Somo la 1: Tanuru la Mchungaji 

Error message

 • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
 • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Zaburi 23
Swahili
Year: 
2022
Quarter: 
3
Lesson Number: 
1

Somo la 1: Tanuru la Mchungaji

(Zaburi 23)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Kuna mvutano katika Biblia linapokuja suala la mateso. Kwa upande mmoja Mungu anatutaka tuwe watiifu ili kuwa na ukomo wa mateso yetu na kutupatia mafanikio. Kwa upande mwingine, tunaona kwamba Yesu na wanafunzi wake wa karibu kabisa walipitia mateso ya kutisha. Na kwa kuongezea, tunayaona mateso miongoni mwa wale tunaowafahamu ambao ni watu wema. Masomo yetu katika robo hii yanatuleta uso kwa uso kwenye mvutano huu. Hebu tuianze hii safari ya tafakuri na tujifunze kwa kujifunza Zaburi 23!

 1. Kutopungukiwa
  1. Soma Zaburi 23:1. Hitimisho ni kwamba hatupungukiwi. Inamaanisha nini “kutopungukiwa?”
   1. Kama umemsikia mtu akielezewa kama “hajapungukiwa kitu chochote,” utahitimisha nini juu ya utajiri wa mtu huyo?
    1. Je, kifungu hiki kinazungumzia utajiri?
    1. Je, umekutana na watu wasio matajiri na hawajapungukiwa? (Kuna aina ya tabia ambayo mara zote inaonekana kutaka kitu asichonacho. Tabia zingine huridhika na kile wanachomiliki.)
   1. Miaka mingi iliyopita, Daniel Pink aliandika kitabu kizuri kinachoitwa “Drive.” Katika kitabu hicho alichunguza mambo yanayowapa motisha waajiriwa kuwa wafanyakazi bora. Alihitimisha kwamba kikizidi kiwango fulani (cha wastani) cha mapato, waajiriwa hawamotishwi na fedha ili kufanya kazi kwa bidi. Badala yake, hamasa yao inafungamanishwa na aina ya kazi yao. Je, hii inaendana na kile ambacho Biblia inakisema kuhusu “kutopungukiwa?”
  1. Hebu tuangalie sehemu ya kwanza ya Zaburi 23:1. Kiambato (ingredient) muhimu cha “kutopungukiwa” ni kipi? (Kuwa na Bwana kama mchungaji wetu.)
   1. Unadhani inamaanisha nini kwa Mungu kuwa Mchungaji wetu?
    1. Tunatakiwa kufanya nini? (Kumfuata Yeye. Kumruhusu atuongoze,)
  1. Soma Zaburi 23:2. Je, hii ndio taswira ya utulivu?
   1. Hebu tuzame kwa kina kwenye taswira hii:
    1. Je, “malisho ya majani mabichi” yanamaanisha nini kwako? (Angalao wanamaoni wawili wanabainisha kuwa neno la Kiebrania lililotafsiriwa kama “malisho” kwa kawaida humaanisha makao, nyumba ambayo mtu anaishi.)
    1. Unahitimisha nini juu ya kuwa na makao yenye “malisho ya majani mabichi?” (Una makao mazuri na chakula kingi kizuri cha kutosha.)
    1. Malisho ya majani mabichi yanamaanisha nini kwa kondoo? (Alikuwa na chakula kingi cha kutosha.)
  1. Hebu tuchunguze sehemu ya kwanza ya nusu ya kwanza ya Zaburi 23:2. Inamaanisha nini kunilaza? Je, Mungu analazimisha jambo? (Wachungaji huongoza. Nyakati zingine hulazimisha/hushurutisha.)
   1. Je, unahitaji kushurutishwa ili kulala? (Mara zote nimekuwa na tatizo hili. Ninapata wakati mgumu kupumzika tu. Nimekataa kustaafu kikamilifu kwa sababu sidhani kama ninaweza kusimamia/kutawala mapumziko yote hayo, na baadhi ya mapumziko yana mvuto mdogo sana kwangu kuliko baadhi ya kazi zangu.)
  1. Soma 1 Petro 5:2-3. Hii inaashiria nini juu ya kulazimishwa?
   1. Tunapaswa kuhitimisha nini kutoka kwenye “kutengenezwa” hadi “kulazwa katika malisho ya majani mabichi?” (Sehemu ya hili ni kubadilisha mioyo yetu ili kupokea pumziko na amani.)
  1. Sasa angalia sehemu ya mwisho ya Zaburi 23:2. Unadhani “maji ya utulivu” yanamaanisha nini kwa kondoo? Inamaanisha nini kwako?
   1. Ninapenda “maji meupe.” Kama nawe pia unayapenda, kwa nini unayapenda? (Ni changamoto. Ni mpambano wa kuokoka maji yenye hasira.)
   1. Ahadi ya Mungu ni ipi basi hapa? (Kwamba tuwe na uwezo wa kupatana (refreshed) bila kupigana. Maji ya uzima yatapatikana kwa urahisi na kunyweka.)
 1. Uhuishaji (Restoration)
  1. Soma Zaburi 23:3. Kama ningejitolea “kuhuisha nafsi yako” unatarajia manufaa gani?
   1. Je, sehemu ya mwisho ya kifungu cha 3 ni ya msaada katika kuelewa kinachomaanishwa na uhuishaji wa nafsi? (Nadhani kuiendea njia ya haki ni sehemu yake kubwa.)
   1. Kifungu hiki na kile cha Zaburi 23:2 vinamrejelea Mungu akituongoza. Hiyo inaashiria nini kuhusu hali yetu ya sasa? (Bado hatujafika pale ambapo Mungu anatutaka tuwepo. Tunatakiwa kupiga hatua kwa kumfuata Mungu.)
  1. Sehemu ya mwisho ya Zaburi 23:3 inafurahisha. Kwa nini Mungu anatoa ofa hii ya uhuishaji? (Inamuakisi vizuri sana.)
   1. Ni kitu gani hasa kinachomuakisi Mungu vizuri? (Mara ngapi unawasikia wapagani wakimlaumu Mungu kwa matukio yote mabaya? Mungu anatutaka tuwe mfano hai wa kile kinachomaanishwa katika kumruhusu Mungu ayaongoze maisha yetu. Mungu anataka watu wengine waone kwamba analeta baraka, sio maovu.)
   1. Hebu tulitafakari hili kwa kuzingatia vifungu viwili vya mwanzo vya Zaburi 23. Je, baraka zote hizi zinakusudia kumpa Mungu utukufu?
   1. Kama umebarikiwa, na humpi Mungu utukufu, hiyo inaashiria kuwa unapaswa kufanya nini?
 1. Hofu
  1. Soma Zaburi 23:4. Inamaanisha nini kupita “kati ya bonde la uvuli wa mauti?”
   1. Kwa nini kifungu kinasema “kutembea” na sio “kukimbia?”
   1. Rafiki, hatuko kwenye malisho ya majani mabichi tena! Unadhani neno “bonde” linamaanisha nini linapotumika maishani mwako? (Sehemu ya chini kwa kimo.)
   1. Tunafahamu maana ya kifo, uvuli wa mauti ni kitu gani? (Tunatoa kivuli kwenye mwanga sahihi. Nadhani “uvuli” wa mauti unakaribiana na jambo halisi – kifo.)
  1. Zaburi 23:4 inasema kuwa hatuogopi mabaya, changamoto kubwa kwenye taaluma yangu ni kazi yangu ya kwenda mahakamani. Kwa kawaida kazi hiyo huleta hofu – ikizingatiwa kwamba kwa ujumla huwa ninashughulika na mahakama, hakimu, na wanasheria nisiowafahamu. Kifungu hiki kinasema kuwa njia ya kuondoa hofu ni ipi? (Kutambua kwamba Mungu yu pamoja nasi. Sina maelezo ya kutosha kuelezea jinsi jambo hilo lilivyo la faraja kwangu kwenye mazingira ya kesi mahakamani ambayo yana shinikizo kubwa. Kwa kutambua tu kwamba Mungu yu pamoja nami ni chanzo cha faraja kubwa!)
   1. Kifungu hiki kinasema kuwa “gongo na fimbo” ya Mungu huleta faraja. Hilo linatendekaje? (Kwanza, nadhani hizi ni silaha zenye kudhuru dhidi ya watu wanaoweza kunidhuru. Pili, nadhani zinanipa ulinzi ninapokuwa na tatizo lenye shinikizo.)
  1. Soma Zaburi 23:5. Je, kifungu hiki kinasema kuwa maadui wetu wanatutizama tulapo? (Hapana. Inamaanisha kuwa maadui wetu wanashuhudia ushindi wetu. Robo iliyopita tulimjadili Yusufu. Ndugu zake waliona ushindi wake. Waliona namna alivyokula chakula katikati ya baa la njaa.
   1. Soma Zaburi 45:7. Hii inatuambia nini kuhusu vichwa vyetu kupakwa mafuta? (Tuna furaha!)
   1. Ni nini maana ya kikombe chetu kujaa hadi kufurika? (Tuna kinywaji cha kutosha. Kuna mwelekeo thabiti katika hii sura unaotuambia kuwa Mungu hutupatia zaidi ya mahitaji yetu.)
  1. Soma Zaburi 23:6. Sehemu gani ya maisha yako Mungu anaahidi kukuonyesha wema na rehema? (“Siku zote za Maisha yako.”)
   1. Unaposoma “nyumbani mwa Bwana,” je, unazifikiria mbingu?
    1. Kama unazifikiria, unaelezeaje nukuu ya awali katika siku zote za Maisha yangu? Nadhani mtunga Zaburi anatuambia kwamba tunaweza kuwa na uzoefu wa “nyumba ya Bwana” sasa hivi. Hapa hapa duniani.)
    1. Vipi kuhusu msemo kwamba sisi hapa ni wageni, na dunia sio makao yetu? (Kwa hakika dunia ni makao yetu sasa na maisha ya baadaye. Angalia Ufunuo 21:1-3.)
  1. Je, Zaburi 23 inaonekana kuwa njia ya ajabu kuanza kujifunza juu ya mateso? (Nadhani ni njia kamilifu. Sio tu kwamba inatutia hamasa kwa ujumla, mateso hukaa katika bonde la uvuli wa mauti.)
  1. Rafiki, je, utarejea kwenye sura hii utakapokabiliana na nyakati ngumu? Mungu ametupatia sura hii ili kututia moyo na kutufurahisha.
 1. Juma lijalo: Matanuru Yajayo.