Hapo Mwanzo

(Mwanzo 1-3, Ayubu 38, Warumi 5)
Swahili
Year: 
2012
Quarter: 
1
Lesson Number: 
2

Utangulizi: Juma lililopita niliandika kuwa huwezi kuwa Mkristo kama huamini katika Utatu Mtakatifu. Hapo nilimaanisha kuwa Mkristo lazima aamini kuwa Yesu ni Mungu kamili. Juma hili tunajifunza fundisho jingine la msingi kabisa la Biblia – kwamba Mungu alitamka na dunia ikawepo. Dunia haikuibuka, na Mungu “hakusimamia” masuala ya bahati kutokea na matukio ya kiasili. Je, ni kwa njia gani imani katika Uumbaji inahusika? Hebu tuzame kwenye Biblia zetu na kubaini zaidi!

  1. Maelezo ya Mungu ya Mianzo
    1. Soma Mwanzo 1:1-5. Je, Biblia inasema kuwa nani aliyeumba “mbingu na nchi?” (Mungu!)
      1. Ujumbe wa msingi wa Mungu ni kwamba yeye ndiye Muumba. Lakini, ana ujumbe wa pili kuhusiana na kazi yake ya uumbaji. Je, ujumbe huo ni upi? (Hakuhitaji msaada wowote. Alianzia kwenye “ukiwa na utupu” na akatamka tu na ulimwengu ukawepo. Hakuhitajika “kuinua kidole.”)
    2. Angalia tena Mwanzo 1:5. Je, ilimchukua Mungu muda gani kutenda hili? (Biblia inasema kuwa siku moja. Kama tungetakiwa kutafsiri hii “siku” kama kipindi kirefu cha muda, Mungu anaelezea siku kwa namna ambayo sote tunaielewa kutokana na uzoefu.)
      1. Kwa nini Mungu anaziita “jioni” na “asubuhi” kuwa ni siku? Katika Mambo ya Walawi 23:32 tunaona kwamba kuanzia jioni hadi jioni ndicho kipimo cha siku. Tatizo linakwisha kama utasema kuwa “jioni” ni usiku (giza) na “asubuhi” ni mchana (nuru). Hiyo ndio siku kamili kwa kutumia jua likitumika kiuzoefu kama kipima muda.)
      2. Vipi kuhusiana na ukweli kwamba jua bado halikuwepo, lakini baadaye liliumbwa (Mwanzo 1:16)? (Mungu anatumia kipima muda chenye uwiano sawa katika juma kabla na baada ya uumbaji wa jua. Lazima Mungu atakuwa aliumba jua bandia – hili sio tatizo kwa mtu anayeweza kuumba jua halisi!)
  2. Kwa Nini Uumbaji Unahusika Sana kwa Mungu
    1. Watu wengi wananukuu Ayubu 13:15 kusema kwamba Ayubu angekuwa mwaminifu kwa Mungu hata kama Mungu angemuua. Ukisoma sura yote (Ayubu 13) kile ambacho Ayubu anakisema ni kwamba “Ningependa kumshitaki Mungu kwenye mahakama ya mbinguni. Mungu atapaswa kuniletea mashtaka dhidi yangu na nitakuwa na fursa ya kujitetea. Nikipata kusikilizwa kwa haki, basi nitashinda. Nisiposhinda, basi nitasalia kuwa kimya na nitakufa.” Hiyo ndio sababu ambayo sehemu ya pili ya Ayubu 13:15 inasema kuwa, “nitaithibitisha njia yangu mbele zake.” Ayubu anampa Mungu changamoto. Soma Ayubu 38:1-3. Je, Mungu anaijibuje changamoto ya Ayubu? (Anasema kuwa, “nitakuuliza neno! Ewe mwanadamu mpumbavu, nitakutaka unijibu maswali machache.”)
      1. Soma Ayubu 38:4-6. Je, majibu kwa maswali ya Mungu ni yapi? (Ayubu hakuwa shahidi.)
        1. Je, ni swali gani hasa analoliuliza Mungu? (Wewe ni nani hata umpe changamoto Muumba?)
      2. Pitia kwa haraka haraka sura yote ya Ayubu 38. Je, dhana ya Mungu ni ipi? (Kwamba yeye ni muweza wa yote na ana maarifa yote yanayohitajika. Uumbaji unatokea kutokana na kanuni na Mungu ndiye aliyeziumba kanuni.)
        1. Je, uumbaji una umuhimu gani kwa madai ya Mungu kuwa yeye ni Mungu wetu? (Hii inaingia kwenye kiini cha suala lenyewe. Katika Biblia Mungu ananukuu kwa kurudia rudia Uumbaji wake kama msingi wa madai yake ya mamlaka juu ya Ayubu (na mtu mwingine yeyoye yule). Mjadala wa Uumbaji dhidi ya uibukaji unahusu uwezo na mamlaka ya Mungu. Mungu anatangaza kuwa “Mimi nina uwezo mkubwa kiasi kwamba nilitamka tu na kitu kikatokea.” Kimsingi, uibukaji unadai kuwa Mungu alihitaji msaada mkubwa na muda mwingi sana.)
      3. Soma Mwanzo 1:26-27. Je maelezo haya yanakinzana vipi na nadharia ya uibukai? (Tulifanywa kwa mujibu wa ubunifu. Mungu alibuni kwamba wanadamu wanapaswa kuumbwa kwa sura na mfano wake. Mungu alibuni kwamba wanadamu wanapaswa kuwatawala wanyama.)
        1. Je, kwa nini hili ni muhimu kwa Mungu? (Mungu ana uhusiano maalum na wanadamu. Hakujikwaa kwetu alipokuwa akitembea.)
        2. Fikiria kwa muda mfupi kuhusu kile ambacho Biblia inakisema kuhusu uhusiano kati ya wanadamu na wanyama na uniambie kama uhusiano huo unakinzana na nadharia ya uibukaji? (Uibukaji unasema kuwa wanadamu sio tu kwamba walitokana na wanyama, bali pia matukio ya asili kwa kiasi kikubwa yalikuwa ni matokeo ya muingiliano na wanyama. (Ikimaanisha kwamba aidha tuliwashinda kwa mbio au tulikuwa werevu zaidi (tuliwashinda kwa akili) ya wanyama au tulikufa.) Biblia inasema kwa utofauti mkubwa kwamba “tuliwatawala” wanyama.)
      4. Soma Kumbukumbu la Torati 30:19-20. Katika nadharia ya uibukaji, je, ni nani aliye mbunifu wa kweli wa wanadamu? (Mauti. Tulibuniwa na kifo. Kama kifo ndicho mbunifu wetu, basi Mungu alitudanganya kuhusu uchaguzi wa msingi sana aliouweka mbele yetu.)
      5. Soma Mwanzo 3:1-4. Fungu hili pamoja na fungu tulilolisoma hivi punde katika Kumbukumbu la Torati linatuashiria kwenye kitu cha msingi sana kinacholeta mantiki. Je, ni “kisa” gani cha jumla ambacho Mungu anatuelezea kumhusu yeye na sisi? (Kwamba alituumba tukiwa wakamilifu. Hatukumtumaini, hatukumwamini na hatukumtii Mungu, na matokeo yake tukajiingiza kwenye utumwa wa unyonge, magonjwa na mauti ya milele.)
        1. Je, ni kisa gani cha jumla ambacho nadharia ya uibukaji inatufundisha? (Kwamba tulitoka kwenye unyonge hadi kuwa wakakamavu na kuwa mnyama mwenye umiliki mkubwa – na kwa hiyo tukastahili kuwa na maisha bora zaidi!)
        2. Je, hivi “visa” viwili vinaendana?
        3. Je, unaweza kuhusianisha neema na matendo kwenye huu mchakato wa mawazo yenye mantiki? (Ndiyo! Biblia inasema kuwa uumbaji na ukombozi wetu ulitokana na neema na uwezo wa Mungu usiokuwa na mipaka. Uibukaji ni njia ya “matendo” ya kuupata wokovu na uzima. Tunaimarika kutokana na juhudi zetu wenyewe.)
      6. Rafiki, unaweza kuona kuwa uibukaji unamvua Mungu utambulisho wake na kupindua kisa chake?
    2. . Kwa Nini Uumbaji Unahusika Sana kwa Wanadamu
      1. Huenda sababu ya msingi sana ya kwa nini Uumbaji unahusika sana kwa wanadamu ni kwamba unasema kuwa tulitoka mikononi mwa Mungu. Lakini mitazamo yetu mingi ya msingi kuhusiana na maisha inahusianishwa moja kwa moja na mchakato mzima wa Uumbaji. Soma Mwanzo 2:20-23. Hoja moja inayosema kwamba “Mungu alisimamia uibukaji” ni kwamba waandishi wa Biblia hawakuweza kuelezea kwa uzuri kabisa mbinu za uibukaji, na kwa hiyo walielezea kisa ambacho kiliwasilisha wazo lililo sawa na uibukaji. Je, hoja hiyo inakubaliana na fungu la Biblia? (Hapana! Mungu ana maelezo ya kina sana. Undani wa taarifa anaoutoa unakinzana kabisa na wazo la masuala ya bahati na yale ya asili.)
        1. Je, dhana hii inatuambia nini kuhusiana na uhusiano kati ya wanaume na wanawake? (Kwamba waliumbwa ili wawe sawa. Hawa alitoka ubavuni na sio kichwani au kwenye mguu wa Adamu.)
          1. Je, uibukaji unatufundisha nini kuhusu uhusiano kati ya wanaume na wanawake? (Kwamba yeyote anayeweza kutawala anapaswa kufanya hivyo.)
        2. Soma Mwanzo 2:24. Je, ndoa na uumbaji vinahusianishwaje? (Kama uibukaji ndio maelezo sahihi ya asili ya mwanadamu, basi ndoa ya “mwili mmoja” kati ya mwanamume na mwanamke haina maana yoyote.)
          1. Soma Waefeso 5:28-31. Je, suala la “mwili mmoja” linatufundisha nini kuhusiana na jinsi ambavyo wanawake wanapaswa kutendewa kwenye ndoa?
        3. Soma tena Mwanzo 3:2-4. “Utawala wa sheria” ni wa muhimu sana kwa jamii iliyo huru. Wanadamu wanapaswa kutawaliwa kwa sheria, sio mawazo holela ya mtawala. Je, mjadala wa uumbaji dhidi ya uibukaji unatufundisha nini kuhusiana na utawala wa sheria? (Mungu alituumba ili tutawaliwe kwa sheria. Anaamini (na aliifia) katika utawala wa sheria. Uibukaji unatoa hoja kukubaliana na wazo kwamba mtu mwenye uwezo kuliko wote ndiye anayeweka sheria.)
        4. Soma Mwanzo 2:2-3. Je, Sabato inahusianaje na dhana nzima ya Uumbaji? (Ni sherehe na ukumbusho wa kila juma wa siku sita halisi za uumbaji. Kama vile kwenye ndoa, nguzo/uimara wa Sabato unaondolewa na nadharia ya uibukaji.)
        5. Soma Warumi 5:12-15. Je, Paulo anaielezeaje injili? (Kwamba Adamu alituingiza dhambini na Yesu alituokoa kutoka dhambini. Yesu alishinda ilhali Adamu alishindwa.)
          1. Vipi kama kamwe Adamu hakuwepo? Je, hiyo ingefanya nini kwenye mtazamo wetu wa wokovu?
        6. Soma 1 Wakorintho 15:23-26. Je, ujumbe huu ni sehemu ya muhimu sana ya injili? (Ndiyo. Kwamba Yesu anashinda dhidi ya dhambi na anatuokoa kutoka kwenye mauti.)
          1. Utabaini kwamba kifo ndio “adui wa mwisho,” na kinaangamizwa na Yesu. Je, kifo ni cha muhimu kwa namna gani kwenye nadharia ya uibukaji? (Ni suala zito. Utokeaji wa vitu kwa kufuata asili unawachukulia washindi na washindwa kama matokeo ya kifo.)
        7. Soma Ufunuo 21:1-4. Kama huamini maelezo/dhana ya Mungu ya uumbaji wa asili, je, ni kwa nini sasa uamini maelezo yake ya uumbaji mpya?
          1. Kama tunaamini kuwa dhana ya uumbaji ni analojia inayoelezea uibukaji, je, hiyo inatufundisha nini kuhusiana na makao yetu mapya ya mbinguni? (Angalia fungu la 4 – kwamba vitu vilivyoishia mbinguni ni vya msingi kwenye uibukaji, wenye nguvu ndio watakaoishi na wanyonge watakufa! Nadharia ya uibukaji haiendani kabisa na injili.)
        8. Leo tumegusia tu matatizo ya uibukaji yakiwa ni maelezo ya mianzo (asili). Rafiki, kama umeikubali nadharia ya uibukaji kama maelezo ya kweli ya asili ya wanadamu, je, utatupilia mbali fikra hiyo na kuijenga imani yako kwenye kauli za asili za Mungu na mpango wake wa injili?
      2. Juma lijalo: Mungu Kama Mkombozi/