Somo la 6: Uwezekano Usio na Kikomo
Somo la 6: Uwezekano Usio na Kikomo
(1 Wakorintho 12, Mathayo 25)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Ni nini hasa maana ya kushuhudia? Je, ni lazima iwe ufafanuzi wa injili? Ikiwa ndivyo, je, ni kweli kwamba kila Mkristo ana wajibu wa kushuhudia? Vipi kuhusu karama tofautitofauti za roho? Hilo linaendanaje na mjadala huu kuhusu ushuhudiaji? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!
- Kuongozwa na Roho
-
- Soma 1 Wakorintho 12:1-3. Je, kuna tatizo la kielimu katika kanisa la Korintho? (Ndiyo, baadhi yao walikuwa na “hali moja” na Paulo alitaka kutatua tatizo hilo.)
-
-
- Je, bado tatizo hili lipo katika makanisa yetu leo?
-
-
-
- Kama unaabudu sanamu, je, “huna taarifa sahihi?” (Kifungu kinasema waabudu sanamu “wanaongozwa upotevuni.” Hiyo inaashiria kwamba wanazo taarifa, lakini ni taarifa potofu.)
-
-
- Hebu tujikite kwenye 1 Wakorintho 12:3. Je, elimu ni karama ya Roho Mtakatifu? Je, tunamchagua Roho Mtakatifu badala ya sanamu kwa kuwa tuna taarifa sahihi? (Dhana ya kwamba hili ni suala tu la taarifa sahihi sio ujumbe wa Paulo. Naam, uabudu sanamu unaakisi taarifa potofu. Lakini, kusema kwamba “Yesu ni Bwana” kunaakisi uwezo wa Roho Mtakatifu. Hakuakisi taarifa njema – bila kujali uzuri wa taarifa hizo.)
-
-
- Je, hii inamaanisha kuwa kila asemaye “Yesu ni Bwana” amejazwa Roho Mtakatifu? (Sidhani kama Paulo pia anaashiria hivyo. Bali, anachokimaanisha Paulo ni kwamba unapojazwa Roho Mtakatifu, utasema mambo sahihi. Haya si matokeo ya taarifa njema, bali ni matokeo ya “kunena katika Roho wa Mungu.”)
-
-
-
- Je, hapa kuna ujumbe unaohusu ushuhudiaji? (Ikiwa unanena katika Roho, hutanena mambo mabaya.)
-
- Uanuwai wa Kiroho
-
- Soma 1 Wakorintho 12:4-6. Tuna mambo matatu tofauti: karama, huduma, na utendaji kazi. Je, unayaona hayo miongoni mwa watenda kazi wenzako? Je, unayaona hayo miongoni mwa washiriki wenzako wa kanisa?
-
-
- Je, unadhani kwamba karama zako, huduma zako, au utendaji kazi wako ni wa hali ya chini au wa hali ya juu kuliko wa wengine?
-
-
-
- Ni nini chanzo cha hizo karama, huduma, na utendaji kazi? (Roho Mtakatifu.)
-
-
-
-
- Ikiwa karama, huduma, na utendaji kazi vinawezeshwa na Roho Mtakatifu, je, tunaweza kuwa watu wa hali ya chini au wa hali ya juu? (Hapana. Wako tofauti tu.)
-
-
-
- Soma 1 Wakorintho 12:7. Kwa nini tunapewa karama za roho? Kwa nini tunatenda huduma za kiroho? Kwa nini tunajihusisha kwenye matendo ya kiroho? (Kwa lengo la kutenda wema.)
-
- Soma 1 Wakorintho 12:8. Je, hekima na maarifa vinafanana? (Utakumbuka mwanzoni mwa sura hii (1 Wakorintho 12:1) Paulo anatuambia kuwa hataki “tukose kufahamu.” Paulo anatupatia ufahamu sasa hivi.)
-
-
- Unakumbuka tumejadili kuwa Mkristo aliyejazwa Roho hawezi kusema jambo baya? Je, unaweza kutoa kauli “sahihi” lakini isiyo ya busara? Yaani, unaweza kusema jambo lililo sahihi lakini lisilo jambo bora wakati huo huo?
-
-
-
-
- Je, unaweza kusema jambo la kweli lakini lisilo la busara wakati huo huo likiwa limevuviwa na Roho Mtakatifu? (Ikiwa karama hizo ni tofauti, hilo linawezekana.)
-
-
-
- Soma 1 Wakorintho 12:9. Je, imani inalingana na karama ya kuponya, ambayo Wakristo fulani tu ndio wanayo?
-
-
- Soma Waebrania 11:6. Hili linawezaje kuwa kweli wakati si Wakristo wote wanapewa karama ya imani? (Ili kupatanisha hivi vifungu viwili, lazima tuhitimishe kwamba Wakristo wote wanafanyia kazi suala la imani, lakini baadhi yao wana imani kubwa zaidi.)
-
-
-
- Hebu tupitie mjadala wetu kuhusu maarifa na hekima. Je, hiyo inafanana na imani, ikimaanisha kwamba kila Mkristo ana kiwango fulani cha chini cha hekima? (Nadhani. Vinginevyo, lazima tuzichukulie kwa ukawaida kauli zenye madhara zilizo za kweli. Kibaya zaidi ni kwamba tutahitimisha kuwa mtu aliyejazwa Roho alikuwa anatenda madhara.)
-
-
- Soma 1 Wakorintho 12:10. Je, hii inamaanisha kwamba baadhi ya washiriki wa kanisa watakuwa na karama fulani na wengine hawatakuwa na karama hizo hizo? (Hiyo ndio maana ya dhahiri ya jambo hili.)
-
-
- Hiyo inafanyaje kazi kwenye dhana ya kwamba sote tunafanya ushuhudiaji?
-
-
- Soma 1 Wakorintho 14:3. Hapa unabii unarejelea kuwajenga, kuwafariji na kuwatia moyo watu. Je, unaweza kushuhudia bila kuwa na huo uwezo?
-
- Soma 1 Wakorintho 12:11. Ukiangalia nyuma kwenye orodha ya karama tulizozijadili, je, nyingi ya karama hizo zinakosekana kanisani kwako?
- Ukuaji Kiroho
-
- Angalia tena 1 Wakorintho 12:11. Unaelewa nini kuhusu tofauti kati ya elimu na karama? Kuna tofauti gani kati ya talanta za asili na karama?
-
- Soma Mathayo 25:14-15. Tunayo mambo mawili yanayotofautiana yaliyotajwa kwenye mfano huu – talanta (kile ambacho bwana anakitoa) na uwezo (kile ambacho tayari mtumwa anacho). Hii inaashiria nini kuhusu tofauti kati ya talanta za asili na karama za roho? (Hii inaendeleza mjadala wetu kuhusu kutofautisha uwezo wa Roho Mtakatifu na talanta zetu za asili. Katika mfano huo, ikiwa bwana anamwakilisha Mungu, basi talanta za asili na karama za roho hutoka kwa Mungu.)
-
-
- Je, mfano huu unafundisha kwamba wale wenye talanta kubwa za asili (uwezo), wanapewa karama nyingi za roho (talanta)?
-
-
- Unakaribishwa kusoma Mathayo 25:16-23. Kwa ufupi, watumwa waliopewa ama talanta tano au mbili walizizalisha mara mbili zaidi, walisifiwa na bwana, na kupewa wajibu mkubwa. Soma Mathayo 25:24-25. Mtumwa mwenye talanta moja aliogopa nini? Kushindwa? Ubepari? Alimwogopa bwana?
-
-
- Je, mtumwa huyu alikuwa anatafuta “mahali salama” ambapo asingeweza kupewa changamoto yoyote?
-
-
-
- Je, hapa kuna fundisho kuhusu karama za roho?
-
-
-
-
- Je, tunaweza kuziogopa karama za roho? Je, tunaweza kuogopa kushindwa kwa karama zetu za Roho?
-
-
-
-
-
- Je, tunaweza kudhani kwamba ushuhudiaji, uinjilisti, ni dhana mbaya?
-
-
-
-
-
- Je, tunaweza kumwogopa Mungu, ikimaanisha kwamba tunadhani Yeye ni “mtu mgumu?”
-
-
-
- Soma Mathayo 25:28. Una maoni gani kuhusu kuchukua talanta moja kutoka kwa mtumwa huyu na kumpatia mtumwa mwenye talanta kumi?
-
- Soma 1 Wakorintho 12:28. Je, mfano wa talanta ni kielelezo sahihi cha karama za roho?
-
-
- Kwa mfano, je, “mitume” wanalingana na watumwa wenye talanta tano, na kuendelea vivyo hivyo hadi kwenye orodha ya chini?
-
-
- Soma 1 Wakorintho 12:29-30. Je, tunafedheheshwa kwa kupewa karama zilizo za chini kwenye orodha? (Tuliruka 1 Wakorintho 12:12-27. Inatuambia kuwa karama zote ni za muhimu kanisani, na hakuna karama hata moja inayopaswa kuchukuliwa kuwa na hadhi ndogo.)
-
- Soma 1 Wakorintho 12:31. Hapo awali tuliona kwenye mfano wa bwana na watumwa kwamba bwana ndiye aliyepanga idadi ya talanta zilizotolewa. Kwenye somo letu la karama za roho, tulisoma katika 1 Wakorintho 12:11 kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayeamua nani apate karama ipi. Hapa tunaona taarifa gani mpya kuhusu kupokea karama? (Kwamba tunaweza kuwa na wajibu kwenye karama za roho tunazopewa. Haitakuwa na maana, kimsingi inaweza kusababisha husuda, endapo “tungetaka sana” “karama zilizo kuu” wakati hatuna uwezo wa kuzihifadhi. Lazima hii imaanishe kuwa Roho Mtakatifu atatupatia karama zilizo kuu ikiwa tunazitaka na kuzitumia.)
-
- Rafiki, mjadala wetu kuhusu karama za roho unabainisha kuwa ushuhudiaji si jambo moja tu ambalo sote tunalifanya. Bali, tunaufanya kwa namna anuwai. Tuna vipawa vya asili tofautitofauti na karama mbalimbali za roho. Tunapofanya ushuhudiaji kama timu tunafanya vipawa na karama zetu zote kuzaa kwa namna ya ufanisi zaidi. Je, utazitumia karama za roho ulizopewa na “kuzitaka sana” zaidi na zaidi?
- Juma lijalo: Kushiriki Neno.