Mungu Mtoaji wa Sheria
Utangulizi: Somo lililopita tulijifunza kitabu cha Wagalatia, somo ambalo lilitupatia mtazamo wa “sheria dhidi ya neema.” Mtazamo huo utatupotosha isipokuwa tu kama tutafungua macho yetu kwenye mtazamo mpana zaidi. Hebu angalia hapa duniani kwenye nchi zinazoongozwa kwa sheria na uzilinganishe na nchi zinazoongozwa na chochote kile ambacho mtawala anaamua kwa muda huo. Nchi ambazo zinaongozwa kwa “utawala wa sheria” zina mafanikio zaidi na zina uhuru zaidi. Uhuru wa kidini, uhuru wetu wa msingi sana, unapatikana tu kwenye nchi zinazoongozwa chini ya utawala wa sheria. Kama wazo lako la “neema” lina dhana ya kwamba unafanya jambo lolote unalodhani kuwa ni zuri kulifanya kwa wakati huo, basi hapo utakuwa umekosea kabisa dhana ya sheria ya Mungu. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tuweze kujifunza zaidi kuhusu sheria ya Mungu.
- Utoaji (“Ofa”)
- Soma Kutoka 19:3-6. Je, Mungu anatoa ofa ya kitu gani? (Anatoa ofa ya mkataba. Yaani kama watu “watatunza agano langu” watakuwa watu maalum kwa Mungu.)
- Unadhani Mungu alikuwa anamaanisha nini aliposema kuwa watu watakuwa “ufalme wa makuhani?” (Je, makuhani wanafanya nini? Wao ni wawakilishi wa mungu wao. Mungu anatupatia mahusiano maalum endapo tutamtii.)
- Kwa nini watu watake kukubali ofa hii? (Kama Mungu alivyokwishawaelezea, alikuwa na uwezo mkubwa kabisa wa kushughulikia matatizo yote waliyokabiliana nayo.)
- Soma Kutoka 19:7-8. Je, watu waliikubali ofa ya Mungu?
- Soma Kutoka 19:3-6. Je, Mungu anatoa ofa ya kitu gani? (Anatoa ofa ya mkataba. Yaani kama watu “watatunza agano langu” watakuwa watu maalum kwa Mungu.)
- Muhtasari
- Soma Mathayo 22:37- 40. Yesu aliposema kuwa “Torati na Manabii” “inaning’inia” kwenye hizi amri mbili, je, alimaanisha nini? (Hizo ndizo msingi na umuhimu wa sheria.)
- Angalia wajibu wetu kwa Mungu. Je, ni sehemu yetu gani ambayo Mungu anaitaka? (Yote.)
- Yesu anaporejea “moyo,” “roho” na “akili,” je, unadhani kuwa anamaanisha nini? Je, hivi vitu vitatu ni tofauti?
- 3. Je, ni kwa jinsi gani amri ya pili (mpende jirani yako) ina utofauti kwa muktadha wa kujitoa kwayo na ile ya kwanza (mpende Mungu wako)? (Hatuambiwi kuwapenda majirani zetu kikamilifu kabisa, bali tuwapende kama tunavyojipenda wenyewe.)
- Je, unajipenda kwa kiwango gani?
- Je, ni sahihi kujipenda wewe mwenyewe? (Ama kwa hakika kabisa!)
- Je, unadhani kuwa Yesu anaanzisha njia mpya ya kuiangalia sheria? (Soma Kumbukumbu la Torati 10:12. Yesu haanzishi kitu kipya.)
- Soma Mathayo 22:37- 40. Yesu aliposema kuwa “Torati na Manabii” “inaning’inia” kwenye hizi amri mbili, je, alimaanisha nini? (Hizo ndizo msingi na umuhimu wa sheria.)
- Amri Kumi za Mungu - Upendo kwa Mungu
- Soma Kutoka 19:16-19. Utabaini kuwa hii ni tofauti na njia ambayo Yesu aliutangaza msingi wa sheria kwenye Mathayo 22. Kwa nini Mungu aliwatisha watu? (Alitaka kusisitizia umuhimu wa sheria. Pia alitaka (ukisoma mafungu yanayofuatia) kuwaweka watu mbali ili kwamba wasijaribu kumwona na wafe.)
- Soma Kutoka 20:1-2. Je, Mungu angeongezea kitu gani kwenye wasifu wake hivi leo? (Mimi ni Bwana Mungu wako niliyekuokoa kutoka katika mauti ya milele.)
- Je, haya ni madai makubwa zaidi kuliko yale ya awali?
- Soma Kutoka 20:3. Je, hii inapendekeza nini kuhusiana na Mtoaji wetu wa sheria? (Kwamba anahitaji utii wetu uwe wa kwanza kabisa.)
- Soma Kutoka 20:4-6. Ni kwa nini hii amri ya pili ni ya muhimu ukizingatia kuwa tayari tunayo ile amri ya kwanza? (Hii inahusiana na heshima/hadhi/utu wa Mungu. Mungu hataki kushushwa na kuonekana kuwa kama “kitu fulani hivi” – hususan, sio kuwa kama kitu alichokiumba, au kitu kilichofanywa/kilichotengenezwa na kimojawapo cha uumbaji wake.)
- Je, ninapindisha maneno ya Mungu? Anasema kuwa ana “wivu” na nilipendekeza kuwa hiyo ndio ilikuwa hadhi yake. Je, vitu hivi viwili vinatofautiana? (Yesu anaionea wivu nafasi yake – hadhi yake.)
- Nini kinatokea kwa kumpa Mungu kile anachokistahili? (Mibaraka! Mibaraka hadi kwa watoto wetu.)
- Je, unawezaje kuzielezea kwa ufupi hizi amri mbili za kwanza? (Zinaakisi somo letu la juma lililopita – zinaonyesha kuwa Mungu ni mtakatifu, amewekwa wakfu, na ni wa kipekee.)
- Soma Kutoka 20:7. Je, ni kitu gani cha kwanza kabisa kinakujia akilini unapoisoma amri hii? (Kuapa.)
- Je, unadhani kuwa ni tatizo gani lililopo ambalo Mungu analielezea? Je, ni kwa jinsi gani kuapa ni tatizo kubwa kwenye hilo tatizo lililoelezewa? (Kwa mara nyingine tena, ni utu/hadhi, utukufu wa Mungu, ndilo lililo suala la msingi.)
- Je, utakuwa unakiuka amri hii kwa wewe kudai kuwa Mkristo na kufanya mambo ambayo yatampa Mungu sifa mbaya? (Nadhani hili ni tatizo kubwa zaidi kuliko kuapa. Watu wanafikiria kwa uchache kuhusiana na kuapa, kwa sababu kwa ujumla wale wanaoapa sio watu wanaodai kuwa wawakilishi wa Mungu. Ni wale wanaodai kuwa wawakilishi, na wale wanaofanya uovu, ndio wanaolitumia vibaya jina lake.)
- Amri Kumi – Kipindi cha Mpito
- Soma Kutoka 20:8-11. Je, hii amri ya nne inahusu kumpenda Mungu au inahusu kuwapenda wanadamu wenzetu? (Inamheshimu Mungu kwa kuwa Muumba wetu, lakini wanadamu wote (hadi waajiriwa wetu) wanafurahia pumziko hili la kila juma.)
- Amri Kumi - Upendo kwa Jirani
- Soma Kutoka 20:12. Je, kwa nini heshima kwa wazazi wetu inahusishwa na urefu wa maisha yetu? Je, Mungu anatuambia kuwa “atatushambulia/atatupiga” kwa kutowaheshimu wazazi? (Kwa ujumla wazazi wana busara. Kama tukijifunza kutoka kwao maisha yetu yatakuwa bora na marefu. Kuwapenda wazazi wetu, kama kuwapenda wenzi wetu, ndio njia ya kujipenda sisi wenyewe.)
- Soma Kutoka 20:13-16. Je, ni kitu gani kinachofanana kinachoonekana kwenye hizi amri zote? (Soma Warumi 13:8-10. Upendo wa watu wengine. Tunapotoa/tunapochukua kutoka kwa watu kitu chao cha haki, tunaonyesha ubinafsi na upungufu wa upendo.)
- Je, ni kitu gani alichotutendea Yesu? (Alikufa badala yetu. Aliyatoa maisha yake kwa ajili yetu.)
- Je, amri hizi zinaakisije kile alichotutendea Yesu? (Msingi wa injili ni kujitoa sisi wenyewe kwa ajili ya watu wengine. Matendo yaliyoelezewa kwenye hizi amri yanachukua vitu kutoka kwa watu wengine kwa faida yetu. Amri hizo ni kinyume cha injili.)
- Je, ni kitu gani alichotutendea Yesu? (Alikufa badala yetu. Aliyatoa maisha yake kwa ajili yetu.)
- Soma Kutoka 20:17. Je, hii inahusianaje na amri nne ambazo tumejifunza hivi punde? (Hii ni sehemu ya mtazamo wa amri zilizotangulia. Ukijiepusha kutaka vitu vya jirani yako, kama ukiridhika na kitu chako, basi hutachukua kitu chochote cha jirani yako.)
- Je, upendo kwa jirani yako unaingiaje kwenye hii amri ya mwisho?
- Je, hizi kanuni za Kibiblia zinapaswa kujihusisha na sera za kodi za kitaifa?
- Kama umesema kuwa ndiyo, Marekani inapokuwa inaingia kwenye miezi ya mwisho ya uchaguzi wa urais, kuna mjadala mkubwa kuhusu kuongeza kodi ya ziada kwa matajiri. Je, huu ni ukiukwaji wa amri ya kumi? Je, huu ni wivu na matamanio?
- Amri Kumi za Neema
- Soma Isaya 48:17. Je, haya ni maelezo ya Amri Kumi? (Haya ni sehemu ya maelekezo ya Mungu “ya jinsi ambavyo unapaswa kuenenda.”)
- Soma Isaya 48:18-19. Je, matokeo ya kuitii sheria ya Mungu ni yapi? (Amani. Haki. Hadhi. Familia. Haya ndio mambo yote tunayoyataka. Mungu anatufundisha kuwa sheria yake haipo kwa ajili ya kutukosesha. Haipo kwa ajili ya kutuhukumu/kutushutumu. Mungu alitupatia sheria yake kwa sababu anatupenda na anafahamu vizuri zaidi kuwa ni mtazamo na matendo ya aina gani yatakuwa mbaraka maishani mwetu.)
- Juma lijalo: Bwana wa Sabato
