Somo la 12: Falsafa ya Maisha ya Kibiblia

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Mwanzo 1 & 3, 1 Wakorintho 6, 1 Wathesalonike 5, 1 Yohana 3
Swahili
Year: 
2022
Quarter: 
4
Lesson Number: 
12

Somo la 12: Falsafa ya Maisha ya Kibiblia

(Mwanzo 1 & 3, 1 Wakorintho 6, 1 Wathesalonike 5, 1 Yohana 3)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2020, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Siku nilipoandika maneno haya kesi muhimu ya uhuru wa dini ilikuwa inaendelea mbele ya Mahakama Kuu ya Marekani. Kanisa langu liliandaa waraka mdogo wa kuunga mkono uhuru wa dini katika kesi hii. Mtu aliyesimama mbele ya Mahakama kujenga hoja kwa niaba ya uhuru wa kuabudu alikuwa ni mhitimu wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Regent – ambapo ninafundisha.  Katika upande mmoja wa kesi kuna binti anayeamini kwamba anapaswa kuendesha biashara yake kwa namna inayoendana na mafundisho ya Biblia. Upande mwingine katika kesi hii limesimama Jimbo la Colorado linalojenga hoja kwamba ikiwa matendo yako ya kidini yanakinzana na mitazamo yake basi haupaswi kuendelea na biashara hiyo. Kesi hii inaakisi mgawanyiko mkubwa na mkingamizo (polarization) wa mitazamo ya kidunia: mmoja uliojengwa juu ya Biblia na mwingine usio juu ya Biblia. Je, una ufahamu na jambo hili? Je, Ufunuo 13 inatuonya juu ya siku ambayo hatutaweza kufanya biashara (“hakuna atakaye nunua wala kuuza”) isipokuwa tu kama tutakuwa na alama iliyoidhinishwa na serikali? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

I.  Fundisho la Kwanza Chungu la Mungu

A.  Soma Mwanzo 3:2-5. Tunaonekana kurejea mara kwa mara kujadili kisa hiki. Kwa nini? Kwa sababu kisa hiki kina mafundisho mengi ya msingi sana. Hebu tuangalie mafundisho yanayohusu mitazamo ya kidunia:

1.  Mungu ana mtazamo gani wa kidunia juu ya uhuru wa dini? (Lazima utakuwa mmojawapo wa mambo anayoyathamini sana, vinginevyo kamwe asingeruhusu mazungumzo haya yatokee.)

2.  Mungu ana mtazamo gani wa kidunia juu ya umuhimu wa sheria yake? (Tunafahamu kwamba adhabu ya kukiuka sheria ya Mungu ni kifo – na Yesu alilipa adhabu hiyo.)

a.  Mungu alikuwa na mbadala gani? (Angeweza kuweka mambo ya pekee yasiyofuata hali ya kawaida. Ama kwa uhuru wa dini au kwenye sheria yake. Angeweza kuunda sheria mpya. Ukweli kwamba alikufa kutokana na sheria yake iliyopo inastahili tafakari ya kina.)

B.  Angalia tena Mwanzo 3:5. Hii inatufundisha nini juu ya mtazamo wa Shetani wa kidunia? (Wema na ubaya ni uchaguzi unaofanana. Kujua kila kitu bila ubaguzi ndilo jambo lenye thamani kuu.)

1.  Je, hicho ndicho kiini cha mkingamizo wa mitazamo hii leo? (Huu ndio mgongano haswa uliopo katika kesi iliyopo mbele ya Mahakama Kuu. Mtazamo mmoja wa kidunia unasema kuwa mawazo yote yako sawa na huwezi kuibagua mitazamo hii. Mtazamo mwingine (wa Kibiblia) ni kwamba baadhi ya mambo ni sahihi, mambo mengine hayako sahihi, na tunapaswa kutenganisha kati ya usahihi na ubaya.)

C.  Hoja iliyopo mbele ya Mahakama Kuu ni ya kisiasa, inahusu jinsi tunavyoielewa Katiba ya Marekani. Soma Mwanzo 2:15-17. Je, Mungu anakuwa mwanasiasa? (Ndiyo, anamwambia Adamu kanuni zinazoiongoza bustani (na ulimwengu).)

D.  Soma Mathayo 4:23. Wakristo wengi leo wanajenga hoja kwamba tunapaswa kuiepuka siasa na kujikita kwenye kuihubiri injili pekee. Je, huo ni mtazamo wa Kibiblia? (Kiini cha “habari njema ya ufalme” ni utawala wa sheria. Mungu alikufa kwa sababu hakuwa radhi kuuacha utawala wa sheria na alitupenda zaidi ya alivyoyapenda maisha yake mwenyewe.)

1.  Watu wengi wasiyoijua historia wanazishambulia nchi za “Magharibi” kutokana na makosa yaliyofanyika huko nyuma. Wengi wanajisikia vibaya kutokana na historia hii ya kale (ambayo hata hawakuhusika nayo). Kwa nini mtu aombe radhi kwa jambo ambalo hakulitenda? (Hili linatokea pale tu watu wanapoamini katika utawala wa sheria. Bila utawala wa sheria kuna nguvu pekee, na wenye nguvu kamwe hawahitaji kuomba msamaha. Sheria pekee ndio inayosimama juu ya uwezo (power).)

II.  Mfano wa Mungu

A.  Soma Mwanzo 1:26-27. Tukielewa kwamba tumeumbwa kwa “mfano” wa Mungu, wajibu wetu kwenye utawala wa sheria unapaswa kuwa upi?

1.  Utaona kwamba Mungu aliwapa wanadamu “utawala” juu ya wanyama. Hiyo inaonekana kama mamlaka ya kiuonevu (raw), haionekani kuwa kama utawala wa sheria. Kuna ushahidi gani wa Kibiblia kwamba uhusiano kati ya wanadamu na wanyama ulijengwa juu ya utawala wa sheria? (Soma Mwanzo 9:3. Wanadamu walikuwa hawaruhusiwi kula wanyama hadi kufikia hapa. Soma Mambo ya Walawi 11:2. Hapa tunaona kuwa mamlaka ya kula wanyama hayakuwa juu ya wanyama wote. Utawala wa sheria – uliowatenganisha wanyama – ulitumika ili kuweka ukomo wa chaguzi za wanadamu.)

B.  Soma 1 Wakorintho 6:18-20. Tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, na miili yetu ni “hekalu la Roho Mtakatifu.” Hii inatufundisha nini juu ya utawala wa sheria na chaguzi za kingono? Inazungumzia nini juu ya chaguzi zinazodhuru miili yetu? (Mungu anasema kwamba utawala wake wa sheria unahusika kwenye miili yetu. Vitendo vya ngono ambavyo ni kinyume na mafundisho ya Biblia sio uchaguzi sawa wala unaoruhusiwa.)

1.  Kifungu hiki kinazungumzia nini juu ya mtazamo wa sasa wa kitabibu kwamba ukiamua kupendelea jinsi nyingine, hata kama wewe ni mtoto, mwili wako unapaswa kubadilishwa kwa njia ya upasuaji ili uendane na uchaguzi wako?

2.  Hii inazungumzia nini juu ya haki za uhuru wa dini kwa wale wanaokataa kupatiwa chanjo wanayodhani kuwa inaweza kuidhuru miili yao?

III.  Msaada wa Kimtazamo

A.  Soma Yohana 16:12-13. Je, Yesu analinganisha uongozi wa Roho Mtakatifu na maneno yake mwenyewe? (Yesu anasema kuwa baadhi ya ukweli ambao angeweza kuutoa kabla utatolewa baadaye na Roho Mtakatifu. Kifungu hiki kinasisitiza kuwa ukweli unaofundishwa na Roho Mtakatifu unatokana na Mungu Baba.)

1.  Sote tumewasikia watu wanaodai kunena (au ambao kimsingi wananena) jambo ambalo Roho Mtakatifu amewafunulia. Je, tunapaswa kuzipokea kauli hizo bila kuzitafakari kwa kina? (Roho Mtakatifu hatakinzana na Biblia. Lakini angalia Matendo 15.)

B.  Soma 1 Wathesalonike 5:20-21.  Inamaanisha nini “kuyajaribu” maneno ya nabii? (Kwa uchache, inamaanisha lazima tuyajaribu maneno hayo kwa kutumia Biblia. Hatupaswi kuyapokea maneno ya mtu anayedai kuwa nabii wa Mungu bila kuyatafakari kwa kina.)

C.  Soma 2 Timotheo 2:15. Unadhani inamaanisha nini “kutumia kwa halali neno la kweli?” (Hata pale tunaposhughulika na mafundisho ya Biblia, tunatakiwa kuwa makini jinsi tunavyoyaelewa na kuyatumia.)

D.  Soma Yoeli 2:28-29. Kanisa litarajie kuwa na manabii wangapi? (Wengi!)

1.  Hili linatendeka lini? (Soma Matendo 2:16-18. Hii inathibitisha kwamba kipindi cha kuenea kwa unabii kilianza baada ya kufufuka kwa Yesu. Hawa ndio manabii wanaopaswa kujaribiwa kwa uthabiti.)

2.  Nimeipa sehemu hii kichwa cha habari “Msaada wa Kimtazamo.” Je, ingekuwa vizuri zaidi kama ningekipa jina kichwa cha habari “Mkanganyiko wa Kimtazamo?” (Ninadhani tahadhari juu ya kujaribu ni suala la “ishara dhidi ya kelele.” Patakuwepo na unabii mwingi usio sahihi (kelele), lakini Roho Mtakatifu analeta ishara ya muhimu ili kutusaidia kuielewa Biblia.)

3.  Je, nabii anaweza kuwa na kauli sahihi na zisizo sahihi? (Maelekezo ya kuujaribu unabii (1 Wathesalonike 5:20) yamelengwa kwenye unabii mahsusi na sio kwa nabii. Hii inafungua mlango kuelewa kwamba hata nabii wa Mungu anaweza kukosea jambo.)

IV.  Kuupeleka Utawala wa Sheria Katika Ufalme wa Mungu

A.  Soma 1 Yohana 3:1-2. Je, tutakuwa wakamilifu katika upande huu wa mbingu? (Hali yetu ya kimbingu “bado haijadhihirika.” Tunachoweza kukijua ni kwamba tutafanana na Yesu.)

B.  Soma 1 Yohana 3:3. Sasa wajibu wetu ni upi? (Kujaribu kufuata utawala wa sheria wa Mungu. Lengo letu ni kutenganisha kati ya wema na uovu, na kufuata kilicho chema.)

C.  Soma 1 Yohana 3:4. Dhambi ina tatizo gani? (Ni kutofuata sheria. Inakinzana na utawala wa sheria.)

D.  Rafiki, Mungu anatuita kwenye mtazamo unaoheshimu utawala wa sheria, utawala wa sheria wa Mungu. Dhambi ni ukataaji wa sheria. Dhambi ni kutoifuata sheria. Je, utafanya uchaguzi wa kutegemeza mtazamo wako wa kidunia kwenye sheria ya Mungu? Je, utajaribu kufanya kila utendalo, hata katika biashara yako, liendane na kanuni za Mungu? Kwa nini usiamue kufanya hivyo sasa hivi?

V.  Juma lijalo: Mchakato wa Hukumu.