Kuelezea Maana na Uinjilisti na Ushuhudiaji

(Luka 24, Matendo 1, 5 & 10)
Swahili
Year: 
2012
Quarter: 
2
Lesson Number: 
1

Utangulizi: Kushiriki injili na watu wengine ni jambo ambalo Wakristo wote wanaweza kulifanya. Swali ni kuwa, “Je, ni kwa jinsi gani tunafanya hivyo kwa uzuri kabisa?” Kwa kawaida, huwa ninachukulia kuwa uinjilisti na ushuhudiaji ni kitu kimoja. Hata hivyo, nilipoliangalia jambo hilo kwa jicho la kisheria, vitu hivi viwili ni tofauti. Kwenye masuala mengi ya kisheria, kweli zinazohusiana na kesi zinajadiliwa kwanza. Kisha zinafuatia hoja za kisheria. Sehemu ya kwanza inawahusu mashahidi na kile wanachokisema kuwa kilitokea. Sehemu ya pili inahusu ushawishi. Ninapoandika kweli zinazohusiana na kesi kwa ufupi, lengo langu ni kushawishi. Hata hivyo, hakuna mwanasheria mzuri atakayechanganywa akili kuhusu tofauti kati ya kuelezea ukweli na kufanya hoja ya kisheria. Je, hiyo ni kweli kwa Wakristo wanaotaka kushiriki injili na watu wengine? Je, tunapaswa kuwa na uhakika kwamba tunaelewa tofauti kati ya kweli na ushawishi? Je, tuna jukumu la ushawishi kwa kiasi gani? Hebu tuzame kwenye Biblia zetu tuone kile tunachoweza kujifunza!

  1. Ushuhudiaji Dhidi ya Uinjilisti
    1. Soma Luka 24:45-48. Haya ni baadhi ya maneno ya mwisho ya Yesu yaliyoandikwa na kuwekwa kwenye kumbukumbu na wanafunzi wake kabla hajarejea mbinguni. Yesu anawaambia kuwa watakuwa “mashahidi.” Hata hivyo, alianza (fungu la 45) kwa kuwafundisha Biblia. Je, wanafunzi wanaambiwa kushuhudia au kushawishi? (Jukumu lao la kipekee kabisa ni kushuhudia. Yesu aliwafundisha kuwa Biblia ilitabiri baadhi ya matukio kwenye maisha yake. Wanafunzi ni mashuhuda wa kweli kwamba hili lilitokea kama jinsi Biblia ilivyotabiri.)
    2. Soma 2 Wakorintho 5:20-21. Je, huu ni ushuhuda au ushawishi? (Kwa wazi kabisa huu ni ushawishi.)
    3. Soma Matendo 1:8. Haya ni maneno mengine ya mwisho ya Yesu kabla hajarejea mbinguni. Je, ni kwa nini tuwe na hitaji la Roho Mtakatifu ili tuweze kushuhudia?
    4. Soma Matendo 5:30-32. Je, tunaona kitu gani hapa? Ushuhuda au ushawishi? (Petro anaanza kwa kusema kuhusu kweli, kisha anajiingiza kwenye hoja ya kisheria “toba na msamaha wa dhambi”).
      1. Hebu angalia ili ubaini jinsi Roho Mtakatifu anavyotumika. Sijasoma mahali palipoandikwa kuwa Roho Mtakatifu anaelezea kweli za aina yoyote ile. Je, ni kwa jinsi gani Roho Mtakatifu ni “shuhuda?”
    5. Hebu tuangalie kwa haraka haraka kile kilichotangulia jambo hili. Soma Matendo 5:12-18. Hii ndio sababu iliyowafanya Petro na wanafunzi wakamatwe na kuwekwa gerezani. Je, ni kwa jinsi gani Roho Mtakatifu ni shuhuda? (Roho Mtakatifu anathibitisha ushuhuda wa kweli na hoja ya kisheria ya wanafunzi kwa kutenda miujiza kupitia kwao.)
    6. Hebu tuone jinsi ambavyo wanafunzi wanayaweka haya mambo yote pamoja. Soma Matendo 10:39-41. Nini kinaendelea hapa? (Ushuhuda. Wanafunzi wanaghani (wanakariri) kweli wanazozijua.)
    7. Soma Matendo 10:42-43. Nini kinaendelea Hapa? (Huu ni upande wa pili wa hoja ya kisheria)
    8. Soma Matendo 10:44-46. Nini kinaendelea hapa? (Huu ni uthibitisho wa Roho Mtakatifu wa ukweli wa kweli na usahihi wa hoja ya kisheria.)
  2. Ushuhuda wa leo?
    1. Maneno ya kusikia/kuambiwa ni kauli za kweli ambazo hazijashuhudiwa na mtu anayeshuhudia mahakamani. Je, kuna ubaya gani kwenye mambo ya kuambiwa/kusikia? (Huwezi kuyathibitisha ili kuwa na uhakika kuwa ni ya kweli. Nikishuhudia kwamba nimemwona mtu akimpiga mtu mwingine, ninaweza kuulizwa na kuchunguzwa kuhusu uwezo wangu wa kuona tukio na kuulizwa kuhusu upendeleo/ubaguzi wangu. Nikishuhudia kwamba kaka yangu aliniambia kuwa alimwona mtu akimpiga mtu mwingine, ushuhuda wangu hauwezi kuthibitishwa ili kuona kama ni sahihi.)
    2. Je, Wakristo hivi leo wanag’ang’ania injili ya kuambiwa? (Kwa hakika kwetu sisi hii ni habari ya kuambiwa kwamba Yesu aliishi, akafa na kufufuliwa kutoka katika wafu. Wanafunzi walikuwa mashuhuda wa hilo, lakini sisi sio mashuhuda.)
      1. Kwa hiyo, je, kazi ya ushuhuda ni kazi iliyopo kwa ajili yetu? (Hapana. Tunaweza kuelezea kile alichotutendea Yesu.)
    3. Utakumbuka nilisema kwamba kila maelezo yanahitaji kauli zakweli kabla ya hukumu ya kisheria. Pia nilisema kuwa wanasheria wababaishaji wanachangaya haya mambo mawili. Je, kazi zetu zote za injili zinapaswa kuanza kwa ushuhuda kabla hatujajiingiza kwenye ushawishi? Au, je, muda/wakati umeondoa umuhimu/msingi wa kweli kwa sababu kweli zetu sio za kupendeza sana kama habari za kufufuliwa kwa Yesu kutoka katika wafu?
    4. Siku moja nilitembelea kanisa moja, na mtu mmoja mwenye mwili mkubwa sana akasimama kutoa sifa kuhusu ushuhuda wake kwa alichokitenda katika lile juma. Kisa chake kilikuwa hiki: alikuwa akifanya huduma gerezani, na akamwona afisa magereza anayesimamia nidhamu alikuwa akila pande la sandwichi (vipande vya mkate vyenye nyama, jibini, nk katikati). Alimwambia yule afisa kuwa kula pande hilo la sandwichi kutamsababisha aende motoni. Mtu yule ambaye uzito wake ulikuwa umezidi kwa kilo 23-34 alikuwa akimshukuru Mungu kwa kumpa fursa ya kumshuhudia yule afisa.
      1. Hebu tuliangalie hili kwa vipengele tulivyojifunza. Je, yule mshiriki wa kanisa alishuhudia kweli zozote? (Alikuwa na ujumbe wa afya, lakini “kweli” zake zisizokuwa za vitendo (uzito wa mwili wake) zilikuwa na ujumbe wenye mkanganyiko kikweli kweli.)
      2. Je, ujumbe wa kisheria (ushawishi) ulikuwa upi? (Kwamba amri ya Mambo ya Walawi 11 inayokataza kula nyama isiyo safi ilikuwa ni ujumbe wa wokovu. Bila kujali kama huyu mtu alikuwa sahihi au la kwenye teolojia yake, hii haionekani kijihusisha kivyovyote vile na ujumbe wa injili wa maisha, kifo na ufufuo wa Yesu.)
      3. Je, ushuhuda wa Roho Mtakatifu ulikuwa upi? (“Lile pandikizi la mtu” halikuripoti kitu chochote.)
    5. Soma Mathayo 15:16-18. Hii inapendekeza kuwa yule mtu alihitajika kufanya kazi zaidi kwenye upande wa kisheria (ushuhuda) wa uinjilisti wake. Muhimu zaidi, je, inatufundisha nini kuhusu ushuhudiaji? (Kitu cha msingi ni kile tunachokisema.)
    6. Soma Mathayo 12:36. Je, hii inapendekeza nini kuhusu ushuhuda? (Kwamba kila neno tulisemalo ni la msingi.)
      1. Je, hivyo ndivyo unavyouangalia uinjilisti - mchakato wa kila wakati na kila neno?
      2. Angalia tena lile pandikizi la mtu. Je, unadhani kuwa tumaini lake lilikuwa lipi? (Kwamba afisa magereza msimamizi wa nidhamu angetubu kuhusiana na ulaji wake, na kisha angebadili dini na kuwa mshiriki wa kanisa lake. Haikuwa hivyo. Lakini, yule mtu alidhani kuwa alipaswa kuelezea tukio lile kwenye kipindi cha “kusifu” ili mtu fulani amchukulie kuwa alistahili kusifiwa kwa angalao kujaribu. Bila shaka hili ndilo lilikuwa tukio pekee la ushuhuda aliloweza kulikumbuka huyu mtu katika juma lile.)
    7. Soma Marko 4:13-16. Je, Yesu analinganisha suala la kushirikiana injili na kitu gani? (Kama maneno yaliyotupwa kando ya barabara ya uzima.)
    8. Kuna kitabu maarufu nilichokisoma kiitwacho kuwa “Nudge.” Kinahusu serikali, uchumi na kufanya uamuzi. Wakati huo huo, kuna kitabu kisicho maarufu cha kidini ninachokisoma ambacho pia kinaitwa kuwa “Nudge.” Kitabu cha kidini kinahusu uinjilisti. Vitabu hivi viwili vina kitu kimoja kinachofanana: kujaribu vitu vidogo vidogo vyenye ushawishi kunaweza kuleta matokeo maubwa. Je, unalinganishaje wazo la “nudge” na mafungu matatu ya Biblia tuliyoyasoma hivi punde: a) kila neno linahesabiwa hukumuni;” b) “kile kinachotoka kinywani ni cha msingi zaidi, sio kinachoingia kinywani;” na, c) “uinjilisti ni upandaji wa maneno?” (Kauli zote za Yesu zinatuambia kuwa kila neno letu lina athari ya “nudge.” Aidha tutawaleta (nudge?) watu kwenye injili au tutawapeleka mbali na ijili.)
    9. Je, utayaangaliaje mabadiliko ya uinjilisti na ushuhudiaji kama utavichukulia kama suala la kila wakati, badala ya “fursa moja kubwa inayopatikana baada ya miezi kadhaa ya kuingia nyumbani kwa mtu na kumbadilisha mtu kumkiri Yesu” ya yule mtu?
  3. . Roho Mtakatifu Kama Shahidi
    1. Soma Marko 16:19-20. Tunawaona wanafunzi wakishiriki neno na watu wengine. Je, jukumu la Roho Mtakatifu katika hili ni lipi? (Kuthibitisha usahihi wa neno ambalo linashirikishwa kwa watu wengine. Anathibitisha ushuhuda wa mtu.)
    2. Soma Yohana 16:7-11. Je, ni jukumu gani la Roho Mtakatifu tunaloliona hapa? (Kwamba Roho Mtakatifu anauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, hatia, haki na hukumu.)
    3. Soma Matendo 8:29-31. Je, ni jukumu gani la Roho Mtakatifu tunaloliona hapa? (Roho anamwongoza Filipo kwa mtu ambaye anataka kuielewa injili.)
    4. Je, mafungu haya matatu yanatufundish nini kuhusu jukumu la Roho Mtakatifu katika ushuhudiaji wetu? (Kwamba atatuongoza kwa watu sahihi, atawagusa mioyo, na atathibitisha ushuhuda wetu.)
      1. Je, umewahi kuwa na uzoefu wa hili maishani mwako? (Ubashiri wangu ni kwamba unavyo visa vinavyoonyesha Roho Mtakatifu kukukutanisha pamoja na mhitaji (mtafutaji wa ukweli) na akamgusa moyo.)
      2. Je, ni wangapi kati yenu mmewahi kuwa na uzoefu wa Roho Mtakatifu kuthibitisha ushuhuda wako kwa ishara?
        1. Kama ambavyo unaweza kuwa umebashiri, ninadhani kuwa ushuhuda wa “yule mtu” haukuwa wa msaada. Badala yake nina uhakika kuwa watu wengi wana shuhuda zisizokuwa na maana, na mara nyingine huwa ninafikiria na kujiuliza sana kuhusu ushuhuda wangu mwenyewe. Je, huna uhakika kuhusu njia bora zaidi ya kushuhudia?
        2. Tukiona kuwa ushuhuda wetu hauna uthibitisho wa Roho Mtakatifu ama kupitia kwenye ishara au uguswaji wa moyo, je, tunapaswa kulichukulia hili kama ishara kuwa hatufanyi ipasavyo?
    5. Rafiki, ndio kwanza tu tumeanza somo letu kuhusu ushuhudiaji. Je, utafanya mambo awili? Mwombe Roho Mtakatifu akupe mwangaza kwenye ushuhudiaji, na ujifunze pamoja nasi tunapoendelea kuchimbua neno la Mungu kwenye hili somo!
  4. Juma lijalo: Huduma ya Kila Mshiriki.