Somo la 13: Ahadi ya Kurudi Kwake
Utangulizi: Wanasayansi wapumbavu. Wanaendelea kufanya utabiri kuhusu mwisho wa dunia, utabiri usiotimia. Utabiri mmoja unaposhindwa kutimia na kuwa wa uongo, wanafanya utabiri mwingine ambao msingi wake unajengwa kwenye tukio jingine tofauti. Nilipokuwa mdogo, walitabiri kuhusu kuwepo kipindi cha theluji, kipindi ambacho maisha yataganda. Nilipokuwa mtu mzima, walitabiri kuhusu kuongezeka kwa joto duniani, kipindi ambacho maisha yatakuwa kama vile yameunguzwa na moto na kuteketea. Lazima wanasayansi hao watakuwa ni kikundi cha watu wapumbavu ambao wanaongozwa kirahisi na imani kuendelea kutabiri mambo ambayo kamwe hayajawahi kutokea katika historia ya dunia. Hebu subiri kidogo! Je, hivyo sivyo wanavyosema kuhusu Wakristo? Kwamba tunaendelea kutabiri kuhusu mwisho wa dunia kwa sababu sisi ni wapumbavu na tunaendeshwa tu kirahisi? Je, tunafanana kabisa na wanasayansi wapumbavu? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na kujifunza zaidi!
- Historia Inajirudia Yenyewe
- Soma Matendo 1:1-2 na Matendo 1:6-11. Je, malaika waliwaahidi nini wanafunzi? (Kwamba Yesu atarudi.)
- Marafiki zetu wanasayansi wanatabiri mwisho ambao kamwe haujawahi kuwa sehemu ya historia ya dunia. Je, Wakristo wapo tofauti kwa namna gani? (Yesu alikuja duniani kutoka mbinguni. Hii ni sehemu ya historia iliyoandikwa. Malaika waliahidi kuwa Yesu atafanya hivyo mara ya pili, atarejea.)
- Soma 2 Petro 3:3-7. Je, ni changamoto gani inayojibiwa na hili fungu la Biblia? (Je, twawezaje kujua kwamba Yesu atakuja tena ukichukulia kwamba ni muda mrefu sasa umepita tangu aondoke?)
- Ni jibu gani linalotolewa? (Uthibitisho wa kihistoria!)
- Je, ni uthibitisho gani wa kihistoria unaotolewa na Biblia katika kuthibitisha ujio wa Yesu wa Mara ya Pili? (1. Yesu aliumba ulimwengu. Kwa hiyo, ana uwezo na nia ya kurudi. 2. Mungu aliangamiza uumbaji wake kwa gharika. 3. Huu ni uthibitisho zaidi kuwa Mungu atakuja tena na kuuangamiza uovu na dunia.)
- Angalia kwa makini neno “kusahau kwa makusudi.” Je, huo ndio ukweli kwa watu wenye kudhihaki hivi leo? Je, wale wanaoukana Uumbaji na gharika pia wanaukana ujio wake wa Mara ya Pili?
- Soma 2 Petro 3:8-9. Je, ni maelezo gani tunayoyapata hapa kuhusiana na muda wa kurudi kwa Yesu Mara ya Pili?
- Hebu turejee kwenye Matendo 1. Je, wanafunzi wanauliza kuhusu kitu gani kwenye Matendo 1:6? (Wanataka kujua kama Yesu atauangusha utawala wa Rumi.)
- Je, hii inatuonyesha kitu gani? (Kwamba wanafunzi bado walikuwa hawajaelewa kikamilifu ujio wa Yesu wa mara ya kwanza.)
- Je, hiyo inapaswa kutufundisha somo gani? (Tuna ahadi ya Ujio wa Yesu Mara ya Pili, tuna uthibitisho wa ujio wake wa mara ya kwanza, lakini tunahitajika kujiuliza kwa makini kwamba yawezekana hatuna uelewa sahihi wa suala hilo lote kwa ujumla wake.)
- Kutokana na mafungu tuliyojifunza, nini tunachoweza kukifahamu kuhusu ujio wa Yesu Mara ya Pili? (Matendo 1:11: Yesu alipaa mbinguni na kupotelea mawinguni. Kwenye ujio wa Mara ya Pili atawasili akiwa kwenye mawingu na kushuka kutoka mbinguni. 2 Petro 3: Tuna jambo kubwa sana kwenye ushahidi ulioandikwa linaloonyesha kuwa Mungu ana uwezo na nia ya kutenda jambo hili.)
- Je, hii inatuonyesha kitu gani? (Kwamba wanafunzi bado walikuwa hawajaelewa kikamilifu ujio wa Yesu wa mara ya kwanza.)
- Soma Yohana 4:1-3. Je, ni suala gani la msingi analolisema Yesu kuhusu ujio wake wa Mara ya Pili? (Huu ni uthibitisho binafsi wa Yesu kwamba atakuja tena. Atakapokuja tena itakuwa ni suala la kutuchukua na kutupeleka mbinguni.)
- Soma 1 Wakorintho 11:26. Je, suala la ujio wa Mara ya Pili ni fundisho dogo tu (lisilokuwa la msingi) la Ukristo? (Hapana. Mungu anaambatisha kumbukizi kwenye yale mambo anayoyachukulia kuwa ni ya umuhimu wa kipekee. Sabato ni ukumbusho kuwa Yeye ndiye Muumba wetu. Ushirika/Umoja ni ukumbusho kuwa alikufa kwa ajili ya dhambi zetu na kufufuka kutoka kaburini. Mungu anatuelekeza kuendelea kujikumbusha kuhusiana na mambo haya hadi pale atakaporejea. Hiyo hatimaye inatukumbusha kuhusu ahadi ya kurejea kwake.)
- Soma Matendo 1:1-2 na Matendo 1:6-11. Je, malaika waliwaahidi nini wanafunzi? (Kwamba Yesu atarudi.)
- . Jaribu
- Soma Mathayo 24:1-3. Je, wanafunzi walimwuliza Yesu swali moja au maswali mawili? (Ni punde tu Yesu alikuwa ameelezea kuangamizwa kwa hekalu Yerusalemu. Wanafunzi walidhani kuwa hili litakapotokea, huo ndio utakuwa mwisho wa dunia. Walifikiri kuwa walikuwa wanauliza swali moja, lakini twafahamu kuwa walikuwa wanauliza maswali mawili.)
- Soma Mathayo 24:4-5. Je, ni kitu gani cha kwanza anachotuambia Yesu kuhusu ujio wake wa Mara ya Pili? (Kwamba patakuwepo watu walaghai/matapeli.)
- Soma Mathayo 24:23-25. Je, Yesu anatuonya kuhusu kitu gani? (Kwamba mmojawapo wa hawa matapeli, Kristo wa uongo, atatenda miujiza mikubwa na ishara.)
- Soma 2 Wathesalonike 2:1-4. Je, ni kitu gani kitakachotangulia marejeo ya Yesu? (Mpinga Kristo atakuja na kujifanya kuwa Mungu!)
- Soma 2 Wathesalonike 2:9-12. Je, ni nani aliye mmojawapo wa hawa matapeli? (“Asiyetii sheria.” Huyu ni wakala wa Shetani atakayetenda “miujiza, ishara na maajabu ya bandia.”)
- Soma Mathayo 24:26-27 na Ufunuo 1:7. Je, tunawezaje kuuelezea kwa uhakika kabisa ujio wa Yesu Mara ya Pili wa kweli dhidi ya ujio wa uongo wa mpinga Kristo? (Ujio wa Yesu utakuwa ni tukio la ulimwengu wote, tukio litakaloonekana mawinguni na “kila jicho” kwa wakati mmoja. Litakuwa kama radi duniani kote.)
- Soma 1 Wathesalonike 4:16-18. Je, ni ishara gani nyingine zisizo na makosa tutakazoziona? (Waliokufa katika Kristo watafufuliwa. Waamini walio hai watampokea Yesu mawinguni.)
- Je, Yesu ataendelea kuwepo na kuzungukazunguka duniani? (Hapana.)
- Soma 2 Wathesalonike 2:8. Je, Yesu wa bandia, mpinga Kristo, yupo anazungukazunguka duniani? (Ndiyo. Inaonekana kuwa Yesu anakuja mara tu baada ya yule wa bandia. Yule wa bandia anaangamizwa kwa pumzi ya kinywa cha Yesu na uwezo wa Yesu.)
- Hebu tupitie tena. Tunawezaje kuuelewa ujio wa Yesu Mara ya Pili dhidi ya ule wa bandia wa Shetani? (Kama mtu fulani anadai kuwa yeye ni Yesu, lakini haonekani kwa kila mtu katika dunia nzima, kama wafu hawafufuliwi, na kama hatumlaki Bwana wetu mawinguni tukielekea mbinguni, basi tunajua kuwa huyu sio Yesu, ni Yesu wa bandia.)
- I. Hatma ya Waaminifu
- Soma Ufunuo 21:1. Je, nini kinachotokea baada ya wenye haki kuchukuliwa kwenda mbinguni? (Yesu anaumba nchi mpya.)
- Je, nini kilicho tofauti kuhusu hii nchi mpya? (Haina bahari tena. Nimesoma kwamba takriban asilimia 70 ya dunia imefunikwa na maji.)
- Je, maelezo haya yanapendekeza kitu gani? (Yanapendekeza mambo mawili. Kwamba dunia kwa namna nyingine itatambulika. Hata hivyo, nyongeza ya asilimia 70 inamaanisha kuwa mahali/sehemu kwa ajili ya wanadamu kuishi itaongezeka kwa kiwango kikubwa sana. Nilisoma kitabu kilichopendekeza kuwa kwenye dunia itakayofanywa upya tutatambua sehemu tunazozifahamu hivi sasa.)
- Je, nini kilicho tofauti kuhusu hii nchi mpya? (Haina bahari tena. Nimesoma kwamba takriban asilimia 70 ya dunia imefunikwa na maji.)
- Soma Ufunuo 21:2-4. Yesu alipokuja mara ya pili, aliwachukua wenye haki kwenda mbinguni. Je, kitu gani kinaendelea hapa? (Hii inaleta mantiki kamilifu kabisa. Waliookolewa wanakwenda mbinguni, na Yesu anaangamiza na kuijenga upya dunia na mbingu zake. Kisha Yerusalemu Mpya inashuka kutoka mbinguni, sambamba na Mungu pamoja nasi. Baada ya hapo sote tutaishi kwenye nchi mpya. Dunia iliyofanywa upya ndio itakayokuwa kiini cha utawala wa ulimwengu, kwa kuwa Mungu anakaa pamoja nasi! Kama unataka kusoma maelezo ya Yerusalemu Mpya, soma Ufunuo 21:10-21.)
- Soma Ufunuo 22:1-3. Kauli ya kwamba hatutakuwa tena na bahari yoyote ilinisikitisha kidogo kwa sababu mimi ni mtu ninayependa maji. Je, ni aina gani ya maji tunayoyaona kwenye nchi iliyofanywa upya? (Kwa hakika, Mungu anapenda maji pia, kwani ana maji yanayotiririka kutoka kwenye kiti chake cha enzi!)
- Soma Ufunuo 22:4-5. Je, unatarajia nini kizuri zaidi kwenye nchi itakayofanywa upya? (Kuwa pamoja na Mungu!)
- Rafiki, hiki ni kiashiria cha ajabu kiasi gani kwenye hatma yetu! Sote tunafanya utabiri kuhusu hatma yetu ya siku zijazo. Tofauti kati yetu na wanasayansi wapumbavu ni kuwa tuna historia iliyo upande wetu. Mungu wetu alikuja duniani akiwa kama mwanadamu. Mungu wetu aliumba dunia na kuiangamiza dunia. Mungu wetu aliahidi kuwa atakuja tena, atatuchukua kwenda mbinguni, ataiangamiza dunia ya zamani, na kisha ataumba nchi mpya ambayo tutaishi pamoja naye milele! Ninaipenda ahadi hiyo zaidi kuliko utabiri wa ujio wa kipindi cha theluji/barafu na kuongezeka kwa joto duniani. Vipi kuhusu wewe – je, ungependa kuwa kwenye mbingu katika siku zako zijazo? Kwa nini usitubu hivi sasa na kukiri dhambi zako kwa Mungu, na kumwombaYesu akupatie vazi la haki ambalo yupo radhi kukupatia?
- Soma Ufunuo 21:1. Je, nini kinachotokea baada ya wenye haki kuchukuliwa kwenda mbinguni? (Yesu anaumba nchi mpya.)
- . Juma lijalo: Tutaanza mfululizo mpya kuhusu Uinjilisti.
