Simulizi za Upendo

Simulizi za Upendo
Swahili
Year: 
2012
Quarter: 
1
Lesson Number: 
12
  1. Wimbo wa Kushtusha
    1. Soma Wimbo Ulio Bora 4:1. Macho yako ni kama ya hua, nywele zako ni kama kundi la mbuzi. Je, kuna kitu kinachokosekana kwenye hiyo tafsiri?
      1. Je, ni sifa zipi unazoziona kwenye haya maneno? (Macho ya rangi ya kijivu? Nywele nyingi na laini?)
    2. Soma Wimbo Ulio Bora 4:2. Je, kondoo walionyolewa manyoya bado ni weupe? Je, ni sifa zipi tunazoziona hapa? (Ninachukulia kuwa bado ni weupe. Meno ya mwanamke huyu ni masafi na meupe sana, ni ya kawaida na bado yapo yote. Ninawapenda wanawake walio na meno yao yote.)
    3. Soma Wimbo Ulio Bora 4:3. Mwanamke huyu ana mdomo kama uzi mwekundu na kinywa kizuri. Hata hivyo, je, nini kinaendelea kwenye panja (sehemu ya kulia na kushoto mwa uso) yake? Je, komamanga lina rangi gani? Yale niliyoyaona yanaonekana kuwa ya kijani! (Tafsiri ya Biblia inaniambia kuwa “panja” zilikuwa ni “sehemu ya juu ya kidevu” na kwamba sehemu ya ndani ya komamanga ina rangi ya uekundu. Alama ya uzuri/urembo katika nchi za magharibi ni sehemu ya kidevu iliyo ndefu ndefu, iliyo na aina fulani hivi ya urembo unaoonyesha kwa ung’avu sehemu ya kidevu. Mwanamke huyu ana kidevu chenye rangi ya uekundu.)
    4. Soma Wimbo Ulio Bora 4:4. Lazima Sulemani atakuwa na upendo kwa twiga! Je, unaweza kuona sifa katika hili? (Ndiyo. Shingo nzuri ya kupendeza. Nina uhakika ngao ni njozi/ishara ya vito anavyovifaa shingoni mwake.)
    5. Soma Wimbo Ulio Bora 4:5. Miaka mingi iliyopita nakumbuka mshiriki wa kanisa aliniambia (nilipokuwa na watu wengine) kuwa daktari wake alimwambia kuwa alikuwa na “matiti mazuri.” Je, hii inapaswa kuwa sehemu ya mazungumzo yetu miongoni mwa washiriki wa kanisa? (Ushauri wangu kwa masuala ya ndoa ni kwamba unapaswa kuepuka kuwaambia washiriki wa kanisa ambao sio mwenzi wako kile unachokifikiria kuhusu matiti yao!)
    6. Soma Wimbo Ulio Bora 4:6-7. Je, siku inaisha wakati gani na kivuli kinatoweka wakati gani? (Asubuhi!)
      1. Je, unadhani kuwa ni kitu gani kinachorejelewa hapa? Tumia misamiati inayokubalika kanisani unapojibu! (Nadhani hii inarejelea tendo la ngono. Nimesoma tafsiri za Biblia zinazorejelea mafungu yaliyotangulia na haya mafungu kwa mujibu wa mandhari ya kikanisa. Matiti yanarejelea “maadili rutubishi Kanisani” na “mlima wa manemane” ni Kalvari au Mlima Moria. Huo unaonekana kuwa ni upuuzi. Kama Mungu alitaka kutufundisha kuhusu Mlima Moria, angesema kuwa “Mlima Moria!” Kwa sababu fulani hivi Mungu anazungumzia kuhusu ngono.)
  2. Kwa Nini Ngono Ipo Kwenye Biblia?
    1. Hadi hivi sasa unajiuliza kuwa, “Kwa nini anayapitia mafungu haya? Hii inatahayarisha!” Je, tunapaswa kuomba msamaha kwa kujifunza Biblia? (Nimeyapitia haya mafungu katika kitabu cha Wimbo Ulio Bora kwa sababu ya msingi sana. Kama haya ni mambo ambayo ingekuwa vyema yasijadiliwe kanisani, ni kwa nini basi yamo kwenye Biblia? Je, lengo la Mungu kwenye upendo wa kimahaba ni lipi?
    2. Soma Mwanzo 2:21-25 na Mwanzo 1:27-28. Mafungu haya yapo wazi kabisa kwamba kabla dhambi haijaingia, Mungu aliumba ngono. Aliwaambia Adamu na Hawa “waongezeke” na alisema kuwa wawili watakuwa “mwili mmoja.” Je, sasa tumefikia sababu halisi inayohusu upendo wa kimahaba? Kwa ajili ya mafungu ya kupendeza kwenye kitabu cha Wimbo Ulio Bora.
      1. Kama umesema kuwa, “ndiyo,” jibu hili. Kwa dhahiri kabisa hakuna ishara katika Biblia kwamba Mungu anazaliana kwa njia hii. Kwa nini alitufanya tuzaliane kwa njia hii (ingawaje Mungu anasema kuwa tumeumbwa kwa mfano wake)?
        1. Je, ngono ni kama urembo/uzuri – kitu ambacho Mungu alikiumba sio kwa sababu nyingine tofauti na kutupatia raha?
        2. Fikiria suala hili kutokana na muktadha wa Mungu. Je, Mungu angeweza kutupatia uwezo wa kuwafanya/kuwatengeneza watu kama alivyomfanya Adamu na Hawa? (Mungu anaweza kufanya jambo lolote, lakini kwa sababu za msingi naweza kuona kuwa ni kwa nini hakutaka kutufanya kuwa waumbaji kwa namna ile ile ambayo yeye ni Muumba. Badala yake, Mungu alifanya namna ambayo sisi tunawafanya/tunawatengeneza watoto.)
        3. Je, unadhani Mungu alipata raha yoyote katika kuwaumba Adamu na Hawa? (Ninadhani kuwa hili ni kweli.)
          1. Je, hii inaweza kuelezea kuwa ni kwa nini Mungu anatupatia raha katika kuwafanya/kuwatengeneza watoto? (Inaleta mantiki kwangu kwamba Mungu alijaribu kuzalisha ndani yetu uzoefu wake kwa kadri ilivyowezekana kabisa kimantiki.)
    3. Soma Mwanzo 2:25 na Mwanzo 3:6-7. Baada ya dhambi kuingia, kuna kitu kilichotokea kwenye mahusiano ya kingono kati ya Adamu na Hawa. Je, yalikuwa ni mahusiano yapi hayo? (Macho yao yalifumbuliwa na waliona haya kwa kuwa uchi.)
      1. Soma Mwanzo 3:4-5. Je, nyoka alibashiri kitu gani? (Kwamba macho yao yatafumbuliwa.)
        1. Je, unawezaje kulielezea suala hili? (Katika mambo mengi mazuri Shetani ana jambo baya sambamba na jambo zuri. Uovu upo karibu kabisa na wema. Kwa mfano, nikihubiri somo zuri, majivuno yapo karibu kabisa baada ya kujiridhisha kufanya kazi/jambo zuri. Furaha na raha ya upendo wa kimahaba kwenye ndoa pembeni yake kuna uzinzi na picha za sinema za ngono. Haya ndio mambo ya bandia ya Shetani.)
  3. . Usambamba wa Upendo wa Kimahaba
    1. Soma Isaya 62:5. Ukiangalia muktadha huo, utabaini kuwa dhana ya fungu hili ni Yerusalemu. Je, Mungu analinganisha uhusiano wake na Mji wa Yerusalemu na kitu gani? (Mungu ni kama bwana arusi na Yerusalemu ni kama bibi arusi.)
    2. Soma Ufunuo 19:7-8. Je, Mwanakondoo ni nani na bibi harusi ni nani? (Mwanakondoo ni Yesu na bibi harusi ni kanisa – wale waliookolewa. Wale waliovaa vazi la haki walilopewa na Mungu.)
      1. Je, kwa nini Mungu ajilinganishe na Bwana Harusi na kanisa na bibi harusi?
      2. Je, inawezekana kwamba Mungu aliumba ndoa na ngono, sio tu kwa ajili ya furaha/raha ya mwanadamu, sio tu kwa ajili ya kufunua raha/furaha yake katika kutuumba, lakini pia kutufundisha masomo makuu kuhusu mahusiano yake na sisi?
    3. Soma Hosea 1:1-3. Je, ni kwa nini Mungu anampa Hosea maelekezo yasiyokuwa ya kawaida namna hii? (Kuelezea ni kwa namna gani kutokuwa na uaminifu kwetu kwa Mungu ni kama uzinzi wa wanadamu.)
      1. Je, Adamu na Hawa walijigundua kuwa wapo uchi wakati gani? (Walipofanya uzinzi dhidi ya Mungu. Wakati ambapo hawakuwa waaminifu kwa Mungu.)
      2. Je, hali ya Hosea ni mara ya kwanza aina hii ya kielelezo ilimjia Mungu mawazoni mwake? (Kimsingi hapana. Nadhani Mungu alitupatia upendo wa kimahaba kwa sehemu fulani ili kutufundisha hisia kuu zinazohusika katika kuvunja na kubomoa gundi ya upendo ya kimahaba. Hizo hisia kuu zilizopo kwenye uzinzi zinatufundisha kuhusu hisia za Mungu tunapofanya uzinzi dhidi yake, tunapokuwa hatuwi waaminifu kwake.)
      3. Kama umewahi kujihusisha kwenye hali ambayo kuna kutokuwa na uaminifu kwenye ndoa, je, mwonekano wa “mvunjaji wa nyumba/mahusiano” unaleta tofauti yoyote? (Kama “uvunjaji wa nyumba/mahusiano” sio suala zuri, au suala lililo baya zaidi kuliko mwenzi, basi hii inaongeza ukatishaji tamaa zaidi. Tunaweza kufikiria vitu vingine vingi tunavyoweza kuvilinganisha – fedha, akili nyingi, nafasi katika jamii/ofisi. Kama mvunja nyumba/mahusiano yupo chini kwenye kimojawapo kati ya vipimo hivi kuliko mwenzi, basi tunasema kuwa, “Nini kinachoendelea hapa!”)
        1. Je, ni nani aliye mshindani wa Mungu? (Hii inatuonyesha dhana nyingine ya ukataji tamaa wa Mungu dhidi yetu!)
    4. Soma Yeremia 2:1-3. Je, ni aina gani ya mahusiano ambayo Mungu anataka kuwa nayo dhidi yetu? (Mahusiano mapya yenye kupendeza tunayoyaona kwenye upendo wa kimahaba wa ujanani.)
    5. Soma Yeremia 2:20-22. Je, Mungu anatuonya kuwa tuwe kinyume na kitu gani?
      1. Je, ukomo wa hizi hisia za aina mbili unatufundisha nini kuhusu aina ya mahusiano ambayo Mungu anayatamania kwetu? (Mungu ana hisia kubwa kwa ajili yetu. Anatamani kuwa na mahusiano ya dhati kabisa na chanya dhidi yetu. Lakini, tunapomgeuka inamfanya ateseke maumivu makali sana.)
    6. Rafiki, je, una kila fikra kwamba Mungu anataka kuwa na mahusiano ya karibu na ya dhati kabisa nawe? Ninadhani kuwa Mungu alianzisha ngono kwa ajili ya sisi kujiburudisha na pia kwa ajili ya kuzaliana. Lakini, ninaamini pia kuwa aliuumba upendo wa kimahaba kwa lengo la kutusaidia kuelewa upendo mkuu na gundi ya kihisia anayotaka kuwa nayo dhidi yetu.
  4. Juma lijalo: Ahadi ya Kurudi Kwake.