Somo la 11: Kujizoeza Uaminifu Mkuu kwa Kristo

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Waefeso 6:1-9
Swahili
Year: 
2023
Quarter: 
3
Lesson Number: 
11

Somo la 11: Kujizoeza Uaminifu Mkuu kwa Kristo

(Waefeso 6:1-9)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2023, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Hebu tuendelee na safari yetu juu ya umoja na amani. Tumeona kile ambacho Biblia inakisema kuvihusu kanisani na katika ndoa. Vipi kuhusu umoja na amani baina yetu na watoto wetu? Vipi kuhusu kuangalia uhusiano wetu katika maeneo ya kazi – ama kama mwajiriwa au mwajiri? Paulo anajikita kwenye uhusiano wa aina hii katika Waefeso 6:1-9 hivyo fuatana nami ili tuone anachokisema Paulo!

I.  Watoto na Wazazi

A.  Soma Waefeso 6:1-3. Paulo anapowaambia watoto kuwatii wazazi wao “katika Bwana,” je, huu ni ukomo wa utii? (Huu ni ukomo ule ule tunaouona katika Waefeso 5:21-22 ambapo Paulo anasema kuwa washiriki wa kanisa wanapaswa kunyenyekeana “katika kicho cha Kristo” na wake (wives) wanapaswa “kutii” “kama kumtii Bwana.” Uhusiano wote huu wa kilimwengu unazingatia wajibu wetu mkuu wa kumtii Mungu.)

1.  Paulo anasema utii kwa wazazi “ndiyo haki.” Hiyo inamaanisha nini? Ni kwa namna gani utii huo uko sahihi? (Katika Waefeso 6:2-3 Paulo anatuambia hii ni sehemu ya Amri Kumi.)

B.  Linganisha Waefeso 6:2-3 na amri inayopatikana katika kitabu cha Kutoka 20:12 na Kumbukumbu la Torati 5:16. Paulo anasema kuwa hii ni “amri ya kwanza yenye ahadi.” Ni ahadi gani hiyo? (Maisha yako yatakuwa marefu na mazuri.)

1.  Unapaswa kuwaambia watoto wako! Unaweza kuwaelezeaje suala hili? (Amri zote za Mungu ni kwa ajili ya manufaa yetu. Wazazi tayari wameshaishi maisha ambayo watoto wanayaingia. Wazazi wachamungu wamejifunza jambo kutokana na hili. Jambo ambalo litawaepusha watoto kufanya makossa yasiyo na maana.)

2.  Televisheni inawaonesha wazazi kuwa ni watu wa namna gani, hususan akina baba (fathers)? (Inawaonesha kama watu wapumbavu.)

3.  Je, umeyasikia mashambulizi kwa “mababu?” Ni kwa jinsi gani falsafa hiyo na mashambulizi ya televisheni kwa akina baba yanaendana na Waefeso 6:2-3? (Ni muhimu kwa Wakristo kutafakari na kuangalia jinsi misemo na hoja na mijadala ya kisasa inavyoendana na pambano kuu kati ya wema na uovu. Mungu ni Baba yetu. Kama tulivyojadiliana juma lililopita, Waefeso 5 inatoa wajibu wa msingi kwa akina baba. Mashambulizi haya ni ya kishetani sio kwa kuwa yanakinzana na Biblia, bali kwa sababu ikiwa yatakubalika yanawanyima watoto ahadi ya amri.)

C.  Soma Waefeso 6:4. Kwa nini akina baba pekee ndio wanaoonywa dhidi ya kuwachokoza watoto wao? (Mtoa maoni mmoja alibainisha kuwa neno lile lile lililotumika hapa pia lilitumika kwa wazazi wa Musa katika Waebrania 11:23. Kwa kuwa mpangilio wa familia tuliojifunza juma lililopita unamweka baba juu (chini ya Mungu) inaleta mantiki kwamba yeye ndiye ana uwezekano mkubwa wa kuwa na hasira.)

1.  Kama wewe ni mzazi, je, watoto wako huwa wanakasirika hata kwenye miongozo yenye mantiki? 

2.  Unadhani Paulo anamaanisha nini anapoonya dhidi ya kutowachokoza watoto? (Sote tunawafahamu watu wasiojua namna ya kusimamia (handle) mamlaka. Wakati mwingine adhabu zisizo na maana zinatokana na matumizi yasiyo ya lazima ya mamlaka.) 

3.  Utaona kuwa kitabu cha Waefeso kina hoja mbadala kwenye suala la uchokozi: “adabu na maonyo ya Bwana.” Kuna tofauti gani katika maonyo ya Bwana? (Waebrania 12:6 inarejelea kuadhibu kwa upendo. Mungu anataka nidhamu endelevu na ya upendo ya watoto wetu.)

D.  Unapoitafakari Waefeso 6:3-4, je, unaona “ulinzi” wa jinsi wazazi wanavyopaswa kuwarudi watoto wao? (Wazazi wazipowarudi watoto wao, au watoto wasipoyasikiliza makaripio, basi kuna uwezekano mkubwa serikali itawaadhibu watakapokuwa watu wazima. Hii haiendani na “kupata heri” na “kuishi kwingi.” Wakati huo huo wazazi wanaotoa adhabu kali kupitiliza wanaweza kusababisha (kuamsha) uasi katika kipindi chote cha maisha dhidi ya kanisa na Mungu.)

II.  Waajiri na Waajiriwa

A.  Soma Waefeso 6:5. Tafsiri ya Biblia ya ESV inatafsiri kifungu hiki kama “Bondservants” na tafsiri ya KJV inakitafsiri kama “servants” (watumwa). Neno hili linaweza kuwarejelea watumwa wa hiari au watumwa wa lazima. Kwa kuwa ninyi wasomaji ama ni waajiriwa au waajiri, na sio watumwa au wamiliki wa watumwa, tutaliangalia suala hili kwa muktadha wa uhiari. Je, waajiriwa wanafanana na watoto, kwamba wanapaswa kumtii mwajiri wao “kwa hofu na kutetemeka?”

1.  Je, hii inatoa ufafanuni wa sababu ya Paulo kujiajiri kwa kutengeneza mahema?

2.  Utaona kuwa Paulo analinganisha utii wa waajiriwa na utii wa Kristo. Je, kuna mtu anadhani kuwa Yesu anatutaka tumtii “kwa hofu na kutetemeka?” (Maoni ya John MacArthur yanasema kuwa “hii sio hofu/tisho, bali heshima kwa mamlaka yao.”)

3.  Unadhani kwa nini Paulo anamuweka Yesu kwenye taswira ya kuwa mwajiriwa mtiifu na mwenye juhudu? (Hii inaashiria kwamba kuwa mwajiriwa mzuri ni sehemu ya wajibu wetu kwa Mungu na ushuhuda wetu kwa ulimwengu.)

a.  Hii inaashiria nini juu ya kuwa mwanachama wa chama cha wafanyakazi?

b.  Je, vyama vya wafanyakazi vinachochea kutokuwa na furaha na uasi? Vinatoa mtazamo wa namna gani kwa waajiri?

B.  Soma Waefeso 6:6-7. Huu sio utii mrahisi, hii inahitaji mtazamo. Waajiriwa wanapaswa kuwa na mtazamo gani kwa waajiri wao? (Mtazamo ni kwamba tunamfanyia Mungu kazi, sio kwa mwajiri fulani hali inayoweza kusababisha tabia isiyo ya kiuchamungu.)

1.  Swali la msingi ni endapo Paulo anatufundisha kuwa utii, upendo, juhudi, na uchamungu ndilo lengo katika uhusiano wetu wa aina zote na watu wengine, ikiwemo mwajiri wetu?

C.  Soma Waefeso 6:8. Biblia inatoa ahadi gani halisi kwa waajiriwa wema? (Mungu atatupatia thawabu. Mungu “atakurejeshea” chochote ulichokitoa kwa mwajiri wako.)

1.  Najua unafahamu ninaamini kuwa amri za Mungu kwa sehemu kubwa zinajihimiza zenyewe katika utekelezaji wake. Kama ungekuwa mwajiri, ungemtendeaje mwajiriwa mwenye mtazamo na juhudi ambazo Paulo anazishauri? (Mwajiriwa kama huyo ni wa thamani sana.)

D.  Soma Waefeso 6:9. Waajiri wanatakiwa kufanya nini? (Wanapaswa kuwa na mtazamo chanya kwa wafanyakazi wao.)

1.  Kwa nini? (Kwa sababu Mungu atawawajibisha.)

2.  Je, ungependa kumfanyia kazi mwajiri anayewatendea wafanyakazi wake kama asemavyo Paulo waajiriwa wanavyopaswa kuwatendea waajiri wao? (Kwa dhahiri jibu ni, “Ndiyo.” Tafakari, waajiri, jinsi itakavyoisaidia biashara yako kama wewe na wafanyakazi wako mtafanya kazi kwa kuheshimiana na upendo?)

3.  Kama una mwajiri mbaya, je, unatakiwa kuendelea kumfanyia kazi? (Hizo ni baraka za huduma ya hiari. Kama una mwajiri mbaya, badili kazi. Fanya kazi kwa mwajiri anayerahisisha kufuata ushauri wa Paulo kwa waajiriwa.)

E.  Unadhani kwa nini Paulo anatoa ushauri wa jinsi watumwa wanavyopaswa kuwajibu mabwana wao wakati analiandikia kanisa mahsusi lisilo la kimagharibi? (Utumwa ulikuwa dhambi ya ulimwengu wote. Wapinzani wa Ukristo katika zama za leo wanajaribu kuliweka kama doa kuu kwenye usasa wa Kimagharibi na Ukristo. Ukweli ni kwamba usasa wa Kikristo wa Kimagharibi ulijitahidi, kwa gharama kubwa kwao wenyewe, kuuondosha utumwa.)

III.  Kiini cha Jambo

A.  Ni kanuni ipi ya jumla ambayo Paulo anaisisitiza kwenye uhusiano wa aina zote uliojadiliwa katika waefeso 6:1-9? (Anafundisha juu ya heshima, upendo, na uchamungu kwenye uhusiano wa pande mbili katika aina zote za uhusiano. Matendo yetu yanapotendeka kwa kumnyenyekea na kumtii Kristo, yanatoa mwelekeo wa namna tunavyotendeana sisi kwa sisi.)

B.  Mafundisho haya yanaakisije ujumbe wa Yesu wa upendo na unyenyekevu? (Yesu alikuja sio kwa ajili ya kutumikiwa bali kuwatumikia wengine. Mafundisho haya yanahamasisha mtazamo huo huo wa kuwahudumia wengine kwa unyenyekevu.)

1.  Utawafafanuliaje watoto wako kwamba utiifu wao kwako unaakisi upendo wako kwao?

C.  Je, inaleta mantiki na ni matakwa ya Kibiblia kwa sisi “kuelewa wajibu wetu” katika jamii? Au hii inakinzana na mtazamo wa kwamba sisi ni sehemu ya “ukuhani wa kifalme” (angalia 1 Petro 2:9) ya waumini? (Sehemu ya tatizo katika kupatikana kwa amani kwenye uhusiano wa aina mbalimbali ni kuwa na unyenyekevu wa kuelewa wajibu wetu. Kuishi kwa kuzingatia kanuni hizi sio tu kwamba kunaimarisha uhusiano wetu binafsi bali pia kunatumika kama ushuhuda kwenye nguvu ya Injili ibadilishayo maishani mwetu.)

D.  Rafiki, je, utauchukulia kwa umakini uhusiano anaoubainisha Paulo katika kitabu cha Waefeso? Je, utachukua hatua ili kuifanya nyumba yako na kazi yako kuwa mahali pazuri pa kufurahia?

IV.  Juma lijalo: Wito wa Kusimama.