana haja ya kujitetea. Kwa nini? (Wanamkumbusha tu Nebukadreza juu ya kile alichokikiri katika Danieli 2:46-47. Kimsingi wanasema, “unamjua Mungu wetu na unafahamu kwa nini hatuwezi kufanya hivi.”)

 

  1.     Soma Danieli 3:17-18. Hii ni kauli ya kufurahisha sana katika somo letu la juma hili. Je, wanaelezea upungufu wa imani kwa Mungu wanapokiri kwamba anaweza asiwaokoe? (Ninapenda kauli hii. Kwanza, wanakiri kwamba Mungu wao ana uwezo wa kuwaokoa. Pili, wanakiri kwamba wanaamini kuwa Mungu atawaokoa. Lakini, wanakiri kwamba hawana udhibiti na wanaweza kufa.)

 

   1.     Kwa nini kukiri kwamba inawezekana wasiokolewe? (Tafakari kile kilicholitokea taifa lao. Hawatamtabiri Mungu wao au kumpa masharti. Sehemu ya uaminifu wao kwa Mungu ni kukiri kwamba yeye ndiye mwenye udhibiti.)

 

  1.     Soma Danieli 3:19-20. Je, Nebukadreza ana tatizo la kushindwa kudhibiti hasira? Unadhani ana hasira kwa sababu ana ufahamu zaidi? (Tunafahamu kwamba hapo baadaye Nebukadreza anadhihirisha tatizo kubwa la ugonjwa wa akili (Danieli 4:29-33) ambalo ni matokeo ya majivuno yake.)

 

   1.     Soma tena sehemu ya mwisho ya Danieli 3:15. Hii inakuambia nini kuhusu majivuno ya Nebukadreza?

 

  1.     Soma Danieli 3:21-23. Kama ungetupwa motoni, je, ungedhani kwamba Mungu aliamua kutokukuokoa?

 

  1.     Soma Danieli 3:24-25. Je, Mungu atasubiri hadi dakika ya mwisho ili kukuokoa?

 

   1.     Una mtazamo gani kuhusu mtu wa nne ndani ya moto? (Nebukadreza anamuita “mwana wa miungu.” Ninaamini kwamba huyu ni Yesu (kabla hajafanyika kuwa mwanadamu) Mwana wa Mungu.)

 

   1.     Hii inatuambia nini kuhusu Yesu? (Anaweza asituepushe na matatizo, lakini yu pamoja nasi motoni.)

 

 1. Matokeo

 

  1.     Soma Danieli 3:26-27. Kwa nini Nebukadreza anawaita “watumishi wa Mungu Aliye Juu,” na kwa nini hana ghadhabu tena?

 

   1.     Je, uamuzi wa marafiki watatu wa Danieli umempa Mungu utukufu?

 

  1.     Soma Danieli 3:28-29. Utaona Mfalme akikiri kwamba wamemshinda, lakini ghadhabu yake imeisha na mtazamo wake umebadilika kabisa. Hii inatufundisha nini kuhusu matatizo yako na mwajiri wako? (Mungu anaweza kubadili mambo ikiwa tutasalia kuwa waaminifu.)

 

   1.     Je, unaona kwamba Nebukadreza ana tabia ya kipekee?

 

  1.     Jiweke kwenye nafasi ya wanajibu waliotoa taarifa juu yao. Maisha yanawaendeaje?

 

   1.     Hii inatuambia nini kuhusu matatizo maishani? (Bila kujali kama tunamfuata Mungu au la, tutakabiliana na matatizo. Manufaa ya kumfuata Mungu ni kwamba ana mamlaka juu ya kila kitu na kila tatizo.)

 

  1.     Rafiki, je, umetafakari upande wa kuchukua maishani? Kwa nini usidhamirie, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kuwa mwaminifu na kumpa Mungu utukufu? Patakuwepo na kupandishwa daraja kutokana na hilo!

 

 1.   Juma lijalo: Toka Kiburi Hadi Unyenyekevu.