Somo la 1: Elimu Katika Bustani ya Edeni
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, inaonekana kama kuna jambo lisilo sahihi kwa namna tunavyowaelimisha vijana wadogo? Kwa miaka mingi nimesikia malalamiko ya aina mbalimbali juu ya mfumo wa elimu, hususani elimu inayotolewa kwenye shule za umma nchini Marekani. Wazazi wangu wote wawili walikuwa walimu katika shule za umma wakati ninaanza shule. Jambo la kushangaza ni kwamba tofauti na shule ya awali (ambayo nilihudhuria kwenye jengo ambalo mama yangu alikuwa akifundisha), wazazi wangu walinipeleka kwenye shule binafsi zinazoendeshwa kwa misingi ya Kikristo kwa elimu yangu yote iliyosalia. Mteja wangu mkubwa alikuwa mwalimu wa shule ya umma. Hilo liliniunganisha na mambo ambayo chama cha walimu kikubwa kabisa kuliko vyama vyote kilihanikiza yafundishwe katika shule za umma. Miongo kadhaa iliyopita niligundua jambo la kutisha, na nikaamini kuwa endapo umma ungelielewa ungelikomesha. Leo tunaona matokeo, na sina ujasiri tena kuamini kuwa umma unayapinga. Biblia inatufundisha nini kuhusu elimu bora? Hebu tuzame kwenye mwanzo wa Biblia!
- Mwanzo wa Elimu
-
- Soma Mwanzo 2:7-8. Adamu alitakiwa kujifunza nini? (Bustani.)
-
- Soma Mwanzo 2:9 na tujikite kwenye nusu ya kwanza. Adamu alijifunza nini kutokana na miti? (Ilipendeza kuiangalia na ilizalisha chakula kizuri.)
-
- Sasa hebu tuangalie nusu ya pili ya Mwanzo 2:9. Kwa nini Muumbaji/Muelimishaji wetu anaweka hiyo miti miwili katikati ya kila kitu?
-
- Hebu turuke na kusoma Mwanzo 2:16-17. Unapata elimu gani kwenye amri ya kutokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya? (1. Mungu anatupatia uchaguzi. 2. Mungu alianzisha mamlaka na mipaka. 3. Mungu anatutarajia tutii mamlaka yake. 4. Adhabu, zikiwemo adhabu kali, zitafuatia endapo hatutayatii mamlaka.)
-
-
- Je, unahangaishwa akili kwa kitendo cha Mungu kuweka “mti wa mauti” katikati ya bustani karibu kabisa na mti wa uzima? Je, huu ni uchaguzi wa busara wa elimu? (Sidhani kama hili lilikuwa wazo la Mungu. Bali, ninaamini hii ilikuwa ni matokeo ya makubaliano kati ya Yesu na Shetani kuhusu vigezo vya jaribu la Shetani.)
-
-
-
-
- Ikiwa niko sahihi, je, kuna fundisho lolote katika jambo hili kwa ajili ya elimu yetu leo? (Kuingia kwa dhambi kunasababisha ulegezaji masharti (compromises) kwenye programu ya elimu yetu.)
-
-
-
-
-
-
- Je, unakubali kuwa hii ni “compromise?”
-
-
-
-
- Soma Mwanzo 2:15. Adamu alijifunza nini kutokana na hili? Tunapaswa kujifunza nini kutokana na hili? (Matokeo ya elimu ya kweli ni ujuzi wa kazi. Ninakumbuka nilipoanza chuo, sayansi ya siasa ndio ilikuwa kozi yangu kuu (major) na elimu ya biashara ilikuwa masomo yangu ya chini (minor). Mara moja niliamua kubadili vipaumbele hivi viwili kimasomo endapo ingetokea nisiweze kujiunga na shule ya sheria. Nilitaka niwe na uwezo wa kupata kazi nzuri.)
-
- Soma Mwanzo 2:19. Hii inatufundisha nini juu ya mtazamo wa Mungu kuhusu elimu? (Mungu anamruhusu Adamu awe mbunifu – na nakubali kile ambacho Adamu anakiamua.)
-
- Soma Mwanzo 2:20. Nani aliyefanya uamuzi wa msaidizi wa “kufanana?” (Huu unaonekana kama uamuzi wa pamoja! Inaonekana kuwa Mungu anamnaibisha (delegate) Adamu sehemu ya mamlaka ya Mungu.)
-
- Soma Mwanzo 2:21-22. Hii inatufundisha nini kuhusu njia ya Mungu ya elimu? (Anataka iwe ya kufurahisha. Anataka tufurahi.)
-
- Zingatia kile tulichokisoma hivi punde, na usome Mwanzo 2:23. Kwa nini Adamu alimwita jina mwanamke? (Inaonekana kama vile Mungu alimpa Adamu mamlaka hayo, kama ambavyo alikuwa na mamlaka ya kuwapa wanyama majina.)
-
-
- Tafakari kile tunachoambiwa katika Mwanzo 2:21-23. Tunapaswa kujifunza nini kutokana na hili kuhusiana na uhusiano kati ya wanaume na wanawake? (Adamu aliumbwa kwanza na alikuwa na haki za kutoa majina. Lakini, mkewe alitengenezwa kutoka kwenye ubavu wa Adamu, na si kutokana na matope, wala kutoka kichwani au miguuni mwa Adamu. Hii inaashiria ubora/ukuu wa adamu miongoni mwa usawa.)
-
- Elimu ya Shetani
-
- Soma Mwanzo 3:1. Hii inaonesha kuwa katika elimu yetu, sauti za uovu zitatufikia. Tunawezaje kuzitambua? (Picha haijakamilika hadi tusome Mwanzo 3:4, lakini chochote kinacholitia changamoto neno la Mungu ni kiovu.)
-
- Soma Mwanzo 3:2. Tunapaswa kukabilianaje na sauti ovu katika elimu? Je, Eva alipaswa kupuuzia swali hili? (Bado nyoka alikuwa hajamkaidi wala kumbishia Mungu. Hadi kufikia hapa lilikuwa tu ni swali kuhusu kile ambacho Mungu alikisema. Ilikuwa kawaida kushirikishana neno la Mungu.)
-
-
- Unalichukuliaje swali la Shetani katika Mwanzo 3:1? Je, halionekani kuwa swali la dhihaka? Kwa nini Mungu aseme kuwa hawatakiwi kula matunda ya kila mti? Kwa dhahiri, nyoka huyu alikuwa ametoka nje ya mji!
-
-
-
- Shetani si mpumbavu. Je, unadhani huu ni mkakati ovu kabisa – kutia chumvi kile ambacho Mungu anakikataza? (Hubiri la mwisho nililolisikiliza lilinikumbusha jambo lililotokea shuleni kwangu. Niliambiwa na mamlaka za shule kuwa sitakiwi kuangalia filamu, lakini mamlaka za shule zilionesha filamu kwenye televisheni zake. Kwa dhahiri, palikuwepo na tatizo la utiaji chumvi!)
-
-
- Hebu tuongezee kifungu cha 3. Soma Mwanzo 3:2-3. Linganisha na Mwanzo 2:17. Je, Eva ameielezea kanuni kwa usahihi? (Hapana. Pia aliitia chumvi kanuni.)
-
-
- Tunapaswa kujifunza elimu gani? (Ninaona mafundisho kadhaa. Zingatia kile anachokisema Mungu. Usitafsiri vibaya/usihudhurishe au usiwasilishe visivyo neno la Mungu. Usitie chumvi neno la Mungu.)
-
-
-
- Nilipokuwa kijana mdogo na mamlaka za elimu zikatia chumvi neno la Mungu kwenye suala la kuangalia filamu, je, walikuwa na nia njema? (Walitaka kutuepusha kuangalia filamu ambazo zingeakisi sauti ovu – nia njema. Walidhani kuwa uamuzi wao ulikuwa bora kuliko wangu. Kwa kuwa walikuwa walimu nami nilikuwa mwanafunzi, yumkini hilo lilikuwa jambo sahihi.)
-
-
-
-
- Je, kulikuwa na jambo ambalo halikuwa sahihi kwenye utiaji chumvi? (Ndiyo. Walimhudhurisha Mungu visivyo. Wangepaswa tu kusema kuwa palikuwepo na filamu nzuri na mbaya, hivyo tutawaamulia filamu za kuangalia.)
-
-
-
- Soma Kumbukumbu la Torati 4:1-2. Je, unadhani kuna umuhimu wowote kwenye ukweli kwamba wote wawili, yaani Shetani na Eva, walitia chumvi katazo la Mungu? (Tunalichukulia hili kama jambo dogo, lakini nadhani ni kitendo hatarishi – hatarishi kama ilivyo katika kurahisisha/kuhafifisha amri za Mungu.)
-
-
- Soma Mathayo 12:1-2. Hatutasoma haya makabiliano yote kati ya Yesu na Mafarisayo. Je, hii inakukumbusha kuwa sehemu kubwa ya karipio la Yesu kwa viongozi wa dini ilikuwa ni kutia chumvi matakwa ya sheria?
-
-
- Hebu turejee kwenye kisa chetu katika kitabu cha Mwanzo. Soma Mwanzo 3:4-5. Je, sasa hali iko dhahiri? Tuna ukinzani wa moja kwa moja kwenye neno la Mungu. Tunapaswa kujifunza elimu gani kutokana na hili? (Tunapokuwa na mgongano wa moja kwa moja usiopatana kati ya Biblia na ujumbe mwingine, tunatakiwa kuukataa huo ujumbe mwingine.)
-
-
- Shetani anadai kuwa kuna manufaa gani yanayotokana na kulikataa neno la Mungu? (Utafanana na Mungu, utaelemika zaidi.)
-
-
-
-
- Je, bado Shetani anaeneza hoja hii hii ya kale? (Ndiyo. Ukikubali mambo ya bahati badala ya kumkubali Mungu Muumbaji, utaambiwa kuwa wewe ni mwerevu zaidi na umeelimika sana.)
-
-
-
- Hebu tuzingatie Mwanzo 3:5. Eva alipaswa kufanya nini pale alipogundua kuwa nyoka alikuwa anakinzana na Mungu? (Alipaswa kumuuliza Mungu kuhusu jambo hilo. Angetafuta ushauri kutoka kwa Adamu.)
-
-
- Kwa nini hakufanya hivyo? (Majisifu – anaweza kufanya uamuzi bila kupata msaada. Anapaswa kufanya uamuzi bila kusaidiwa kwa sababu Mungu (na Adamu?) hawakuwa na mawazo mazuri kama aliyoyawazia. Kutomwamini Mungu ni sababu nyingine. Sidhani kama ni haki kusema kuwa Eva hakuwa mtu anayetafakari kwa makini.)
-
-
- Soma Mwanzo 3:6. Angalia mfuatano. “Alitwaa katika matunda yake” kabla hajayala. Jiweke kwenye nafasi ya Hawa. Ungehitimisha nini pale ulipoligusa tunda na hukufa? (Hii inaonesha matokeo ya kutisha ya kutia chumvi makatazo ya Mungu. Muda mfupi tu uliopita ametoka kusema (Mwanzo 3:3) kuwa Mungu amemwambia kwamba kama angeugusa angekufa. Alipougusa na hakufa, ilidhihirisha kuwa nyoka, na si Mungu, alikuwa amemwambia ukweli.)
-
-
- Je, tunaweza kumudu kuwa hobelahobela (sloppy) au kujisifu kwa elimu ya dini?
-
-
-
- Kuna fundisho gani kwa waume?
-
-
-
- Kwa nini Shetani alimwendea Eva kwanza badala ya Adamu?
-
-
- Rafiki, je, njia ya Shetani inaonekana kufanana na njia ya ulimwengu? Je, utadhamiria, sasa hivi, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kuyashikilia mafundisho ya Biblia na kuyakataa mafundisho ya ulimwengu?
- Juma lijalo: Familia.