Somo la 10: Umizimu Wafichuliwa

Error message

  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
  • Deprecated function: unserialize(): Passing null to parameter #1 ($data) of type string is deprecated in css_injector_init() (line 53 of /home/krwester/gobibletranslations.org/sites/all/modules/css_injector/css_injector.module).
1 Samweli 28, Mathayo 10:28, 2 Wathesalonike 2
Swahili
Year: 
2024
Quarter: 
2
Lesson Number: 
10

Somo la 10: Umizimu Wafichuliwa

(1 Samweli 28, Mathayo 10:28, 2 Wathesalonike 2)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ya Kiingereza, marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya ESV® (Biblia Takatifu, English Standard Version®) copyright © by Crossway, wachapishaji wa “Good News Publishers.” Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya ESV® inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na likakupotea kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyinginezo kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Je, umewahi kumchukulia mtu kuwa ni rafiki, badala yake ukagundua kuwa ni adui? Kuwa na uwezo wa kumbainisha rafiki na adui ni jambo la muhimu katika pambano. Waefeso 6:12 inatuambia kuwa tupo kwenye pambano la mieleka “juu ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” Ninapowasikia marafiki au familia inayowazungumzia wanafamilia waliofariki wanaowatembelea au wanaowatumia ujumbe kwa njia ya “ndege,” kipimo changu cha kupima hatari kinaamka mara moja. Ama kwa hakika ndugu hawa waliofariki ni marafiki, na ni watu wa kuaminika, si ndio? Vipi kama sio marafiki waliofariki au wanafamilia, bali ni pepo wachafu? Hebu tuzame kwenye Biblia na tuone kile tunachoweza kujifunza juu ya kumtofautisha rafiki na adui!

I.  Roho Yako?

A.  Soma Mathayo 10:28. Bwana wetu anafundisha nini kuhusiana na endapo wanadamu wana roho inayojitegemea? (Yesu anatuambia kuwa mwili wetu na roho yetu ni vitu viwili tofauti.)

1.  Unadhani roho ni kitu gani hasa?

B.  Soma Mwanzo 3:3-5. Shetani anasema nini kuhusu kifo? (Alimwambia Hawa kuwa hatakufa – tofauti na ambavyo Mungu alikuwa amemwambia.)

1.  Ongezea Mathayo 10:28 kwenye uongo wa Shetani katika bustani ya Edeni. Yesu anasema nini? (Kwamba vyote viwili, yaani mwili wetu na roho yetu ni vitu vinavyokufa. Vyote viwili vinaweza kuangamizwa.)

C.  Soma Warumi 8:16. Hii inatufundisha nini kuhusu endapo wanadamu wana roho? (Inafafanua kuwa roho yetu inawasiliana na Roho Mtakatifu. Kama hujasoma Warumi 8:1-15 kwa muda mrefu, fanya hivyo sasa hivi. Mada ya jumla kwenye vifungu hivyo ni kwamba nyama yetu, mwili wetu, hauna matumaini. Lakini Roho Mtakatifu anatenda kazi kupitia katika mawazo yetu, roho yetu, kuishi kama wana na binti wa Mungu.)

1.  Nimesoma vitabu vingi maarufu kuhusu akili ya mwanadamu. Mojawapo ya matatizo makubwa kwa wanaounga mkono dhana ya uibukaji ni dhana ya kwamba kuibua na kuendeleza kiwango cha juu cha mantiki sio jambo la muhimu kwenye masuala ya asili. Kwa nini tuihitaji roho? Utaiendelezaje roho?

2.  Kwenye kitabu kimoja nilichokisoma kilidai kuwa kiasili watu wanajua kuwa wana utambulisho ambao upo tofauti na mwili wao. Je, hilo ni kweli kwako? (Kama ambavyo tumejifunza hivi punde Biblia inauita ufahamu uliobainishwa tofauti na mwili wetu kama roho yetu.)

3.  Kama ulikuwa na ufahamu kutoka kwenye Biblia kwa kiasi kidogo ambacho tumekipitia hivi punde, utahitimisha nini kuhusu hekima ya kupata ushauri na maelekezo kutoka kwa marafiki na ndugu waliofariki? (Ushauri wa asili kwa Wakristo unatokakana na roho yetu kuwasiliana na Roho Mtakatifu. Kuna hatari kubwa ya kutenda jambo jingine lolote, kama tutakavyoona katika sehemu inayofuata.)

II.  Pepo Wachafu

A.  Soma Isaya 8:18-20. Hii inatufundisha nini kuhusu kutafuta ushauri kutoka kwa wafu? (Kwa nini ufanye hivyo, kama afanyavyo Isaya, wakati unaweza kupata ushauri kutoka kwa Mungu?

B.  Soma Kumbukumbu la Torati 18:9-12. Hii inatufundisha nini kuhusu mtazamo wa Mungu juu ya kushauriana na watu waliofariki, lakini wanaonekana kama wako hai? (Mungu sio tu kwamba analiita hili chukizo, lakini kifungu kinasema kuwa wewe ni chukizo mbele za macho ya Mungu ukilitenda hili.)

C.  Hebu tuangalie kisa cha Biblia kinachofafanua tatizo. Soma 1 Samweli 28:3. Tunajifunza nini kuhusu mshauri mkuu wa Mfalme Sauli? (Samweli amefariki. Kifungu pia kinabainisha kuwa mfalme amewapiga marufuku wale wanaodai kuwa na uwezo wa kuwasiliana na wafu.)

D.  Soma 1 Samweli 28:5-7. Muktadha unaashiria kuwa jambo gani linamhamasisha Sauli kukiuka kanuni zake mwenyewe? (Sauli ana wasiwasi na anaonekana kukata tamaa.)

E.  Soma 1 Samweli 28:8-9. Sauli aliwaondoaje wenye pepo wa utambuzi na wachawi kutoka katika nchi? (Adhabu ya kifo.)

F.  Soma 1 Samweli 28:11-13. Je, hii itaendana na kile unachokifahamu kuhusu maisha ya Samweli kwa yeye kujitokeza mbele ya mungu? (Alikuwa mjumbe wa Mungu, hakudai kuwa yeye ni Mungu.)

G.  Soma 1 Samweli 28:14. Je, Sauli alimwona Samweli? (Hapana. Hii ni taarifa ya pepo wa utambuzi.)

1.  Una maoni gani juu ya undani wa ufafanuzi wa Samweli? (Mzee aliyevaa nguo? Kwa hakika, Sauli alitaka huyu awe Samweli kwa sababu ufafanuzi huu hautoshelezi.)

H.  Soma 1 Samweli 28:15-16. Wanamaoni wengi wanaamini kwamba huyu ni Samweli. Mjadala huu unaimarishaje hitimisho la kwamba huyu ni pepo mchafu na sio Samweli? (Katika 1 Samweli 28:6 Mungu anakataa kumjibu Sauli kwa kutumia njia za mawasiliano zilizothibitishwa – na hiyo iliwajumuisha manabii. Kwa nini Mungu abadili mawazo yake na kutumia njia ambayo kwake ilikuwa ni chukizo? Utaona kwamba “Samweli” anajibu kuwa sasa Sauli ni adui. Kwa nini Mungu amjibu adui wake?

I.  Soma 1 Mambo ya Nyakati 10:13-14. Kati ya dhambi zote za Mfalme Sauli, hii inataja dhambi mbili tu – mojawapo ikiwa ni kushauriana na pepo wa utambuzi. Kama kweli huyu aliyekuwa akiongea alikuwa Samweli, kwa nini hii ichukuliwe kama dhambi kubwa?

J.  Angalia tena 1 Mambo ya Nyakati 10:14. Kifungu kinawezaje kusema kuwa Sauli hakutafuta mwongozo kutoka kwa Mungu, wakati anakwenda mbali zaidi kusikia kutoka kwa Mungu? (Kile ambacho lazima kitakuwa kinamaanishwa kwenye kifungu cha 14 ni kwamba Sauli hakuwa akitafuta mwongozo wa Mungu. Ilikuwa ni dhambi kushauriana na pepo wa utambuzi, na ujumbe wa pepo wa utambuzi haukutoka kwa Mungu, ulitoka kwa pepo mchafu.)

1.  Je, roho wachafu wanaweza kuzungumza? Je, pepo wanaweza kuzungumza? (Soma Mathayo 8:28-31. Wanaweza kuzungumza nasi.)

K.  Soma 1 Samweli 28:19-20. Kwa nini ni kwa maslahi ya Shetani kumwambia Mfalme Sauli kwamba yeye pamoja na wanaye watakufa vitani siku inayofuata? (Shetani anatuchukia. Aliwachukia watu wa Mungu. Njia bora ya kuwa na uhakika kuwa Sauli atashindwa siku inayofuata ni kuangamiza kabisa uwezo wake wa kupigana. Sasa Sauli anaamini kuwa Mungu alimwambia kwamba atashindwa. Alikuwa amekwisha.)

1.  Hii inatufundisha nini kuhusu kushauriana na wafu? (Unaweza kupata ushauri potofu unaodhamiria kukudhuru.)

III.  Pepo Wachafu na Mustakabali Ujao

A.  Soma Ufunuo 16:13-15. Roho wachafu wana nafasi gani katika matukio ya siku za mwisho? (Wanatenda ishara kubwa. Wanawashawishi viongozi wa dunia kumpinga Mungu.)

1.  Kwa nini kifungu cha 15 kipo hapa? (Ni onyo la “kukesha” linapokuja suala la kazi ya roho wachafu.)

B.  Soma 2 Wathesalonike 2:1-2. Mada gani inajadiliwa hapa? (Ujio wa Yesu Mara ya Pili na taarifa za uongo kutoka kwa roho na wanadamu wengine.)

C.  Soma 2 Wathesalonike 2:3-4. Nani ambaye lazima atokee kabla ya ujio wa Yesu Mara ya Pili? (Muasi anayedai kuwa yeye ni Mungu.)

D.  Soma 2 Wathesalonike 2:9-11. Muasi huyu ana nguvu kiasi gani? (“Uwezo wote na ishara na ajabu za uongo.”)

1.  Hebu tusome unabii huu juu ya madanganyo kwenye kisa cha Mfalme Sauli. Je, anaweza kudanganywa? Je, alitaka kudanganywa? (Unabii unafafanua hali ya Sauli kwa usahihi. Alitaka kudanganywa kwa maana ya kwamba alitaka sana kuzungumza na Mungu.)

E.  Soma 2 Wathesalonike 2:12. Jambo gani linawahamasisha wale wanaodanganywa? (Hawakuuamini ukweli.)

F.  Soma 1 Samweli 15:23-26. Kwa nini Mfalme Sauli alikataliwa? (Hakumtii Mungu. Aliasi dhidi ya Mungu. Utaona kwamba uasi unawekwa kwenye kundi moja na ubashiri/uaguzi (uchawi).)

G.  Soma 1 Samweli 15:35. Hii inazungumzia nini kuhusu Samweli kumwona Sauli? (Kamwe hakumwona tena. Huu ni uthibitisho zaidi kwamba Mungu alikataa kuwasiliana na Sauli na hakufanya hivyo kupitia kwa pepo wa utambuzi.)

H.  Hebu turejee kwenye Wathesalonike. Soma 2 Wathesalonike 2:7-8. Je, tunapaswa kujali kuhusu umizimu sasa hivi? (Ndiyo. “Siri ya kutozingatia sheria” ilikuwa inatenda kazi katika kipindi cha Wathesalonike na pia ipo kazini sasa hivi.)

I.   Rafiki, kama unawasiliana na marehemu, unawasiliana na pepo mchafu. Ni adui na sio rafiki. Tafakari jinsi jambo hili lilivyomtendea Mfalme Sauli. Ukihitaji msaada, basi mwombe Roho Mtakatifu ayaongoze mawazo yako! Mungu amemwahidi Roho Mtakatifu. Kwa nini usiidai ahadi hiyo sasa hivi?

IV.  Juma lijalo: Pambano Linalokaribia.