Somo la 8: Sabato na Mwisho

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Ufunuo 13 & 14, Kutoka 20, Kumbukumbu la Torati 5
Swahili
Year: 
2023
Quarter: 
2
Lesson Number: 
8

Somo la 8: Sabato na Mwisho

(Ufunuo 13 & 14, Kutoka 20, Kumbukumbu la Torati 5)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2023, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, umetafakari kwamba jina “kutunza/kulinda (conservative)” linamaanisha mtazamo wa kutunza vitu? Kutunza vitu jinsi vilivyo kwa sasa? Nchini Marekani tunakabiliana na vuguvugu linaalojaribu kufuta historia yetu badala ya kuihifadhi. Historia inayoakisiwa kwenye sanamu na majina ya majengo inafutwa kwa kubomoa sanamu na kuyapa majengo majina mapya. Kama hili ni jambo jema au baya inategemeana na mtazamo wako. Lakini ubomoaji huu sio jambo jipya. Ufunuo 14:17 inatuambia tumsujudie Mungu Muumbaji wetu. Shetani amekuwa akibomoa masalia ya Mungu Muumbaji wetu kwa muda mrefu sasa. Tumeangalia jinsi alivyoshambulia suala la uumbaji na jinsi anavyoshambulia ndoa kwa njia kadhaa. Juma hili tunageukia kwenye somo letu linalohusu jinsi ambavyo Shetani amekuwa akiishambulia Sabato, kumbukizi ya kila juma ya Uumbaji. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

I.  Kusujudu

A.  Soma Ufunuo 14:7 na Ufunuo 14:9. Kuna wito gani kinzani katika suala la kusujudu? (Wito wa kwanza ni wa kumsujudu Mungu Muumbaji. Wito mwingine unahusu kuvisujudu vitu vinavyoitwa “mnyama” na “sanamu yake.”)

B.  Soma Ufunuo 13:4-6. Joka ni nani na ana uhusiano gani na mnyama? (Tunafahamu kutoka Ufunuo 12:7-9 kwamba joka ni Shetani. Hiyo inamfanya mnyama kuwa wakala wa Shetani.)

C.  Soma Ufunuo 13:7-8. Mnyama anafanya nini kwa niaba ya Shetani? (Anafanya vita dhidi ya watu wa Mungu. Anataka kusujudiwa.)

1.  Uamuzi wa nani tutamsujudu ni wa muhimu kiasi gani? (Tukimsujudu mnyama, ambaye anamsujudu Shetani, basi tumepotea. Wale ambao majina yao yameandikwa kwenye kitabu cha uzima wanamsujudu Mungu na wala si mnyama au Shetani.)

D.  Soma tena Ufunuo 14:9 na usome Ufunuo 14:11. Tunaweza kuwatambuaje wale wanaomsujudu mnyama? (Wamsujuduo mnyama hupokea “chapa katika kipaji cha uso wao au katika mikono yao.” Alama hii inawakilisha jina la mnyama.)

1.  Angalia uhusiano kati ya alama na jina. Unauelewaje uhusiano huu? (Alama inaakisi tabia ya mnyama, ambaye ni wakala wa Shetani.)

E.  Soma Ufunuo 14:12. Hii inatuambia kuwa jibu kwa wale wanaoamua kumsujudu mnyama na kupokea alama yake ni lipi? (Watakatifu wana imani katika Yesu kwa ajili ya wokovu wao na wanazichukulia amri za Mungu kwa umakini.)

II.  Sabato

A.  Soma Mwanzo 2:1-3. “Siku ya saba” inawakilisha nini? (Ni ukumbusho mtakatifu wa uumbaji.)

1.  Hivi punde tumejifunza kuwa alama ya mnyama inaakisi tabia ya wakala wa Shetani. Je, Sabato inawakilisha tabia ya Yesu? Tabia ya kazi yake bunifu?

B.  Soma Kutoka 20:8-11. Kwa mara nyingine tunaambiwa kuwa Sabato ya siku ya saba ni “takatifu.” Unadhani maneno “siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako” yanamaanisha nini?

1.  Watu walitakiwa kufanya nini badala ya kufanya kazi? (Siku iliwekwa kwa ajili ya kumsujudu Mungu Muumbaji wetu. Hii inafafanua kwa nini Ufunuo 14:11-12 inahusianisha kati ya washika amri na suala la kupokea alama. Wale walio na imani kwa Yesu na kuzishika amri zake (ikiwemo amri ya nne) wanamsujudu Mungu na sio Shetani.)

2.  Je, inaleta mantiki kuhitimisha kwamba “alama” ya ibada ya uongo ni siku ambayo mtu anaabudu? (Mjadala wa kwa nini tunaabudu siku ya Sabato utatusaidia kuweka wazi suala hili. Katika sehemu inayofuata tunageukia kwenye sababu za kuabudu katika Sabato ya siku ya saba.)

III.  Sababu za Kuabudu Siku ya Sabato

A.  Soma tena Kutoka 20:11. Kwa nini tunaambiwa kuabudu siku ya Sabato? (Inatambua uwezo wa Mungu wa uumbaji na uamuzi wake wa kupumzika.)

B.  Soma Kumbukumbu la Torati 5:15. Amri za Mungu zinatamkwa tena katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati 5. Hapa inatolewa sababu gani ya kuabudu siku ya Sabato? (Uhuru kutoka utumwani kutokana na “mkono wa Mungu wenye nguvu.”)

C.  Soma Luka 23:54-56. Tunaona kundi gani likiishika Sabato? (Hawa ni wafuasi wa Yesu katika kipindi cha kusulubiwa na kuzikwa kwake.)

D.  Soma Yohana 19:31-33 na Yohana 20:17. Ingawa wafuasi wa Yesu walikuwa wakipumzika siku ya Sabato, vifungu hivi (na muktadha wake mpana) vinaonesha kuwa Yesu pia alikuwa amepumzika kaburini katika siku ya saba. Siku ya Jumapili anaelezea kuwa alikuwa bado hajapaa mbinguni. Kwa nini pumziko? Kwa nini kuchelewa katika ufufuo wake? Kwa nini asiruke na kupaa hadharani kutoka msalabani mbele ya macho ya wale waliomuua na kumdhihaki?

E.  Tumeona kwamba Sabato inaadhimisha Uumbaji na inaadhimisha kushindwa kwa mabwana wa Kimisri waliomiliki watumwa. Yesu aliitumia kuadhimisha ushindi wake dhidi ya dhambi na yule aliyedai kuwa ndiye mtawala wa dunia. Angalia Mathayo 4:8-9. Je, unaweza kuelezea kwa ufupi sababu za Kibiblia za kuabudu siku ya saba? (Inahusiana na uwezo wa Mungu kutubariki na kutupatia uhuru. Yesu hakubadili chochote kwenye uumbaji mkamilifu. Aliwashinda Wamisri wenye uwezo mkubwa (pamoja na miungu yao) ili kuwaweka huru watu wake. Yesu alimshinda Shetani ili kutukomboa kutoka dhambini na mauti ya milele.)

F.  Hebu turejee kwenye suala la “alama” linaloakisi tabia na uwezo wa Shetani. Unapoipuuzia Sabato, matendo yako yanazungumza nini? (Kwamba unakataa uwezo wa Yesu wa uumbaji, uhuru wake, na wokovu wake. Badala yake unaungana na adui wa mambo hayo.)

1.  Je, suala hili linaloendelea limetiwa chumvi?

G.  Soma Isaya 66:22-23. Mambo haya yanatendeka wapi? (Mbinguni!)

1.  Lengo la Sabato mbinguni ni lipi? (Kusujudu! Hii inaimarisha dhana ya kwamba Sabato ni suala la msingi kwenye suala la kumsujudu Mungu.)

2.  Watu hawa wamemchagua Mungu. Hawajaipokea alama ya mnyama. Je, Sabato sio historia ya Kale? Jambo lenye umuhimu katika siku za nyuma pekee? (Tafakari ibada hii ya Sabato kwa mujibu wa historia ya ibada ya Sabato. Katika kuadhimisha Uumbaji tunaongezea, uhuru kutoka utumwani, kushindwa kwa dhambi na Shetani, kuiadhimisha mbingu mpya, nchi mpya, na kukoma kwa dhambi. Kimsingi Sabato bado inaadhimishwa mbinguni!)

H.  Angalia tena Kutoka 20:11. Tunaona sababu ya msingi ya pumziko. Je, bado pumziko lina umuhimu mbinguni? (Bado tunapumzika katika uwezo na ushindi wa Mungu wetu.)

IV.  Angalizo Kali Dhidi ya Hoja Kinzani

A.  Ikiwa unakubaliana kuwa Shetani anazivunjavunja kwa hasira kumbukumbu zote za Mungu Muumbaji wetu, una mtazamo gani juu ya mbadala wa kumbukizi tofauti na Sabato? Kwa umahsusi, je, imani juu ya ndoa ya jinsia moja inaweza kuwa mbadala unaokubalika kwa kile ambacho Mungu alikibuni katika bustani ya Edeni? Je, mtazamo wa kwamba jinsia ni alama holela inayopachikwa wakati unapozaliwa ni mbadala unaokubalika kwa ajili ya jinsia mbili zilizobuniwa na Mungu?

1.  Kama umejibu, “hapana,” kwenye maswali haya, basi je, kubadili siku ya kwanza ya juma ni kumbukumbu inayokubalika?

B.  Hakuna mahala popote kwenye Biblia penye amri ya kuishika Jumapili. Hoja iliyopo ni kwamba siku maalumu sio suala la kulijali sana. Je, hiyo ni kweli? (Kama siku haijalishi basi kumbukizi nyinginezo zinazotoka Edeni pia hazijalishi. Kimsingi, Sabato pekee ndio inayotolewa na kuwekewa kumbukumbu ya Uumbaji.)

C.  Baraza la Laodikia lilifanyika mwaka 363 hadi 264 BK. Kanuni/sheria ya Kanisa namba 29 ya Baraza hilo inaelezea kwa umahsusi mabadiliko ya siku ya kuabudu: “Wakristo hawatakiwi kujiyahudisha kwa kupumzika siku ya Sabato, bali wanatakiwa kufanya kazi siku hiyo, kuiheshimu Siku ya Bwana; na, wakiweza, wapumzike kama Wakristo. Lakini kama kuna yeyote atakayeonekana kuyahudisha, hebu na walaaniwe na kuachana na Kristo.”

1.  Kwa uelewa wangu haya ndio mamlaka pekee yaliyoandikwa kwa ajili ya mabadiliko. Unapoyaangalia, yamejengwa juu ya nini? (Ubaguzi/chuki dhidi ya Wayahudi.)

2.  Kama chuki ya Wayahudi inatosha kubadili Amri ya Nne, vipi kuhusu amri zilizosalia? Je, pia sio za Kiyahudi?

3.  Ikiwa chuki ya Wayahudi inatosha kupuuzia kauli thabiti za Biblia kuhusu Sabato, vipi kuhusu mambo mengine yaliyoandikwa katika vitabu vya injili? Vipi kuhusu maandiko ya Paulo?

D.  Rafiki, kuna vita inayoendelea juu ya kumbukizi ya Uumbaji wa Mungu. Vita juu ya kusujudu. Je, utaungana na wale wanaosimama dhidi ya kuzifuta kumbukumbu? Je, utasimama na wale wanaomwabudu Mungu? Kwa nini, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, usifanye uamuzi sasa hivi?

V.  Juma lijalo: Mji Unaoitwa Machafuko.