Somo la 11: Toka Vita Hadi Ushindi
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Juma hili tunaanza somo letu la njozi kubwa ya mwisho ya Danieli. Sasa Danieli ni mzee, yumkini ana umri wa takriban miaka 90. Katika njozi zilizotangulia Danieli ameonyeshwa mkondo wa historia miongoni mwa mataifa. Juma hili tunaona kipengele kingine makinifu cha historia – upande usio wa kawaida wa pambano. Hebu tuzame kwenye somo letu la Danieli na tuliangalie jambo hili kwa mtazamo tofauti!
- Ufunuo
-
- Soma Danieli 10:1. Tarehe hii, mwaka wa tatu baada ya Koreshi, inatuambia nini? (Kwa mujibu wa “Bible Knowledge Commentary” huu ni mwaka 536 K.K. Mateka wa Kiyahudi wameanza kurejea na kujenga upya hekalu. Danieli 1:21 inaashiria kwamba hivi karibuni Danieli amestaafu nafasi yake ya juu katika utawala wa kifalme.)
-
-
- Ufunuo huu unajihusisha na kitu gani? (“Vita vikubwa.”)
-
-
-
- Je, Danieli analielewa hilo? (Inaonekana maono yaliyomjia mara baada ya jambo hilo yalimsaidia Danieli kuelewa.)
-
-
- Soma Danieli 10:2-3. Kwa nini Danieli anaomboleza? (Soma Danieli 10:12. Danieli amefadhaika kutokana na maono ya vita vikubwa na anaomba na kufunga ili Mungu amsaidie kuelewa yanachomaanisha. Inaonekana kwamba maono ya “mara baada ya hapo” ni majuma matatu baadaye.)
-
-
- Soma Danieli 1:8 na Danieli 1:12-13. Angalia jambo tuliloligusia hapo kabla, chakula cha Danieli kimebadilika. Kwa nini? Je, ni kwa sababu unapofikisha umri wa miaka 90 unaweza kula chochote unachokitaka? (Hii inaimarisha hitimisho letu la awali kwamba matendo ya Danieli katika sura ya 1 sio kwamba yanaunga mkono chakula cha aina ya mbogamboga, bali ni kuepuka nyama iliyotolewa kwa ajili ya miungu na ambayo haijaandaliwa vizuri. Katika hatua hii maishani mwake Danieli ana udhibiti juu ya namna chakula chake kinavyoandaliwa.)
-
- Mjumbe
-
- Soma Danieli 10:4-5 na Danieli 10:12. Ujumbe gani unapelekwa kwa Danieli? (Maombolezo ya Danieli na kufunga kwake ili kuelewa maono haya kuhusu vita vikubwa yamesikiwa. Mjumbe huyu amekuja kumpa Danieli uelewa.)
-
- Soma Danieli 10:5-6 na Ufunuo 1:13-16. Kama ungekuwa polisi, na ukawa unachukua maelezo ya Danieli na Yohana, je, ungedhani kwamba walimwona mtu mmoja?
-
-
- Unadhani mjumbe huyu ni nani? Kwa taarifa za ziada soma Danieli 10:10-13. (Ingawa maelezo ya kwanza yanaonekana kama maelezo ya Yesu katika kitabu cha Ufunuo yanaashiria kwamba huyu ni Yesu katika maeneo yote mawili, ni vigumu kuamini kwamba Yesu “alipelekwa” au angeweza kucheleweshwa kutokana na upinzani. Kwa kuongezea, kuna sababu za kutosha kuamini kwamba Mikaeli ni Yesu (angalia Ufunuo 12:7), na Mikaeli ni tofauti na mjumbe huyu. Hiyo inanifanya nihitimishe kwamba Gabrieli ndiye mjumbe aliyekuja kwa mara nyingine tena kwa Danieli.)
-
-
- Soma Danieli 10:7-9. Kwa nini watu wale ambao hawakumwona mjumbe wala maono walijificha? (Hii inaakisi uwezo wa kutisha wa viumbe wa mbinguni. Hatupaswi kusahau kipengele hiki cha malaika.)
-
- Soma Danieli 10:10-11. Tunajifunza nini kuhusu jinsi Mungu anavyojali uelewa wetu? (Danieli ni kielelezo kwetu katika kutafuta kuyaelewa mapenzi ya Mungu kwa dhati. Mungu anajibu kiu ya kutaka kuelewa neno lake.)
- Vita ya Kiroho
-
- Soma Danieli 10:12-13. Je, mfalme wa duniani angeweza kumchelewesha Gabrieli kwa muda wa siku 21? Je, Yesu (Mikaeli) alikuwa na haja ya kumsaidia Gabrieli ili kumshinda mwanadamu? (Kwa dhahiri jibu ni “hapana.” Kumbuka kwamba wale watu waliokuwa karibu na Danieli walitishwa na uwepo wa Gabrieli. Danieli aliachwa peke yake bila msaada (Danieli 10:7-8).)
-
-
- Soma Yohana 12:28-31, Yohana 14:30-31 na Yohana 16:10-11. Vifungu hivi na muktadha wa Danieli 10 vinaashiria nini kwako kuhusu asili ya “mkuu wa ufalme wa Uajemi? (Hii inaashiria kwamba mkuu huyu ni malaika aliyeangushwa.)
-
-
-
-
- Vifungu vya kitabu cha Yohana vinamzungumzia Shetani kama mkuu wa ulimwengu. Hii inaashiria nini kuhusu malaika aliyeangushwa aitwaye mkuu wa Uajemi? (Hii inanifanya nifikiri kwamba huyu si Shetani mwenyewe, bali mmojawapo wa makanali wake aliyepewa jukumu la kufanya kazi na Koreshi.)
-
-
-
-
- Je, hii inatuambia kilichomhamasisha Shetani kujaribu kumzuia Gabrieli asimpe Danieli ujumbe wake? Au, Gabrieli anaelezea tu matatizo ya kikazi ambayo amekumbana nayo hivi karibuni? (Soma tena Danieli 10:12. Gabrieli analeta tafsiri ya maono haya ambayo Danieli ameyapokea. Hoja nzuri inaweza kujengwa kwamba Shetani alimchelewesha Gabrieli kwa sababu hataki Danieli aelewe maono haya.)
-
-
-
-
- Tutaendelea kujifunza maono haya katika kipindi cha majuma mawili yajayo. Hii inaashiria nini kuhusu umuhimu wa maono haya?
-
-
-
-
- Je, umewahi kuombea jambo fulani na ikaonekana kana kwamba jibu limecheleweshwa? Je, umewahi kuchukulia kwamba panaweza kuwepo na viashiria visivyo vya kawaida katika jambo hili? (Soma Waefeso 6:12. Paulo anatuambia kwamba pambano kuu tunalokabiliana nalo ni dhidi ya nguvu za kiroho zinazoambatana na Shetani!)
-
-
- Soma Danieli 10:14. Danieli anaambiwa kwamba maono yanawahusu “watu wako” katika “siku nyingi bado.” Watu wa Danieli ni akina nani? (Israeli. Wayahudi.)
-
-
- Kwa kuwa somo letu juu ya maono litaendelea kwa majuma mawili yanayofuata, na yanafikia mwisho wa nyakati, nataka ukumbuke kwamba Gabriel anasema kuwa hii inawahusu Wayahudi. Nina wasiwasi kwamba hatuchukulii kuhusishwa kwa “watu wa Danieli” kwa umakini wa kutosha tunapotafakari nyakati za mwisho.)
-
-
- Soma Danieli 10:15-17. Kwa nini maelezo ya siku zijazo yanamtaka Danieli azungumze? Nilidhani wajibu wake ulikuwa ni kusikiliza kwa makini tu! (Hii haileti mantiki yoyote isipokuwa kama mazungumzo ni ya kubadilishana mawazo. Lazima inamaanisha kwamba Danieli anauliza maswali pale asipoelewa.)
-
- Soma Danieli 10:18-19. Malaika wa Mungu watatufanyia nini? (Watatutia nguvu. Wanaweza kututia moyo.)
-
- Soma Danieli 10:20. Gabrieli anakwenda wapi baada ya hapa? (“Kupigana” dhidi ya mkuu wa Uajemi na mkuu wa Uyunani.)
-
-
- Mkuu wa Uyunani ni nani? (Lazima huyu atakuwa mmojawapo wa makanali wa juu wa Shetani ambaye anaangalia masuala ya Uyunani. Utaona kwamba maono ya awali ya Danieli yanabainisha kwamba Uyunani unaufuatia Umedi na Uajemi kama mtawala wa dunia.)
-
-
- Soma Danieli 10:21. Gabrieli anawezaje kusema kuwa hana wa kumsaidia isipokuwa usaidizi kutoka kwa Yesu (Mikaeli)? Kwani mbingu yote haipo chini yake? (Sidhani kama Gabrieli anazungumzia kile kinachoweza kutokea, anamwambia tu Danieli kuhusu mtu aliyepewa jukumu kwenye hili pambano mahsusi.)
-
-
- Gabrieli anaposema kuwa Mikaeli ni mkuu wa Danieli, je, hii inamaanisha kwamba Danieli ni mtu wa muhimu sana kiasi kwamba Mikaeli amepewa jukumu la kuwa naye? (Kama kweli Mikaeli amekabidhiwa kwa Danieli, hiyo inasababisha matatizo makubwa kwa imani ya kwamba Mikaeli ni Yesu. Huenda Gabrieli anathibitisha tu kwamba Mikaeli yuko upande “wetu,” upande wa watu wa Mungu.)
-
-
- Hebu tupitie tena Danieli 10:13. Tulipojadili ucheleweshaji huu hapo awali, nilidhani ulihusisha jambo linaloonekana kivitendo, kwa sababu Gabrieli alihitaji msaada. Ikiwa Gabrieli anarejea kwenye hili “pambano” (Danieli 10:20), je, hili linaonekana kuwa pambano halisi kivitendo? (Kama ungekuwa unapambana kimwili, kuna uwezekano mdogo kwamba ungechukua mapumziko na kurudi baadaye.)
-
-
- Hili linaweza kuwa pambano la namna gani? (Tunafahamu kwamba Mfalme Koreshi wa Uajemi alikuwa anawasaidia watu wa Mungu kurejea Yerusalemu na kulijenga upya hekalu. Pia tulijifunza jinsi ambavyo jambo hili halikwenda vizuri. Hitimisho lenye mantiki ni kwamba Gabrieli (kwa msaada wa Mikaeli) anamtia moyo Koreshi kutenda jambo sahihi. Mkuu wa Uajemi, mshirika wa Shetani, anamtia moyo Koreshi kutenda jambo lisilo sahihi.)
-
-
-
- Una wajibu gani kwenye aina hii ya pambano la kiroho? (Unatakiwa kuwa na ufahamu wa pambano linaloendelea katika mazingira yanayokuzunguka. Na, unatakiwa kuwa na ufahamu kwamba unaweza kuwa wa msaada kwenye pambano linalohusisha vita ya kiroho ya watu wengine!)
-
-
- Rafiki, je, utamwomba Roho Mtakatifu akusaidie umfuate Mungu na kuwa mshirika hai na makinifu katika vita vya kiroho vinavyoendelea mahali kote kutuzunguka?
- Juma lijalo: Toka Kaskazini na Kusini Hadi Nchi Nzuri.