Somo la 8: Yesu, Mpatanishi wa Agano Jipya
Somo la 8: Yesu, Mpatanishi wa Agano Jipya
(Waebrania 8)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: “Agano” katika lugha ya kisasa ni “mkataba.” Asili ya mikataba ni rahisi sana katika sheria za Marekani. Pande zinazohusika kwenye mkataba zinabadilishana ahadi za kutenda jambo fulani, na jambo hilo lina thamani. Jambo hilo linaitwa “uzingativu.” Kwa mfano, ninaahidi kukupatia kiasi fulani cha fedha, nawe unaahidi kunipatia gari lako. Fedha na gari ni uzingativu wenye thamani, na ahadi za pamoja zinahusisha mkataba. Mara kwa mara wanateolojia wanaona ahadi nyingi katika Agano la Kale. Somo letu juma hili linahusu agano moja, lililopewa jina lenye utata la Agano “Jipya.” Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tulielewe vizuri zaidi hili agano jipya, na tuone kama kweli ni jipya, au “limeboreshwa” tu.
- Kulifafanua Agano
-
- Soma Waebrania 8:6-7. Hii inatuambia nini kuhusu ahadi na agano? (Tunaambiwa kuna agano la zamani (“la kwanza”) na agano (“la pili”) lililo bora zaidi. Tofauti kati ya maagano haya mawili inahusiana na “ahadi bora.”
-
- Soma Waebrania 8:8-9. Kulikuwa na kasoro gani kwenye ahadi za zamani? (Watu “hawakudumu katika agano langu.” Hiyo inamaanisha watu hawakuitunza ahadi yao. Walivunja mkataba.)
-
-
- Hebu tuangalie ahadi ya kwanza. Vifungu hivi vinatusaidiaje kuelewa kile kinachojumuishwa kwenye ahadi ya asili? (Hizi ni Amri Kumi. Tunalifahamu hilo kutokana na muktadha wa “nchi ya Misri.”)
-
-
- Soma Waebrania 8:10. Elezea juu ya “ahadi bora?” (Sehemu iliyo bora ni kwamba sheria za Mungu zinawekwa “katika nia zao” na kuandikwa “katika mioyo yao.”)
-
-
- Je, unaweza kuvunja ahadi iliyowekwa katika nia yako na kuandikwa katika moyo wako? (Inaonekana jibu sahihi ni “hapana,” lakini tatizo halisi ni kwamba bado hatutii.)
-
-
-
- Tofauti ya muhimu kwenye ahadi mpya ni ipi? (Ni ya ndani badala ya nje. Inakuwa sehemu ya fikra yetu na matamanio yetu ya ndani.)
-
-
-
- Je, kimsingi sheria ni mpya? Au je, kuna nguvu mpya? Je, sasa ni nguvu itokayo ndani yetu?
-
-
-
- Angalia maoni yanayohusu muda katika Waebrania 8:10. Inasema kuwa sheria ya Mungu imewekwa katika nia na mioyo yetu “baada ya siku zile.” Ni siku gani hizo? (Soma Waebrania 1:2. Rejea ya muda haiko wazi, lakini inatumika angalao katika kipindi ambacho kitabu cha waebrania kiliandikwa, kwani mwandishi anakiita kipindi hicho “mwisho wa siku hizi.”)
-
- Agano Jipya?
-
- Soma Kumbukumbu la Torati 6:5-6 na Kumbukumbu la Torati 11:18. Vifungu hivi vinarejelea agano la kale. Je, Mungu alikuwa na lengo lile lile kwa agano hilo? (Ndiyo. Dhana ya kwamba sheria itaandikwa mioyoni mwetu na kwenye nia zetu ilikuwa dhana ya asili.)
-
-
- Ikiwa lengo halijabadilika, tunawezaje kusema kuwa agano “jipya” kweli ni jipya? Au, je, kuna kipengele kingine cha agano “jipya” kinacholifanya liwe jipya?
-
-
- Soma Zekaria 7:11-12. Utakumbuka kwamba mkataba unajumuisha ahadi za pamoja. Jambo gani limetokea kwenye upande wa watu katika ahadi hiyo? (Hawana nia ya kutunza upande wao wa ahadi. Wana mioyo kama ya “jiwe gumu.”)
-
- Soma Ezekieli 36:26-27. Jambo gani zuri sana linaendelea hapa? Hii inatofautianaje na mkataba wa kawaida? (Kwenye mkataba wa kawaida, kila upande unawajibika kutoa uzingatiaji wake. Hii inatuambia kuwa Mungu anafanya kazi katika pande zote mbili za mkataba. Amekuja “upande wetu” na kutusaidia kuitunza ahadi yetu.)
-
-
- Hebu tuvunjevunje kile anachokifanya Mungu kutusaidia katika kuitunza sehemu yetu ya mkataba. Unadhani moyo wetu “wa jiwe” unabadilishwaje? (Lazima iwe ni kwamba kifo cha Yesu kwa ajili ya dhambi zetu hutubadilisha. Dhihirisho la upendo la ajabu namna gani.)
-
-
-
- “Roho mpya ndani yenu” ni ipi?
-
-
- Soma Yohana 14:15-16. Tafakari vifungu hivi. Je, vinatoa majibu kwa Ezekieli 36:26-27? (Vifungu hivi viwili vinaendana barabara na mchezo fumbo (jigsaw puzzle). Lengo ni kwa sisi kuitunza ahadi yetu ya utii. Yohana 14:15 inatuambia kuwa upendo wa Yesu huamsha utii. Hicho ndicho kinachobadilisha moyo wa jiwe. Yohana 14:16 inafafanua Roho Mtakatifu akitolewa kwetu kama Msaidizi wa “milele.” Mambo haya mawili yanajumuisha “ahadi bora” kutoka kwa Mungu na ahadi bora kutoka kwetu.)
-
-
- Yohana 14:15 inaponukuliwa kwa ajili yangu, kinachotakiwa ni kwamba ninapaswa kuzishika Amri Kumi kwa sababu ninatakiwa kumpenda Mungu. Je, hicho ndicho kinachozungumziwa na Yohana? (Tunapoona jinsi Ezekieli 36 na Yohana 16 zinavyoendana, kilichokusudiwa ni kinyume chake tu. Mungu anapotupatia huu moyo mpya wa upendo, tutazishika amri za Mungu.)
-
- Ahadi Bora
-
- Soma Wagalatia 3:10-11. Hii inaendanaje na mjadala wetu wa wanadamu kutunza ahadi yao ya utii? Kifungu hiki kinasema kuwa wale wanaojaribu kutunza ahadi hii “hawahesabiwi haki” na hata “wamelaaniwa!” (Laana inatokana na kutoitunza ahadi. Lakini, lugha ya “kutohesabiwa haki” inatuambia kuwa hakuna anayeweza kuitunza ahadi.)
-
- Soma Wagalatia 3:13. Hebu turejee kwenye mjadala wetu wa msingi kuhusu mkataba. Upande mmoja unatoa fedha na upande mwingine unatoa gari. Je, upande unaotoa gari pia unaupatia upande mwingine fedha? Je, upande huo unaweza kukopesha fedha ili kuusaidia upande mwingine kulipia gari?
-
-
- Je, Yesu anatusaidia kuitunza ahadi yetu? Au, je, analipa adhabu kwa sisi kutoitunza ahadi yetu? (Katika sehemu iliyotangulia kwenye mjadala wetu, tumejifunza kuwa Yesu anatusaidia kuitunza ahadi yetu. Lakini hapa tunaona kuwa hata anatenda zaidi. Analipa adhabu kwa ajili ya ahadi zilizovunjika.)
-
-
- Soma Waebrania 7:18-19 na Waebrania 7:22. Vipi kama muuzaji wa gari akiamua kudhamini ili kwamba mnunuzi awe na fedha za kutosha kulipia gari? (Kwa kadri ambavyo jambo hili linaonekana kuwa la ajabu, hicho ndicho hasa ambacho Yesu anakifanya hapa. Maisha yake makamilifu ndio “mdhamini” wa ahadi yetu ya utii.)
-
-
- Hebu tuhakikishe tunaelewa taswira kamili ya kile ambacho Yesu anakifanya kwa ajili yetu ili kutusaidia kuitunza ahadi yetu. Kwanza, anatoa njia kwa ajili ya moyo mpya. Pili, anatuongoza kwenye utii. Tatu, anahakikisha utii wetu kwa kutii kwa ajili yetu.)
-
-
-
- Je, hiyo ni ahadi bora? Nitakuuzia gari langu na nitahakikisha una fedha za kutosha kulinunua!
-
-
- Hebu tuangalie Waebrania 7:22 kwa mtazamo tofauti. Waebrania 8:6 inasema kuwa Yesu “anatupatanisha” wakati Waebrania 7:22 inamwita “Mdhamini” wetu. Je, akilini mwako mambo hayo mawili yanafanana? (Hapana. Mpatanishi ni yule anayejaribu kutatua mgogoro kati ya pande mbili zinazohasimiana. Mdhamini anachukua upande mmoja kati ya pande mbili. Katika huu “mgogoro” wa kimkataba Yesu yuko upande wetu.)
-
-
- Hali hii inabadilije ufafanuzi wa “mgogoro?” (Hatuko kwenye mgogoro katika mkataba huu. Yesu anafanya kila linalowezekana ili kuhakikisha kuwa ahadi zetu zinatimizwa. Mungu mkuu kiasi gani!)
-
-
- Rafiki, “Agano Jipya” sio mkataba wako wa kawaida. Badala yake, Yesu anazishughulikia na kuzijali pande zote mbili za makubaliano. Anadhamini na kutuhakikishia ahadi yetu! Je, ungependa kuingia kwenye mkataba huu saa hivi?
- Juma lijalo: Yesu, Dhabihu Kamilifu.