Somo la 6: Siri ya Injili

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
Waefeso 3
Swahili
Year: 
2023
Quarter: 
3
Lesson Number: 
6

Somo la 6: Siri ya Injili

(Waefeso 3)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2023, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Fikiria kuwa umepokea barua kutoka kwa mwanasheria ikikutaarifu kuwa una ndugu, ambaye hapo kabla hukuwa ukimfahamu, ambaye amefariki na kukuachia mali. Unaweza kusema kuwa siri imefunuliwa, unao uhusiano ambao hapo awali hukuwa ukiufahamu. Paulo anawaambia Mataifa katika Efeso jambo linalofanana na hilo. Anawaambia kuwa sasa wao ni sehemu ya familia ambayo matokeo yake ni manufaa makubwa kwao. Fikiria mbali zaidi kwamba wanafamilia wa familia mpya hawakukaribishi vizuri sana. Huo ni mfanano mwingine wa kile kinachoendelea katika Efeso. Hebu tuzame kwenye somo letu na Biblia na tujifunze zaidi!

I.  Mfungwa

A.  Soma Waefeso 3:1. Paulo anaanza kwa kusema “Kwa sababu hiyo.” Anazungumzia sababu gani? (Anarejelea Waefeso 2, ambayo tulijifunza juma lililopita. Katika somo la juma lililopita tulijifunza kuhusu kuhesabiwa haki kwa imani pekee. Kwa jinsi ilivyo habari njema, Waefeso 2 pia inafafanua kuwa Mataifa ni sehemu ya wale wanaojumuishwa kwenye hizi habari njema!)

1.  Unaweza kutafakari kwa nini Paulo yuko gerezani kwa kupeleka habari njema kwa Mataifa?

2.  Paulo anaonekana kuwa na kifungo cha ajabu. Anasema kuwa yeye ni “mfungwa wake Kristo Yesu.” Anawezaje kuwa mfungwa wa Yesu?

a.  Tunafahamu kuwa Paulo alikuwa anazuiliwa na Warumi. Unaweza kulinganishaje ukweli huu na kile anachokiandika Paulo? (Tunatakiwa kuendelea kusoma.)

B.  Soma Matendo 21:27-29. Hii inatatuaje mkanganyiko? (Paulo ni mfungwa wa Yesu kwa sababu alikamatwa kuhusiana na kufanya kazi ya Yesu – kupeleka habari njema kwa Mataifa.)

1.  Hii inahusianaje na kanisa katika Efeso? (Je, umegundua kuwa madai ni kwamba Paulo alimleta mtu wa Mataifa kutoka Efeso na kumwingiza hekaluni?)

C.  Soma Waefeso 3:2. Paulo anachukulia kwamba msomaji ana ufahamu kuhusu uwakili (kazi) ambao Mungu amempatia kwa kuzingatia suala la Waefeso. Ni kazi gani hiyo? (Kinachochukuliwa hapa ni kwamba msomaji anafahamu kuwa Paulo ana kazi maalumu aliyopewa na Mungu, ya kupeleka injili kwa Mataifa. Sasa mkanganyiko unakuwa wazi – Paulo anaandika kuwa amezuiliwa kwa sababu amekuwa akitenda kile hasa ambacho Mungu amemwitia: kuhubiri injili kwa Mataifa. Katika muktadha huu ni kwa wale waliopo Efeso.)

1.  Kwa nini Paulo anajiingiza kwenye masuala haya? Je, Paulo anafanana na watu unaowafahamu ambao hawawezi kwenda kwenye mada inahohusika moja kwa moja? Itakubidi wakuelezee kwa njia ya kisa?

2.  Kwa nini kisa cha Paulo ni cha muhimu? (Jiweke kwenye nafasi ya Mataifa ndani ya Efeso. Paulo, ambaye ni mfungwa, anajenga hoja kuwa mtu aliyesulubiwa kama mvunja sheria ni Masihi hasa! Inaonekana kama kampeni ya “mhalifu.”)

II.  Kisingizio

A.  Soma tena Waefeso 3:2 na uongezee Waefeso 3:3. Paulo anaandika kuwa amepewa kazi maalumu kwa Mataifa ili kulifafanua fumbo. Kwa nini anarejelea ujumbe wake kama “siri?” (Watu wanapenda mafumbo/miujiza. Watu wanapenda kujifunza siri. Fumbo hili linaanza kwa kisa cha mfungwa kufafanua kwa nini mhalifu aliyefungwa alimchagua kwa ajili ya kazi hii. Je, hilo lingevuta usikivu wako kama ungekuwa unaishi Efeso?

1.  Wana maoni wanasema kuwa kuanzia hapa hadi kwenye kifungu cha 14 Paulo anatumia muda wake kufafanua mgogoro huu wa kusikitisha dhidi ya sheria sio tu kwamba uko sawa, bali ni wa muhimu sana. Hili sio kundi la wafungwa wanaojaribu kukushawishi, kufumbua siri hii ni suala la uzima na kifo!

B.  Hebu turukie mbele na tusome Waefeso 3:6. Sasa Paulo anafunua siri. Ni siri gani hiyo? (Sio injili. Bali ni kwamba sasa Mataifa ni “warithi pamoja nasi” Wayahudi kwenye “ahadi katika Kristo kwa njia ya injili.” Sasa Mataifa ni sehemu ya familia ya Mungu.)

C.  Kwa kuwa sasa tumesoma sehemu ya nyuma ya kitabu ili kujua jinsi mamabo yalivyo, hebu tusome Waefeso 3:4-5. Siri hii ilifunuliwa lini? (Paulo anasema kuwa ni katika kizazi cha sasa, na sio vizazi vilivyopita.)

1.  Je, Paulo pekee ndiye anayefafanua fumbo hili? (Anayaita maandiko yake “ufahamu wangu” katika “siri yake Kristo.”)

2.  Kizazi hiki cha sasa kiligunduaje siri hii? (Kwa njia ya Roho Mtakatifu.)

3.  Washiriki wa sasa wa familia wanakuwa na mwitiko gani kwenye ingizo jipya katika familia? (Hapo kabla tulisoma jambo gani katika Matendo 21:27-29? Angalao baadhi ya familia hazikubaliani na jambo hili.)

D.  Soma Waefeso 3:7. Unadhani Paulo anamaanisha nini anaposema kuwa “alifanywa kuwa mhudumu?” (Badala ya cheo, hii inaonekana kuielezea kazi yake, utume wake. Mwanamaoni mmoja anasema kuwa neno la Kiebrania lililotumika hapa kwa ajili ya mhudumu ni sawa na mhudumu katika mgahawa. Utume wa Paulo ni karama ya neema.)

E.  Soma Waefeso 3:8. Je, hii haionekani kutokuwa na mantiki? Paulo alikuwa mtu mwenye elimu, aliyefundishwa na Gamalieli, mmojawapo wa walimu wa awali wa Kiebrania. Angalia Matendo 2:3. Hakuwa mvuvi asiye na elimu. Unaielezeaje kauli ya Paulo? (Kwanza, Paulo hakutumia muda wa miaka mitatu kufundishwa na Yesu. Pili, Matendo 22:4 inafunua kuwa hapo kabla alikuwa mtesaji wa Wakristo. Tatu, inawezekana kamwe Paulo asingeingia kwenye msitari sahihi isingekuwa kwa Yesu kuingilia kati pale Dameski. Angalia Matendo 22:6-8.)

F.  Soma Waefeso 3:9. Mpango wa kuwaleta Mataifa katika familia ya Mungu umekuwepo kwa muda gani? (Mara zote ulikuwepo moyoni mwa Mungu.)

1.  Angalia kile kinachoweza kuchukuliwa kama rejea “ya kubahatisha” kwa Mungu Muumbaji wetu. Je, ni ya nasibu? (Uibukaji unahusisha bahati na mpangilio wa asili. Mungu Muumbaji anawakilisha mpangilio na mpango. Kama ambavyo Yesu aliumba na kupagilia uumbaji, vivyo hivyo aliupanga wokovu wetu.)

G.  Soma Waefeso 3:10. “Falme na mamlaka katika ulimwengu wa kiroho” ni akina nani? (Soma Waefeso 6:12. Paulo anatumia lugha hiyo hiyo kuwarejelea malaika wapotovu.)

1.  Je, inaleta mantiki yoyote kwako kwamba kanisa linashirikishana “hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi” na pepo wachafu? (Habari hizi ziliwafadhaisha Shetani na malaika wake wapotovu. Sasa wanapambana ili kupata mioyo na akili za kila mtu, sio Waebrania tu.)

H.  Soma Waefeso 3:11-13. Vifungu hivi vinaishia na ombi kwamba Waefeso “wasikate tamaa” kwa Paulo kuwa mtumwa. Unaweza kuelezeaje kwa ufupi “kisingizio” cha Paulo cha kuwa gerezani? (Paulo anazuiliwa sio kwa sababu ni mtu mbaya, bali kwa sababu anapeleka injili kwa Mataifa. Kuchunguza ujumbe wa kwamba Mataifa ni sehemu ya familia ya Mungu ni muhimu sana kwa Shetani.)

III.  Ombi

A.  Baada ya uthibitisho mrefu huo kwa hali hii, Paulo anawaombea Waefeso. Soma Waefeso 3:14-15. Tunaitwaje kwa jina la Baba yetu wa mbinguni? (Huo ndio ujumbe – Mungu ni Baba yetu. Yesu ametufanya (Wayahudi na Mataifa) kuwa sehemu ya familia ya Mungu.)

B.  Soma Waefeso 3:16. Hivi karibuni, sehemu kubwa ya maisha yangu imegeukia kwenye betri. Zana na vifaa vingi vinatumia betri na haviendeshwi kwa kutumia nishati ya gesi. Nguvu yetu ni nani? (Roho Mtakatifu. Ninasisitiza zaidi umuhimu wa kujawa na Roho Mtakatifu. Bila yeye wewe ni sawa na kifaa kilico na betri zilizokwisha nguvu.)

C.  Soma Waefeso 3:17-19. Tunazungumzia taswira yenye mionekano mitatu (three dimensional), Paulo anapendekeza pande nne za upendo wa Mungu. Upendo huu wenye pande nne upo kwa ajili ya nani? (Kwa ajili yetu, kwa njia ya Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu.)

1.  Mara zote huwa ninatumia mantiki pamoja na uzoefu wako ili kusaidia kuichambua na kuielewa Biblia. Paulo anaelezea jambo gani la muhimu kuhusu maarifa na upendo? (Upendo wa Mungu ni zaidi ya mantiki na akili. Maarifa hayawezi kuuelezea.)

D.  Soma Waefeso 3:20-21. Huu “upendo upitao ufahamu” unatenda nini kwa ajili ya utume wetu? (Hutoa zaidi ya tuyaombayo au tuyawazayo.)

1.  Je, “kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu” humaanisha nini?

E.  Pitia upya ombi la Paulo tulilolijadili hivi punde: Waefeso 3:14-21. Kuna tofauti gani kati ya ombi la Paulo na ombi lako la kawaida? (Maombi yangu hunizingatia mimi. Ombi la Paulo linajikita na kuwazingatia watu wengine. Kwa kuwa yumkini maombi yako yanafanana na maombi yangu, jifariji katika Sala ya Bwana (Mathayo 6:9-13) ambayo inamhusu zaidi mtu anayeomba.)

F.  Angalia tena Waefeso 3:21. Ni nini lengo la kazi yako? (Kumtukuza Mungu.)

G.  Rafiki, karibu katika familia ya Mungu! Kwa kuutafakari uzoefu na urithi, je, utafanya uamuzi wa kujiunga na familia hii sasa hivi?

IV.  Juma lijalo: Mwili wa Kristo Uliounganishwa.