Somo la 7: Agano na Ibrahimu

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Mwanzo 15-19
Swahili
Year: 
2022
Quarter: 
2
Lesson Number: 
7

Somo la 7: Agano na Ibrahimu

 

(Mwanzo 15-19)

 

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua  pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, unatilia mashaka ahadi za Mungu kwako? Je, mashaka yako yanakufanya ujisikie vibaya. Somo letu juma hili linabainisha kwamba mtu aliyesifiwa kwa imani yake kwenye ahadi za Mungu kiuhalisia alikuwa mtu aliyepambana na mashaka nafsini mwake. Tutakachokiona ni kwamba licha ya mashaka ya Abramu, Mungu anaendelea kuwa mwaminifu kwake. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

  1.    Imani (Belief)
    1.    Soma Mwanzo 15:1-3. Jiweke kwenye nafasi ya Abramu. Umetenda kile ambacho Mungu amekuagiza kwa kuacha mji wako na kwenda Kaanani ili pawepo nafasi ya wewe kuwa “taifa kubwa” (Mwanzo 12:2). Je, maneno ya Mungu yanaonekana kuwa matupu (yanaonekana kutokuwa na maana) kwako kwa kuwa huna mtoto? (Naam. Kwa nini amehama? Inaonekana amehama pasipo na sababu yoyote.)
    1.    Soma Mwanzo 15:4. Mungu anashughulikaje na mwanadamu anayeitia changamoto ahadi yake? (Mungu anaelewa. Anajibu kwa ujumbe mahsusi.)
    1.    Soma Mwanzo 15:5. Hapo awali (Mwanzo 13:16) alimuahidi Abramu kwamba uzao wake utakuwa kama “mavumbi ya nchi.” Kuifanya ahadi ijikite kwenye nyota badala ya mavumbi kunaifanya ahadi iwe kubwa zaidi. Je, umewahi kumwona mtu anayeonekana kuvunja ahadi yake kwako, na pale unapompa changamoto, anatoa ahadi ya kustaajabisha zaidi? Unakuwa na mwitiko gani kwenye jambo hilo?
    1.    Soma Mwanzo 15:6. Katika muktadha huu, unaifafanuaje imani kwa Mungu? (Ni imani katika neno la Mungu isiyotii uhalisia unaouona.)
      1.    Sasa swali la muhimu kabisa. Je, Mungu alimwambia Abramu ukweli? (Ndiyo! Sasa tunafahamu kuwa ahadi kuu ya Mungu ilikuwa sahihi.)
      1.    Hebu tumwangalie Abramu kidogo. Utakumbuka katika somo la juma lililopita Abramu aliendelea kudanganya kuhusu uhusiano wake na Sara kwa sababu hakumwamini Mungu katika kuyaokoa maisha yake dhidi ya watawala wapagani. Kitu gani kimetokea kwa Abramu?
        1.    Je, kuna namna yenye mantiki ya kuelezea jambo hili isiyohitaji ufanywaji upwa wa kiroho kwa Abramu? (Abramu anaweza kumwamini Mungu pale Mungu anaponena moja kwa moja. Hata hivyo, Abramu anapotumia mantiki (akili ya kawaida) ya ahadi ya Mungu mbele ya uhalisia wa wapagani wenye nguvu, anashindwa.)
        1.    Je, hili ni tatizo katika maisha yetu? Yumkini Mungu haneni nasi moja kwa moja. Tunapoziweka kivitendo ahadi za Mungu katika muktadha tofauti, je, tunashindwa?
    1.    Soma Mwanzo 15:7-8. Hebu subiri kidogo! Je, Abramu anamwamini Mungu kuhusu kuimiliki nchi hii? (Hapana. Kimsingi Abramu anasema, “Nitajuaje kama unaniambia ukweli?”)
    1.    Soma Warumi 4:2-4. Kitabu cha Warumi kinawasilisha imani ya Abramu kwa namna iliyo chanya zaidi. Hiyo inatutiaje moyo? (Kama badala yake kitabu cha Warumi kingenukuu Mwanzo 15:8, na kusema kwamba “Abramu alitaka uthibitisho kutoka kwa Mungu,” tungeliangalia jambo hili kwa utofauti. Kwa upande wangu hamasa ni kwamba hata Abramu aliakisi aina ya tabia tulizonazo. Lakini, Mungu alimwangalia Abramu kwa namna ya kupendeza zaidi kwa kadiri ilivyowezekana.)
    1.    Pitia kwa haraka haraka Mwanzo 15:9-21. Mungu anaadhimisha sherehe ya agano, jambo linalofanana na mkataba ulioandikwa katika zama za leo. Hilo linazungumzia nini kuhusu tabia ya Mungu kwamba yuko radhi kumpa Abramu mkataba rasmi ili kuthibitisha ahadi yake? (Mungu anakwenda mbali zaidi ili kututia moyo.)
  1.   Kutoamini
    1.    Soma Mwanzo 16:2. Sara anamlaumu Mungu kwa kutopata kwake watoto. Anadai Mungu “amemfunga tumbo” ili asizae watoto. Unadhani hili ni kweli?
      1.    Kama Mungu ndiye mwangalizi wa mambo yote, je, uwajibikaji upo miguuni mwake?
      1.    Angalia suluhisho la Sara, kwamba Abramu anapaswa kupata mtoto na Hajiri, mjakazi wa Sara. Je, anatilia shaka ahadi ya Mungu kwa Abramu? Je, Mungu aliwahi kumwahidi kwamba atakuwa mama wa taifa kubwa? (Soma Mwanzo 17:15-16. Ahadi hii kwa Sara inakuja baadaye. Sioni ahadi yoyote huko nyuma. Kwa sababu hiyo, Sara angeweza kuamini hili linaendana na ahadi ya Mungu kwa Abramu.)
        1.    Je, kuna lolote linalokutatiza kuhusu hitimisho la Sara kwamba anapaswa kumsaidia Mungu kwenye ahadi yake? (Tumejadili kisa cha Nuhu ambapo Mungu anashirikiana na wanadamu ili kutimiza mapenzi yake. Tofauti hapa ni kwamba Mungu aliomba kuingia ubia na Nuhu, na hakupendekeza mpango wowote wa aina hii kwa Abramu na Sara. Badala yake, ilikuwa kinyume na mpango wake. Angalia Mwanzo 2:24.)
        1.    Angalia Wagalatia 4:21-23. Paulo analitazamaje jambo hili? (Analiangalia kupitia kwenye lenzi ya kuhesabiwa haki kwa imani. Sara anatafuta suluhisho, hamwamini Mungu.)
    1.    Soma Mwanzo 16:3-5. Wanaume, unapaswa kufanya nini mke wako anapopendekeza jambo baya?
      1.    Sara anadai kuwa yeye ndiye mwathirika hapa. Nani aliyemkosea? Abramu? Mungu? Hajiri?
      1.    Kwani mpango wa Sara haukwenda kama alivyotarajia? Je, ameshindwa tu kutafakari jinsi Hajiri atakavyoitikia jambo hili? (Utaona kwamba Sara anamwambia Abramu kuwa kosa ni lake yeye Abramu. Anamwomba Mungu ahukumu kati yake na Abramu. Hii inaonyesha kuwa Sara anamlaumu Abramu badala ya kumlaumu Mungu au Hajiri.)
    1.    Soma Mwanzo 17:5-7. Je, hii ni ahadi ambayo Abramu aliisikia kabla?
      1.    Mara hii Mungu anabadili jina la Abramu kumaanisha “baba wa mataifa mengi.” Je, hili linafedhehesha kwa kuwa Abramu ni baba wa mtoto mmoja pekee kupitia kwa Hajiri?
      1.    Unadhani kwa nini Mungu anaendelea kuirudia ahadi kila mara na sio kuitimiza?
    1.    Soma Mwanzo 17:9-11. Tulijifunza hapo kabla kuhusu mkataba rasmi ambao Mungu aliuingia na Abramu. Kwa nini mkataba wa pili unaohusisha mada ile ile? Kwa nini mkataba huu uhusishe kumwekea alama Ibrahimu na uzao wake wa kiume?
    1.    Tumekuwa tukijadili sababu ya Mungu kuendelea kuirudia ahadi yake badala ya kuitimiza. Swali la kina ni kwamba “Ni nani anayeonekana kupungukiwa imani?” Kisa hiki kinashughulikaje na kushindwa kwa imani ya Abramu kwa kujrudiarudia? (Jibu moja ni kwamba Mungu anachelewa kutimiza ahadi yake kwa kutumaini kwamba imani ya Ibrahimu itaimarika. Kumwekea Ibrahimu alama mahala hapa kunaimarisha ahadi ambayo Mungu aliitoa kwake. Ni kukumbushia ahadi mara kwa mara.)
  1. Imani Imetimizwa – Takriban
    1.    Soma Mwanzo 18:10-14. Kuna manufaa gani kwa Mungu kusubiri kutimiza ahadi yake hadi muda ambao kibinadamu haiwezekani? Kwamba linakuwa jambo la kichekesho kwa mtazamo wa kibinadamu? (Soma Kumbukumbu la Torati 8:17-18. Hili ni jibu jingine kwa nini kuitimiza ahadi kulicheleweshwa. Tunaona rejea za kujirudiarudia kwenye Biblia kwa Mungu kusubiria hadi dakika ya mwisho ili kudhihirisha kwamba anawajibika kwa ushindi, sio wanadamu.)
      1.    Utaona kwamba mara hii Mungu anatoa kipindi cha muda mahsusi. Kwa nini?
    1.    Soma Mwanzo 18:17-19. Unadhani kwa nini Mungu aliona ni muhimu kushirikisha hukumu ambayo alikuwa anataka kuileta Sodoma na Gomora? (Ni muhimu kushirikisha sio tu upande wa upendo, bali pia upande wa hukumu wa Mungu na watoto wetu.) Mungu anajua kwamba atatimiza ahadi yake kwa Ibrahimu na anafanya uamuzi kutokana na uhakika huo.)
  1.   Sodoma na Gomora
    1.    Soma Mwanzo 13:10 na Mwanzo 18:20-21. Nini kimetokea mahali ambapo panafanana na Bustani ya Edeni? (Panajihusisha na dhambi “ya kutisha.”)
    1.    Ibrahimu anasihi kwa ajili ya Sodoma, mahali anapoishi Lutu. Soma Mwanzo 18:32-33. Ibrahimu na Mungu wanaoneshaje rehema kwa Sodoma? (Wanakubaliana kwamba kama watu waaminifu kumi pekee watapatikana pale, Sodoma haitaangamizwa.)
      1.    Utafakari mtazamo wa Mungu na jinsi unavyoweza kuwa baraka kwa wengine kwa kuwa mwenye haki?
    1.    Soma Mwanzo 19:1-5. Uovu umeenea kwa kiasi gani Sodoma?
      1.    Ni nini asili ya dhambi iliyofafanuliwa kwenye vifungu hivi? (Soma Yuda 1:7. Hii leo ni maarufu kujenga hoja kwamba tatizo la Sodoma lilikuwa utendaji dhambi wa jumla na sio “uasherati” na “mambo ya mwili yasiyo ya asili.”  Hakuna ubishi kwamba palikuwepo na dhambi ya jumla, lakini Biblia iko wazi sana juu ya dhambi maarufu ya mji ule.)
    1.    Soma Mwanzo 19:23-25. Jua linachomoza asubuhi, kama ilivyo kwa siku yoyote ile pale Sodoma, mahali kama Edeni. Mungu alitaka Ibrahimu awafundishe nini uzao wake kuhusu Sodoma?
    1.    Rafiki, je, Mungu anaaminika? Je, analishika neno lake? Je, utamwomba Roho Mtakatifu akusaidie, kama ilivyokuwa kwa Abramu, kukua katika imani yako?
  1.    Juma lijalo: Ahadi.