Somo la 7: Kuhamasishwa na Tumaini

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
1 Wathesalonike 4, Luka 12
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
2
Lesson Number: 
7

Somo la 7: Kuhamasishwa na Tumaini

(1 Wathesalonike 4, Luka 12)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Wikiendi iliyopita tulikuwa na mahafali katika Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Regent. Mojawapo ya mambo ninayoyapenda kuhusu kufanya kazi na vijana ni matumaini waliyo nayo kuhusu kesho (future) yao. Mustakabali wa siku zijazo (future) pia husababisha mashaka. Vipi kama mambo yataenda vibaya? Wanakabiliana na changamoto ya kufaulu mtihani wa Shule ya Sheria na kupata kazi inayoendana na malengo yao. Kama Wakristo, tumaini letu la mwisho lipo kwenye ujio wa Yesu Mara ya Pili. Unalizungumziaje kundi la Wakristo waliokuwa wanafunzi makini wa Biblia, na ambao waliutafsiri unabii kuashiria kwamba Yesu anakuja tena katika kipindi fulani? Walikuwa na tumaini, lakini Yesu hakuja. Tumaini lililowekwa mahali pasipostahili (misplaced) linaendanaje na pambano kati ya wema na uovu? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tuone Mungu ana mafundisho gani kwa ajili yetu!

I.  Ahadi ya Marejeo

A.  Soma 1 Wathesalonike 4:13. Kuna “tumaini” gani kwa wasomaji wa kifungu hiki? (Tumaini la maisha baada ya kifo. Kifo sio mwisho kwa Wakristo. Hatuna haja ya kuhuzunikia kifo cha marafiki na wanafamilia kwa sababu tunalo tumaini.)

B.  Soma 1 Wathesalonike 4:14-15. Swali gani linamaanishwa kwenye jibu hili? (Wasomaji wanaamini kuwa Yesu atakuja katika kipindi cha uhai wao, na wanauliza kama lazima wawe hai ili kuchukuliwa mbinguni Yesu atakaporejea.)

1.  Ni nini jibu la swali hilo? (Wale walio hai hawatafika mbinguni kabla ya wale Wakristo waliofariki.)

2.  Je, mtu anaweza kuuliza swali hili kama mwenye haki anakwenda mbinguni wakati anafariki?

C.  Soma 1 Wathesalonike 4:16-17. Nini kinatokea wakati wa ujio wa Yesu Mara ya Pili? (Waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza kutoka ardhini, na kisha wale walio hai wataungana nao “mawinguni” ili kumlaki Yesu. Tutaishi na Yesu milele.)

1.  Elezea wale walio hai Yesu atakapokuja wataona nini? (Watawaona watu waliokufa zamani wakitoka ardhini! Wow!)

D.  Soma 1 Wathesalonike 4:18. Tunapaswa kuwa na mtazamo gani kuhusiana na hili? (Hili linatupatia tumaini!)

1.  Tumaini hili litatimia lini?

II.  Muda wa Marejeo

A.  Angalia tena 1 Wathesalonike 4:17. Kwa nini Paulo, mwandishi wa barua hii kwa Wathesalonike, anaandika “sisi,” kinyume na “wale,” “tulio hai ... tutanyakuliwa?” (Paulo anaamini kuwa atakuwa hai Yesu atakapokuja.)

1.  Hili ni la kawaida kiasi gani – kwamba Wakristo wanaamini kuwa watakuwa hai Yesu atakaporejea? (Kwa maoni yangu ni kwamba ni jambo la kawaida sana.)

B.  Je, una ufahamu na njozi ya Danieli 2? Ikiwa jibu ni hapana, chukua dakika chache uisome. Mungu alimpa Mfalme Nebukadreza njozi ambayo Danieli aliitafsiri. Njozi hii ilitabiri matukio yajayo ulimwenguni kwa usahihi hadi kipindi cha ujio wa Yesu Mara ya Pili. Hiyo inaashiria nini kuhusu unabii mwingine uliotafsiriwa katika kitabu cha Danieli?

C.  Soma Danieli 8:13-14. Katika maoni ya Guzik kuhusiana na unabii huu anabainisha kuwa William Miller aliwatia moyo Wakristo wengi kuamini kuwa Yesu atarejea mwaka 1844. Miller alifikia tarehe hiyo kwa sababu ilikuwa miaka 2,300 baada ya “nchi ya Cyprus kutoa amri ya kulijenga upya hekalu.” Miller aliwezaje kuamini kuwa unabii huu unafika hadi nyakati za sasa kwani unarejelea siku (“jioni na asubuhi?)? (Miller aliamini jambo ambalo Guzik analikataa, kwamba siku zilikuwa ishara ya miaka.)

D.  Soma Danieli 8:27. Tumeruka sehemu kubwa ya njozi aliyooneshwa Danieli. Je, aliielewa? (Hapana. Alikuwa mgonjwa kiasi cha kutoielewa.)

E.  Soma Danieli 9:21-23. Hali ya Danieli inabadilikaje? (Gabrieli anakuja kutoka mbinguni ili kumfafanulia njozi hiyo ya kinabii.)

F.  Soma Danieli 9:24-27. Hatutaingia kwa kina kwenye ufafanuzi wa Gabrieli. Badala yake, nitakwambia kuwa kulikuwa na makubaliano ya jumla miongoni mwa wasomi wa Kikristo miaka mia mbili iliyopita (na hata sasa) kwamba muda huu uliobainishwa (kwa kutumia kanuni ya siku moja = mwaka mmoja) ilitabiri kwa usahihi muda wa kuja kwa Yesu mara ya kwanza (“kuja kwa mtiwa mafuta”), kipindi cha kusulubiwa kwake (“masihi atakatiliwa mbali”) na kuangamizwa kwa hekalu la pili mwaka 70 BK (“watauangamiza mji na patakatifu.”).)

1.  Hii inatufundisha nini kuhusu wale (kama akina Guzik) wanaoikataa kanuni ya siku 1 = mwaka mmoja kwa ajili ya ufafanuzi wa kinabii? (Kwa kuwa kanuni hiyo ilitabiri kwa usahihi ujio wa Yesu mara ya kwanza, kuitakaa kunasababisha tatizo kubwa la kiteolojia kwa wale wanaompokea Yesu kama Masihi.)

G.  Soma tena Danieli 8:14 na 2 Petro 3:5-7. Katika tafsiri ya Biblia ya ESV patakatifu pa Danieli 8:14 “panatakaswa” na kwenye tafsiri ya KJV (na nyinginezo) “panatakaswa.” Dhana ya jumla miongoni mwa tafsiri kadhaa za Biblia ni kwamba patakatifu patatakaswa. Petro anasema kuwa nini kitatokea duniani katika hukumu ya mwisho? (Waovu wataangamizwa kwa moto. Dunia itasafishwa waovu hao.)

H.  Hebu tujadili hili. Bado Wakristo wanaelewa unabii wa Danieli 8 na 9 kuwa sahihi kwa kuzingatia historia ya dunia, kuja kwa Yesu, kipindi alichokaa duniani, na kuangamizwa kwa Yerusalemu. Wengi hawakukubali mwendelezo wa William Miller wa unabii wa siku 2,300 kukoma mwaka 1844. Kimsingi, sasa tunafahamu kwamba Miller hakuwa sahihi. Nimesoma ufafanuzi wa Miller na kama ningeishi katika kipindi chake ningekubaliana naye – isipokuwa utabiri wake wa muda kamili. Angalia Mathayo 24:36. Tunapaswa kuuchukuliaje ufafanuzi huu uliofeli?

1.  Je, tunapaswa kuamini kuwa unabii aliopewa Danieli sio wa kweli au Biblia haiaminiki?

2.  Kama tunaukubali unabii kuwa uko sahihi na Biblia inaaminika, tunapaswa kuhitimisha nini? (Kosa la kibinadamu ndilo linalowajibika.)

I.  Soma Mathayo 24:30 na Mathayo 24:32-35. Kama ingekuwa ulikuwa unamsikiliza Yesu, ungedhani kuwa atarejea lini? (Katika “kizazi hiki,” ikimaanisha katika kipindi cha uhai wangu.)

1.  Angalia cheti cha usahihi (certificate of accuracy) ambacho Yesu anakiweka kwenye maneno yake katika kifungu cha 35. Tunapaswa kuhitimisha nini kuhusiana na hilo? (Hitimisho pekee lenye mantiki kwa Mkristo anayeiamini Biblia ni kwamba tunatakiwa kuwa makini sana kuhusu kuuelewa unabii.) 

III.  Pambano Kuu na Unabii Ulioeleweka Visivyo (Misunderstood)

A.  Nani anayeshinda wafuasi wa Yesu wanapouelewa unabii visivyo?

1.  Je, kuna shaghalabaghala yoyote kwenye ufafanuzi wa unabii ambao hatimaye unafeli? (Nadhani ipo. Kwanza, unawatia watu moyo wa kupenda kuijua Biblia ambao vinginevyo wanaweza kuipuuza. Pili, mwitiko (reaction) wenye mantiki kwenye kuelewa visivyo (misunderstanding) ni kwamba utajifunza Biblia kwa juhudi zaidi ili kujaribu kuielewa kwa usahihi kwa mara ya pili.)

2.  Utakumbuka kwamba hivi karibuni nililalamika kwa uchungu kuhusu Wakristo wanaowashambulia Wakristo wenzao. Shambulio linaibuka kwa sababu wanaamini wakati fulani katika siku zijazo Wakristo wenzao wataweka ukomo wa uhuru wao wa dini. Kushindwa kwa Wayahudi kuelewa unabii wa kutabiri ujio wa Yesu mara ya kwanza na kushindwa kwa Miller kuelewa unabii kuhusu ujio wa Yesu Mara ya Pili inatufundisha nini? (Unyeyekevu.)

B.  Soma Luka 12:35-37. Mfano huu unahusu nini? (Kuwa tayari kwa marejeo ya Yesu.)

C.  Soma Luka 12:38-40. Je, inaonekana kama Yesu alidhani wafuasi wake watakuwa na kipindi cha kutokea kwa unabii kutabiri lini atarejea? (Ni kinyume chake! Yesu anasema (na huu ni unabii) kwamba atakuja muda tusiotarajia. Kuwa tayari nyakati zote.)

D.  Je, inamaanisha kuwa ni “upumbavu” kujaribu kutegua fumbo la unabii wa siku za mwisho?

1.  Kama umejibu, “ndiyo,” kwa nini Mungu alitupatia unabii? (Ninaona mgogoro katika hili. Unabii uliotimia unatupatia imani (confidence) kwenye Biblia na uwezo wa Mungu. Kuuelewa unabii ambao haujatimia kunahitaji unyenyekevu wa kweli.)

2.  Rafiki, tunalo tumaini! Yesu alituahidi uzima baada ya kifo. Atakuja tena na kuwachukua wafuasi wake waaminifu kwenda mbinguni pamoja naye milele! Je, uko tayari? Je, utampokea Yesu sasa hivi ili uishi pamoja naye milele?

IV.  Juma lijalo: Nuru Kutoka Patakatifu.