Somo la 6: Kupambana kwa Nguvu Zote
Somo la 6: Kupambana kwa Nguvu Zote
(Wakolosai 1, Yohana 16, 1 Petro 1)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, unayachukulia maisha ya Kikristo kama mapambano? Mapambano yako? Uzoefu wangu unaonyesha yale ninayoyaona kama kasoro mbili. Kwa upande mmoja ni wale wanaoishi katika uchumi wa soko huria na wamejifunza kwamba kufanya kazi kwa bidi na kwa ueledi ndio ufunguo wa mafanikio. Wanahamisha mawazo hayo kwenye uhusiano wao na Mungu. Wanaamini kwamba bidii ya kazi tena yenye ueledi huwaleta karibu na Mungu. Kasoro kwa upande mwingine ni kwamba haki kwa imani pekee inaeleweka kumaanisha kwamba tunapitia tu kwenye mkondo wa maisha yetu ya Kikristo. Kutokujali juu ya huduma na tabia si jambo baya kwa sababu hatuna lolote la kufanya kwa ajili ya kujipatia wokovu wetu. Msitari wa ukweli uko wapi? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuone kile tunachoweza kujifunza kwenye somo hili!
- Asili ya Sulubu Yetu
-
- Soma Wakolosai 1:18-20. Mgogoro gani ulitakiwa kupatanishwa? Na, Yesu alkiuchukuliaje mgogoro huo na kuleta amani? (Mgogoro ulikuwa kati ya utakatifu mkamilifu wa Mungu na hali ya dhambi ya wanadamu. Yesu alileta amani kwa kifo chake msalabani.)
-
- Soma Wakolosai 1:21-22. Tulianza na nia ya kiuhasama na matendo mabaya. Tulikuwaje “pasipo na mawaa wala lawama mbele zake?” (Kwa kile alichokifanya Yesu (kifo chake) na sio kile tulichokifanya.)
-
- Soma Wakolosai 1:23. Je, hatuna wajibu wowote katika huu upatanishi? (Tunao wajibu. Lazima “tudumu katika imani ... bila kuliacha tumaini la injili.” Pia tunaambiwa kuwa “imara.”)
-
-
- Je, hii ni sawa na mafanikio kazini kwetu?
-
-
-
- “Tumaini la injili” ni kitu gani? (Kwamba Yesu ametupatia zawadi ya uzima wa milele. Sio sawa na kufanikiwa katika kazi yetu.)
-
-
- Soma Wakolosai 1:24. Paulo anatuambia kuwa anapitia mateso katika “mwili” wake. Paulo anayalinganisha maisha yake na ya nani? (Yesu. Paulo anaashiria kwamba anapitia mateso ambayo Shetani hakuweza kumpiga nayo Yesu.)
-
-
- Je, Paulo anadhani kuwa anatuokoa kwa mateso yake? (Anasema kuwa mateso yake ni “kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa.” Hivyo, Paulo anaamini kwamba anaongezea kwenye kile ambacho Yesu ametutendea.)
-
-
-
-
- Hilo linawezekanaje? Paulo si Mungu. Hawezi kudai kuchukua nafasi ya Yesu. (Kumbuka mada tuliyokuwa tunajifunza kuhusu mateso. Ayubu aliteseka kutokana na mgogoro kati ya wema na uovu. Alimpa Mungu utukufu. Pia tuliona hali ilikuwa vivyo hivyo kwa wanafunzi wa Yesu. Hilo, ninaamini, ndilo jambo analolizungumzia Paulo hapa. Mateso yake mikononi mwa Shetani yanatupatia mfano wa kile kinachowezekana kwenye vita inayoletwa na Shetani.)
-
-
-
- Soma Wakolosai 1:25-26. Kazi ya Paulo ni nini? (Kuweka bayana “siri” hii kwamba Yesu amekuja kutupatia wokovu.)
-
-
- Soma Waefeso 3:4-5. Hii inatuambia kuwa siri hiyo ni ipi? Na wajibu wa wanafunzi katika siri hiyo ni upi? (Kwamba Mungu alifanyika kuwa mwanadamu ili kutuokoa kutoka dhambini. Wanafunzi waliusambaza ujumbe huo.)
-
-
- Soma Wakolosai 1:27-28. Maarifa gani mapya yanafunuliwa kwa watu wa Mataifa? (Tumaini lao kwa Yesu. Yesu akaapo ndani yetu hutupatia “tumaini la utukufu.”)
-
- Soma Wakolosai 1:29. Paulo anasema kuwa “kujitaabisha” kwake ndicho ambacho amekiweka kwetu? Tunaweza kutumia maneno gani ya haki kuelezea kutaabika kwa Paulo? Je, ni kupambana sana ili kufanikiwa kama Mkristo? (Hapana! Paulo anasema kuwa anapambana na mateso (kama alivyopambana Yesu), na kazi yake ni kusambaza siri za injili – kile alichotutendea Yesu.)
-
-
- Kutokana na kile alichokielezea Paulo, nini inayopaswa kuwa asili ya kazi yetu kama Wakristo? (Kusambaza injili. Kutangaza siri za jinsi Yesu anavyowapatia wadhambi wokovu. Kutambua kwamba mateso yanatoka kwa Shetani na dhambi. Baadhi ya mateso hayo yanatujia kwa sababu sisi ni wafuasi wa Yesu.)
-
- Wajibu wa Roho Mtakatifu
-
- Soma Yohana 16:7. Yesu anaona manufaa gani ya kuondoka kwake na kuwaacha wanafunzi? (Kwamba watampata “Msaidizi” mpya.)
-
- Hebu tutatue siri kuhusu huyu “Msaidizi.” Soma Yohana 16:13, huyu “Msaidizi” ni nani? (Roho Mtakatifu. Roho wa kweli.)
-
- Soma Yohana 16:8-11. Wajibu wa Roho Mtakatifu ni upi? (Kuuhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi na haki.)
-
-
- Hebu tutafakari swali la muhimu sana. Je, umepewa kazi ile ile kama ya Roho Mtakatifu? Je, hii ni sehemu ya kutaabika kwako? (Nadhani kazi yetu ni kusambaza habari za Yesu na za Roho Mtakatifu. Lakini, inaonekana kuwa na mantiki kwamba hatupaswi kuidai kazi ya ama Yesu au Roho Mtakatifu. Hatupaswi kudai kwamba tuna uwezo wa kuwapatanisha watu na Mungu na hatupaswi kudai kuwa na uwezo wa kuwahakikisha watu dhambi.)
-
-
-
- Hii inazungumzia nini kuhusu maisha yetu wenyewe? Je, tunaweza, kwa bidii yetu wenyewe, kugeuka na kuacha dhambi?
-
-
-
- Yohana 16:8 inapotuambia kuwa Roho Mtakatifu “anauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi,” ni nini lengo la huo uhakikisho?
-
-
-
-
- Je, itakuwa na mantiki kujibu, “Ili niweze kugeuka na kuiacha dhambi?”
-
-
-
-
-
- Je, itakuwa na mantiki kujibu, “Ili niweze kutegemea kile ambacho Yesu amenitendea?”
-
-
-
-
-
- Je, kuna lolote lililo katikati ya hayo ambalo lina mantiki?
-
-
-
- Soma Yohana 16:12-15. Utaona kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni “kuongoza” na “kutangaza.” Tunapoongezea hili kwenye kile tulichokijadili hivi punde kuhusu “Kuuhakikisha,” hii inaashiria kuwa jibu sahihi kutoka kwetu ni lipi? (Tunafuata mwongozo. Kiongozi wetu anapotangaza ukweli na mawazo yetu yanahakikishwa kwamba tunatakiwa kubadilika, inaonekana kuwa na mantiki kwamba tunatakiwa kufuata dhamira zetu.)
- Mtazamo Sahihi
-
- Soma 1 Petro 1:3-5. Tunaokolewaje? (Kwa imani katika kile alichotutendea Yesu.)
-
-
- Kitu gani kinatuweka kwenye huo wokovu? (“Tunalindwa kwa njia ya imani.”)
-
-
- Soma 1 Petro 1:6. Kwa nini jaribu liwe na “muhimu?”
-
- Soma 1 Petro 1:7. Je, hiki ndicho kifungu ambacho nimekuwa nikikitafuta – kifungu kinachosema kuwa mateso hututakasa? (Kifungu hiki kinasema mateso hujaribu imani yetu. Imani yetu ni sawa na dhahabu. Imani yetu ya dhahabu inaweza kupotelea motoni.)
-
-
- Ni nini yanayopaswa kuwa matokea ya jaribu? (Kwamba tunampa Yesu sifa, utukufu, na heshima. Hii ni kama ilivyotokea kwa Ayubu na wanafunzi. Majaribu yaliwapima. Majaribu hayakuwatenganisha na Mungu, yalimpa Mungu utukufu.)
-
-
- Hebu angalia mpangilio wa mambo hadi kufikia hapa. Tunaokolewa kwa imani katika Yesu. Imani hiyo inaweza kuwa chini ya kipimo kwa njia ya jaribu. Soma 1 Petro 1:13-16. Wokovu kwa njia ya imani pekee unatupatia wito wa kufanya nini? (Kuwa watakatifu kama Mungu alivyo mtakatifu, badala ya “kujifananisha na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu.”)
-
-
- “Ujinga” unahusianaje na hili? Ni wa muhimu kiasi gani? (Roho Mtakatifu anakuhakikisha kwamba kuifuata njia ya dhambi kuna madhara kwako na madhara kwenye sifa njema ya Mungu. Usingependa kujidhuru wewe mwenyewe au kumdhuru Mungu wako.)
-
-
- Soma 1 Petro 1:17-19. Kifungu hiki kinasema kuwa “tumekombolewa” kwa damu ya Yesu. Lakini, pia kinasema kuwa Mungu anatuhukumu kwa haki kwa mujibu wa “matendo” yetu. Je, Petro anasema mambo yanayokinzana? Ikiwa sivyo, unayalinganishaje mambo hayo? (Hatuokolewi kwa matendo yetu mema. Tunaokolewa kwa imani yetu. Lakini, katika mfululizo wa masomo haya kuhusu mateso tulihitimisha kuwa sababu ya Shetani kutuletea mateso ni ipi? (Ni kututenganisha na Mungu. Hiyo inatuambia kuwa utenganishaji unawezekana. Mungu atatuhukumu kama tu waaminifu kwake. Kwa uongozi wa Roho Mtakatifu tunaweza kuona yanayomtangaza Mungu na yasiyomtangaza. Ninadhani ni katika dhana hiyo ambapo matendo yetu huleta tofauti kwenye hukumu. Matendo yetu hayatuokoi. Yanabainisha tu kama tumeamua kujitenganisha na Mungu.)
-
- Rafiki, je, hili linakusaidia kuiona njia ya kweli? Wokovu sio sawa na biashara, kwamba ukifanya kazi kwa bidi na kwa ueledi utafanikiwa. Yesu ndiye anayetoa wokovu kama zawadi ya bure. Wakati huo huo mtu anayemwamini Yesu kwa dhati, na anakitegemea kifo chake ili kutimiza matakwa ya sheria, anaelewa kwamba tunapaswa kufanya chaguzi za kuutangaza Ufalme wa Mungyu. Je, utadhamiria, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kufanya chaguzi hizo sahihi?
- Juma lijalo: Tumaini Lisilotetereka.