Somo la 9: Uumbaji: Mwanzo Kama Msingi – Sehemu ya 2
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2017, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, kitabu cha Mwanzo na Sayansi haviko sawa? Ikiwa umejibu, “ndiyo,” haipaswi kuwa hivyo. Kama tulivyojadili hapo awali, Zaburi 19:1 inatuambia kuwa mbingu na nchi zauhubiri utukufu wa Mungu. Kiini cha utukufu wa Mungu ni Uumbaji wake. Hivyo, tatizo linaanzia wapi? Je, linatokana na kutoelewa tangazo linalotolewa mbinguni na duniani? Je, linatokana na kutoielewa Biblia? Je, linaibuka kwa sababu nguvu za uovu zinataka kusababisha ugomvi? Hebu tuchimbue Biblia yetu ili tuone kile tunachoweza kujifunza!
- Uongo Mwepesi
-
- Soma Isaya 40:21-22. Je, umesikia kuwa Wakristo wa zamani walijenga hoja kwamba dunia ina umbo bapa?
-
-
- Ikiwa ndivyo, lengo la kutaarifu hoja hiyo ni lipi? (Kuonyesha kwamba wafuasi wa Mungu ni wajinga na wanapingana na sayansi.)
-
-
-
- Kifungu hiki kinafundisha nini kuhusu umbo la dunia? (Kinaiita dunia kuwa ni “duara.”)
-
-
- Soma Ayubu 26:10 katika tafsiri ya KJV au ESV. Tafsiri ya ESV inasema “amepiga duara juu ya uso wa maji.” Tafsiri ya KJV inasema “amepiga mzingo juu ya uso wa maji.” Vifungu hivi vinaelezea umbo la namna gani? (“Mzingo” unarejelea mduara – ambao unaelezea umbo la duara.)
-
-
- Kifungu kinarejelea “maji.” Je, hii inafanana na kuelezea umbo la dunia? (Mwanzo 1:6-7 inazungumzia kutenganisha maji yaliyo juu ya anga na yaliyo chini ya anga. Hii inaashiria duara kati ya maji na maji.)
-
-
-
- Je, duara linafanana na tufe? (Hapana. Lakini inaonekana kuwa na mantiki kuelewa rejea ya duara kuwa kama tufe au umbo lenye duara bapa )circular flat plane.))
-
-
- Soma Ufunuo 20:7-8 na Ufunuo 7:1. Je, duara linaweza kuwa na kona? (Hapana.)
-
-
- Je, vifungu hivi vinajenga msingi wa kuamini katika dunia iliyo na umbo bapa? (Bado tunarejelea “kila pembe ya nchi,” bila kuchukulia kwamba kimsingi umbo la dunia lina pembe/kona.)
-
-
- Unapoendelea kutafakari vifungu tulivyovisoma hivi punde kuhusu umbo la dunia, unapaswa kuhitimishaje? (Biblia haitoi kauli yenye mamlaka kuhusu umbo la dunia. Unaweza kujenga hoja juu ya tufe, au ubapa, au meza.)
-
-
- Ikiwa mtu atadai kuwa Mungu alibainisha kwamba dunia ni bapa, hili linapaswa kuangaliwaje? (Kama kauli ya Biblia iliyokosewa.)
-
- Biblia Kama Utaratibu wa Mpangilio wa Muda
-
- Soma Mwanzo 5:1-3 na Mwanzo 5:32. Kisha pitia kwa haraka haraka vifungu vilivyosalia kati ya kifungu cha 3 na 32. Je, itakuwa na mantiki kuhitimisha kwamba unaweza kukokotoa kipindi cha muda kuanzia kuumbwa kwa Adamu hadi kipindi cha gharika? (Kwangu hiyo inaonekana kuwa na mantiki.)
-
- Soma Mwanzo 11:10-11 na Mwanzo 11:24-26. Kisha pitia kwa haraka haraka vifungu vilivyosalia hapo katikati. Kitu gani kimetokea kwenye umri wa kuishi wanadamu?
-
-
- Unadhani kwa nini Mungu ameweka taarifa hii kwenye Biblia? (Inaonesha kwamba wale walioishi kabla ya gharika waliishi kwa miaka mingi zaidi kuliko wale walioishi baada ya gharika.)
-
-
-
-
- Ukweli huu unaashiria nini kwako? (Dunia ilikuwa tofauti sana baada ya gharika.)
-
-
-
-
- Unadhani tunaweza kutumia mipangilio hii ya mida kubainisha umri wa dunia?
-
-
-
-
- Ikiwa umesema kuwa, “ndiyo,” unalinganishaje mtafaruku wa dhahiri dhidi ya sayansi? (Sayansi inaonekana kuonesha kuwa muda kule mbinguni umeonekana kuwa yunifomu (unalingana). Lakini, upunguaji mkubwa wa umri wa kuishi baada ya gharika unaashiria kwamba hali/tabia za dunia hazikuwa yunifomu. Hivyo, “kutarehesha” vitu hadi katika kipindi kabla ya gharika huhusisha dhana ambazo yumkini hazina sababu/mashiko.)
-
-
- Agano Jipya na Uumbaji
-
- Soma Mathayo 19:4-5. Hivi karibuni tuliangalia kifungu hiki katika kutafakari maelezo ya Uumbaji kama msingi wa kutatua migogoro ya kiteolojia. Hebu tuliangalie katika mtazamo mwingine. Hii inatuambia kwamba Yesu alifikiria nini kuhusu usahihi wa maelezo ya Uumbaji? (Yesu halichukulii kama uzushi au istiari. Anaichukulia kama ukweli wa kihistoria.)
-
-
- Ikiwa wanadamu waliibuka, itakuwa na athari gani kwa Yesu kurejelea chanzo cha wanaume na wanawake kwa namna hii?
-
-
- Soma Luka 11:50-51. Ni sehemu gani nyingine ya maelezo ya kitabu cha Mwanzo ambayo kwa mahsusi Yesu anaiidhinisha? (Anatoa nukuu ya jumla juu ya “mwanzo wa ulimwengu.” Lakini, baadaye anaidhinisha maelezo ya mauaji ya Habili baada ya anguko. Yesu hana mashaka yoyote kuhusu jinsi kitabu cha Mwanzo kinavyoelezea Uumbaji na anguko la wanadamu.)
-
- Soma Yohana 1:1-3. Tunaamini kwamba Roho Mtakatifu aliivuvia Biblia. Hapa tunajifunza nini kuhusu asili ya wanadamu na Mungu Muumbaji wetu? (Agano la Kale na Jipya yanaendana na maelezo ya Uumbaji. Hakuna dokezo la nadharia ya uibukaji.)
-
- Soma Matendo 14:15. Ukuu wa Mungu wetu umejengwa juu ya nini? (Tofauti na “mambo yasiyo ubatili” (miungu mingine), Mungu wetu aliumba mbingu na nchi.)
-
- Soma Warumi 1:18-20. “Ukweli” gani kumhusu Mungu unakandamizwa? (Ukweli wa Mungu unatokana na uumbaji wake.)
-
-
- Hiki ni mojawapo tu ya vifungu vingi katika Biblia ambavyo Mungu anajenga msingi wa madai yake ya kuabudu kwenye ukweli wa uumbaji wake wa mbingu na nchi. Kama tunayakataa maelezo ya Uumbaji, tumebakiwa na nini kwenye madai yetu ya kumwamini Mungu?
-
-
-
- Kama unaikubali nadharia ya uibukaji, utajengaje hoja kwenye ukuu wa Mungu wetu dhidi ya miungu mingine? Utatumia njia gani?
-
-
- Soma Yakobo 3:9. Yakobo anatumiaje imani yake juu ya maelezo ya Uumbaji kujenga fundisho kuhusu jinsi tunavyopaswa kuwatendea watu wengine? (Kuamini kwamba wanadamu wameumbwa kwa mfano wa Mungu hututia moyo kuwatendea vyema.)
-
-
- Ikiwa unaamini katika utokeaji wa mambo kwa njia ya asili, hiyo inahabarishaje juu ya namna unavyowatendea wanadamu wengine?
-
-
- Soma Warumi 5:12-14. Uelewa wetu wa dhambi umejengwaje juu ya Maelezo ya Uumbaji?
-
- Soma Warumi 5:15. Uelewa wetu juu ya haki kwa imani pekee umejengwaje juu ya Maelezo ya Uumbaji?
-
-
- Imani yetu itakuwa tofauti kiasi gani ikiwa hatukuamini kwamba kitabu cha Mwanzo ni maelezo ya kweli, na kudhani kwamba maelezo hayo yalikuwa ya uongo au analojia?
-
-
- Juma hili nilikuwa ninasikiliza mazungumzo baina ya mke wangu na kaka yake. Walikubaliana kwamba takriban kila mtu aliyekuwepo maeneo yanayozunguka nyumbani kwao wakati walipokuwa wanakua alikuwa marehemu. Je, itakuwa jambo la kawaida sana kumwamini Mungu aliyeweka matamanio yake kwetu, na ambaye ametuahidi uzima wa milele ikiwa tutamwamini?
-
-
- Kuna motisha gani ya kutufanya tuamini kwamba Mungu hana matamanio ya pekee kwa wanadamu au mustakabali wetu?
-
-
- Soma Warumi 1:21-23. Nini kinawafanya wanadamu kuyakana madai ya Mungu kwamba yeye ndiye Muumbaji wao? Kwa nini wamkanie huo utukufu? (Kwa sababu wao ni wapumbavu, wakijidai kwamba ni werevu.)
-
-
- Kama umefanya utafiti juu ya historia ya familia yako, ulitarajia kupata matokeo gani? (Kwamba ufalme au watu waliofanikiwa sana ndio mababu zako.)
-
-
-
- Je, mtu yeyote mwenye busara ana matumaini ya kubaini kwamba mababu zake walikuwa masokwe?
-
-
-
-
- Tafakari kazi ya “mauzo” ambayo Shetani ameweza kuitimiza kwa kufanya asilimia kubwa ya watu waamini kwamba wametokana na ngedere badala ya kuumbwa kwa mfano wa Mungu! (Kwa dhahiri imani hii sio ya kawaida. Inaonesha kwamba kuna wakala hai anayejenga hoja dhidi ya kanuni za Biblia.)
-
-
-
- Rafiki, je, somo hili linakukumbusha kwamba imani yetu katika maelezo ya kitabu cha Mwanzo ndio kiini cha teolojia yetu kwa kiasi kikubwa sana? Je, utadhamiria kuishikiza imani yako katika Biblia, na kuangalia namna ya kuilinganisha na madai ya sayansi?
- Juma lijalo: Biblia Kama Historia.