Somo la 9: Maisha ya Sifa 

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Wafilipi 4, Yoshua 5 & 6, Matendo 16, 2 Mambo ya Nyakati 20
Swahili
Year: 
2022
Quarter: 
3
Lesson Number: 
9

Somo la 9: Maisha ya Sifa 

(Wafilipi 4, Yoshua 5 & 6, Matendo 16, 2 Mambo ya Nyakati 20) 

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza. 

Utangulizi: Mazungumzo ya “TED Talk” niliyoyatazama miaka michache iliyopita yalizungumzia suala la mitazamo ya kiakili. Mzungumzaji mwanamke alisema kuwa kabla hajafanya wasilisho lenye umuhimu kwanza ananyoosha mikono juu ya kichwa chake – ambayo itaonyesha umbo la “Y.” Alisema kuwa kitendo hiki humpa hisia za ujasiri. Zaburi 63:4 inasema “Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai; kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.” Mzungumzaji huyu alijiingiza kwenye jambo ambalo ninaamini Mungu alilibuni ndani yetu – kumtukuza Mungu hubadili mtazamo wetu. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi juu ya kumsifu Mungu na kile inachotutendea! 

I.  Athari za Kusifu 

A.  Soma Wafilipi 4:4. Mwalimu wa Biblia wa chuo kikuu aliwahi kuniambia kuwa kuna nyakati ambazo hakujisikia kumsifu Mungu. Huyu ni mtu ambaye nilikuwa ninamhusudu sana na nikashindwa kujua niichukulieje kauli yake. Wewe una maoni gani juu ya kauli hiyo? 

1.  Kifungu chetu cha Biblia kinatuambia kuwa tufurahi siku zote katika Bwana. Je, inawezekana kufurahi katika Bwana bila kujisikia kumtukuza? 

B.  Soma Wafilipi 4:5. “Upole” wangu unahusianaje na kufurahi katika Bwana? (Baadhi ya tafsiri za kale kabisa zinatafsiri neno hilo kama “wastani,” “uvumilivu,” au “unyenyekevu.” Hiyo inamaanisha kuwa kufurahi katika Bwana hubadili mtazamo wetu. Hutufanya tufikiri vizuri zaidi.) 

C.  Soma Wafilipi 4:6-7. Matokeo ya kufurahi katika Bwana ni kuwa na mtazamo wa namna gani? (Tuna “amani ya Mungu.” Mwalimu wa Biblia wa chuo kikuu hakuelewa somo lisemalo kuwa katika nyakati za kukatisha tamaa ambapo hakujisikia kumtukuza Mungu, angeweza kuboresha hali yake ya akili kwa kumsifu Mungu.) 

1.  Mazungumzo ya “TED talk” ya yule mzungumzaji mwanamke yanaendanaje na vifungu hivi vya Wafilipi? (Alikuwa anainua mikono yake kwenye nafasi ya kusifu. Kwa kufanya hivyo alijipatia amani na ujasiri!) 

D.  Soma Wafilipi 4:8. Mara zote huwa ninawaza kwamba kifungu hiki kinaniambia kuwa sio vizuri “kuyafikiria” mambo machafu au yasiyo na staha. Mara moja hiyo ikanifanya nikumbuke matukio ya jinai ninayoyatizama kwenye televisheni. Tafakari juu ya muktadha tulioujadili. Unadhani kiuhalisia kitabu cha Wafilipi kinatufundisha nini kwenye kifungu hiki? (Nadhani huu ni ushauri juu ya afya ya akili. Je, ungependa kuwa na amani? Basi zingatia mambo yaliyo sahihi na mazuri.) 

1.  Jambo moja ninalopaswa kulibainisha kumhusu mwalimu wa Biblia wa Chuo Kikuu ni kwamba mwanaye wa kiume alikuwa amefariki. Je, tunaahidiwa mtazamo ulioboreshwa kwa Mungu katikati ya janga la kutisha? 

E.  Soma Wafilipi 4:9. Je, mtazamo chanya na wa amani ndio ambao Mungu anataka tuwe nao? (Yeye ni “Mungu wa amani,” na kumtukuza hutupatia amani.) 

II.  Sababu ya Kusifu 

A.  Watu wa Mungu walipoondoka utumwani nchini Misri na kuelekea katika nchi ambayo Mungu aliwaahidia, mji wa Yeriko uliozingirwa kuta ulikuwa tatizo kubwa sana mbele yao. Soma Yoshua 5:13-14. Yoshua ni amiri wa watu wa Mungu. Unaelezeaje jambo hili kwamba “amiri wa jeshi la Bwana” hayuko upande wao? (Anasema, kwa kushangaza, kwamba hayuko upande wowote ingawa anakaribia kuungana na watu wa Mungu.) 

B.  Soma Yoshua 5:15. Huyu “amiri wa jeshi la Bwana” ni nani? (Huyu ni Yesu, hakuna malaika ambaye angesema kwamba mahali asimamapo ni patakatifu kutokana na uwepo wake.) 

1.  Tafakari jambo hili. Mungu anasema kuwa hayuko upande wetu wala upande wa “watu wabaya.” Hilo linakupatia amani kwa kiasi gani? (Mungu yuko upande wa Mungu. Anatusihi tuwe upande wake pia. Hii inaashiria jambo la muhimu juu ya lengo la maisha yetu la kumpa Mungu utukufu.) 

C.  Hebu tusome mpango wa pambano katika Yoshua 6:2-5. Chukulia kwamba hukuwahi kusikia kisa hiki kabla. Je, mpango huu una mantiki yoyote? (Hapana!) 

1.  Tumesoma jambo gani linaloufanya mpango huu uwe na mantiki? (Jeshi la msingi ni lile la Bwana, na sio lile la Yoshua.) 

2.  Tumia dhana hii kwenye changamoto unazokabiliana nazo maishani mwako. Ikiwa uko upande wa Mungu, ikiwa unatenda kazi ili kumpa Mungu utukufu, matatizo gani yanaweza kustahimili jeshi la Mungu? 

a.  Je, mtazamo huu ni kanuni ya amani na kusifu? 

D.  Soma 2 Mambo ya Nyakati 20:1-3. Mfalme Yehoshafati anabaini kwamba majeshi matatu yanakuja kumchukua (na taifa lake) na wamekaribia sana. Jambo la kwanza analolifanya Yehoshafati ni lipi? (Anamgeukia Mungu kwa njia ya maombi.) 

E.  Soma sehemu ya ombi la Yehoshafati linalopatikana katika 2 Mambo ya Nyakati 20:10-12. Je, Yehoshafati anakabiliana na tatizo hili isivyo haki? (Anamwambia Mungu kuwa hii sio haki. Anasema kuwa inawezekana hapo awali Mungu alitoa uamuzi mbaya kuhusu kuyavamia mataifa.) 

F.  Soma 2 Mambo ya Nyakati 20:17. Watu wa Mungu wanaambiwa wafanye nini na pia wanaambiwa wasifanye nini? (Wanaambiwa “kusimama imara” lakini hawaambiwi kupigana.) 

G.  Soma 2 Mambo ya Nyakati 20:20-22. Je, ungeiweka kwaya mbele ya maaskari? 

1.  Angalia mpangilio wa muda katika kifungu cha 22. Ninasoma kifungu hiki kama kwamba kinasema walipoanza “kuimba na kusifu.” Mungu akaandaa mavizio (uvamizi) dhidi ya maadui wao. Kusifu kwao kukaamsha matendo ya Mungu kwa niaba yao. Je, unasoma maneno haya kwa namna hiyo hiyo? 

2.  Utatumiaje “kwaya hii mbele ya maaskari” kwenye matatizo unayokabiliana nayo maishani mwako? 

3.  Unadhani kwa nini jeshi lao lilikuwepo? 

III.  Kutekeleza Sifa Kivitendo 

A.  Yesu anatupatia ombi la mfano katika Mathayo 6:9-13. Soma Mathayo 6:9. Msitari wa kwanza wa ombi letu la mfano unahusu nini? (Kumtukuza Mungu! Jambo la kwanza ambalo Yesu anasema tulifanye tunapomgeukia Mungu ni kumtukuza.) 

B.  Soma Zaburi 145:10. Nani anayemtukuza Mungu kwa mujibu wa kifungu hiki? (Uumbaji wa Mungu na watakatifu wa Mungu.) 

C.  Hebu turejee nyuma na tuangalie baadhi ya maelekezo ya Yesu yaliyotolewa kabla ya Sala ya Bwana. Soma Mathayo 6:6. Sasa ilinganishe na Zaburi 145:10-12. Je, kutukuza kwetu kunapaswa kuwa kwa siri? (Yesu anatuambia kuwa sala zetu, zinazoanza kwa kutukuza, zinapaswa kuwa za siri. Vinginevyo kusifu kwetu kunapaswa kuwa hadharani.) 

1.  Ni lini mara ya mwisho ulimtukuza Mungu hadharani nje ya kanisa? 

D.  Katika Matendo 16 Paulo na Sila wanapigwa na kutupwa jela kwa kukiuka haki zao za uhuru wa dini. Mashtaka yao ni kwamba hotuba zao za kidini na matendo yao ya kidili viliathiri shughuli za wengine. Soma Matendo 16:23-25. Kuna jambo gani lisilo la kawaida kuhusu kusifu huku? 

1.  Je, ungejisikia kumsifu Mungu baada ya kupigwa, kutupwa gerezani, na kufungwa miguu kwa kamba ili usiweze kujongea na kujisikia faraja? 

E.  Soma Matendo 16:26-28. Kwa nini wafungwa wengine wote walikuwepo? Kwa nini hawakukimbia? 

F.  Soma Matendo 16:29-30. Kwa nini bwana jela anawauliza wafungwa wawili juu ya kile anachopaswa “kukifanya ili apate kuokoka?” Unadhani kwa kawaida huwa anawauliza hivyo wafungwa wake? (Sehemu ya msingi ya jibu la kwa nini wafungwa wengine bado waliendelea kuwepo na kwa nini bwana jela aliuliza juu ya wokovu inahusiana na maombi na kusifu kwa Paulo na Sila. Kila aliyesikia kilichotokea alihisi kuwa jambo lisilo la kawaida lilikuwa linatendeka.) 

1.  Kwa nini bwana jela na wafungwa wengine wadhani kuwa jambo hili si la kawaida? (Kwa sababu lilitokea katika muktadha ambao, kwa uzoefu wao, matokeo yake yangekuwa ni hasira na chuki. Kusifu katika kipindi hiki ilikuwa jambo lisilo na kifani.) 

2.  Tunajifunza nini? Kusifu kwetu kunawezaje kuwa na ufanisi zaidi? (Kumsifu Mungu katikati ya taabu na majaribu ndio kutukuza kwenye ufanisi mkubwa. Huko ni kusifu kusikotarajiwa kabisa.) 

G.  Rafiki, kumfifu Mungu huleta baraka! Hukubadilisha. Sio tu kwamba sifa humpa Mungu utukufu, bali pia ni ufunguo wa ushindi dhidi ya majaribu maishani. Unapomsifu Mungu ukiwa katikati ya matatizo, sio tu kwamba Mungu atakupigania, bali pia unadhihirisha ushuhuda kwa Mungu usio na kifani. Je, utadhamiria, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kufanya suala la kumsifu Mungu kuwa sehemu ya muhimu ya maisha yako? 

IV.  Juma lijalo: Unyenyekevu Ndani ya Tanuri (Kalibu)