Kuufuatilia Uinjilisti na Ushuhudiaji

(1 Wakorintho 3, Yohana 6)
Swahili
Year: 
2012
Quarter: 
2
Lesson Number: 
5

Utangulizi: je, hili suala la ushuhudiaji ni gumu kwa kiasi gani? Juma lililopita tulijifunza kwamba yule mtu aliyekuwa na pepo, tena mwehu na aliyekuwa uchi alitumwa kwenda kushuhudia katika mji wake baada ya Yesu kuyaondoa mapepo yake. Yule mtu hakuwa na elimu ya juu kuhusu ushuhudiaji, lakini pamoja na hayo, Yesu alimtuma mara moja! Kichwa cha somo letu kinaonyesha mpangilio (mfululizo) wa uinjilisti. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia na tuvumbue jambo hili ambalo mahesabu na mpangilio vina cha kujihusisha na uinjilisti wenye mafanikio!

  1. Maziwa na Chakula
    1. Soma 1 Wakorintho 3:1-2. Je, ungejisikia kudhalilishwa kama Paulo angekuandikia maneno hayo?
      1. Je, “maziwa” ni mafundisho ya aina gani na “chakula kigumu” ni mafundisho ya aina gani? (Kwa mujibu wa Biblia, chakula kigumu ni chakula ambacho ulimwengu hauko tayari kukipokea.)
      2. Mke wangu aliniambia habari kumhusu mmojawapo wa shangazi zake ambaye alikuwa akienda kanisani, akataka kuwa mshiriki, lakini hakuweza kufanya hivyo kwa sababu kanisa lilizuia ubatizo wake ili awe mshiriki isipokuwa tu kama angeachana na mikufu yake. Hakuwa tayari kuachana na mikufu. Kamwe hakujiunga na kanisa na hatimaye alipoteza kabisa msisimko wa kanisa. Je, kanisa mahalia lilikuwa na hatia ya kosa la maziwa/chakula kigumu?
    2. Soma 1 Wakorintho 3:3-4. Je, “tatizo la maziwa” kwa hawa Wakorintho ni lipi? (Wivu na magomvi kuhusiana na walimu. “Mimi ni bora kuliko wewe kwa sababu ninamfuata mwalimu bora!”)
    3. Soma 1 Wakorintho 3:5-9. Je, jibu la Paulo kwa hili tatizo ni lipi? (Kuwaelezea watu wa “maziwa” kwamba hawana uelewa sahihi kuhusu wajibu wa mwalimu na wajibu wa Mungu.)
      1. Je, umegundua suala hili kwa waamini wapya au wachanga – kwamba wanajikuta kwenye magomvi na matatizo yanayoakisi aina ya majivuno yaliyojengwa kwenye upungufu wa maarifa?
      2. Hapa chini ni mifano yangu miwili kutokana na ufundishaji wangu wa siku za nyuma: Wageni au waumini wapya huja darasani kwangu na kunishutumu/kunilaumu kwa sababu ninafundisha kwa kutumia tafsiri ya Biblia ya Kiingereza ya NIV badala ya KJV.Mgeni aliyehudhuria kwa mara ya kwanza darasani alisema kwamba nilikuwa nimevaa mkufu. Alidhani kwamba ninahitaji uangalizi wa mtu mzima.
      3. Je, mifano hii inaakisi mtizamo wa kujikweza? (Hawa wageni kiukweli wanafikiri kuwa: “Wote waliotangulia kunifundisha ni bora zaidi kuliko mwalimu huyu, kwa hiyo nitamshutumu!” Hakuna hata mmoja kati ya wale walioshadadia tafsiri ya Biblia ya KJV walioongea nami baadaye aliyekuwa hata na maarifa ya msingi ya suala lililojadiliwa. “Mkufu” wangu ulikuwa ni bangili ya plastiki wenye Amri Kumi. Angalia Kumbukumbu la Torati 6:6-8.)
    4. Tumejadili tatizo. Tuna mfano kutoka kwenye Biblia na mifano miwili niliyoitoa. Je, jibu gani la “maziwa” linalopaswa kutolewa? Kama unatakiwa kuanza na maziwa, kitu ambacho ulimwengu unaweza kukikubali, je unakabilianaje na kiwango cha Wakristo wenye msisimko wa kiburi cha maziwa? (Tukipitia tena 1 Wakorintho 3:3-8 tunamwona Paulo akifanya mambo mawili. Kwanza, ingawaje ni Wakristo wa kiwango cha “maziwa,” anawakemea. Pili, anawaelezea mtazamo sahihi wa mambo.)
    5. Soma 1 Petro 2:1-3. Kwa kuwa somo letu linahusiana na mpangilio, je, “unywaji wa maziwa” ndio kiwango cha kwanza cha uinjilisti? (Baini jinsi Roho Mtakatifu na mwanafunzi wanavyofanya kazi kwa pamoja katika suala hili. Suala la kwanza ni kukiri dhambi. Suala la pili ni matamanio ya fundisho zuri la kiroho. Hii inahitaji uamuzi wa mwanafunzi. Utembelewaji na uguswaji wa Roho Mtakatifu ni vya muhimu/vya msingi.)
    6. Hebu tuangalia tatizo jingine lenye uhalisia. Kama tunatakiwa kuanza na maziwa, je, ni njia gani mahsusi ya kivitendo ya uinjilisti inayopendekezwa?
      1. Miaka mingi iliyopita, kanisa langu lilikuwa kwenye majadiliano kuwa ni njia gani bora ambayo linaweza kuifikia jamii. Kundi moja kanisani lilidhani kuwa tulipaswa kusambaza kitabu kinachohusu maisha ya Yesu. Kundi jingine lilidhani kuwa tulipaswa kusambaza kitabu kinachohusu historia ya pambano kati ya wema na uovu na unabii wa siku zijazo. Je, unadhani ni kitabu gani kilichopaswa kusambazwa na kwa nini? (Maisha, kifo na ufufuo wa Yesu ni maziwa. Kitambu kingine kinaonekana zaidi kuwa kama chakula.)
    7. Soma Mathayo 25:34-36 na Luka 9:11. Je, kuna dhana nyingine ya njia ya “maziwa kwanza” ambayo hatujaijadili? Njia iliyopendekezwa kwenye haya mafungu? (Ndiyo! Kumwendea mtu mgeni asiye na nia na kujaribu kumbadili ni vigumu kwa sababu huaminiki. Hatua ya kwanza ni kuwafanya wageni wawe marafiki. Mara wanapokuwa marafiki, tutaaminika kuongea nao kuhusu injili.)
    8. Hebu tupitie upya tena. Kuna mpangilio wa uinjilisti. Hatua ya kwanza ni kuwa rafiki mwenye msaada. Hatua ya pili ni kumkubali Yesu na kutubu dhambi. Hatua ya tatu ni kufundisha mambo ambayo muumini mpya atayakubali, na kuyaacha mafundisho magumu zaidi ili yaje yafundishwe baadaye. Wakati mchakato huu ukiendelea, tunahitajika kuangalia majivuno na makosa, na tusiogope kukemea makosa kwa upole na kuuelezea ukweli.
  2. Chakula
    1. Hebu turejee kwenye Wakorintho wa Kwanza. Soma 1 Wakorintho 3:10. Je, Paulo anaionaje kazi yake? (Yeye ni “mtaalam” ajengaye “msingi.”)
      1. Je, ni onyo gani analolitoa kwa Wakristo wakomavu zaidi? (Kama vile Wakristo wa maziwa wanavyoweza kuwa wenye kujigamba/wenye makuu, vivyo hivyo Wakristo wa chakula wanapaswa kuwa waangalifu jinsi wanavyojenga.)
    2. Soma 1 Wakorintho 3:11. Je, chakula kigumu, chakula ni vitu gani, ambavyo vinapaswa kuwa vya msingi kwenye mafundisho yote? (Yesu! Hivi punde tu tumeongelea jinsi ambavyo Yesu ni maziwa, lakini pia ni chakula. Hatuwezi kuongelea kila kitu kwenye somo letu kinachohusu kile alichotutendea. Fundisho lililojikita kwenye mambo mengine madogo madogo sio msingi sahihi.)
    3. Soma 1 Wakorintho 3:12-13. Je, kuna tofauti kwenye ubora wa kazi ya walimu wa Kikristo?
      1. Je, tunawezaje kuwaelezea walimu wa kiwango cha dhahabu dhidi ya wale wa kiwango cha majani? (Uchunguzi (nuru) utayafunua yote hayo. Moto (majaribu) utayafunua yote hayo.)
      2. Je, vipi kama wewe ni mwalimu, na ( kama ilivyo kwangu) mtu fulani mgeni akakukemea? (Unahitajika kulichukulia kemeo hilo kwa dhati ili uweze kuangalia kama ni majivuno yasiyoelimika au ukweli.)
    4. Soma 1 Wakorintho 3:14-15. Kama wewe ni mwalimu, na unasoma kuhusu hili suala, je, hujafurahia! Nani anayepoteza kwa mwalimu wa kiwango cha majani? (Mwanafunzi! Mwalimu anapona, lakini kwa bahati sana.)Nani anayefaidi kwa mwalimu wa kiwango cha dhahabu? (Mwanafunzi na mwalimu.)
    5. Soma Yohana 14:15-21. Je, ni kweli zipi za msingi za chakula tunazoziona kwenye haya mafungu? (Roho Mtakatifu ni wa msingi kwenye safari yetu ya Kikristo. Utii ni wa msingi kwenye safari yetu ya Kikristo. Utii unaonyesha kuwa tunampenda Mungu.)
  3. Jaribu la Chakula
    1. Soma Yohana 6:35-37. Sasa tunao mfano wa chakula kigumu. (Yesu anakiita mkate badala ya chakula.) Kwa nini Yesu anajilinganisha na mkate? (Unahitaji mkate ili uweze kuishi. Kuna mwendelezo wa asili. Tunaanza na maziwa, tunaendelea kwenye chakula.)
    2. Soma Yohana 6:41-42. Je, Yesu alipaswa kuwapa maziwa badala ya hiki chakula?
    3. Soma Yohana 6:43-51. Je, unaelezeaje hapa kile anachokifundisha Yesu – maziwa au chakula? (Kukubali kuwa Yesu ni Mungu ndio kitu cha msingi. Linapaswa kuwa fundisho la “maziwa.”)
    4. Soma Yohana 6:52-57. Je, haya ni maziwa au chakula? (Nadhani hili ni fundisho kubwa zaidi. Hiki ni chakula.)
    5. Soma Yohana 6:66. Je, hii inatufundisha nini? Kwamba Yesu alikosea kwa kutosalia kwenye ujumbe wa maziwa? (Hapana. Hii inatufundisha kuwa hata kama tunafuata mwendelezo sahihi wa msaada, maziwa na chakula, tutakuwa na watu ambao hawawezi kuukubali ukweli. Maziwa zaidi sio jibu. Badala yake, lazima tutambue kuwa Mungu anatupatia uhuru wa uchaguzi, na kwa watu wengi Ufalme wa Mbingu sio kipaumbele.)
    6. Rafiki, je, utakuwa na utambuzi wa mpangilio wa uinjilisti? Kwanza saidia, kisha maziwa, halafu chakula. Kwa nini usianze leo?
  4. Juma lijalo: Uinjilisti na Ushuhudiaji Binafsi.