Mungu Kama Msanifu

(Mwanzo 1, 1 Petro 3, Isaya 53)
Swahili
Year: 
2012
Quarter: 
1
Lesson Number: 
11

Utangulizi: Fikiria kuhusu kuangalia kitu kilichopakwa rangi nzuri, kuzama kwa jua kunakopendeza, taswira/mandhari nzuri, gari zuri au mtu mzuri. Je, tunawezaje kusema kuwa vyote hivi ni vizuri? Vina utofauti zaidi kuliko kufanana. Je, vina kitu gani hasa ambacho tunakiita kuwa kizuri? Kwangu mimi, uzuri katika hivi vitu vyote vilivyo tofauti ni kwamba ninafurahia kuviangalia. Mara nyingine raha inaonekana kuwa kama pumziko, na kwa watu wengine raha inaonekaza zaidi kuwa kama kitu cha kusisimua. Somo letu juma hili linachunguza upande wa usanifu wa Mungu – uzuri ambao ni sehemu ya haiba ya Mungu. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na kujifunza zaidi!

  1. Uzuri Katika Uumbaji
    1. Soma Mwanzo 1:31. Mungu yupo mwishoni mwa kazi yake ya Uumbaji na anasema kuwa, “chema sana.” Je, hiyo inapendekeza kuwa dunia ilikuwa nzuri?
      1. Je, Mungu angeshindwa kufanya kitu gani ambacho kingeifanya dunia iwe nzuri kidogo?
        1. Je, vipi kama wanyama wangefanana na wanadamu? Wanadamu wote wanaonekana kufanana. Tuna rangi tofauti, vimo tofauti na uzito tofauti, lakini vyote hivi vimewekwa kwa namna moja. Je, vipi kama ukweli huu ungekuwa kwa wanyama pia?
      2. Jibu moja ambalo ningelijibu kwenye swali la “ni kitu gani ambacho Mungu angeweza kukiacha” ni maua. Je, maua yana umuhimu gani maishani mwetu? (Hayana umuhimu. Hii inaonyesha kuwa Mungu anajali uzuri.)
      3. Jibu jingine ambalo ningelijibu ni samaki na ndege wenye rangi. Je, samaki na ndege wanahitaji kuwa na rangi ili waweze kuishi? (Kuna ndege wengi wenye rangi mbaya wanaoweza kuishi. Ndege wenye rangi nzuri wapo ili kuweza kupendezesha.)
      4. Kwa kingine chochote kile unachoweza kukifikiria, je, uzuri wake ni wa muhimu kwa ajili ya kuendeleza uhai wake? (Mungu alikupatia uzuri hata kama haukuhitajika. Jambo hili linasema kitu cha msingi sana kumhusu Mungu na mtazamo wake dhidi yetu.)
    2. Hebu tuzungumzie ubunifu wa ramani kidogo. Nissan alibuni gari (lijulikanalo kwa jina la the Cube) ambalo lina umbo lisilofanana/lisopacha (ikimaanisha kuwa upande mmoja unatofautiana na upande mwingine kwenye baadhi ya sehemu. Mara nyingi the Cube lina ulinganifu (ikimaanisha kuwa pande zote zinafanana). Fikiria kama wanadamu wasingekuwa wanafanana? Je, unahitaji matundu mawili ya pua, kinyume na tundu moja kubwa la hewa kwenye upande mmoja wa kichwa chako?
    3. Soma Zaburi 19:1. Je, umeona picha za nyota? Baadhi ya picha nilizoziona ni nzuri sana. Je, fungu hili linapendekeza nini kuhusu uzuri na utukufu wa Mungu? (Sehemu ya utukufu wa Mungu ni uzuri aliouumba.)
    4. Soma Ezekieli 28:17. Wanafunzi wengi wa Biblia wanaamini kuwa maelezo haya yanamhusu Shetani alipokuwa angali malaika kule mbinguni. Je, hii inasemaje kuhusu namna ambavyo Mungu alimuumba? (Mrembo!)
      1. Katika huu muktadha, uzuri wa Shetani ndio ulikua chanzo cha upotofu wake dhambini. Je, kwa nini Mungu amuumbe malaika mzuri huku akijua kuwa hii italeta tatizo? (Hii inatuambia kuwa uzuri una thamani inayojitegemea mbele za macho ya Mungu.)
  2. Uzuri Katika Wanadamu
    1. Soma Mwanzo 1:26. Je, hii inasema nini kuhusu wanadamu na uzuri? (Inasema kuwa tumeumbwa kwa mfano wa Mungu.)
    2. Soma Isaya 53:2-3. Huu ni unabii kumhusu Yesu. Je, Mungu alifananaje alipofanyika kuwa mwanadamu? (Isaya anasema kuwa Yesu hakuwa mzuri.)
      1. Je, hiyo inamaanisha kuwa Mungu sio mzuri? Je, hiyo ndio sababu tupo sawa, lakini sio wenye mwonekano mbaya wa aina fulani hivi? (Sifa nyingi za maisha ya Yesu kama mwanadamu zinaonekana kuegemea kwenye wazo kuwa alikuja duniani kama “mmoja wetu.” Alikuja kama “Adamu wa pili.” (Angalia Warumi 5:14 na 1 Wakorintho15:45.) Nadhani hiyo iliashiria mambo kadhaa hasi kwa Yesu kama mwanadamu. Alikuwa maskini. Mungu sio maskini. Hakuzaliwa kwenye ufalme. Mungu ni Mfalme wa Wafalme. Kama Yesu angekuwa tajiri, mfalme, mzuri sana ajabu, basi wale wasio hivyo wangesema kuwa Yesu “hakujaribiwa kwa kila namna, kama vile tunavyojaribiwa.” (Waebrania 4:15).)
    3. Soma Ezekieli 16:15. Je, hii inapendekeza kuwa nini chaweza kuwa tatizo la uzuri wa mwanadamu?
    4. Soma Luka 12:27-28 na 1 Petro 3:3-4. Tafsiri nyingi zinaingiza neno “tu,” ili kwamba mantiki ya Petro wa Kwanza ionekane kuwa “uzuri wako usitokane tu na jinsi ambavyo unatengeneza nywele zako, ubora wa mavazi yako, na uvaaji wa vito/dhahabu.” Je, Mungu aliyeyaumba maua yawe mazuri angetutaka sisi tuonekane takataka?
      1. Kama jibu ni, “Hapana, kama Mungu aliuumba uzuri katika maua, basi anahimiza uzuri katika wanadamu,” je, unalielewaje fungu hili katika Petro wa Kwanza? (Petro anasema kuwa uzuri wa kweli haujumuishi kile unachokivaa, jinsi unavyoremba nywele zako au thamani ya vito vyako. Badala yake, uzuri wa kweli unatoka ndani, unatokana na tabia yako.)
        1. Je, hii ni aina fulani hivi ya ulaghai? Nilipokuwa kijana, pale ambapo mtu mzima alinipendekezea kuwa nijiingize kwenye mahusiano na mtu mweye “haiba kubwa” nilijua kuwa hii ilikuwa ni kauli ya ishara ya “mtu mwenye mwonekano mbaya.” Je, Mungu anajaribu tu kuwafanya watu wa kawaida wajisikie vizuri?
    5. Soma Zaburi 96:9. “Uzuri wa utakatifu wake.” Je, hii inaonekana kuwa kama “uzuri wa utakatifu?” Kama ndivyo, je, utakatifu unawezaje kuwa na uzuri/urembo? (Hebu turejee kwenye utangulizi. Je, rangi, gari, kuzama kwa jua na mwanamke vinawezaje kuwa vizuri/virembo? (Tunasema, “Je, ninajibuje suala hilo?”)
    6. Sasa, hebu tusome Mithali 31:30 na kupitia 1 Petro 3:4. Je, “uzuri usioharibika wa roho ya upole na iliyotulia” ni upi? (Mafungu haya yote mawili yanatuambia kuwa uzuri wa mwili una “maisha yaliyo rafu” (uzuri haukai milele). Nimewaona wanawake waliokuwa warembo kwa miongo mingi - lakini nami pia ninakuwa mzee, kwa hiyo umri wangu unaweza kuwa na ushawishi kwenye maoni yangu. Hata hivyo, habari mbaya za Kibiblia kwa ajili yetu sote ni kwamba uzuri wa mwili kwa ujumla unapotea kwa kadri muda unavyokwenda.)
      1. Je, roho ya ukweli inawezaje kuwa nzuri/yenye urembo? (Uzuri/urembo ni “ni kwa jinsi gani ninakabiliana na suala hilo?” Je, ninakabilianaje na mtu mpole?
        1. Je, unawafahamu washiriki wa jinsia tofauti ambao ni wazuri sana kwa kuwaangalia lakini usingependa kuwaoa/kuolewa nao? Watu wazima waliokuwa wakiniambia kuhusu “haiba kubwa” hawakujihusisha kwenye ulaghai.)
      2. Je, ungependelea kitu gani: mwenzi mzuri lakini wa ovyo, au mwenzi wa kawaida lakini mwenye upendo? (Kwa vile uzuri unakwisha/unapotea, uwezekano uliopo ni kwamba kile unachosaliwa nacho ni u-ovyo na ukatili! Kama urembo unamaanisha kufurahia utazamaji, basi u-kawaida na upendo vinashinda.)
    7. Soma 1 Samweli 16:7. Je, tunahitimisha kwa kuangalia maombo ya nje tu?
    8. Soma Mithali 20:29. Hebu tuangalie ubunifu wa Mungu wa uzuri wa mwanadamu kwa mtazamo mwingine. Je, uzuri unaweza kubadilika kutokana na mabadiliko ya umri? (Ndiyo. Nini kinawapendeza vijana? Wana nguvu. Nini kinawapendeza wazee? Kwamba wao ni tofauti. Unaweza kupata raha (kuupata uzuri) kwenye mambo tofauti tofauti kumhusu mwenzi wako kwa kadri muda unavyozidi kwenda. Huenda ulifurahia uzuri wa mwili wa mwenzi wako ulipokuwa kijana, lakini unauona uzuri kwenye haiba, ubunifu, vichekesho, au busara ya mwenzi wako unapokuwa mzee.)
    9. Soma Zaburi 51:10. Kama tukiamua kuwa hatuna roho safi, Je, Mungu anaweza kuchonga ndani yetu tuwe watu wazuri zaidi?
  3. . Uzuri na Muziki
    1. Soma Ufunuo 15:2-3. Je, umewahi kumwona mtu “ameshika” kinubi? Tulikuwa na kinubi kwenye harusi ya binti wangu. Ulipaswa kukivuta hicho kitu kukiingiza kanisani. Rafiki, vifaa hivi ni gitaa! (Ninatania kidogo hapa.) Je, hii inasema nini kuhusu muziki na mbingu? (Itakuwa ni sehemu ya kumsifu Mungu!)
    2. Soma 1 Mambo ya Nyakati 23:1-5. Utabaini hapa kuwa, hii ni kwaya ya pamoja na okestra (kundi la watu wapigao muziki pamoja) yenye watu elfu nne! Je, umewahi kuwa kwenye kundi kubwa lililokuwa likiimba nyimbo za kumsifu Mungu?
    3. Je, kwa nini Mungu aliwapatia wanadamu (wengi wao) na baadhi ya wanyama uwezo wa kuimba? (Kwa mara nyingine tena, hii inaonyesha uzuri ulioumbwa na Mungu.)
  4. Uzuri na Patakatifu
    1. Kutoka 25 inaelezea maelekezo ya kujenga patakatifu jangwani. Soma orodha ya vitu vilivyotumika kwenye ujenzi katika Kutoka 25:2-8. Huu unaonekana kuwa ni uumbaji mzuri. Josephus anaelezea hekalu la Yerusalemu lililoharibiwa na Warumi kuwa lilikuwa ni jengo zuri na mahali pazuri ajabu. Je, kwa nini Mungu anajizungushia uzuri? (Kwa sababu anautambua na kuufurahia na anatutaka sisi pia tuutambue na kuufurahia.)
      1. Habari gani kuhusu kuwasaidia maskini badala ya kujenga makanisa mazuri na yenye kupendeza? (Halipaswi kuwa suala la “aidha/au.” Tunapaswa kujenga makanisa mazuri na tunapaswa kuwasaidia maskini. Vyote viwili, yaani uzuri na utu wema/upole ni sifa za Mungu.)
    2. Rafiki, je, unaweza kutambua na kufurahia kwa namna bora zaidi nafasi ya uzuri – mantiki ya raha unapokuwa mbele zake? Mungu, Msanifu Mkuu, alitubariki kuwa na uzuri!
  5. Juma lijalo: Simulizi za Upendo.