Somo la 10: Udanganyifu wa Mwisho wa Shetani

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Ufunuo 12 na 2 Wathesalonike 2
Swahili
Year: 
2023
Quarter: 
2
Lesson Number: 
10

Somo la 10: Udanganyifu wa Mwisho wa Shetani

(Ufunuo 12 na 2 Wathesalonike 2)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2023, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Jambo moja nililojifunza kwenye kesi nilizoshughulika nazo kwa takribani miaka hamsini ni kwamba matokeo tarajali ya baadhi ya kesi yanaibua mjadala. Nimewahi kuwa na kesi ambazo kwa dhahiri nilipaswa kushinda. Huwa sichukui kesi ambazo kwa dhahiri nitashindwa, lakini ninachukua kesi nyingi ambazo mustakabali wake uko kinyume na matarajio yangu. Hivi karibuni, nilikuwa na kesi mbele ya mahakama kuu na kila jaji alitoa hukumu iliyokuwa kinyume na matarajio yangu – ikiwemo kutoa hukumu ambayo haikuwa upande wangu kwenye suala ambalo kwa dhahiri nilipaswa kushinda. Unaweza kuzifikiria hisia za Mungu kuhusu uchaguzi wetu kati ya Shetani na yeye? Kwa dhahiri Mungu anapaswa kushinda. Hata hakuna mjadala wenye mantiki. Lakini wengi wanamchagua Shetani. Kwa nini? Sababu mojawapo ni kwamba wakati mwingine wanadamu wanadanganyika. Juma hili tunageukia kwenye udanganyifu mkuu wa mwisho wa Shetani. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tujifunze zaidi!

I.  Mdanganyifu Mtaalamu

A.  Soma Ufunuo 12:7-9. Sifa gani moja ya Shetani inabainishwa kwenye kifungu hiki? (Yeye ni “audanganyaye ulimwengu wote.”)

1.  Kwenye vifungu hivi, Shetani amemdanganya nani? (Malaika!)

2.  Ilikuwa vigumu kiasi gani kuwadanganya malaika? (Waliishi mbinguni. Hawakuwa na mvuto wa kutenda dhambi. Waliishi mbele za Mungu.)

a.  Una uwezekano gani wa kudanganywa na Shetani?

B.  Soma Mithali 14:12 na Yakobo 1:26. Kitabu cha Mithali kinaashiria kuwa tunaweza kudhani kwamba tunatenda jambo sahihi wakati kiuhalisia tunafanya makosa. Yakobo anauelezeaje ukweli huo? (Yakobo anafafanua kwamba tunachokisema kinaweza kudanganya mioyo yetu.)

1.  Tunapotafakari jinsi ya kuepuka udanganyifu, jambo gani linapaswa kuibua kengele ya tahadhari? (Tunajua kuwa Shetani na malaika wake anataka kutudanganya. Lakini hatari inaibuka karibu zaidi na nyumbani – tunatakiwa kuwa waangalifu na kile tunachokisema kwa sababu kinaweza kutubadilisha.)

2.  Unajizungumziaje?

II.  Kujiandaa Dhidi ya Udanganyifu

A.  Soma 2 Timotheo 3:12-15. Tunapaswa kufanya kazi gani sasa hivi ili kuepuka udanganyifu wa siku zijazo? (Ni kile unachokifanya sasa hivi – kujifunza Biblia.)

B.  Soma Tito 3:3-7. Msaada gani ni wa muhimu ili kuielewa Biblia kwa usahihi? (Roho Mtakatifu. Tunatakiwa kusafishwa katika kufanywa upya na kuongolewa na Roho Mtakatifu.)

C.  Soma 1 Wakorintho 3:18. Je, tunaweza “kujihadaa” na kujiingiza kwenye udanganyifu? (Ndiyo. Majivuno yetu kuhusu kuwa na busara mbele ya macho ya ulimwengu ni tatizo kubwa.)

D.  Soma 2 Wathesalonike 2:10-11. Badiliko gani la msingi la mtazamo wetu ni la muhimu? (Tukitaka kudanganywa, tukikataa kuupenda ukweli, basi kwa dhahiri tutadanganyika. Roho Mtakatifu anaweza kubadili mioyo yetu kama tukimwomba.)

III.  Udanganyifu Mkuu

A.  Soma 2 Wathesalonike 2:1-2. Ni nini mada ya onyo hili wa waamini? (Madai ya uongo kwamba Yesu amerudi.)

B.  Soma 2 Wathesalonike 2:3-4. Jambo gani litatokea kabla Yesu hajarejea? (“Yule mpingamizi” “akiketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.”)

C.  Soma 1 Wathesalonike 4:15-17. Hii inatuambia kuwa Yesu atakujaje mara ya pili? (Yesu atashuka kutoka mbinguni ili kutuchukua na kwenda naye mbinguni.)

1.  Fikiria namna ambayo Yesu atakuja tena, na onyo la kwamba “yule mpingamizi” wa Shetani atadai kuwa yeye ni Yesu kabla ya ujio wa Yesu Mara ya Pili. Hiyo inatuambia kuwa Shetani atafanya nini? (Ataweka ujio wa Yesu Mara ya Pili wa bandia. Kimsingi, atatakiwa kufanya hivyo kabla Yesu hajarudi tena. Tunaona kuwa ubandia huu ni mojawapo ya ishara kwamba Yesu anakuja.)

D.  Soma 2 Wathesalonike 2:9. Shetani atafanya nini pale atakapojifanya kuwa ndiye Yesu? (Atakuwa na “uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo.”)

1.  Utaona kuwa “yule mpingamizi” ni “mfano wa kutenda kwake Shetani.” Je, hiyo inamaanisha kuwa yule mpingamizi sio Shetani?

2.  Wayahudi wenye kuushikilia Uyahudi bado wanatarajia ujio wa Masihi. Waislamu wengi wanatarajia ujio wa Mahdi (atakayesindikizwa na Yesu). Wahindu wanaamini kuwa Vishnu atajitokeza kutoka mbinguni akiwa na upanga wa moto ili kuwaangamiza watenda maovu. Baadhi ya Wabudha wanamtarajia Budha wa mwisho, Maitreya, kujitokeza kutoka mbinguni ili kuleta baraka kuu za kiroho. Kweli hizi zinaashiria nini kuhusu asili ya “mpingamizi?” (Bila shaka Shetani atadai kupitia baadhi ya wanadamu kwamba matarajio ya dini zote kubwa duniani yamefikiwa katika ujio wa mara ya pili wa bandia!)

E.  Soma Marko 13:21-22. Hatari ya kudanganywa ni kubwa kiasi gani? 

1.  Je, hii inatuambia kwa namna nyingine kuwa wateule hawawezi kudanganyika?

IV.  Kuutambua Udanganyifu Mkuu wa Mwisho

A.  Soma tena 2 Wathesalonike 2:9. Rejea ya “ishara na ajabu za uongo” inaashiria kuwa Yesu wa bandia atakaa kwa muda gani pale atakaporejea? (Hii inaonekana kama kipindi fulani cha muda.)

B.  Soma 2 Wathesalonike 2:10-12. Unadhani hii itachukua muda gani?

C.  Soma 2 Wathesalonike 2:3-4. Itamchukua muda gani yule mpingamizi “kuketi katika hekalu la Mungu?”

D.  Soma 1 Wathesalonike 4:16-17. Hii inachukua muda gani? (Hii inatuambia kuwa Yesu atakapokuja waliokufa “watafufuliwa kwanza” na walio hai “watanyakuliwa pamoja nao [waliokuwa amekufa] ili kumlaki Bwana hewani.” Hiyo inamaanisha kuwa Yesu hatatumia muda wowote kukaa duniani. Tutainuliwa ili kuwa pamoja naye.)

1.  Ni nini ulio ulinzi imara dhidi ya udanganyifu? (Kama huinuliwi kutoka duniani, huyo sio Yesu.)

E.  Soma Mathayo 24:24-27. Hii inatuambia nini kuhusu ujio halisi wa Yesu Mara ya Pili dhidi ya ujio wa bandia? (Kama italazimika kwa mtu kukuambia juu ya ujio huo, basi hilo sio jambo halisi. Kila jicho litauona ujio wa Yesu Mara ya Pili kwa wakati mmoja.)

1.  Litafakari hili. Ukiuona ujio wa Mara ya Pili, na wafu wakianza kutoka makaburini, na unaanza kupaa mbinguni, je, unaweza kuwa na uhakika kuwa huu ni ujio halisi wa Mara ya Pili? (Ndiyo! Lizingatie hili.)

2.  Je, unadhani inawezekana kwa Shetani kufanya kitendo cha wafu kutoka makaburini kuwa cha bandia, wewe kupaa mbinguni, na kila mtu akiyaona haya kwa wakati mmoja?

F.  Rafiki, je, utachukua hatua sasa hivi kujiandaa dhidi ya udanganyifu? Umeianza njia ya kuuepuka. Kwa nini usimwombe Roho Mtakatifu, sasa hivi, abadili moyo wako na kufanya akili yako iwe zingativu ili uweze kusimama miongoni mwa wasiodanganyika?

V.  Juma lijalo: Mhuri wa Mungu na Alama ya Mnyama: Sehemu ya 1.